Esther 9 (BOKCV)

1 Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia. 2 Wayahudi walikusanyika katika miji yao, katika majimbo ya Mfalme Ahasuero kuwashambulia wale waliokuwa wanatafuta kuwaangamiza. Hakuna yeyote aliyeweza kushindana nao, kwa sababu watu wa mataifa mengine yote waliwaogopa. 3 Nao wakuu wote wa majimbo, majemadari, watawala na maafisa wa mfalme wakawasaidia Wayahudi, kwa sababu walimhofu Mordekai. 4 Mordekai alikuwa mtu mashuhuri katika jumba la mfalme; sifa zake zilienea katika majimbo yote naye alipata uwezo zaidi na zaidi. 5 Wayahudi waliwaangusha adui zao wote kwa upanga wakiwaua na kuwaangamiza, nao walifanya kile walichotaka kwa wale waliowachukia. 6 Katika ngome ya Shushani Wayahudi waliua na kuangamiza wanaume 500. 7 Pia waliwaua Parshendatha, Dalfoni, Aspatha, 8 Poratha, Adalia, Ardatha, 9 Parmashta, Arisai, Aridai na Waizatha, 10 wana kumi wa Hamani mwana wa Hamedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchukua nyara. 11 Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani. 12 Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wamewaua wanaume 500 na wana kumi wa Hamani ndani ya ngome ya Shushani. Wamefanyaje katika majimbo mengine ya mfalme yaliyobaki? Je, sasa haja yako ni nini? Nayo pia utapewa. Nalo ombi lako ni nini? Nalo utafanyiwa.” 13 Esta akajibu, “Ikimpendeza mfalme, uwape ruhusa Wayahudi walioko Shushani warudie amri ya leo kesho pia, na wana wa Hamani kumi wanyongwe mahali pa kunyongea watu.” 14 Basi mfalme akaamuru kwamba hili litendeke. Amri ilitolewa huko Shushani, nao wakawanyonga wana kumi wa Hamani. 15 Wayahudi huko Shushani wakakusanyika pamoja siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, nao wakawaua wanaume 300 huko Shushani, lakini hawakuchukua nyara zao. 16 Wakati ule ule, Wayahudi wengine waliokuwa kwenye majimbo ya mfalme, wakakusanyika kujilinda nao wakapata nafuu kutokana na adui zao. Waliua adui zao wapatao 75,000 lakini hawakugusa nyara zao. 17 Hili lilitendeka siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari na siku ya kumi na nne walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha. 18 Wayahudi huko Shushani, hata hivyo, walikuwa wamekusanyika siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne, pia siku ya kumi na tano walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha. 19 Ndiyo sababu Wayahudi wanaokaa vijijini na katika miji midogo huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu, siku ambayo wao hupeana zawadi mmoja kwa mwingine. 20 Mordekai aliandika matukio haya, naye akapeleka barua kwa Wayahudi wote walioko katika majimbo ya Mfalme Ahasuero, majimbo yaliyo mbali na karibu, 21 akiwataka kila mwaka washerehekee siku ya kumi na nne na ya kumi na tano ya mwezi wa Adari 22 kama wakati ambao Wayahudi walipata nafuu kutoka kwa adui zao na kama mwezi ambao huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha na kuomboleza kwao kuwa siku ya kusherehekea. Aliwaandikia kushika siku hizo kama siku za karamu na za furaha na kupeana zawadi za vyakula wao kwa wao na zawadi kwa maskini. 23 Hivyo Wayahudi walikubali kuendeleza sherehe walizokuwa wamezianza, wakifanya lile Mordekai alilokuwa amewaandikia. 24 Kwa maana Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, adui wa Wayahudi wote, alikuwa amepanga hila dhidi ya Wayahudi ili kuwaangamiza, na alikuwa amepiga puri (yaani kura) kwa ajili ya maangamizi na uharibifu wao. 25 Lakini wakati shauri hilo baya lilipoarifiwa kwa mfalme, alitoa amri iliyoandikwa kwamba mipango mibaya ambayo Hamani ameipanga dhidi ya Wayahudi inapasa imrudie juu ya kichwa chake mwenyewe, na kwamba yeye na wanawe waangikwe mahali pa kunyongea watu. 26 (Kwa hiyo siku hizi ziliitwa Purimu, kutokana na neno puri.) Kwa sababu ya kila kitu kilichoandikwa kwenye barua hii na kwa sababu ya yale waliyoyaona na yale yaliyowatokea, 27 Wayahudi wakachukua na kuifanya desturi kwamba wao na wazao wao na wote ambao walijiunga nao wangefanya bila kuacha kushika siku hizi mbili kila mwaka, kwa njia ilivyoelekezwa na kwa wakati wake. 28 Siku hizi zinapasa zikumbukwe na kuadhimishwa katika kila kizazi, kila jamaa na katika kila jimbo na kila jiji. Nazo siku hizi za Purimu kamwe zisikome kusherehekewa na Wayahudi, wala kumbukumbu zake zisipotee miongoni mwa wazao wake. 29 Basi Malkia Esta binti Abihaili, pamoja na Mordekai, Myahudi, waliandika kwa mamlaka yote kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu. 30 Naye Mordekai akatuma barua kwa Wayahudi wote katika majimbo 127 ya ufalme wa Ahasuero, barua zenye maneno ya amani na matumaini, 31 ili kuimarisha siku hizi za Purimu katika majira yake yaliyowekwa, kama Mordekai, Myahudi na Malkia Esta walivyowaamuru, na walivyojiimarisha wenyewe na wazao wao kuhusu nyakati za kufunga na kuomboleza. 32 Amri ya Esta ilithibitisha taratibu hizi kuhusu Purimu, nayo ikaandikwa katika kumbukumbu.

