1 Chronicles 9 (BOKCV)

1 Waisraeli wote waliorodheshwa katika koo zilizoandikwa kwenye kitabu cha wafalme wa Israeli.Watu wa Yuda walichukuliwa mateka kwenda Babeli kwa sababu ya kukosa uaminifu kwa Mungu. 2 Basi watu wa kwanza kurudi kukaa kwenye milki zao katika miji yao walikuwa baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi na watumishi wa Hekalu. 3 Wale waliotoka Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase ambao waliishi Yerusalemu walikuwa: 4 Uthai mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imri, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda. 5 Wazao wa Washiloni waliorudi ni:Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe. 6 Kwa wana wa Zera:Yeueli.Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu 690. 7 Kwa Benyamini walikuwa:Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua; 8 Ibneya mwana wa Yerohamu, Ela mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya. 9 Watu kutoka Benyamini kama walivyoorodheshwa katika koo zao jumla yao ni 956. Watu hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao. 10 Wa jamaa za makuhani walikuwa:Yedaya, Yehoyaribu na Yakini; 11 Azaria mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa afisa kiongozi wa nyumba ya Mungu. 12 Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yahzera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri. 13 Makuhani waliokuwa viongozi wa jamaa zao walikuwa 1,760. Walikuwa watu wenye uwezo, waliowajibika kuhudumu katika nyumba ya Mungu. 14 Jamaa za Walawi walikuwa:Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari. 15 Bakbakari, Hereshi, Galali na Matania mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu. 16 Obadia mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. Berekia mwana wa Asa, mwana wa Elikana, ambao waliishi katika vijiji vya Wanetofathi. 17 Mabawabu katika Hekalu la BWANA waliorudi walikuwa:Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu. 18 Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi. 19 Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya BWANA. 20 Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye BWANA alikuwa pamoja naye: 21 Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania. 22 Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli. 23 Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya BWANA, nyumba iliyoitwa Hema. 24 Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. 25 Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba. 26 Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu. 27 Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi. 28 Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa. 29 Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo. 30 Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo. 31 Mlawi aliyeitwa Matithia, mwana mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, wa ukoo wa Kora, alikabidhiwa wajibu kwa ajili ya kuoka mikate ya sadaka. 32 Baadhi ya ndugu zao wa ukoo wa Kohathi walikuwa viongozi wa kuandaa mikate ya Wonyesho kwa ajili ya kila Sabato, mikate iliyokuwa inawekwa mezani. 33 Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana. 34 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa za Walawi, wakuu kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu. 35 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. Mke wake aliitwa Maaka, 36 mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 37 Gedori, Ahio, Zekaria na Miklothi. 38 Miklothi akamzaa Shimeamu. Wao pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu. 39 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli. Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali. 40 Yonathani akamzaa Merib-Baali,naye Merib-Baali akamzaa Mika. 41 Wana wa Mika walikuwa:Pithoni, Meleki, Tarea, na Ahazi. 42 Ahazi akamzaa Yara, Yara akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 43 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli. 44 Aseli alikuwa na wana sita, na haya ndiyo majina yao:Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Aseli.

