2 Kings 5 (BOKCV)

1 Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, BWANA alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari shujaa, lakini alikuwa na ukoma. 2 Siku hizo vikosi kutoka Aramu vilikuwa vimekwenda na vikawa vimemteka msichana kutoka Israeli, naye akamtumikia mkewe Naamani. 3 Akamwambia bibi yake, “Kama bwana wangu angelimwona nabii aliyeko Samaria! Angemponya ukoma wake.” 4 Naamani akaenda kwa bwana wake na kumwambia alichosema yule msichana kutoka Israeli. 5 Mfalme wa Aramu akamjibu, “Hakika, nenda. Nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo Naamani akaondoka, akiwa amechukua talanta kumi za fedha, shekeli 6,000 za dhahabu, na mivao kumi ya mavazi. 6 Barua aliyopelekea mfalme wa Israeli iliandikwa hivi: “Pamoja na barua hii ninamtuma mtumishi wangu, Naamani, kwako ili uweze kumponya ukoma wake.” 7 Mara mfalme wa Israeli alipomaliza kuisoma ile barua, akararua mavazi yake na kusema, “Je, mimi ni Mungu? Je, mimi naweza kuua na kufufua tena? Kwa nini huyu mtu anamtuma mtu ili mimi nipate kumponya ukoma wake? Tazama jinsi anavyotafuta kuanzisha ugomvi nami!” 8 Elisha mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alikuwa amerarua mavazi yake, akamtumia ujumbe huu: “Kwa nini umerarua mavazi yako? Mwamuru mtu huyo aje kwangu, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.” 9 Kwa hiyo Naamani akaenda, akiwa na farasi zake na magari yake, na kusimama mlangoni mwa nyumba ya Elisha. 10 Elisha akamtuma mjumbe kumwambia, “Nenda uoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itapona, nawe utatakasika.” 11 Lakini Naamani akaondoka akiwa amekasirika, akasema, “Hakika nilidhani kwamba angetoka nje, asimame na kuliitia jina la BWANA Mungu wake, na kuweka mkono wake juu ya mahali pagonjwa, aniponye ukoma wangu. 12 Je, Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora zaidi kuliko mito yoyote ya Israeli? Je, nisingeweza kuoga ndani ya hiyo mito na kutakasika?” Basi akageuka na kuondoka kwa hasira kuu. 13 Watumishi wa Naamani wakamwendea na kumwambia, “Baba yangu, kama huyo nabii angekuambia kufanya jambo lililo kubwa, je, usingelifanya? Je, si zaidi sana basi, anapokuambia, ‘Oga na utakasike!’ ” 14 Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. 15 Kisha Naamani na wahudumu wake wote wakarudi kwa yule mtu wa Mungu. Akasimama mbele yake na kusema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu katika ulimwengu wote isipokuwa katika Israeli. Tafadhali sasa upokee zawadi kutoka kwa mtumishi wako.” 16 Nabii akajibu, “Hakika kama BWANA aishivyo, ambaye ninamtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa. 17 Naamani akasema, “Ikiwa hutapokea, tafadhali mtumishi wako na apewe udongo kiasi cha mzigo wa kuweza kubebwa na punda wawili, kwa sababu mtumishi wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa na dhabihu kwa mungu mwingine isipokuwa BWANA. 18 Lakini BWANA na amsamehe mtumishi wake kwa kitu hiki kimoja: Wakati bwana wangu atakapoingia kwenye hekalu la Rimoni ili kusujudu, naye akiwa anauegemea mkono wangu, nami nikasujudu huko pia, wakati nitakaposujudu ndani ya hekalu la Rimoni, BWANA na amsamehe mtumishi wako kwa ajili ya jambo hili.” 19 Elisha akamwambia, “Nenda kwa amani.”Baada ya Naamani kusafiri umbali fulani, 20 Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akajiambia mwenyewe, “Bwana wangu amemwachia kirahisi sana Naamani, huyu Mwaramu, kwa kutokupokea kutoka kwake vile alivyovileta. Hakika kama BWANA aishivyo, nitamkimbilia na kupata kitu kutoka kwake.” 21 Hivyo Gehazi akaharakisha kumfuatilia Naamani. Naamani alipomwona akikimbia kumwelekea, akashuka chini kutoka kwenye gari lake na kwenda kumlaki. Akauliza, “Je, mambo yote ni sawa?” 22 Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa. Bwana wangu amenituma nikuambie, ‘Vijana wawili kutoka kwa wana wa manabii wamenijia kutoka nchi ya vilima ya Efraimu. Tafadhali wape talanta ya fedha na mivao miwili ya mavazi.’ ” 23 Naamani akasema, “Hakika, chukua talanta mbili za fedha.” Akamsihi Gehazi azipokee, kisha akafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili pamoja na mivao miwili ya mavazi. Akawapa watumishi wake wawili mizigo hiyo, nao wakaibeba wakitangulia mbele ya Gehazi. 24 Gehazi alipofika kwenye kilima, akavichukua vile vitu kutoka kwa wale watumishi na kuvificha ndani ya nyumba. Akawaaga wale watu, nao wakaondoka. 25 Kisha akaingia ndani na kusimama mbele ya Elisha bwana wake.Elisha akamuuliza, “Gehazi, ulikuwa wapi?”Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakwenda popote.” 26 Lakini Elisha akamwambia, “Je, roho yangu haikuwa pamoja nawe wakati yule mtu aliposhuka kutoka kwenye gari lake ili kukulaki? Je, huu ni wakati wa kupokea fedha au kupokea nguo, mashamba ya mizeituni, mashamba ya mizabibu, makundi ya kondoo na mbuzi, makundi ya ngʼombe, au watumishi wa kiume na wa kike? 27 Ukoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako milele.” Kisha Gehazi akaondoka mbele ya Elisha, mwenye ukoma, mweupe kama theluji.

