Exodus 10 (BOKCV)

1 Ndipo BWANA akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao, kwa kuwa nimeufanya moyo wake kuwa mgumu na mioyo ya maafisa wake ili kwamba nipate kutenda ishara hizi zangu za ajabu miongoni mwao 2 ili upate kuwaeleza watoto wako na wajukuu wako jinsi nilivyowatendea Wamisri kwa ukali na jinsi nilivyofanya ishara zangu miongoni mwao, nanyi mpate kujua kuwa Mimi ndimi BWANA.” 3 Kwa hiyo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndilo BWANA, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. 4 Kama ukikataa kuwaachia waende, kesho nitaleta nzige katika nchi yako. 5 Nao watafunika uso wa ardhi hata usionekane. Watatafuna mabaki machache yaliyobakizwa baada ya ile mvua ya mawe, yaani pamoja na kila mti unaoota katika mashamba yenu. 6 Nzige hao watajaza nyumba zako, za maafisa wako wote na za Wamisri wote. Jambo ambalo baba zenu wala babu zenu hawajapata kuona tangu siku ile walipoanza kuishi katika nchi hii mpaka leo hii.’ ” Ndipo Mose akageuka na kumwacha Farao. 7 Maafisa wa Farao wakamwambia, “Mpaka lini huyu mtu atakuwa tanzi kwetu? Waachie hao watu waende zao, ili wapate kumwabudu BWANA Mungu wao. Je, bado hutambui kuwa Misri imeangamia?” 8 Ndipo Mose na Aroni wakaletwa kwa Farao. Farao akawaambia, “Nendeni, mkamwabudu BWANA Mungu wenu. Lakini ni nani hasa watakaokwenda?” 9 Mose akajibu, “Tutakwenda na vijana wetu na wazee, pamoja na wana wetu na binti zetu, pia pamoja na kondoo zetu, ngʼombe, mbuzi, farasi na punda kwa sababu tutaadhimisha sikukuu kwa BWANA.” 10 Farao akasema, “BWANA awe pamoja nanyi, kama nikiwaruhusu mwondoke pamoja na wanawake wenu na watoto wenu! Ni wazi kwamba mna makusudi mabaya. 11 La hasha! Wanaume peke yao na waende, wakamwabudu BWANA, kwa kuwa hilo ndilo mmekuwa mkiomba.” Kwa hiyo Mose na Aroni wakaondolewa mbele ya Farao. 12 Basi BWANA akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako juu ya Misri ili kundi la nzige liweze kuingia juu ya nchi na kutafuna kila kitu kiotacho katika mashamba na kila kitu kilichosazwa na ile mvua ya mawe.” 13 Kwa hiyo Mose akanyoosha fimbo yake juu ya Misri, BWANA akauleta upepo wa mashariki ukavuma katika nchi yote mchana wote na usiku kucha, kufikia asubuhi upepo ukawa umeleta nzige. 14 Wakaivamia Misri yote na kukaa kila eneo la nchi kwa wingi. Kamwe hapajapata kuwepo pigo la nzige kama hilo, wala halitakuwepo tena. 15 Wakafunika ardhi yote mpaka ardhi ikawa nyeusi. Wakatafuna kile chote kilichokuwa kimebakizwa na ile mvua ya mawe, kila kitu kiotacho mashambani pamoja na matunda kwenye miti. Hakuna kitu chochote cha kijani kilichosalia katika miti au mmea katika nchi yote ya Misri. 16 Farao akawaita Mose na Aroni kwa haraka na kuwaambia, “Nimetenda dhambi dhidi ya BWANA Mungu wenu na dhidi yenu pia. 17 Sasa unisamehe dhambi yangu mara moja tena na umwombe BWANA Mungu wako aondoe pigo hili baya kwangu.” 18 Kisha Mose akaondoka kwa Farao akamwomba BWANA. 19 Naye BWANA akaugeuza upepo ukavuma kutoka magharibi, wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka kwenye Bahari ya Shamu. Hakuna nzige hata mmoja aliyebaki popote katika nchi ya Misri. 20 Lakini BWANA akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke. 21 Kisha BWANA akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.” 22 Kwa hiyo Mose akaunyoosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. 23 Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Waisraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi. 24 Ndipo Farao akamwita Mose na kusema, “Nendeni, mkamwabudu BWANA. Hata wanawake na watoto wenu mwaweza kwenda nao pia, lakini kondoo, mbuzi na ngʼombe wenu waacheni.” 25 Lakini Mose akasema, “Huna budi kuturuhusu tuwe na dhabihu na sadaka za kuteketezwa za kutoa mbele za BWANA Mungu wetu. 26 Sisi ni lazima tuondoke na mifugo yetu pia, wala hakuna ukwato utakaoachwa nyuma. Inatupasa kutumia baadhi ya hiyo mifugo katika kumwabudu BWANA Mungu wetu, kwa kuwa mpaka tutakapofika huko hatutakuwa tumefahamu ni nini tutakachotumia katika kumwabudu BWANA.” 27 Lakini BWANA akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, hakuwa radhi kuwaachia waondoke. 28 Farao akamwambia Mose, “Ondoka mbele yangu! Hakikisha kuwa hutakuja mbele yangu tena! Siku ile utakapouona uso wangu utakufa.” 29 Mose akamjibu, “Iwe kama ulivyosema! Kamwe sitauona uso wako tena.”