In Other Versions

Esther 9 in the ANGEFD

Esther 9 in the ANTPNG2D

Esther 9 in the AS21

Esther 9 in the BAGH

Esther 9 in the BBPNG

Esther 9 in the BBT1E

Esther 9 in the BDS

Esther 9 in the BEV

Esther 9 in the BHAD

Esther 9 in the BIB

Esther 9 in the BLPT

Esther 9 in the BNT

Esther 9 in the BNTABOOT

Esther 9 in the BNTLV

Esther 9 in the BOATCB

Esther 9 in the BOATCB2

Esther 9 in the BOBCV

Esther 9 in the BOCNT

Esther 9 in the BOECS

Esther 9 in the BOGWICC

Esther 9 in the BOHCB

Esther 9 in the BOHCV

Esther 9 in the BOHLNT

Esther 9 in the BOHNTLTAL

Esther 9 in the BOICB

Esther 9 in the BOILNTAP

Esther 9 in the BOITCV

Esther 9 in the BOKCV2

Esther 9 in the BOKHWOG

Esther 9 in the BOKSSV

Esther 9 in the BOLCB

Esther 9 in the BOLCB2

Esther 9 in the BOMCV

Esther 9 in the BONAV

Esther 9 in the BONCB

Esther 9 in the BONLT

Esther 9 in the BONUT2

Esther 9 in the BOPLNT

Esther 9 in the BOSCB

Esther 9 in the BOSNC

Esther 9 in the BOTLNT

Esther 9 in the BOVCB

Esther 9 in the BOYCB

Esther 9 in the BPBB

Esther 9 in the BPH

Esther 9 in the BSB

Esther 9 in the CCB

Esther 9 in the CUV

Esther 9 in the CUVS

Esther 9 in the DBT

Esther 9 in the DGDNT

Esther 9 in the DHNT

Esther 9 in the DNT

Esther 9 in the ELBE

Esther 9 in the EMTV

Esther 9 in the ESV

Esther 9 in the FBV

Esther 9 in the FEB

Esther 9 in the GGMNT

Esther 9 in the GNT

Esther 9 in the HARY

Esther 9 in the HNT

Esther 9 in the IRVA

Esther 9 in the IRVB

Esther 9 in the IRVG

Esther 9 in the IRVH

Esther 9 in the IRVK

Esther 9 in the IRVM

Esther 9 in the IRVM2

Esther 9 in the IRVO

Esther 9 in the IRVP

Esther 9 in the IRVT

Esther 9 in the IRVT2

Esther 9 in the IRVU

Esther 9 in the ISVN

Esther 9 in the JSNT

Esther 9 in the KAPI

Esther 9 in the KBT1ETNIK

Esther 9 in the KBV

Esther 9 in the KJV

Esther 9 in the KNFD

Esther 9 in the LBA

Esther 9 in the LBLA

Esther 9 in the LNT

Esther 9 in the LSV

Esther 9 in the MAAL

Esther 9 in the MBV

Esther 9 in the MBV2

Esther 9 in the MHNT

Esther 9 in the MKNFD

Esther 9 in the MNG

Esther 9 in the MNT

Esther 9 in the MNT2

Esther 9 in the MRS1T

Esther 9 in the NAA

Esther 9 in the NASB

Esther 9 in the NBLA

Esther 9 in the NBS

Esther 9 in the NBVTP

Esther 9 in the NET2

Esther 9 in the NIV11

Esther 9 in the NNT

Esther 9 in the NNT2

Esther 9 in the NNT3

Esther 9 in the PDDPT

Esther 9 in the PFNT

Esther 9 in the RMNT

Esther 9 in the SBIAS

Esther 9 in the SBIBS

Esther 9 in the SBIBS2

Esther 9 in the SBICS

Esther 9 in the SBIDS

Esther 9 in the SBIGS

Esther 9 in the SBIHS

Esther 9 in the SBIIS

Esther 9 in the SBIIS2

Esther 9 in the SBIIS3

Esther 9 in the SBIKS

Esther 9 in the SBIKS2

Esther 9 in the SBIMS

Esther 9 in the SBIOS

Esther 9 in the SBIPS

Esther 9 in the SBISS

Esther 9 in the SBITS

Esther 9 in the SBITS2

Esther 9 in the SBITS3

Esther 9 in the SBITS4

Esther 9 in the SBIUS

Esther 9 in the SBIVS

Esther 9 in the SBT

Esther 9 in the SBT1E

Esther 9 in the SCHL

Esther 9 in the SNT

Esther 9 in the SUSU

Esther 9 in the SUSU2

Esther 9 in the SYNO

Esther 9 in the TBIAOTANT

Esther 9 in the TBT1E

Esther 9 in the TBT1E2

Esther 9 in the TFTIP

Esther 9 in the TFTU

Esther 9 in the TGNTATF3T

Esther 9 in the THAI

Esther 9 in the TNFD

Esther 9 in the TNT

Esther 9 in the TNTIK

Esther 9 in the TNTIL

Esther 9 in the TNTIN

Esther 9 in the TNTIP

Esther 9 in the TNTIZ

Esther 9 in the TOMA

Esther 9 in the TTENT

Esther 9 in the UBG

Esther 9 in the UGV

Esther 9 in the UGV2

Esther 9 in the UGV3

Esther 9 in the VBL

Esther 9 in the VDCC

Esther 9 in the YALU

Esther 9 in the YAPE

Esther 9 in the YBVTP

Esther 9 in the ZBP