1 Kings 8 (BOKCV)

1 Kisha Mfalme Solomoni akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la BWANA kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. 2 Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa Mfalme Solomoni wakati wa sikukuu ya mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba. 3 Wazee wote wa Israeli walipofika, makuhani wakajitwika Sanduku la Agano, 4 nao wakalipandisha Sanduku la BWANA, na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani na Walawi wakavibeba, 5 naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ngʼombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa. 6 Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la BWANA hadi mahali pake ndani ya sehemu takatifu ndani ya Hekalu, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi. 7 Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kutia kivuli Sanduku pamoja na mipiko yake ya kubebea. 8 Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilionekana kutoka Mahali Patakatifu mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo. 9 Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili za mawe ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo BWANA alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri. 10 Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la BWANA. 11 Nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa BWANA ulijaza Hekalu lake. 12 Ndipo Solomoni akasema, “BWANA alisema kwamba ataishi katika giza nene; 13 naam, hakika nimekujengea Hekalu zuri sana, mahali pako pa kuishi milele.” 14 Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki. 15 Kisha akasema:“Ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mkono wake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema, 16 ‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’ 17 “Ilikuwa moyoni mwa Daudi baba yangu kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la BWANA, Mungu wa Israeli. 18 Lakini BWANA akamwambia Daudi baba yangu, ‘Kwa sababu ilikuwa moyoni mwako kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu, ulifanya vyema kuwa na jambo hili moyoni mwako. 19 Hata hivyo, sio wewe utakayenijengea hekalu, bali mwanao, ambaye ni nyama yako na damu yako mwenyewe, yeye ndiye atakayejenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’ 20 “BWANA ametimiza ahadi aliyoiweka: Nimeingia mahali pa Daudi baba yangu na sasa ninakikalia kiti cha ufalme cha Israeli, kama vile BWANA alivyoahidi, nami nimejenga Hekalu kwa ajili ya Jina la BWANA, Mungu wa Israeli. 21 Nimetenga nafasi humo kwa ajili ya Sanduku la Agano, ambamo ndani yake kuna lile Agano la BWANA alilofanya na baba zetu wakati alipowatoa Misri.” 22 Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA machoni pa kusanyiko lote la Israeli, akakunjua mikono yake kuelekea mbinguni 23 na kusema:“Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni wala chini duniani, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote. 24 Umetimiza ahadi yako kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, kwa kinywa chako uliahidi na kwa mkono wako umetimiza, kama ilivyo leo. 25 “Sasa BWANA, Mungu wa Israeli, mtimizie mtumishi wako Daudi baba yangu ahadi zako ulizomwahidi uliposema, ‘Kamwe hutakosa kuwa na mtu atakayeketi mbele zangu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli, kama wanao wakiangalia yote wayafanyayo kuenenda mbele zangu kama vile ulivyofanya.’ 26 Sasa, Ee Mungu wa Israeli, acha neno lako lile ulilomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu litimie. 27 “Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga! 28 Hata hivyo sikiliza dua ya mtumishi wako na maombi yake kwa huruma, Ee BWANA Mungu wangu. Sikia kilio na dua ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako siku hii ya leo. 29 Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa. 30 Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia kutoka mbinguni, mahali pa makao yako na usikiapo, samehe. 31 “Mtu anapomkosea jirani yake na akatakiwa kuapa, akija na kuapa mbele ya madhabahu yako ndani ya Hekalu hili, 32 basi, sikia kutoka mbinguni na ukatende. Hukumu kati ya watumishi wako, ukimhukumu yule mwenye hatia na kuleta juu ya kichwa chake yale aliyoyatenda. Umtangazie mwenye haki kwamba hana hatia, hivyo ukathibitishe kuwa haki kwake. 