1 Samuel 2 (BOKCV)

1 Kisha Hana akaomba na kusema:“Moyo wangu wamshangilia BWANA,katika BWANA pembe yangu imeinuliwa juu.Kinywa changu chajisifu juu ya adui zangu,kwa kuwa naufurahia wokovu wako. 2 “Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama BWANA,hakuna mwingine zaidi yako;hakuna Mwamba kama Mungu wetu. 3 “Msiendelee kusema kwa kiburi hivyowala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi,kwa kuwa BWANA ndiye Mungu ajuaye,na kwa yeye matendo hupimwa. 4 “Pinde za mashujaa zimevunjika,lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu. 5 Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyeweili kupata chakula,lakini wale waliokuwa na njaahawana njaa tena.Mwanamke yule aliyekuwa tasaamezaa watoto saba,lakini yule ambaye alikuwa na wana wengiamedhoofika. 6 “BWANA huua na huleta uhai,hushusha chini mpaka kaburini na hufufua. 7 BWANA humfanya mtu maskini naye hutajirisha,hushusha na hukweza. 8 Humwinua maskini kutoka mavumbinina humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu;huwaketisha pamoja na wakuuna kuwafanya warithi kiti cha enzi cha heshima. “Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya BWANA;juu yake ameuweka ulimwengu. 9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake,lakini waovu watanyamazishwa kwenye giza. “Si kwa nguvu mtu hushinda; 10 wale wampingao BWANAwataharibiwa kabisa.Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni; BWANA ataihukumu miisho ya dunia. “Atampa nguvu mfalme wake,na kuitukuza pembeya mpakwa mafuta wake.” 11 Kisha Elikana akaenda nyumbani Rama, lakini mtoto akahudumu mbele za BWANA chini ya kuhani Eli. 12 Wana wa Eli walikuwa watu wabaya kabisa, hawakumheshimu BWANA. 13 Basi ilikuwa desturi ya makuhani pamoja na watu kwamba kila mara yeyote anapotoa dhabihu na huku nyama ikiwa inachemshwa, mtumishi wa kuhani angalikuja na uma wenye meno matatu mkononi mwake. 14 Angeutumbukiza huo uma kwenye sufuria au birika au sufuria kubwa au chungu, naye kuhani angalijichukulia mwenyewe chochote ambacho uma ungekileta. Hivi ndivyo walivyowatendea Waisraeli wote waliokuja Shilo. 15 Lakini hata kabla mafuta ya mnyama hayajachomwa, mtumishi wa kuhani angalikuja na kusema kwa mtu ambaye alikuwa akitoa dhabihu, “Mpe kuhani nyama akaoke, kwani hatapokea nyama iliyochemshwa kutoka kwako, ila iliyo mbichi tu.” 16 Kama mtu akimwambia, “Mafuta ya mnyama na yachomwe kwanza, ndipo uchukue chochote unachotaka,” mtumishi angalijibu, “Hapana, nipe sasa, kama huwezi nitaichukua kwa nguvu.” 17 Hii Dhambi ya hawa vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa BWANA, kwa kuwa waliitendea dhabihu ya BWANA kwa dharau. 18 Lakini Samweli alikuwa akihudumu mbele za BWANA, kijana akivaa kisibau cha kitani. 19 Kila mwaka mama yake alimshonea joho dogo na kumchukulia wakati alipokwea pamoja na mumewe kutoa dhabihu ya mwaka. 20 Eli alikuwa akiwabariki Elikana na mkewe, akisema, “BWANA na akupe watoto kwa mwanamke huyu ili kuchukua nafasi ya yule aliyekuwa amemwomba na akamtoa kwa BWANA.” Kisha wakawa wanakwenda nyumbani. 