1 Kings 18 (BOKCV)

1 Baada ya muda mrefu, katika mwaka wa tatu, neno la BWANA likamjia Eliya kusema, “Nenda ukajionyeshe kwa Ahabu na mimi nitanyesha mvua juu ya nchi.” 2 Kwa hiyo Eliya akaenda kujionyesha kwa Ahabu.Wakati huu njaa ilikuwa kali sana katika Samaria, 3 naye Ahabu alikuwa amemwita Obadia ambaye alikuwa msimamizi wa jumba lake la kifalme. (Obadia alimcha BWANA sana. 4 Wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa BWANA, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja na akawa akiwapa chakula na maji.) 5 Ahabu alikuwa amemwambia Obadia, “Nenda katika nchi yote kwenye vijito vyote na mabonde. Huenda tunaweza kupata majani ya kuwalisha farasi na nyumbu wapate kuishi ili tusilazimike kuwaua hata mmoja wa wanyama wetu.” 6 Kwa hiyo wakagawanya nchi waliyokusudia kutafuta majani, Ahabu akaenda upande mmoja na Obadia upande mwingine. 7 Wakati Obadia alipokuwa akitembea njiani, Eliya akakutana naye. Obadia akamtambua, akamsujudia hadi nchi na kusema, “Je, hivi kweli ni wewe, bwana wangu Eliya?” 8 Eliya akamjibu, “Ndiyo, nenda ukamwambie bwana wako Ahabu, ‘Eliya yuko hapa.’ ” 9 Obadia akamuuliza, “Ni kosa gani nimefanya, hata ukaamua kumkabidhi mtumishi wako mkononi mwa Ahabu ili aniue? 10 Hakika kama BWANA Mungu wako aishivyo, hakuna taifa hata moja au ufalme ambapo bwana wangu hajamtuma mtu kukutafuta. Kila wakati taifa au ufalme walipodai kwamba haupo huko, aliwafanya waape kwamba hawakuweza kukupata. 11 Lakini sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kusema, ‘Eliya yuko hapa.’ 12 Sijui ni wapi Roho wa BWANA ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Kama nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua. Hata hivyo mimi mtumishi wako nimemwabudu BWANA tangu ujana wangu. 13 Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini wakati Yezebeli alipokuwa akiua manabii wa BWANA? Niliwaficha manabii wa BWANA mia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, nami nikawapatia chakula na maji. 14 Nawe sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kumwambia, ‘Eliya yuko hapa.’ Yeye ataniua!” 15 Eliya akasema, “Kama BWANA Mwenye Nguvu Zote aishivyo, yeye ninayemtumikia, hakika nitajionyesha kwa Ahabu leo.” 16 Basi Obadia akaenda kukutana na Ahabu na kumwambia, naye Ahabu akaenda kukutana na Eliya. 17 Ahabu alipomwona Eliya, akamwambia, “Je, ni wewe, mtaabishaji wa Israeli?” 18 Eliya akamjibu, “Mimi sijaitaabisha Israeli. Lakini wewe na jamaa ya baba yako ndio mnaofanya hivyo. Mmeziacha amri za BWANA na mkafuata Mabaali. 19 Sasa waite watu kutoka Israeli yote tukutane nao juu ya Mlima Karmeli. Nawe uwalete hao manabii wa Baali mia nne na hamsini na hao manabii mia nne wa Ashera, walao chakula mezani mwa Yezebeli.” 20 Ndipo Ahabu akatuma ujumbe katika Israeli yote na kuwakusanya manabii hao juu ya mlima Karmeli. 21 Eliya akasimama mbele ya watu na kusema, “Mtasitasita katika mawazo mawili hadi lini? Ikiwa BWANA ndiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye.”Lakini watu hawakusema kitu. 22 Kisha Eliya akawaambia, “Ni mimi peke yangu nabii wa BWANA aliyebaki, lakini Baali ana manabii mia nne na hamsini. 23 Leteni mafahali wawili. Wao na wajichagulie mmoja, wamkate vipande vipande na waweke juu ya kuni lakini wasiiwashie moto. Nitamwandaa huyo fahali mwingine na kumweka juu ya kuni lakini sitawasha moto. 24 Kisha mliitie jina la mungu wenu, nami nitaliitia jina la BWANA Mungu yule ambaye atajibu kwa moto, huyo ndiye Mungu.”Kisha watu wote wakasema, “Hilo unalosema ni jema.” 25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja kati ya hawa mafahali na mwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi mko wengi sana. Liitieni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.” 