1 Kings 12 (BOKCV)

1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Waisraeli wote walikuwa wamekwenda huko kumfanya yeye kuwa mfalme. 2 Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia hili (alikuwa bado yuko Misri alikokuwa amekimbilia awe mbali na Mfalme Solomoni), akarudi kutoka Misri. 3 Kwa hiyo wakatuma watu kumwita Yeroboamu, yeye na kusanyiko lote la Israeli wakamwendea Rehoboamu na kumwambia, 4 “Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini sasa tupunguzie kazi za kikatili na nira nzito aliyoweka juu yetu, nasi tutakutumikia.” 5 Rehoboamu akajibu, “Nendeni kwa muda wa siku tatu na kisha mnirudie.” Basi watu wakaenda zao. 6 Kisha Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee ambao walimtumikia Solomoni baba yake wakati wa uhai wake akawauliza, “Mnanishauri nini katika kuwajibu watu hawa?” 7 Wakajibu, “Kama leo utakuwa mtumishi wa watu hawa na kuwahudumia na kuwapa jibu linaloridhisha, watakuwa watumishi wako daima.” 8 Lakini Rehoboamu akakataa shauri alilopewa na wazee na akataka ushauri kwa vijana wanaume rika lake waliokuwa wakimtumikia. 9 Akawauliza, “Ninyi ushauri wenu ni nini? Tutawajibuje watu hawa wanaoniambia, ‘Ifanye nyepesi nira baba yako aliyoweka juu yetu?’ ” 10 Wale vijana wa rika lake wakamjibu, “Waambie watu hawa waliokuambia, ‘Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini ifanye nira yetu nyepesi,’ kuwa, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. 11 Baba yangu aliweka nira nzito juu yenu, mimi nitaifanya hata iwe nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi, mimi nitawachapa kwa nge.’ ” 12 Siku tatu baadaye, Yeroboamu na watu wote wakamrudia Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amesema, “Rudini kwangu baada ya siku tatu.” 13 Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Akikataa shauri alilopewa na wazee, 14 akafuata shauri la vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi, mimi nitawachapa kwa nge.” 15 Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa jambo hili lilitoka kwa BWANA, ili kutimiza neno ambalo BWANA alikuwa amenena kwa Yeroboamu mwana wa Nebati kupitia Ahiya Mshiloni. 16 Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme:“Tuna fungu gani kwa Daudi?Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese.Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli!Angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!”Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao. 17 Lakini kwa habari ya Waisraeli waliokuwa wakiishi katika miji ya Yuda, Rehoboamu akaendelea kuwatawala bado. 18 Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake na kutorokea Yerusalemu. 19 Hivyo Israeli wakaasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo. 20 Waisraeli wote waliposikia kwamba Yeroboamu amerudi, wakatuma watu na kumwita kwenye kusanyiko na kumfanya mfalme juu ya Israeli yote. Ni kabila la Yuda peke yake lililobaki kuwa tiifu kwa nyumba ya Daudi. 21 Ikawa Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda na kabila la Benyamini, wanaume wapiganaji 180,000, kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha tena ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Solomoni. 22 Lakini neno hili la Mungu likamjia Shemaya mtu wa Mungu: 23 “Mwambie Rehoboamu mwana wa Solomoni mfalme wa Yuda, na nyumba yote ya Yuda na Benyamini, na watu wengine wote, 24 ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu, Waisraeli. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la BWANA na kurudi nyumbani, kama BWANA alivyokuwa ameagiza. 25 Kisha Yeroboamu akajenga Shekemu akaizungushia ngome katika nchi ya vilima ya Efraimu na akaishi huko. Akatoka huko, akaenda akajenga Penueli. 26 Yeroboamu akawaza moyoni mwake, “Sasa inawezekana ufalme ukarudi katika nyumba ya Daudi. 27 Kama watu hawa watapanda kwenda kutoa dhabihu katika Hekalu la BWANA huko Yerusalemu, mioyo yao itamrudia bwana wao, Rehoboamu mfalme wa Yuda. Wataniua mimi na kurudi kwa Mfalme Rehoboamu.” 28 Baada ya kutafuta shauri, mfalme akatengeneza ndama wawili wa dhahabu. Akawaambia watu, “Ni gharama kubwa kwenu kukwea kwenda Yerusalemu. Hii hapa miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.” 29 Ndama mmoja akamweka Betheli na mwingine Dani. 30 Nalo jambo hili likawa dhambi, watu wakawa wanaenda hadi Dani kumwabudu huyo aliyewekwa huko. 31 Yeroboamu akajenga madhabahu mahali pa juu pa kuabudia miungu na kuwateua makuhani kutoka watu wa aina zote, ijapokuwa hawakuwa Walawi. 32 Pia Yeroboamu akaweka sikukuu katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, kama sikukuu iliyokuwa ikifanyika huko Yuda, na akatoa dhabihu juu ya madhabahu. Akafanya hivyo huko Betheli akitoa dhabihu kwa ndama alizotengeneza. Huko Betheli akawaweka makuhani, na pia katika sehemu za juu za kuabudia miungu alizozitengeneza. 33 Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, mwezi aliouchagua mwenyewe, alitoa dhabihu juu ya madhabahu aliyokuwa amejenga huko Betheli. Kwa hiyo akaweka sikukuu kwa ajili ya Waisraeli na akapanda madhabahuni kutoa sadaka.