33 “Wakati watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, watakapokugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili, 34 basi usikie kutoka mbinguni, ukasamehe dhambi ya watu wako Israeli na kuwarudisha katika nchi uliyowapa baba zao. 35 “Wakati mbingu zitakapokuwa zimefungwa kusiwe na mvua kwa sababu watu wako wametenda dhambi dhidi yako, watakapoomba kuelekea mahali hapa na kulikiri jina lako nao wakageuka kutoka dhambi zao kwa sababu umewaadhibu, 36 basi usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi. 37 “Wakati njaa au tauni vikija juu ya nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au wakati adui atakapowazingira katika mji wao wowote, maafa ya namna yoyote au ugonjwa wowote unaoweza kuwajia, 38 wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akitambua taabu za moyo wake mwenyewe, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili: 39 basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote), 40 ili wakuogope kwa wakati wote watakaoishi katika nchi uliyowapa baba zetu. 41 “Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako, 42 kwa maana watu watasikia juu ya Jina lako kuu na juu ya mkono wako wenye nguvu na mkono wako ulionyooshwa, atakapokuja na kuomba kuelekea Hekalu hili, 43 basi na usikie kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, ukafanye lolote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako. 44 “Wakati watu wako watakapokwenda vitani dhidi ya adui zao, popote utakapowapeleka, wakati watakapoomba kwa BWANA kuelekea mji ambao umeuchagua, na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, 45 basi usikie dua na maombi yao kutoka mbinguni, ukawatetee haki yao. 46 “Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu yeyote ambaye hatendi dhambi, nawe ukachukizwa nao na kuwakabidhi kwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi yake mwenyewe, mbali au karibu; 47 na kama watabadilika mioyo yao katika nchi wanakoshikiliwa mateka, nao wakatubu na kukulilia katika nchi ya wale waliowashinda na kusema, ‘Tumetenda dhambi, tumefanya makosa, tumetenda uovu’; 48 kama wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako; 49 basi kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, usikie dua yao na maombi yao na kuitetea haki yao. 50 Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako; uwasamehe makosa yote waliyoyatenda dhidi yako, ukawafanye wale waliowashinda kuwaonea huruma; 51 kwa maana ni watu wako na urithi wako, uliowatoa Misri, kutoka kwenye lile tanuru la kuyeyushia chuma. 52 “Macho yako na yafumbuke juu ya ombi la mtumishi wako na ombi la watu wako Israeli, nawe uwasikilize wakati wowote wanapokulilia. 53 Kwa maana uliwachagua wao kutoka mataifa yote ya ulimwengu kuwa urithi wako mwenyewe, kama ulivyotangaza kupitia mtumishi wako Mose wakati wewe, Ee BWANA Mwenyezi, ulipowatoa baba zetu kutoka Misri.” 54 Wakati Solomoni alipomaliza dua hizi zote na maombi kwa BWANA, akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya BWANA, mahali alipokuwa amepiga magoti, mikono yake ikawa imekunjuliwa kuelekea juu mbinguni. 55 Akasimama na kubariki kusanyiko lote la Israeli kwa sauti kubwa akisema: 56 “Ahimidiwe BWANA, aliyewapa pumziko watu wake Israeli kama vile alivyokuwa ameahidi. Hakuna hata neno moja lililopunguka kati ya ahadi zote nzuri alizozitoa kupitia mtumishi wake Mose. 57 BWANA Mungu wetu na awe pamoja nasi kama alivyokuwa na baba zetu, kamwe asituache wala kutukataa. 58 Yeye na aielekeze mioyo yetu kwake, ili tutembee katika njia zake zote na kuzishika amri na maagizo na masharti aliyowapa baba zetu. 59 Nami maneno yangu haya, ambayo nimeyaomba mbele za BWANA, yawe karibu na BWANA Mungu wetu usiku na mchana, ili kwamba atetee shauri la mtumishi wake na la watu wake Israeli kulingana na hitaji lao la kila siku, 60 ili kwamba mataifa yote ya dunia wajue kwamba BWANA ndiye Mungu na kwamba hakuna mwingine. 61 Lakini ni lazima mwiweke mioyo yenu kikamilifu kwa BWANA Mungu wetu, kuishi kwa maagizo yake na kutii amri zake, kama ilivyo wakati huu.” 62 Kisha mfalme na Israeli wote pamoja naye wakatoa dhabihu mbele za BWANA. 63 Solomoni akatoa dhabihu sadaka za amani kwa BWANA: ngʼombe 22,000, pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na Waisraeli wote walivyoweka wakfu Hekalu la BWANA. 64 Siku iyo hiyo mfalme akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la BWANA na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za BWANA ilikuwa ndogo sana kuweza kubeba sadaka hizo za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya sadaka ya amani. 65 Hivyo Solomoni akaiadhimisha sikukuu kwa wakati ule, na Israeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. Wakaiadhimisha mbele za BWANA Mungu wetu kwa siku saba na siku saba zaidi, yaani, jumla siku kumi na nne. 66 Siku iliyofuata, aliwaruhusu watu waondoke. Wakambariki mfalme, kisha wakaenda nyumbani, wakiwa na mashangilio na furaha rohoni kwa ajili ya mambo yote mema ambayo BWANA ametenda kwa ajili ya Daudi mtumishi wake na watu wake Israeli.