26 Kwa hiyo wakamchukua yule fahali waliyepewa, nao wakamwandaa.Kisha wakaliitia jina la Baali kutoka asubuhi hadi adhuhuri, wakapiga kelele, “Ee Baali, utujibu!” Lakini hapakuwa na jibu; hakuna aliyejibu. Nao wakacheza kuizunguka madhabahu waliyoijenga. 27 Wakati wa adhuhuri, Eliya akaanza kuwadhihaki, akisema, “Pigeni kelele zaidi! Hakika yeye ni mungu! Labda amezama katika mawazo mazito, au ana shughuli nyingi, au amesafiri. Labda amelala usingizi mzito, naye ni lazima aamshwe.” 28 Kwa hiyo wakapiga kelele zaidi na kama ilivyokuwa desturi yao wakajichanja wenyewe kwa visu na vyembe, mpaka damu ikachuruzika. 29 Adhuhuri ikapita, nao wakaendelea na utabiri wao wa kiwazimu mpaka wakati wa dhabihu ya jioni. Lakini hapakuwa na jibu, hakuna aliyejibu, hakuna aliyeangalia. 30 Kisha Eliya akawaambia watu wote, “Sogeeni karibu nami.” Watu wote wakamkaribia, naye akakarabati madhabahu ya BWANA, ambayo ilikuwa imevunjwa. 31 Eliya akachukua mawe kumi na mawili, moja kwa ajili ya kila kabila la wana wa Yakobo, ambaye neno la BWANA lilimjia, likisema, “Jina lako litakuwa Israeli.” 32 Kwa mawe hayo, akajenga madhabahu katika jina la BWANA, na akachimba handaki kuizunguka, ukubwa wa kutosha vipimo viwili vya mbegu. 33 Akapanga kuni, akamkata yule fahali vipande vipande na kuvipanga juu ya kuni. Kisha akawaambia, “Jazeni mapipa manne maji na kuyamwaga juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni.” 34 Akawaambia, “Fanyeni hivyo tena.” Nao wakafanya hivyo tena.Akaagiza, “Fanyeni kwa mara ya tatu.” Nao wakafanya hivyo kwa mara ya tatu. 35 Maji yakatiririka kuizunguka madhabahu na hata kujaza lile handaki. 36 Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na Isaki na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. 37 Unijibu mimi, Ee BWANA, nijibu mimi, ili watu hawa wajue kwamba wewe, Ee BWANA, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena.” 38 Kisha moto wa BWANA ukashuka na kuiteketeza ile dhabihu, zile kuni, yale mawe, ule udongo, na pia kuramba yale maji yaliyokuwa ndani ya handaki. 39 Wakati watu wote walipoona hili, wakaanguka kifudifudi na kulia, “BWANA: yeye ndiye Mungu! BWANA: yeye ndiye Mungu!” 40 Kisha Eliya akawaamuru, “Wakamateni hao manabii wa Baali. Msimwache hata mmoja atoroke!” Wakawakamata, naye Eliya akawaleta mpaka Bonde la Kishoni na kuwachinja huko. 41 Eliya akamwambia Ahabu, “Nenda, ukale na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa.” 42 Hivyo Ahabu akaondoka ili kula na kunywa. Lakini Eliya akapanda kileleni mwa Karmeli, akasujudu na akaweka kichwa chake katikati ya magoti yake. 43 Akamwambia mtumishi wake, “Nenda ukatazame kuelekea bahari.” Akaenda na kutazama.Akasema, “Hakuna kitu chochote huko.”Mara saba Eliya akasema, “Nenda tena.” 44 Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, “Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini.”Hivyo Eliya akasema, “Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ ” 45 Wakati ule ule anga likawa jeusi kwa mawingu, upepo ukainuka na mvua kubwa ikanyesha, naye Ahabu akaenda zake Yezreeli. 46 Nguvu za BWANA zikamjia Eliya, naye akajikaza viuno, akakimbia mbele ya Ahabu njia yote hadi maingilio ya Yezreeli.