In Other Versions

2 Kings 5 in the ANGEFD

2 Kings 5 in the ANTPNG2D

2 Kings 5 in the AS21

2 Kings 5 in the BAGH

2 Kings 5 in the BBPNG

2 Kings 5 in the BBT1E

2 Kings 5 in the BDS

2 Kings 5 in the BEV

2 Kings 5 in the BHAD

2 Kings 5 in the BIB

2 Kings 5 in the BLPT

2 Kings 5 in the BNT

2 Kings 5 in the BNTABOOT

2 Kings 5 in the BNTLV

2 Kings 5 in the BOATCB

2 Kings 5 in the BOATCB2

2 Kings 5 in the BOBCV

2 Kings 5 in the BOCNT

2 Kings 5 in the BOECS

2 Kings 5 in the BOGWICC

2 Kings 5 in the BOHCB

2 Kings 5 in the BOHCV

2 Kings 5 in the BOHLNT

2 Kings 5 in the BOHNTLTAL

2 Kings 5 in the BOICB

2 Kings 5 in the BOILNTAP

2 Kings 5 in the BOITCV

2 Kings 5 in the BOKCV2

2 Kings 5 in the BOKHWOG

2 Kings 5 in the BOKSSV

2 Kings 5 in the BOLCB

2 Kings 5 in the BOLCB2

2 Kings 5 in the BOMCV

2 Kings 5 in the BONAV

2 Kings 5 in the BONCB

2 Kings 5 in the BONLT

2 Kings 5 in the BONUT2

2 Kings 5 in the BOPLNT

2 Kings 5 in the BOSCB

2 Kings 5 in the BOSNC

2 Kings 5 in the BOTLNT

2 Kings 5 in the BOVCB

2 Kings 5 in the BOYCB

2 Kings 5 in the BPBB

2 Kings 5 in the BPH

2 Kings 5 in the BSB

2 Kings 5 in the CCB

2 Kings 5 in the CUV

2 Kings 5 in the CUVS

2 Kings 5 in the DBT

2 Kings 5 in the DGDNT

2 Kings 5 in the DHNT

2 Kings 5 in the DNT

2 Kings 5 in the ELBE

2 Kings 5 in the EMTV

2 Kings 5 in the ESV

2 Kings 5 in the FBV

2 Kings 5 in the FEB

2 Kings 5 in the GGMNT

2 Kings 5 in the GNT

2 Kings 5 in the HARY

2 Kings 5 in the HNT

2 Kings 5 in the IRVA

2 Kings 5 in the IRVB

2 Kings 5 in the IRVG

2 Kings 5 in the IRVH

2 Kings 5 in the IRVK

2 Kings 5 in the IRVM

2 Kings 5 in the IRVM2

2 Kings 5 in the IRVO

2 Kings 5 in the IRVP

2 Kings 5 in the IRVT

2 Kings 5 in the IRVT2

2 Kings 5 in the IRVU

2 Kings 5 in the ISVN

2 Kings 5 in the JSNT

2 Kings 5 in the KAPI

2 Kings 5 in the KBT1ETNIK

2 Kings 5 in the KBV

2 Kings 5 in the KJV

