1 Chronicles 12 (BOKCV)

1 Hawa ndio watu waliomjia Daudi huko Siklagi, wakati alikuwa amefukuzwa mbele ya Sauli mwana wa Kishi (walikuwa miongoni mwa mashujaa waliomsaidia Daudi vitani, 2 walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia; hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini): 3 Mkuu wao alikuwa Ahiezeri, na wa pili Yoashi, wote wana wa Shemaa Mgibeathi; pia Yezieli na Peleti wana wa Azmawethi; Beraka, Yehu Mwanathothi, 4 na Ishmaya Mgibeoni, shujaa miongoni mwa wale Thelathini, ambaye alikuwa kiongozi wa wale Thelathini; Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi, Mgederathi, 5 Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi; 6 Elikana, Ishia, Azareli, Yoezeri na Yashobeamu, wana wa Kora; 7 Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori. 8 Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, waliokuwa tayari kwa vita na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani. 9 Ezeri alikuwa mkuu wao,Obadia alikuwa wa pili katika uongozi, Eliabu wa tatu, 10 Mishmana wa nne, Yeremia wa tano, 11 Atai wa sita, Elieli wa saba, 12 Yohanani wa nane, Elzabadi wa tisa, 13 Yeremia wa kumi, na Makbanai wa kumi na moja. 14 Hawa Wagadi walikuwa majemadari. Aliyekuwa wa mwisho kuliko wote aliweza kuongoza askari 100, na aliyekuwa na uweza zaidi ya wote aliongoza 1,000. 15 Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi. 16 Wabenyamini wengine na baadhi ya watu kutoka Yuda pia walikuja kwa Daudi katika ngome yake. 17 Daudi akatoka nje kuwalaki na akawaambia, “Kama mmekuja kwangu kwa amani, kunisaidia, mimi niko tayari kuwaruhusu ninyi kuungana nami. Lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu wakati mimi mikono yangu haina hatia, basi Mungu wa baba zetu aone na awahukumu.” 18 Kisha Roho akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema:“Sisi tu watu wako, ee Daudi!Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese!Ushindi, naam, ushindi uwe kwako,pia ushindi kwa wale walio upande wako,kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.”Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi. 19 Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alikwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”) 20 Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase. 21 Walimsaidia Daudi dhidi ya makundi ya uvamizi, kwa kuwa wote walikuwa mashujaa hodari na walikuwa majemadari katika jeshi lake. 22 Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu. 23 Hawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kama BWANA alivyokuwa amesema: 24 watu wa Yuda, wanaochukua ngao na mikuki walikuwa 6,800 wote wakiwa tayari kwa vita. 25 Watu wa Simeoni, mashujaa waliokuwa tayari kwa vita walikuwa 7,100. 26 Watu wa Lawi walikuwa 4,600, 27 pamoja na Yehoyada, kiongozi wa jamaa ya Aroni, aliyekuwa pamoja na watu 3,700, 28 na Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake. 29 Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo. 30 Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao. 31 Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000. 32 Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao. 33 Watu wa Zabuloni, askari wenye uzoefu mkubwa walioandaliwa tayari kwa vita wakiwa na silaha za kila aina, ili kumsaidia Daudi kwa uaminifu thabiti, walikuwa 50,000. 34 Watu wa Naftali, maafisa 1,000, pamoja na watu 37,000 waliochukua ngao na mikuki. 35 Watu wa Dani 28,600 waliokuwa tayari kwa vita. 36 Watu wa Asheri, askari 40,000 wenye uzoefu mkubwa waliondaliwa kwa ajili ya vita. 37 Na pia watu kutoka mashariki ya Yordani, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakiwa na kila aina ya silaha, watu 120,000. 38 Wote hawa walikuwa watu wapiganaji waliojitolea kutumika katika safu zao. Walikuja Hebroni wakiwa wameamua kikamilifu kumfanya Daudi mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wengine wote walikuwa pia na nia hiyo moja ya kumfanya Daudi kuwa mfalme. 39 Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao. 40 Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwepo na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ngʼombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.