In Other Versions

1 Kings 18 in the ANGEFD

1 Kings 18 in the ANTPNG2D

1 Kings 18 in the AS21

1 Kings 18 in the BAGH

1 Kings 18 in the BBPNG

1 Kings 18 in the BBT1E

1 Kings 18 in the BDS

1 Kings 18 in the BEV

1 Kings 18 in the BHAD

1 Kings 18 in the BIB

1 Kings 18 in the BLPT

1 Kings 18 in the BNT

1 Kings 18 in the BNTABOOT

1 Kings 18 in the BNTLV

1 Kings 18 in the BOATCB

1 Kings 18 in the BOATCB2

1 Kings 18 in the BOBCV

1 Kings 18 in the BOCNT

1 Kings 18 in the BOECS

1 Kings 18 in the BOGWICC

1 Kings 18 in the BOHCB

1 Kings 18 in the BOHCV

1 Kings 18 in the BOHLNT

1 Kings 18 in the BOHNTLTAL

1 Kings 18 in the BOICB

1 Kings 18 in the BOILNTAP

1 Kings 18 in the BOITCV

1 Kings 18 in the BOKCV2

1 Kings 18 in the BOKHWOG

1 Kings 18 in the BOKSSV

1 Kings 18 in the BOLCB

1 Kings 18 in the BOLCB2

1 Kings 18 in the BOMCV

1 Kings 18 in the BONAV

1 Kings 18 in the BONCB

1 Kings 18 in the BONLT

1 Kings 18 in the BONUT2

1 Kings 18 in the BOPLNT

1 Kings 18 in the BOSCB

1 Kings 18 in the BOSNC

1 Kings 18 in the BOTLNT

1 Kings 18 in the BOVCB

1 Kings 18 in the BOYCB

1 Kings 18 in the BPBB

1 Kings 18 in the BPH

1 Kings 18 in the BSB

1 Kings 18 in the CCB

1 Kings 18 in the CUV

1 Kings 18 in the CUVS

1 Kings 18 in the DBT

1 Kings 18 in the DGDNT

1 Kings 18 in the DHNT

1 Kings 18 in the DNT

1 Kings 18 in the ELBE

1 Kings 18 in the EMTV

1 Kings 18 in the ESV

1 Kings 18 in the FBV

1 Kings 18 in the FEB

1 Kings 18 in the GGMNT

1 Kings 18 in the GNT

1 Kings 18 in the HARY

1 Kings 18 in the HNT

1 Kings 18 in the IRVA

1 Kings 18 in the IRVB

1 Kings 18 in the IRVG

1 Kings 18 in the IRVH

1 Kings 18 in the IRVK

1 Kings 18 in the IRVM

1 Kings 18 in the IRVM2

1 Kings 18 in the IRVO

1 Kings 18 in the IRVP

1 Kings 18 in the IRVT

1 Kings 18 in the IRVT2

1 Kings 18 in the IRVU

1 Kings 18 in the ISVN

1 Kings 18 in the JSNT

1 Kings 18 in the KAPI

1 Kings 18 in the KBT1ETNIK

1 Kings 18 in the KBV

1 Kings 18 in the KJV

1 Kings 18 in the KNFD

1 Kings 18 in the LBA

1 Kings 18 in the LBLA

1 Kings 18 in the LNT

1 Kings 18 in the LSV

1 Kings 18 in the MAAL

1 Kings 18 in the MBV

1 Kings 18 in the MBV2

1 Kings 18 in the MHNT

1 Kings 18 in the MKNFD

1 Kings 18 in the MNG

1 Kings 18 in the MNT

1 Kings 18 in the MNT2

1 Kings 18 in the MRS1T

1 Kings 18 in the NAA

1 Kings 18 in the NASB

1 Kings 18 in the NBLA

1 Kings 18 in the NBS

1 Kings 18 in the NBVTP

1 Kings 18 in the NET2

1 Kings 18 in the NIV11

1 Kings 18 in the NNT

1 Kings 18 in the NNT2

1 Kings 18 in the NNT3

1 Kings 18 in the PDDPT

1 Kings 18 in the PFNT

1 Kings 18 in the RMNT

1 Kings 18 in the SBIAS

1 Kings 18 in the SBIBS

1 Kings 18 in the SBIBS2

1 Kings 18 in the SBICS

1 Kings 18 in the SBIDS

1 Kings 18 in the SBIGS

1 Kings 18 in the SBIHS

1 Kings 18 in the SBIIS

1 Kings 18 in the SBIIS2

1 Kings 18 in the SBIIS3

1 Kings 18 in the SBIKS

1 Kings 18 in the SBIKS2

1 Kings 18 in the SBIMS

1 Kings 18 in the SBIOS

1 Kings 18 in the SBIPS

1 Kings 18 in the SBISS

1 Kings 18 in the SBITS

1 Kings 18 in the SBITS2

1 Kings 18 in the SBITS3

1 Kings 18 in the SBITS4

1 Kings 18 in the SBIUS

1 Kings 18 in the SBIVS

1 Kings 18 in the SBT

1 Kings 18 in the SBT1E

1 Kings 18 in the SCHL

1 Kings 18 in the SNT

1 Kings 18 in the SUSU

1 Kings 18 in the SUSU2

1 Kings 18 in the SYNO

1 Kings 18 in the TBIAOTANT

1 Kings 18 in the TBT1E

1 Kings 18 in the TBT1E2

1 Kings 18 in the TFTIP

1 Kings 18 in the TFTU

1 Kings 18 in the TGNTATF3T

1 Kings 18 in the THAI

1 Kings 18 in the TNFD

1 Kings 18 in the TNT

1 Kings 18 in the TNTIK

1 Kings 18 in the TNTIL

1 Kings 18 in the TNTIN

1 Kings 18 in the TNTIP

1 Kings 18 in the TNTIZ

1 Kings 18 in the TOMA

1 Kings 18 in the TTENT

1 Kings 18 in the UBG

1 Kings 18 in the UGV

1 Kings 18 in the UGV2

1 Kings 18 in the UGV3

1 Kings 18 in the VBL

1 Kings 18 in the VDCC

1 Kings 18 in the YALU

1 Kings 18 in the YAPE

1 Kings 18 in the YBVTP

1 Kings 18 in the ZBP