In Other Versions

1 Kings 12 in the ANGEFD

1 Kings 12 in the ANTPNG2D

1 Kings 12 in the AS21

1 Kings 12 in the BAGH

1 Kings 12 in the BBPNG

1 Kings 12 in the BBT1E

1 Kings 12 in the BDS

1 Kings 12 in the BEV

1 Kings 12 in the BHAD

1 Kings 12 in the BIB

1 Kings 12 in the BLPT

1 Kings 12 in the BNT

1 Kings 12 in the BNTABOOT

1 Kings 12 in the BNTLV

1 Kings 12 in the BOATCB

1 Kings 12 in the BOATCB2

1 Kings 12 in the BOBCV

1 Kings 12 in the BOCNT

1 Kings 12 in the BOECS

1 Kings 12 in the BOGWICC

1 Kings 12 in the BOHCB

1 Kings 12 in the BOHCV

1 Kings 12 in the BOHLNT

1 Kings 12 in the BOHNTLTAL

1 Kings 12 in the BOICB

1 Kings 12 in the BOILNTAP

1 Kings 12 in the BOITCV

1 Kings 12 in the BOKCV2

1 Kings 12 in the BOKHWOG

1 Kings 12 in the BOKSSV

1 Kings 12 in the BOLCB

1 Kings 12 in the BOLCB2

1 Kings 12 in the BOMCV

1 Kings 12 in the BONAV

1 Kings 12 in the BONCB

1 Kings 12 in the BONLT

1 Kings 12 in the BONUT2

1 Kings 12 in the BOPLNT

1 Kings 12 in the BOSCB

1 Kings 12 in the BOSNC

1 Kings 12 in the BOTLNT

1 Kings 12 in the BOVCB

1 Kings 12 in the BOYCB

1 Kings 12 in the BPBB

1 Kings 12 in the BPH

1 Kings 12 in the BSB

1 Kings 12 in the CCB

1 Kings 12 in the CUV

1 Kings 12 in the CUVS

1 Kings 12 in the DBT

1 Kings 12 in the DGDNT

1 Kings 12 in the DHNT

1 Kings 12 in the DNT

1 Kings 12 in the ELBE

1 Kings 12 in the EMTV

1 Kings 12 in the ESV

1 Kings 12 in the FBV

1 Kings 12 in the FEB

1 Kings 12 in the GGMNT

1 Kings 12 in the GNT

1 Kings 12 in the HARY

1 Kings 12 in the HNT

1 Kings 12 in the IRVA

1 Kings 12 in the IRVB

1 Kings 12 in the IRVG

1 Kings 12 in the IRVH

1 Kings 12 in the IRVK

1 Kings 12 in the IRVM

1 Kings 12 in the IRVM2

1 Kings 12 in the IRVO

1 Kings 12 in the IRVP

1 Kings 12 in the IRVT

1 Kings 12 in the IRVT2

1 Kings 12 in the IRVU

1 Kings 12 in the ISVN

1 Kings 12 in the JSNT

1 Kings 12 in the KAPI

1 Kings 12 in the KBT1ETNIK

1 Kings 12 in the KBV

1 Kings 12 in the KJV

