1 Kings 9 (BOKCV)

1 Solomoni alipomaliza kujenga Hekalu la BWANA na jumba la kifalme, alipokwisha kufanya yote aliyotaka kufanya, 2 BWANA akamtokea mara ya pili, kama alivyokuwa amemtokea huko Gibeoni. 3 BWANA akamwambia:“Nimesikia dua na maombi uliyofanya mbele zangu, nimeliweka wakfu Hekalu hili ambalo umelijenga, kwa kuweka Jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwa humo siku zote. 4 “Kukuhusu wewe, kama ukienenda kwa unyofu wa moyo na uadilifu, kama baba yako Daudi alivyofanya na kutenda yote ninayoyaagiza kwa kutunza maagizo yangu na sheria, 5 nitakiimarisha kiti chako cha enzi juu ya Israeli milele kama nilivyomwahidi Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe kuwa na mtu kwenye kiti cha enzi cha Israeli.’ 6 “Lakini kama ninyi au wana wenu mkigeukia mbali nami na kuziacha amri na maagizo yangu niliyowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, 7 basi nitakatilia mbali Israeli kutoka nchi niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Ndipo Israeli itakuwa kitu cha kudharauliwa na watu na kuwa kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote. 8 Ingawa hekalu hili linavutia sasa, wote watakaolipita watashangaa na kudhihaki wakisema, ‘Kwa nini BWANA amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’ 9 Watu watajibu, ‘Kwa sababu wamemwacha BWANA Mungu wao, aliyewatoa baba zao Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu BWANA ameyaleta maafa haya yote juu yao.’ ” 10 Miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Solomoni alijenga majengo haya mawili, yaani Hekalu la BWANA na jumba la kifalme, 11 Mfalme Solomoni akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi yote, misunobari na dhahabu yote aliyohitaji. 12 Lakini Hiramu alipotoka Tiro kwenda kuiona ile miji ambayo Solomoni alikuwa amempa, hakupendezwa nayo. 13 Hiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?”Naye akaiita nchi ya Kabul, jina lililoko hadi leo. 14 Basi Hiramu alikuwa amempelekea mfalme talanta 120 za dhahabu. 15 Haya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Solomoni, alivyowafanyiza watu ili kulijenga hekalu la BWANA, na jumba lake la kifalme, na Milo, ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri. 16 (Farao mfalme wa Misri alikuwa ameushambulia na kuuteka mji wa Gezeri. Alikuwa ameuchoma moto. Akawaua Wakanaani waliokuwa wakikaa humo na kisha kuutoa kwa binti yake, yaani mkewe Solomoni, kama zawadi ya arusi. 17 Solomoni akaujenga tena Gezeri.) Akajenga Beth-Horoni ya Chini, 18 akajenga Baalathi na Tamari kwenye jangwa katika eneo la nchi yake, 19 vilevile miji ya ghala na miji kwa ajili ya magari yake na kwa ajili ya farasi wake: chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika eneo yote aliyotawala. 20 Watu wote waliosalia kutoka kwa Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi (mataifa haya hayakuwa Waisraeli), 21 yaani, wazao wao waliobakia katika nchi, ambao Waisraeli hawangeweza kuwaangamiza kabisa: hawa Solomoni akawalazimisha kuwa watumwa katika shokoa, kama ilivyo hadi leo. 22 Lakini Solomoni hakumfanya yeyote wa Waisraeli kuwa mtumwa; wao ndio waliokuwa wapiganaji wake, maafisa wake wa serikali, maafisa wake, wakuu wake, majemadari wa jeshi wa magari yake ya vita na wapanda farasi. 23 Pia walikuwa maafisa wakuu wasimamizi wa miradi ya Solomoni: maafisa 550 waliwasimamia watu waliofanya kazi. 24 Baada ya binti Farao kuja kutoka Mji wa Daudi na kuingia jumba la kifalme ambalo Solomoni alikuwa amemjengea, akajenga Milo. 25 Solomoni akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka, juu ya madhabahu aliyokuwa amejengea kwa ajili ya BWANA, akifukiza uvumba mbele za BWANA pamoja na dhabihu hizo, hivyo kutimiza kanuni za hekalu. 26 Mfalme Solomoni pia akatengeneza pia meli huko Esion-Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu. 27 Naye Hiramu akawatuma watu wake; mabaharia walioijua bahari, kuhudumu katika hizo meli pamoja na watu wa Solomoni. 28 Wakasafiri kwa bahari mpaka Ofiri na kurudi na talanta 420 za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Solomoni.

