2 Chronicles 7 (BOKCV)

1 Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa BWANA ukalijaza Hekalu. 2 Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la BWANA kwa sababu utukufu wa BWANA ulilijaza. 3 Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa BWANA ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru BWANA wakisema,“Yeye ni mwema;upendo wake unadumu milele.” 4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za BWANA Mungu. 5 Naye Mfalme Solomoni akatoa dhabihu ya ngʼombe 22,000 pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu. 6 Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya BWANA ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu BWANA, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama. 7 Solomoni akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la BWANA na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba aliyokuwa ametengeneza haikutosha kuweka sadaka hizo zote za kuteketezwa, sadaka za nafaka na za mafuta. 8 Hivyo Solomoni akaiadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, na Israeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. 9 Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba zaidi. 10 Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Solomoni akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi BWANA Mungu aliomtendea Daudi na Solomoni na kwa ajili ya watu wake Israeli. 11 Solomoni alipomaliza kujenga Hekalu la BWANA na jumba la kifalme, naye akiwa amefanikiwa kutenda yale yote aliyokuwa nayo moyoni mwake kufanya katika Hekalu la BWANA na katika jumba lake mwenyewe la kifalme, 12 BWANA akamtokea Solomoni usiku na kumwambia:“Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu. 13 “Wakati nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu, 14 kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao. 15 Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa. 16 Kwa maana sasa nimechagua na kutakasa Hekalu hili ili kwamba Jina langu lipate kuwa huko milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwepo huko daima. 17 “Kwa habari yako wewe, kama ukienenda mbele zangu kama Daudi baba yako alivyoenenda na kufanya yote nikuamuruyo, nawe ukizishika amri zangu na sheria zangu, 18 Nitakiimarisha kiti chako cha enzi kama nilivyoagana na Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe mtu wa kutawala juu ya Israeli.’ 19 “Lakini kama ukigeuka na kuyaacha maagizo na amri nilizowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, 20 ndipo nitakapoingʼoa Israeli kutoka nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote. 21 Ingawa Hekalu hili linavutia sana sasa, wote watakaolipita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini BWANA amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’ 22 Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu ameyaleta maafa haya yote juu yao.’ ”

