Esther 4 (BOKCV)
1 Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake na kuvaa nguo za magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini, akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu. 2 Alikwenda akasimama nje ya lango la mfalme, kwa sababu hakuna yeyote aliyeruhusiwa kuingia akiwa amevaa nguo za magunia. 3 Katika kila jimbo ambapo amri na agizo la mfalme lilifika, kulikuwa na maombolezo makuu miongoni mwa Wayahudi pamoja na kufunga, kulia na kuomboleza. Watu wengi wakalala juu ya nguo za magunia na majivu. 4 Wajakazi wa Esta na matowashi walipokuja na kumwambia kuhusu Mordekai, alipatwa na huzuni kuu. Alimtumia nguo avae badala ya nguo za magunia, lakini Mordekai hakuzikubali. 5 Ndipo Esta akamwita Hathaki, mmojawapo wa matowashi wa mfalme ambaye alikuwa amewekwa kumhudumia Esta, akamwagiza kutafuta ni nini kilikuwa kikimtaabisha Mordekai na ni kwa nini. 6 Basi Hathaki alitoka nje kumwendea Mordekai kwenye uwanja ulio wazi wa mji mbele ya lango la mfalme. 7 Mordekai akamwambia kila kitu ambacho kimempata, pamoja na hesabu kamili ya fedha ambazo Hamani aliahidi kulipa katika hazina ya mfalme kwa ajili ya maangamizi ya Wayahudi. 8 Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonyesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake. 9 Hathaki akarudi kwa Esta na kumwarifu alilolisema Mordekai. 10 Kisha Esta akamwamuru Hathaki amweleze Mordekai, 11 “Maafisa wote wa mfalme na watu wa majimbo ya ufalme wanajua kuwa mwanaume au mwanamke yeyote ambaye ataingia kumwona mfalme katika ua wa ndani bila kuitwa, mfalme ana sheria moja tu: Atauawa. Njia pekee kinyume na hili ni mfalme kumnyooshea fimbo ya dhahabu ili aishi. Lakini siku thelathini zimepita tangu nilipoitwa kwenda kwa mfalme.” 12 Wakati Mordekai aliarifiwa maneno ya Esta, 13 Mordekai alirudisha jibu hili: “Usifikiri kwamba kwa sababu uko katika nyumba ya mfalme wewe pekee katika Wayahudi wote utapona. 14 Kwa kuwa kama utakaa kimya wakati huu, msaada na ukombozi kwa Wayahudi utatoka mahali pengine, lakini wewe na jamaa ya baba yako mtaangamia. Nani ajuaye kwamba hukuja kwenye nafasi ya mamlaka kwa ajili ya wakati kama huu?” 15 Kisha Esta alituma jibu hili kwa Mordekai: 16 “Nenda, kusanya pamoja Wayahudi wote walioko Shushani, nanyi mfunge kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitakwenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.” 17 Kwa hiyo Mordekai alikwenda zake na kutekeleza maagizo yote ya Esta.