1 Kings 12 in the KNFD

1 Kings 12 in the LBA

1 Kings 12 in the LBLA

1 Kings 12 in the LNT

1 Kings 12 in the LSV

1 Kings 12 in the MAAL

1 Kings 12 in the MBV

1 Kings 12 in the MBV2

1 Kings 12 in the MHNT

1 Kings 12 in the MKNFD

1 Kings 12 in the MNG

1 Kings 12 in the MNT

1 Kings 12 in the MNT2

1 Kings 12 in the MRS1T

1 Kings 12 in the NAA

1 Kings 12 in the NASB

1 Kings 12 in the NBLA

1 Kings 12 in the NBS

1 Kings 12 in the NBVTP

1 Kings 12 in the NET2

1 Kings 12 in the NIV11

1 Kings 12 in the NNT

1 Kings 12 in the NNT2

1 Kings 12 in the NNT3

1 Kings 12 in the PDDPT

1 Kings 12 in the PFNT

1 Kings 12 in the RMNT

1 Kings 12 in the SBIAS

1 Kings 12 in the SBIBS

1 Kings 12 in the SBIBS2

1 Kings 12 in the SBICS

1 Kings 12 in the SBIDS

1 Kings 12 in the SBIGS

1 Kings 12 in the SBIHS

1 Kings 12 in the SBIIS

1 Kings 12 in the SBIIS2

1 Kings 12 in the SBIIS3

1 Kings 12 in the SBIKS

1 Kings 12 in the SBIKS2

1 Kings 12 in the SBIMS

1 Kings 12 in the SBIOS

1 Kings 12 in the SBIPS

1 Kings 12 in the SBISS

1 Kings 12 in the SBITS

1 Kings 12 in the SBITS2

1 Kings 12 in the SBITS3

1 Kings 12 in the SBITS4

1 Kings 12 in the SBIUS

1 Kings 12 in the SBIVS

1 Kings 12 in the SBT

1 Kings 12 in the SBT1E

1 Kings 12 in the SCHL

1 Kings 12 in the SNT

1 Kings 12 in the SUSU

1 Kings 12 in the SUSU2

1 Kings 12 in the SYNO

1 Kings 12 in the TBIAOTANT

1 Kings 12 in the TBT1E

1 Kings 12 in the TBT1E2

1 Kings 12 in the TFTIP

1 Kings 12 in the TFTU

1 Kings 12 in the TGNTATF3T

1 Kings 12 in the THAI

1 Kings 12 in the TNFD

1 Kings 12 in the TNT

1 Kings 12 in the TNTIK

1 Kings 12 in the TNTIL

1 Kings 12 in the TNTIN

1 Kings 12 in the TNTIP

1 Kings 12 in the TNTIZ

1 Kings 12 in the TOMA

1 Kings 12 in the TTENT

1 Kings 12 in the UBG

1 Kings 12 in the UGV

1 Kings 12 in the UGV2

1 Kings 12 in the UGV3

1 Kings 12 in the VBL

1 Kings 12 in the VDCC

1 Kings 12 in the YALU

1 Kings 12 in the YAPE

1 Kings 12 in the YBVTP

1 Kings 12 in the ZBP