21 BWANA akawa mwenye neema kwa Hana, naye akapata mimba akazaa wana watatu na binti wawili. Wakati huo, kijana Samweli akaendelea kukua mbele za BWANA. 22 Basi Eli, ambaye alikuwa mzee sana, alisikia kuhusu kila kitu ambacho wanawe walikuwa wakiwafanyia Israeli wote na jinsi walivyokutana kimwili na wanawake waliohudumu kwenye ingilio la Hema la Kukutania. 23 Hivyo akawaambia, “Kwa nini mmefanya mambo kama haya? Nimesikia kutoka kwa watu wote juu ya haya matendo yenu maovu. 24 Sivyo, wanangu, hii si habari nzuri ambayo ninasikia ikienea miongoni mwa watu wa BWANA. 25 Kama mtu akifanya dhambi dhidi ya mtu mwenzake, mtu mwingine aweza kumwombea kwa Mungu, lakini kama mtu akimfanyia Mungu dhambi, ni nani atakayemwombea?” Hata hivyo wanawe hawakusikia maonyo ya baba yao, kwa sababu BWANA alitaka kuwaua. 26 Naye kijana Samweli akaendelea kukua katika kimo, akimpendeza BWANA na wanadamu. 27 Basi mtu wa Mungu akaja kwa Eli na kumwambia, “Hivi ndivyo asemavyo BWANA: ‘Je, sikujifunua waziwazi kwa nyumba ya baba yako wakati walikuwa huko Misri chini ya Farao? 28 Nilimchagua baba yako kati ya makabila yote ya Israeli kuwa kuhani wangu, kukwea kwenye madhabahu yangu, kufukiza uvumba na kuvaa kisibau mbele yangu. Pia niliwapa nyumba ya baba yako sadaka zote zilizotolewa kwa moto na Waisraeli. 29 Kwa nini unadharau dhabihu zangu na sadaka zile nilizoziamuru kwa ajili ya makao yangu? Kwa nini unawaheshimu wanao kuliko mimi kwa kujinenepesha wenyewe kwa kula sehemu zilizo bora za kila sadaka zinazotolewa na watu wangu wa Israeli?’ 30 “Kwa hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli asema: ‘Niliahidi kuwa nyumba yako na nyumba ya baba yako wangehudumu mbele zangu milele.’ Lakini sasa BWANA anasema: ‘Jambo hili na liwe mbali nami! Wale wanaoniheshimu nitawaheshimu, wale wanaonidharau mimi watadharauliwa. 31 Wakati unakuja nitakapozipunguza nguvu zenu na nguvu ya nyumba ya baba yenu, ili pasiwepo mtu katika mbari yenu atakayeishi kuuona uzee 32 nanyi mtaona huzuni katika makao yangu. Ingawa Israeli watafanyiwa mema, katika mbari yenu kamwe hapatakuwepo mtu atakayeishi hadi kuwa mzee. 33 Kila mmoja wenu ambaye sitamkatilia mbali kutoka madhabahuni pangu atabakizwa tu kupofusha macho yenu kwa machozi na kuihuzunisha mioyo yenu, nao wazao wenu wote watakufa watakapokuwa wamefikia umri wa kustawi. 34 “ ‘Kile kitakachotokea kwa wanao wawili, Hofni na Finehasi, kitakuwa ishara kwako. Wote wawili watakufa katika siku moja. 35 Mimi mwenyewe nitajiinulia kuhani mwaminifu, ambaye atafanya sawasawa na kile kilichoko moyoni mwangu na akilini mwangu. Nitaifanya nyumba yake kuwa imara, naye atahudumu mbele ya mpakwa mafuta wangu daima. 36 Kisha kila mmoja aliyeachwa katika mbari yenu atakuja na kusujudu mbele yake kwa ajili ya kipande cha fedha na ganda la mkate akisema, “Niteue katika baadhi ya ofisi ya ukuhani ili niweze kupata chakula.” ’ ”