In Other Versions
Esther 4 in the ANGEFD
Esther 4 in the ANTPNG2D
Esther 4 in the AS21
Esther 4 in the BAGH
Esther 4 in the BBPNG
Esther 4 in the BBT1E
Esther 4 in the BDS
Esther 4 in the BEV
Esther 4 in the BHAD
Esther 4 in the BIB
Esther 4 in the BLPT
Esther 4 in the BNT
Esther 4 in the BNTABOOT
Esther 4 in the BNTLV
Esther 4 in the BOATCB
Esther 4 in the BOATCB2
Esther 4 in the BOBCV
Esther 4 in the BOCNT
Esther 4 in the BOECS
Esther 4 in the BOGWICC
Esther 4 in the BOHCB
Esther 4 in the BOHCV
Esther 4 in the BOHLNT
Esther 4 in the BOHNTLTAL
Esther 4 in the BOICB
Esther 4 in the BOILNTAP
Esther 4 in the BOITCV
Esther 4 in the BOKCV2
Esther 4 in the BOKHWOG
Esther 4 in the BOKSSV
Esther 4 in the BOLCB
Esther 4 in the BOLCB2
Esther 4 in the BOMCV
Esther 4 in the BONAV
Esther 4 in the BONCB
Esther 4 in the BONLT
Esther 4 in the BONUT2
Esther 4 in the BOPLNT
Esther 4 in the BOSCB
Esther 4 in the BOSNC
Esther 4 in the BOTLNT
Esther 4 in the BOVCB
Esther 4 in the BOYCB
Esther 4 in the BPBB
Esther 4 in the BPH
Esther 4 in the BSB
Esther 4 in the CCB
Esther 4 in the CUV
Esther 4 in the CUVS
Esther 4 in the DBT
Esther 4 in the DGDNT
Esther 4 in the DHNT
Esther 4 in the DNT
Esther 4 in the ELBE
Esther 4 in the EMTV
Esther 4 in the ESV
Esther 4 in the FBV
Esther 4 in the FEB
Esther 4 in the GGMNT
Esther 4 in the GNT
Esther 4 in the HARY
Esther 4 in the HNT
Esther 4 in the IRVA
Esther 4 in the IRVB
Esther 4 in the IRVG
Esther 4 in the IRVH
Esther 4 in the IRVK
Esther 4 in the IRVM
Esther 4 in the IRVM2
Esther 4 in the IRVO
Esther 4 in the IRVP
Esther 4 in the IRVT
Esther 4 in the IRVT2
Esther 4 in the IRVU
Esther 4 in the ISVN
Esther 4 in the JSNT
Esther 4 in the KAPI
Esther 4 in the KBT1ETNIK
Esther 4 in the KBV
Esther 4 in the KJV
Esther 4 in the KNFD
Esther 4 in the LBA
Esther 4 in the LBLA
Esther 4 in the LNT
Esther 4 in the LSV
Esther 4 in the MAAL
Esther 4 in the MBV
Esther 4 in the MBV2
Esther 4 in the MHNT
Esther 4 in the MKNFD
Esther 4 in the MNG
Esther 4 in the MNT
Esther 4 in the MNT2
Esther 4 in the MRS1T
Esther 4 in the NAA
Esther 4 in the NASB
Esther 4 in the NBLA
Esther 4 in the NBS
Esther 4 in the NBVTP
Esther 4 in the NET2
Esther 4 in the NIV11
Esther 4 in the NNT
Esther 4 in the NNT2
Esther 4 in the NNT3
Esther 4 in the PDDPT
Esther 4 in the PFNT
Esther 4 in the RMNT
Esther 4 in the SBIAS
Esther 4 in the SBIBS
Esther 4 in the SBIBS2
Esther 4 in the SBICS
Esther 4 in the SBIDS
Esther 4 in the SBIGS
Esther 4 in the SBIHS
Esther 4 in the SBIIS
Esther 4 in the SBIIS2
Esther 4 in the SBIIS3
Esther 4 in the SBIKS
Esther 4 in the SBIKS2
Esther 4 in the SBIMS
Esther 4 in the SBIOS
Esther 4 in the SBIPS
Esther 4 in the SBISS
Esther 4 in the SBITS
Esther 4 in the SBITS2
Esther 4 in the SBITS3
Esther 4 in the SBITS4
Esther 4 in the SBIUS
Esther 4 in the SBIVS
Esther 4 in the SBT
Esther 4 in the SBT1E
Esther 4 in the SCHL
Esther 4 in the SNT
Esther 4 in the SUSU
Esther 4 in the SUSU2
Esther 4 in the SYNO
Esther 4 in the TBIAOTANT
Esther 4 in the TBT1E
Esther 4 in the TBT1E2
Esther 4 in the TFTIP
Esther 4 in the TFTU
Esther 4 in the TGNTATF3T
Esther 4 in the THAI
Esther 4 in the TNFD
Esther 4 in the TNT
Esther 4 in the TNTIK
Esther 4 in the TNTIL
Esther 4 in the TNTIN
Esther 4 in the TNTIP
Esther 4 in the TNTIZ
Esther 4 in the TOMA
Esther 4 in the TTENT
Esther 4 in the UBG
Esther 4 in the UGV
Esther 4 in the UGV2
Esther 4 in the UGV3
Esther 4 in the VBL
Esther 4 in the VDCC
Esther 4 in the YALU
Esther 4 in the YAPE
Esther 4 in the YBVTP
Esther 4 in the ZBP