In Other Versions

1 Kings 9 in the ANGEFD

1 Kings 9 in the ANTPNG2D

1 Kings 9 in the AS21

1 Kings 9 in the BAGH

1 Kings 9 in the BBPNG

1 Kings 9 in the BBT1E

1 Kings 9 in the BDS

1 Kings 9 in the BEV

1 Kings 9 in the BHAD

1 Kings 9 in the BIB

1 Kings 9 in the BLPT

1 Kings 9 in the BNT

1 Kings 9 in the BNTABOOT

1 Kings 9 in the BNTLV

1 Kings 9 in the BOATCB

1 Kings 9 in the BOATCB2

1 Kings 9 in the BOBCV

1 Kings 9 in the BOCNT

1 Kings 9 in the BOECS

1 Kings 9 in the BOGWICC

1 Kings 9 in the BOHCB

1 Kings 9 in the BOHCV

1 Kings 9 in the BOHLNT

1 Kings 9 in the BOHNTLTAL

1 Kings 9 in the BOICB

1 Kings 9 in the BOILNTAP

1 Kings 9 in the BOITCV

1 Kings 9 in the BOKCV2

1 Kings 9 in the BOKHWOG

1 Kings 9 in the BOKSSV

1 Kings 9 in the BOLCB

1 Kings 9 in the BOLCB2

1 Kings 9 in the BOMCV

1 Kings 9 in the BONAV

1 Kings 9 in the BONCB

1 Kings 9 in the BONLT

1 Kings 9 in the BONUT2

1 Kings 9 in the BOPLNT

1 Kings 9 in the BOSCB

1 Kings 9 in the BOSNC

1 Kings 9 in the BOTLNT

1 Kings 9 in the BOVCB

1 Kings 9 in the BOYCB

1 Kings 9 in the BPBB

1 Kings 9 in the BPH

1 Kings 9 in the BSB

1 Kings 9 in the CCB

1 Kings 9 in the CUV

1 Kings 9 in the CUVS

1 Kings 9 in the DBT

1 Kings 9 in the DGDNT

1 Kings 9 in the DHNT

1 Kings 9 in the DNT

1 Kings 9 in the ELBE

1 Kings 9 in the EMTV

1 Kings 9 in the ESV

1 Kings 9 in the FBV

1 Kings 9 in the FEB

1 Kings 9 in the GGMNT

1 Kings 9 in the GNT

1 Kings 9 in the HARY

1 Kings 9 in the HNT

1 Kings 9 in the IRVA

1 Kings 9 in the IRVB

1 Kings 9 in the IRVG

1 Kings 9 in the IRVH

1 Kings 9 in the IRVK

1 Kings 9 in the IRVM

1 Kings 9 in the IRVM2

1 Kings 9 in the IRVO

1 Kings 9 in the IRVP

1 Kings 9 in the IRVT

1 Kings 9 in the IRVT2

1 Kings 9 in the IRVU

1 Kings 9 in the ISVN

1 Kings 9 in the JSNT

1 Kings 9 in the KAPI

1 Kings 9 in the KBT1ETNIK

1 Kings 9 in the KBV

1 Kings 9 in the KJV

1 Kings 9 in the KNFD

1 Kings 9 in the LBA

1 Kings 9 in the LBLA

1 Kings 9 in the LNT

1 Kings 9 in the LSV

1 Kings 9 in the MAAL

1 Kings 9 in the MBV

1 Kings 9 in the MBV2

1 Kings 9 in the MHNT

1 Kings 9 in the MKNFD

1 Kings 9 in the MNG

1 Kings 9 in the MNT

1 Kings 9 in the MNT2

1 Kings 9 in the MRS1T

1 Kings 9 in the NAA

1 Kings 9 in the NASB

1 Kings 9 in the NBLA

1 Kings 9 in the NBS

1 Kings 9 in the NBVTP

1 Kings 9 in the NET2

1 Kings 9 in the NIV11

1 Kings 9 in the NNT

1 Kings 9 in the NNT2

1 Kings 9 in the NNT3

1 Kings 9 in the PDDPT

1 Kings 9 in the PFNT

1 Kings 9 in the RMNT

1 Kings 9 in the SBIAS

1 Kings 9 in the SBIBS

1 Kings 9 in the SBIBS2

1 Kings 9 in the SBICS

1 Kings 9 in the SBIDS

1 Kings 9 in the SBIGS

1 Kings 9 in the SBIHS

1 Kings 9 in the SBIIS

1 Kings 9 in the SBIIS2

1 Kings 9 in the SBIIS3

1 Kings 9 in the SBIKS

1 Kings 9 in the SBIKS2

1 Kings 9 in the SBIMS

1 Kings 9 in the SBIOS

1 Kings 9 in the SBIPS

1 Kings 9 in the SBISS

1 Kings 9 in the SBITS

1 Kings 9 in the SBITS2

1 Kings 9 in the SBITS3

1 Kings 9 in the SBITS4

1 Kings 9 in the SBIUS

1 Kings 9 in the SBIVS

1 Kings 9 in the SBT

1 Kings 9 in the SBT1E

1 Kings 9 in the SCHL

1 Kings 9 in the SNT

1 Kings 9 in the SUSU

1 Kings 9 in the SUSU2

1 Kings 9 in the SYNO

1 Kings 9 in the TBIAOTANT

1 Kings 9 in the TBT1E

1 Kings 9 in the TBT1E2

1 Kings 9 in the TFTIP

1 Kings 9 in the TFTU

1 Kings 9 in the TGNTATF3T

1 Kings 9 in the THAI

1 Kings 9 in the TNFD

1 Kings 9 in the TNT

1 Kings 9 in the TNTIK

1 Kings 9 in the TNTIL

1 Kings 9 in the TNTIN

1 Kings 9 in the TNTIP

1 Kings 9 in the TNTIZ

1 Kings 9 in the TOMA

1 Kings 9 in the TTENT

1 Kings 9 in the UBG

1 Kings 9 in the UGV

1 Kings 9 in the UGV2

1 Kings 9 in the UGV3

1 Kings 9 in the VBL

1 Kings 9 in the VDCC

1 Kings 9 in the YALU

1 Kings 9 in the YAPE

1 Kings 9 in the YBVTP

1 Kings 9 in the ZBP