In Other Versions

1 Samuel 2 in the ANGEFD

1 Samuel 2 in the ANTPNG2D

1 Samuel 2 in the AS21

1 Samuel 2 in the BAGH

1 Samuel 2 in the BBPNG

1 Samuel 2 in the BBT1E

1 Samuel 2 in the BDS

1 Samuel 2 in the BEV

1 Samuel 2 in the BHAD

1 Samuel 2 in the BIB

1 Samuel 2 in the BLPT

1 Samuel 2 in the BNT

1 Samuel 2 in the BNTABOOT

1 Samuel 2 in the BNTLV

1 Samuel 2 in the BOATCB

1 Samuel 2 in the BOATCB2

1 Samuel 2 in the BOBCV

1 Samuel 2 in the BOCNT

1 Samuel 2 in the BOECS

1 Samuel 2 in the BOGWICC

1 Samuel 2 in the BOHCB

1 Samuel 2 in the BOHCV

1 Samuel 2 in the BOHLNT

1 Samuel 2 in the BOHNTLTAL

1 Samuel 2 in the BOICB

1 Samuel 2 in the BOILNTAP

1 Samuel 2 in the BOITCV

1 Samuel 2 in the BOKCV2

1 Samuel 2 in the BOKHWOG

1 Samuel 2 in the BOKSSV

1 Samuel 2 in the BOLCB

1 Samuel 2 in the BOLCB2

1 Samuel 2 in the BOMCV

1 Samuel 2 in the BONAV

1 Samuel 2 in the BONCB

1 Samuel 2 in the BONLT

1 Samuel 2 in the BONUT2

1 Samuel 2 in the BOPLNT

1 Samuel 2 in the BOSCB

1 Samuel 2 in the BOSNC

1 Samuel 2 in the BOTLNT

1 Samuel 2 in the BOVCB

1 Samuel 2 in the BOYCB

1 Samuel 2 in the BPBB

1 Samuel 2 in the BPH

1 Samuel 2 in the BSB

1 Samuel 2 in the CCB

1 Samuel 2 in the CUV

1 Samuel 2 in the CUVS

1 Samuel 2 in the DBT

1 Samuel 2 in the DGDNT

1 Samuel 2 in the DHNT

1 Samuel 2 in the DNT

1 Samuel 2 in the ELBE

1 Samuel 2 in the EMTV

1 Samuel 2 in the ESV

1 Samuel 2 in the FBV

1 Samuel 2 in the FEB

1 Samuel 2 in the GGMNT

1 Samuel 2 in the GNT

1 Samuel 2 in the HARY

1 Samuel 2 in the HNT

1 Samuel 2 in the IRVA

1 Samuel 2 in the IRVB

1 Samuel 2 in the IRVG

1 Samuel 2 in the IRVH

1 Samuel 2 in the IRVK

1 Samuel 2 in the IRVM

1 Samuel 2 in the IRVM2

1 Samuel 2 in the IRVO

1 Samuel 2 in the IRVP

1 Samuel 2 in the IRVT

1 Samuel 2 in the IRVT2

1 Samuel 2 in the IRVU

1 Samuel 2 in the ISVN

1 Samuel 2 in the JSNT

1 Samuel 2 in the KAPI

1 Samuel 2 in the KBT1ETNIK

1 Samuel 2 in the KBV

1 Samuel 2 in the KJV

1 Samuel 2 in the KNFD

1 Samuel 2 in the LBA

1 Samuel 2 in the LBLA

1 Samuel 2 in the LNT

1 Samuel 2 in the LSV

1 Samuel 2 in the MAAL

1 Samuel 2 in the MBV

1 Samuel 2 in the MBV2

1 Samuel 2 in the MHNT

1 Samuel 2 in the MKNFD

1 Samuel 2 in the MNG

1 Samuel 2 in the MNT

1 Samuel 2 in the MNT2

1 Samuel 2 in the MRS1T

1 Samuel 2 in the NAA

1 Samuel 2 in the NASB

1 Samuel 2 in the NBLA

1 Samuel 2 in the NBS

1 Samuel 2 in the NBVTP

1 Samuel 2 in the NET2

1 Samuel 2 in the NIV11

1 Samuel 2 in the NNT

1 Samuel 2 in the NNT2

1 Samuel 2 in the NNT3

1 Samuel 2 in the PDDPT

1 Samuel 2 in the PFNT

1 Samuel 2 in the RMNT

1 Samuel 2 in the SBIAS

1 Samuel 2 in the SBIBS

1 Samuel 2 in the SBIBS2

1 Samuel 2 in the SBICS

1 Samuel 2 in the SBIDS

1 Samuel 2 in the SBIGS

1 Samuel 2 in the SBIHS

1 Samuel 2 in the SBIIS

1 Samuel 2 in the SBIIS2

1 Samuel 2 in the SBIIS3

1 Samuel 2 in the SBIKS

1 Samuel 2 in the SBIKS2

1 Samuel 2 in the SBIMS

1 Samuel 2 in the SBIOS

1 Samuel 2 in the SBIPS

1 Samuel 2 in the SBISS

1 Samuel 2 in the SBITS

1 Samuel 2 in the SBITS2

1 Samuel 2 in the SBITS3

1 Samuel 2 in the SBITS4

1 Samuel 2 in the SBIUS

1 Samuel 2 in the SBIVS

1 Samuel 2 in the SBT

1 Samuel 2 in the SBT1E

1 Samuel 2 in the SCHL

1 Samuel 2 in the SNT

1 Samuel 2 in the SUSU

1 Samuel 2 in the SUSU2

1 Samuel 2 in the SYNO

1 Samuel 2 in the TBIAOTANT

1 Samuel 2 in the TBT1E

1 Samuel 2 in the TBT1E2

1 Samuel 2 in the TFTIP

1 Samuel 2 in the TFTU

1 Samuel 2 in the TGNTATF3T

1 Samuel 2 in the THAI

1 Samuel 2 in the TNFD

1 Samuel 2 in the TNT

1 Samuel 2 in the TNTIK

1 Samuel 2 in the TNTIL

1 Samuel 2 in the TNTIN

1 Samuel 2 in the TNTIP

1 Samuel 2 in the TNTIZ

1 Samuel 2 in the TOMA

1 Samuel 2 in the TTENT

1 Samuel 2 in the UBG

1 Samuel 2 in the UGV

1 Samuel 2 in the UGV2

1 Samuel 2 in the UGV3

1 Samuel 2 in the VBL

1 Samuel 2 in the VDCC

1 Samuel 2 in the YALU

1 Samuel 2 in the YAPE

1 Samuel 2 in the YBVTP

1 Samuel 2 in the ZBP