In Other Versions

1 Chronicles 12 in the ANGEFD

1 Chronicles 12 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 12 in the AS21

1 Chronicles 12 in the BAGH

1 Chronicles 12 in the BBPNG

1 Chronicles 12 in the BBT1E

1 Chronicles 12 in the BDS

1 Chronicles 12 in the BEV

1 Chronicles 12 in the BHAD

1 Chronicles 12 in the BIB

1 Chronicles 12 in the BLPT

1 Chronicles 12 in the BNT

1 Chronicles 12 in the BNTABOOT

1 Chronicles 12 in the BNTLV

1 Chronicles 12 in the BOATCB

1 Chronicles 12 in the BOATCB2

1 Chronicles 12 in the BOBCV

1 Chronicles 12 in the BOCNT

1 Chronicles 12 in the BOECS

1 Chronicles 12 in the BOGWICC

1 Chronicles 12 in the BOHCB

1 Chronicles 12 in the BOHCV

1 Chronicles 12 in the BOHLNT

1 Chronicles 12 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 12 in the BOICB

1 Chronicles 12 in the BOILNTAP

1 Chronicles 12 in the BOITCV

1 Chronicles 12 in the BOKCV2

1 Chronicles 12 in the BOKHWOG

1 Chronicles 12 in the BOKSSV

1 Chronicles 12 in the BOLCB

1 Chronicles 12 in the BOLCB2

1 Chronicles 12 in the BOMCV

1 Chronicles 12 in the BONAV

1 Chronicles 12 in the BONCB

1 Chronicles 12 in the BONLT

1 Chronicles 12 in the BONUT2

1 Chronicles 12 in the BOPLNT

1 Chronicles 12 in the BOSCB

1 Chronicles 12 in the BOSNC

1 Chronicles 12 in the BOTLNT

1 Chronicles 12 in the BOVCB

1 Chronicles 12 in the BOYCB

1 Chronicles 12 in the BPBB

1 Chronicles 12 in the BPH

1 Chronicles 12 in the BSB

1 Chronicles 12 in the CCB

1 Chronicles 12 in the CUV

1 Chronicles 12 in the CUVS

1 Chronicles 12 in the DBT

1 Chronicles 12 in the DGDNT

1 Chronicles 12 in the DHNT

1 Chronicles 12 in the DNT

1 Chronicles 12 in the ELBE

1 Chronicles 12 in the EMTV

1 Chronicles 12 in the ESV

1 Chronicles 12 in the FBV

1 Chronicles 12 in the FEB

1 Chronicles 12 in the GGMNT

1 Chronicles 12 in the GNT

1 Chronicles 12 in the HARY

1 Chronicles 12 in the HNT

1 Chronicles 12 in the IRVA

1 Chronicles 12 in the IRVB

1 Chronicles 12 in the IRVG

1 Chronicles 12 in the IRVH

1 Chronicles 12 in the IRVK

1 Chronicles 12 in the IRVM

1 Chronicles 12 in the IRVM2

1 Chronicles 12 in the IRVO

1 Chronicles 12 in the IRVP

1 Chronicles 12 in the IRVT

1 Chronicles 12 in the IRVT2

1 Chronicles 12 in the IRVU

1 Chronicles 12 in the ISVN

1 Chronicles 12 in the JSNT

1 Chronicles 12 in the KAPI

1 Chronicles 12 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 12 in the KBV

1 Chronicles 12 in the KJV

1 Chronicles 12 in the KNFD

1 Chronicles 12 in the LBA

1 Chronicles 12 in the LBLA

1 Chronicles 12 in the LNT

1 Chronicles 12 in the LSV

1 Chronicles 12 in the MAAL

1 Chronicles 12 in the MBV

1 Chronicles 12 in the MBV2

1 Chronicles 12 in the MHNT

1 Chronicles 12 in the MKNFD

1 Chronicles 12 in the MNG

1 Chronicles 12 in the MNT

1 Chronicles 12 in the MNT2

1 Chronicles 12 in the MRS1T

1 Chronicles 12 in the NAA

1 Chronicles 12 in the NASB

1 Chronicles 12 in the NBLA

1 Chronicles 12 in the NBS

1 Chronicles 12 in the NBVTP

1 Chronicles 12 in the NET2

1 Chronicles 12 in the NIV11

1 Chronicles 12 in the NNT

1 Chronicles 12 in the NNT2

1 Chronicles 12 in the NNT3

1 Chronicles 12 in the PDDPT

1 Chronicles 12 in the PFNT

1 Chronicles 12 in the RMNT

1 Chronicles 12 in the SBIAS

1 Chronicles 12 in the SBIBS

1 Chronicles 12 in the SBIBS2

1 Chronicles 12 in the SBICS

1 Chronicles 12 in the SBIDS

1 Chronicles 12 in the SBIGS

1 Chronicles 12 in the SBIHS

1 Chronicles 12 in the SBIIS

1 Chronicles 12 in the SBIIS2

1 Chronicles 12 in the SBIIS3

1 Chronicles 12 in the SBIKS

1 Chronicles 12 in the SBIKS2

1 Chronicles 12 in the SBIMS

1 Chronicles 12 in the SBIOS

1 Chronicles 12 in the SBIPS

1 Chronicles 12 in the SBISS

1 Chronicles 12 in the SBITS

1 Chronicles 12 in the SBITS2

1 Chronicles 12 in the SBITS3

1 Chronicles 12 in the SBITS4

1 Chronicles 12 in the SBIUS

1 Chronicles 12 in the SBIVS

1 Chronicles 12 in the SBT

1 Chronicles 12 in the SBT1E

1 Chronicles 12 in the SCHL

1 Chronicles 12 in the SNT

1 Chronicles 12 in the SUSU

1 Chronicles 12 in the SUSU2

1 Chronicles 12 in the SYNO

1 Chronicles 12 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 12 in the TBT1E

1 Chronicles 12 in the TBT1E2

1 Chronicles 12 in the TFTIP

1 Chronicles 12 in the TFTU

1 Chronicles 12 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 12 in the THAI

1 Chronicles 12 in the TNFD

1 Chronicles 12 in the TNT

1 Chronicles 12 in the TNTIK

1 Chronicles 12 in the TNTIL

1 Chronicles 12 in the TNTIN

1 Chronicles 12 in the TNTIP

1 Chronicles 12 in the TNTIZ

1 Chronicles 12 in the TOMA

1 Chronicles 12 in the TTENT

1 Chronicles 12 in the UBG

1 Chronicles 12 in the UGV

1 Chronicles 12 in the UGV2

1 Chronicles 12 in the UGV3

1 Chronicles 12 in the VBL

1 Chronicles 12 in the VDCC

1 Chronicles 12 in the YALU

1 Chronicles 12 in the YAPE

1 Chronicles 12 in the YBVTP

1 Chronicles 12 in the ZBP