2 Kings 5 in the KNFD

2 Kings 5 in the LBA

2 Kings 5 in the LBLA

2 Kings 5 in the LNT

2 Kings 5 in the LSV

2 Kings 5 in the MAAL

2 Kings 5 in the MBV

2 Kings 5 in the MBV2

2 Kings 5 in the MHNT

2 Kings 5 in the MKNFD

2 Kings 5 in the MNG

2 Kings 5 in the MNT

2 Kings 5 in the MNT2

2 Kings 5 in the MRS1T

2 Kings 5 in the NAA

2 Kings 5 in the NASB

2 Kings 5 in the NBLA

2 Kings 5 in the NBS

2 Kings 5 in the NBVTP

2 Kings 5 in the NET2

2 Kings 5 in the NIV11

2 Kings 5 in the NNT

2 Kings 5 in the NNT2

2 Kings 5 in the NNT3

2 Kings 5 in the PDDPT

2 Kings 5 in the PFNT

2 Kings 5 in the RMNT

2 Kings 5 in the SBIAS

2 Kings 5 in the SBIBS

2 Kings 5 in the SBIBS2

2 Kings 5 in the SBICS

2 Kings 5 in the SBIDS

2 Kings 5 in the SBIGS

2 Kings 5 in the SBIHS

2 Kings 5 in the SBIIS

2 Kings 5 in the SBIIS2

2 Kings 5 in the SBIIS3

2 Kings 5 in the SBIKS

2 Kings 5 in the SBIKS2

2 Kings 5 in the SBIMS

2 Kings 5 in the SBIOS

2 Kings 5 in the SBIPS

2 Kings 5 in the SBISS

2 Kings 5 in the SBITS

2 Kings 5 in the SBITS2

2 Kings 5 in the SBITS3

2 Kings 5 in the SBITS4

2 Kings 5 in the SBIUS

2 Kings 5 in the SBIVS

2 Kings 5 in the SBT

2 Kings 5 in the SBT1E

2 Kings 5 in the SCHL

2 Kings 5 in the SNT

2 Kings 5 in the SUSU

2 Kings 5 in the SUSU2

2 Kings 5 in the SYNO

2 Kings 5 in the TBIAOTANT

2 Kings 5 in the TBT1E

2 Kings 5 in the TBT1E2

2 Kings 5 in the TFTIP

2 Kings 5 in the TFTU

2 Kings 5 in the TGNTATF3T

2 Kings 5 in the THAI

2 Kings 5 in the TNFD

2 Kings 5 in the TNT

2 Kings 5 in the TNTIK

2 Kings 5 in the TNTIL

2 Kings 5 in the TNTIN

2 Kings 5 in the TNTIP

2 Kings 5 in the TNTIZ

2 Kings 5 in the TOMA

2 Kings 5 in the TTENT

2 Kings 5 in the UBG

2 Kings 5 in the UGV

2 Kings 5 in the UGV2

2 Kings 5 in the UGV3

2 Kings 5 in the VBL

2 Kings 5 in the VDCC

2 Kings 5 in the YALU

2 Kings 5 in the YAPE

2 Kings 5 in the YBVTP

2 Kings 5 in the ZBP