In Other Versions

1 Chronicles 9 in the ANGEFD

1 Chronicles 9 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 9 in the AS21

1 Chronicles 9 in the BAGH

1 Chronicles 9 in the BBPNG

1 Chronicles 9 in the BBT1E

1 Chronicles 9 in the BDS

1 Chronicles 9 in the BEV

1 Chronicles 9 in the BHAD

1 Chronicles 9 in the BIB

1 Chronicles 9 in the BLPT

1 Chronicles 9 in the BNT

1 Chronicles 9 in the BNTABOOT

1 Chronicles 9 in the BNTLV

1 Chronicles 9 in the BOATCB

1 Chronicles 9 in the BOATCB2

1 Chronicles 9 in the BOBCV

1 Chronicles 9 in the BOCNT

1 Chronicles 9 in the BOECS

1 Chronicles 9 in the BOGWICC

1 Chronicles 9 in the BOHCB

1 Chronicles 9 in the BOHCV

1 Chronicles 9 in the BOHLNT

1 Chronicles 9 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 9 in the BOICB

1 Chronicles 9 in the BOILNTAP

1 Chronicles 9 in the BOITCV

1 Chronicles 9 in the BOKCV2

1 Chronicles 9 in the BOKHWOG

1 Chronicles 9 in the BOKSSV

1 Chronicles 9 in the BOLCB

1 Chronicles 9 in the BOLCB2

1 Chronicles 9 in the BOMCV

1 Chronicles 9 in the BONAV

1 Chronicles 9 in the BONCB

1 Chronicles 9 in the BONLT

1 Chronicles 9 in the BONUT2

1 Chronicles 9 in the BOPLNT

1 Chronicles 9 in the BOSCB

1 Chronicles 9 in the BOSNC

1 Chronicles 9 in the BOTLNT

1 Chronicles 9 in the BOVCB

1 Chronicles 9 in the BOYCB

1 Chronicles 9 in the BPBB

1 Chronicles 9 in the BPH

1 Chronicles 9 in the BSB

1 Chronicles 9 in the CCB

1 Chronicles 9 in the CUV

1 Chronicles 9 in the CUVS

1 Chronicles 9 in the DBT

1 Chronicles 9 in the DGDNT

1 Chronicles 9 in the DHNT

1 Chronicles 9 in the DNT

1 Chronicles 9 in the ELBE

1 Chronicles 9 in the EMTV

1 Chronicles 9 in the ESV

1 Chronicles 9 in the FBV

1 Chronicles 9 in the FEB

1 Chronicles 9 in the GGMNT

1 Chronicles 9 in the GNT

1 Chronicles 9 in the HARY

1 Chronicles 9 in the HNT

1 Chronicles 9 in the IRVA

1 Chronicles 9 in the IRVB

1 Chronicles 9 in the IRVG

1 Chronicles 9 in the IRVH

1 Chronicles 9 in the IRVK

1 Chronicles 9 in the IRVM

1 Chronicles 9 in the IRVM2

1 Chronicles 9 in the IRVO

1 Chronicles 9 in the IRVP

1 Chronicles 9 in the IRVT

1 Chronicles 9 in the IRVT2

1 Chronicles 9 in the IRVU

1 Chronicles 9 in the ISVN

1 Chronicles 9 in the JSNT

1 Chronicles 9 in the KAPI

1 Chronicles 9 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 9 in the KBV

1 Chronicles 9 in the KJV

1 Chronicles 9 in the KNFD

1 Chronicles 9 in the LBA

1 Chronicles 9 in the LBLA

1 Chronicles 9 in the LNT

1 Chronicles 9 in the LSV

1 Chronicles 9 in the MAAL

1 Chronicles 9 in the MBV

1 Chronicles 9 in the MBV2

1 Chronicles 9 in the MHNT

1 Chronicles 9 in the MKNFD

1 Chronicles 9 in the MNG

1 Chronicles 9 in the MNT

1 Chronicles 9 in the MNT2

1 Chronicles 9 in the MRS1T

1 Chronicles 9 in the NAA

1 Chronicles 9 in the NASB

1 Chronicles 9 in the NBLA

1 Chronicles 9 in the NBS

1 Chronicles 9 in the NBVTP

1 Chronicles 9 in the NET2

1 Chronicles 9 in the NIV11

1 Chronicles 9 in the NNT

1 Chronicles 9 in the NNT2

1 Chronicles 9 in the NNT3

1 Chronicles 9 in the PDDPT

1 Chronicles 9 in the PFNT

1 Chronicles 9 in the RMNT

1 Chronicles 9 in the SBIAS

1 Chronicles 9 in the SBIBS

1 Chronicles 9 in the SBIBS2

1 Chronicles 9 in the SBICS

1 Chronicles 9 in the SBIDS

1 Chronicles 9 in the SBIGS

1 Chronicles 9 in the SBIHS

1 Chronicles 9 in the SBIIS

1 Chronicles 9 in the SBIIS2

1 Chronicles 9 in the SBIIS3

1 Chronicles 9 in the SBIKS

1 Chronicles 9 in the SBIKS2

1 Chronicles 9 in the SBIMS

1 Chronicles 9 in the SBIOS

1 Chronicles 9 in the SBIPS

1 Chronicles 9 in the SBISS

1 Chronicles 9 in the SBITS

1 Chronicles 9 in the SBITS2

1 Chronicles 9 in the SBITS3

1 Chronicles 9 in the SBITS4

1 Chronicles 9 in the SBIUS

1 Chronicles 9 in the SBIVS

1 Chronicles 9 in the SBT

1 Chronicles 9 in the SBT1E

1 Chronicles 9 in the SCHL

1 Chronicles 9 in the SNT

1 Chronicles 9 in the SUSU

1 Chronicles 9 in the SUSU2

1 Chronicles 9 in the SYNO

1 Chronicles 9 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 9 in the TBT1E

1 Chronicles 9 in the TBT1E2

1 Chronicles 9 in the TFTIP

1 Chronicles 9 in the TFTU

1 Chronicles 9 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 9 in the THAI

1 Chronicles 9 in the TNFD

1 Chronicles 9 in the TNT

1 Chronicles 9 in the TNTIK

1 Chronicles 9 in the TNTIL

1 Chronicles 9 in the TNTIN

1 Chronicles 9 in the TNTIP

1 Chronicles 9 in the TNTIZ

1 Chronicles 9 in the TOMA

1 Chronicles 9 in the TTENT

1 Chronicles 9 in the UBG

1 Chronicles 9 in the UGV

1 Chronicles 9 in the UGV2

1 Chronicles 9 in the UGV3

1 Chronicles 9 in the VBL

1 Chronicles 9 in the VDCC

1 Chronicles 9 in the YALU

1 Chronicles 9 in the YAPE

1 Chronicles 9 in the YBVTP

1 Chronicles 9 in the ZBP