In Other Versions

2 Chronicles 7 in the ANGEFD

2 Chronicles 7 in the ANTPNG2D

2 Chronicles 7 in the AS21

2 Chronicles 7 in the BAGH

2 Chronicles 7 in the BBPNG

2 Chronicles 7 in the BBT1E

2 Chronicles 7 in the BDS

2 Chronicles 7 in the BEV

2 Chronicles 7 in the BHAD

2 Chronicles 7 in the BIB

2 Chronicles 7 in the BLPT

2 Chronicles 7 in the BNT

2 Chronicles 7 in the BNTABOOT

2 Chronicles 7 in the BNTLV

2 Chronicles 7 in the BOATCB

2 Chronicles 7 in the BOATCB2

2 Chronicles 7 in the BOBCV

2 Chronicles 7 in the BOCNT

2 Chronicles 7 in the BOECS

2 Chronicles 7 in the BOGWICC

2 Chronicles 7 in the BOHCB

2 Chronicles 7 in the BOHCV

2 Chronicles 7 in the BOHLNT

2 Chronicles 7 in the BOHNTLTAL

2 Chronicles 7 in the BOICB

2 Chronicles 7 in the BOILNTAP

2 Chronicles 7 in the BOITCV

2 Chronicles 7 in the BOKCV2

2 Chronicles 7 in the BOKHWOG

2 Chronicles 7 in the BOKSSV

2 Chronicles 7 in the BOLCB

2 Chronicles 7 in the BOLCB2

2 Chronicles 7 in the BOMCV

2 Chronicles 7 in the BONAV

2 Chronicles 7 in the BONCB

2 Chronicles 7 in the BONLT

2 Chronicles 7 in the BONUT2

2 Chronicles 7 in the BOPLNT

2 Chronicles 7 in the BOSCB

2 Chronicles 7 in the BOSNC

2 Chronicles 7 in the BOTLNT

2 Chronicles 7 in the BOVCB

2 Chronicles 7 in the BOYCB

2 Chronicles 7 in the BPBB

2 Chronicles 7 in the BPH

2 Chronicles 7 in the BSB

2 Chronicles 7 in the CCB

2 Chronicles 7 in the CUV

2 Chronicles 7 in the CUVS

2 Chronicles 7 in the DBT

2 Chronicles 7 in the DGDNT

2 Chronicles 7 in the DHNT

2 Chronicles 7 in the DNT

2 Chronicles 7 in the ELBE

2 Chronicles 7 in the EMTV

2 Chronicles 7 in the ESV

2 Chronicles 7 in the FBV

2 Chronicles 7 in the FEB

2 Chronicles 7 in the GGMNT

2 Chronicles 7 in the GNT

2 Chronicles 7 in the HARY

2 Chronicles 7 in the HNT

2 Chronicles 7 in the IRVA

2 Chronicles 7 in the IRVB

2 Chronicles 7 in the IRVG

2 Chronicles 7 in the IRVH

2 Chronicles 7 in the IRVK

2 Chronicles 7 in the IRVM

2 Chronicles 7 in the IRVM2

2 Chronicles 7 in the IRVO

2 Chronicles 7 in the IRVP

2 Chronicles 7 in the IRVT

2 Chronicles 7 in the IRVT2

2 Chronicles 7 in the IRVU

2 Chronicles 7 in the ISVN

2 Chronicles 7 in the JSNT

2 Chronicles 7 in the KAPI

2 Chronicles 7 in the KBT1ETNIK

2 Chronicles 7 in the KBV

2 Chronicles 7 in the KJV

2 Chronicles 7 in the KNFD

2 Chronicles 7 in the LBA

2 Chronicles 7 in the LBLA

2 Chronicles 7 in the LNT

2 Chronicles 7 in the LSV

2 Chronicles 7 in the MAAL

2 Chronicles 7 in the MBV

2 Chronicles 7 in the MBV2

2 Chronicles 7 in the MHNT

2 Chronicles 7 in the MKNFD

2 Chronicles 7 in the MNG

2 Chronicles 7 in the MNT

2 Chronicles 7 in the MNT2

2 Chronicles 7 in the MRS1T

2 Chronicles 7 in the NAA

2 Chronicles 7 in the NASB

2 Chronicles 7 in the NBLA

2 Chronicles 7 in the NBS

2 Chronicles 7 in the NBVTP

2 Chronicles 7 in the NET2

2 Chronicles 7 in the NIV11

2 Chronicles 7 in the NNT

2 Chronicles 7 in the NNT2

2 Chronicles 7 in the NNT3

2 Chronicles 7 in the PDDPT

2 Chronicles 7 in the PFNT

2 Chronicles 7 in the RMNT

2 Chronicles 7 in the SBIAS

2 Chronicles 7 in the SBIBS

2 Chronicles 7 in the SBIBS2

2 Chronicles 7 in the SBICS

2 Chronicles 7 in the SBIDS

2 Chronicles 7 in the SBIGS

2 Chronicles 7 in the SBIHS

2 Chronicles 7 in the SBIIS

2 Chronicles 7 in the SBIIS2

2 Chronicles 7 in the SBIIS3

2 Chronicles 7 in the SBIKS

2 Chronicles 7 in the SBIKS2

2 Chronicles 7 in the SBIMS

2 Chronicles 7 in the SBIOS

2 Chronicles 7 in the SBIPS

2 Chronicles 7 in the SBISS

2 Chronicles 7 in the SBITS

2 Chronicles 7 in the SBITS2

2 Chronicles 7 in the SBITS3

2 Chronicles 7 in the SBITS4

2 Chronicles 7 in the SBIUS

2 Chronicles 7 in the SBIVS

2 Chronicles 7 in the SBT

2 Chronicles 7 in the SBT1E

2 Chronicles 7 in the SCHL

2 Chronicles 7 in the SNT

2 Chronicles 7 in the SUSU

2 Chronicles 7 in the SUSU2

2 Chronicles 7 in the SYNO

2 Chronicles 7 in the TBIAOTANT

2 Chronicles 7 in the TBT1E

2 Chronicles 7 in the TBT1E2

2 Chronicles 7 in the TFTIP

2 Chronicles 7 in the TFTU

2 Chronicles 7 in the TGNTATF3T

2 Chronicles 7 in the THAI

2 Chronicles 7 in the TNFD

2 Chronicles 7 in the TNT

2 Chronicles 7 in the TNTIK

2 Chronicles 7 in the TNTIL

2 Chronicles 7 in the TNTIN

2 Chronicles 7 in the TNTIP

2 Chronicles 7 in the TNTIZ

2 Chronicles 7 in the TOMA

2 Chronicles 7 in the TTENT

2 Chronicles 7 in the UBG

2 Chronicles 7 in the UGV

2 Chronicles 7 in the UGV2

2 Chronicles 7 in the UGV3

2 Chronicles 7 in the VBL

2 Chronicles 7 in the VDCC

2 Chronicles 7 in the YALU

2 Chronicles 7 in the YAPE

2 Chronicles 7 in the YBVTP

2 Chronicles 7 in the ZBP