In Other Versions

1 Kings 8 in the ANGEFD

1 Kings 8 in the ANTPNG2D

1 Kings 8 in the AS21

1 Kings 8 in the BAGH

1 Kings 8 in the BBPNG

1 Kings 8 in the BBT1E

1 Kings 8 in the BDS

1 Kings 8 in the BEV

1 Kings 8 in the BHAD

1 Kings 8 in the BIB

1 Kings 8 in the BLPT

1 Kings 8 in the BNT

1 Kings 8 in the BNTABOOT

1 Kings 8 in the BNTLV

1 Kings 8 in the BOATCB

1 Kings 8 in the BOATCB2

1 Kings 8 in the BOBCV

1 Kings 8 in the BOCNT

1 Kings 8 in the BOECS

1 Kings 8 in the BOGWICC

1 Kings 8 in the BOHCB

1 Kings 8 in the BOHCV

1 Kings 8 in the BOHLNT

1 Kings 8 in the BOHNTLTAL

1 Kings 8 in the BOICB

1 Kings 8 in the BOILNTAP

1 Kings 8 in the BOITCV

1 Kings 8 in the BOKCV2

1 Kings 8 in the BOKHWOG

1 Kings 8 in the BOKSSV

1 Kings 8 in the BOLCB

1 Kings 8 in the BOLCB2

1 Kings 8 in the BOMCV

1 Kings 8 in the BONAV

1 Kings 8 in the BONCB

1 Kings 8 in the BONLT

1 Kings 8 in the BONUT2

1 Kings 8 in the BOPLNT

1 Kings 8 in the BOSCB

1 Kings 8 in the BOSNC

1 Kings 8 in the BOTLNT

1 Kings 8 in the BOVCB

1 Kings 8 in the BOYCB

1 Kings 8 in the BPBB

1 Kings 8 in the BPH

1 Kings 8 in the BSB

1 Kings 8 in the CCB

1 Kings 8 in the CUV

1 Kings 8 in the CUVS

1 Kings 8 in the DBT

1 Kings 8 in the DGDNT

1 Kings 8 in the DHNT

1 Kings 8 in the DNT

1 Kings 8 in the ELBE

1 Kings 8 in the EMTV

1 Kings 8 in the ESV

1 Kings 8 in the FBV

1 Kings 8 in the FEB

1 Kings 8 in the GGMNT

1 Kings 8 in the GNT

1 Kings 8 in the HARY

1 Kings 8 in the HNT

1 Kings 8 in the IRVA

1 Kings 8 in the IRVB

1 Kings 8 in the IRVG

1 Kings 8 in the IRVH

1 Kings 8 in the IRVK

1 Kings 8 in the IRVM

1 Kings 8 in the IRVM2

1 Kings 8 in the IRVO

1 Kings 8 in the IRVP

1 Kings 8 in the IRVT

1 Kings 8 in the IRVT2

1 Kings 8 in the IRVU

1 Kings 8 in the ISVN

1 Kings 8 in the JSNT

1 Kings 8 in the KAPI

1 Kings 8 in the KBT1ETNIK

1 Kings 8 in the KBV

1 Kings 8 in the KJV

1 Kings 8 in the KNFD

1 Kings 8 in the LBA

1 Kings 8 in the LBLA

1 Kings 8 in the LNT

1 Kings 8 in the LSV

1 Kings 8 in the MAAL

1 Kings 8 in the MBV

1 Kings 8 in the MBV2

1 Kings 8 in the MHNT

1 Kings 8 in the MKNFD

1 Kings 8 in the MNG

1 Kings 8 in the MNT

1 Kings 8 in the MNT2

1 Kings 8 in the MRS1T

1 Kings 8 in the NAA

1 Kings 8 in the NASB

1 Kings 8 in the NBLA

1 Kings 8 in the NBS

1 Kings 8 in the NBVTP

1 Kings 8 in the NET2

1 Kings 8 in the NIV11

1 Kings 8 in the NNT

1 Kings 8 in the NNT2

1 Kings 8 in the NNT3

1 Kings 8 in the PDDPT

1 Kings 8 in the PFNT

1 Kings 8 in the RMNT

1 Kings 8 in the SBIAS

1 Kings 8 in the SBIBS

1 Kings 8 in the SBIBS2

1 Kings 8 in the SBICS

1 Kings 8 in the SBIDS

1 Kings 8 in the SBIGS

1 Kings 8 in the SBIHS

1 Kings 8 in the SBIIS

1 Kings 8 in the SBIIS2

1 Kings 8 in the SBIIS3

1 Kings 8 in the SBIKS

1 Kings 8 in the SBIKS2

1 Kings 8 in the SBIMS

1 Kings 8 in the SBIOS

1 Kings 8 in the SBIPS

1 Kings 8 in the SBISS

1 Kings 8 in the SBITS

1 Kings 8 in the SBITS2

1 Kings 8 in the SBITS3

1 Kings 8 in the SBITS4

1 Kings 8 in the SBIUS

1 Kings 8 in the SBIVS

1 Kings 8 in the SBT

1 Kings 8 in the SBT1E

1 Kings 8 in the SCHL

1 Kings 8 in the SNT

1 Kings 8 in the SUSU

1 Kings 8 in the SUSU2

1 Kings 8 in the SYNO

1 Kings 8 in the TBIAOTANT

1 Kings 8 in the TBT1E

1 Kings 8 in the TBT1E2

1 Kings 8 in the TFTIP

1 Kings 8 in the TFTU

1 Kings 8 in the TGNTATF3T

1 Kings 8 in the THAI

1 Kings 8 in the TNFD

1 Kings 8 in the TNT

1 Kings 8 in the TNTIK

1 Kings 8 in the TNTIL

1 Kings 8 in the TNTIN

1 Kings 8 in the TNTIP

1 Kings 8 in the TNTIZ

1 Kings 8 in the TOMA

1 Kings 8 in the TTENT

1 Kings 8 in the UBG

1 Kings 8 in the UGV

1 Kings 8 in the UGV2

1 Kings 8 in the UGV3

1 Kings 8 in the VBL

1 Kings 8 in the VDCC

1 Kings 8 in the YALU

1 Kings 8 in the YAPE

1 Kings 8 in the YBVTP

1 Kings 8 in the ZBP