In Other Versions

Exodus 10 in the ANGEFD

Exodus 10 in the ANTPNG2D

Exodus 10 in the AS21

Exodus 10 in the BAGH

Exodus 10 in the BBPNG

Exodus 10 in the BBT1E

Exodus 10 in the BDS

Exodus 10 in the BEV

Exodus 10 in the BHAD

Exodus 10 in the BIB

Exodus 10 in the BLPT

Exodus 10 in the BNT

Exodus 10 in the BNTABOOT

Exodus 10 in the BNTLV

Exodus 10 in the BOATCB

Exodus 10 in the BOATCB2

Exodus 10 in the BOBCV

Exodus 10 in the BOCNT

Exodus 10 in the BOECS

Exodus 10 in the BOGWICC

Exodus 10 in the BOHCB

Exodus 10 in the BOHCV

Exodus 10 in the BOHLNT

Exodus 10 in the BOHNTLTAL

Exodus 10 in the BOICB

Exodus 10 in the BOILNTAP

Exodus 10 in the BOITCV

Exodus 10 in the BOKCV2

Exodus 10 in the BOKHWOG

Exodus 10 in the BOKSSV

Exodus 10 in the BOLCB

Exodus 10 in the BOLCB2

Exodus 10 in the BOMCV

Exodus 10 in the BONAV

Exodus 10 in the BONCB

Exodus 10 in the BONLT

Exodus 10 in the BONUT2

Exodus 10 in the BOPLNT

Exodus 10 in the BOSCB

Exodus 10 in the BOSNC

Exodus 10 in the BOTLNT

Exodus 10 in the BOVCB

Exodus 10 in the BOYCB

Exodus 10 in the BPBB

Exodus 10 in the BPH

Exodus 10 in the BSB

Exodus 10 in the CCB

Exodus 10 in the CUV

Exodus 10 in the CUVS

Exodus 10 in the DBT

Exodus 10 in the DGDNT

Exodus 10 in the DHNT

Exodus 10 in the DNT

Exodus 10 in the ELBE

Exodus 10 in the EMTV

Exodus 10 in the ESV

Exodus 10 in the FBV

Exodus 10 in the FEB

Exodus 10 in the GGMNT

Exodus 10 in the GNT

Exodus 10 in the HARY

Exodus 10 in the HNT

Exodus 10 in the IRVA

Exodus 10 in the IRVB

Exodus 10 in the IRVG

Exodus 10 in the IRVH

Exodus 10 in the IRVK

Exodus 10 in the IRVM

Exodus 10 in the IRVM2

Exodus 10 in the IRVO

Exodus 10 in the IRVP

Exodus 10 in the IRVT

Exodus 10 in the IRVT2

Exodus 10 in the IRVU

Exodus 10 in the ISVN

Exodus 10 in the JSNT

Exodus 10 in the KAPI

Exodus 10 in the KBT1ETNIK

Exodus 10 in the KBV

Exodus 10 in the KJV

Exodus 10 in the KNFD

Exodus 10 in the LBA

Exodus 10 in the LBLA

Exodus 10 in the LNT

Exodus 10 in the LSV

Exodus 10 in the MAAL

Exodus 10 in the MBV

Exodus 10 in the MBV2

Exodus 10 in the MHNT

Exodus 10 in the MKNFD

Exodus 10 in the MNG

Exodus 10 in the MNT

Exodus 10 in the MNT2

Exodus 10 in the MRS1T

Exodus 10 in the NAA

Exodus 10 in the NASB

Exodus 10 in the NBLA

Exodus 10 in the NBS

Exodus 10 in the NBVTP

Exodus 10 in the NET2

Exodus 10 in the NIV11

Exodus 10 in the NNT

Exodus 10 in the NNT2

Exodus 10 in the NNT3

Exodus 10 in the PDDPT

Exodus 10 in the PFNT

Exodus 10 in the RMNT

Exodus 10 in the SBIAS

Exodus 10 in the SBIBS

Exodus 10 in the SBIBS2

Exodus 10 in the SBICS

Exodus 10 in the SBIDS

Exodus 10 in the SBIGS

Exodus 10 in the SBIHS

Exodus 10 in the SBIIS

Exodus 10 in the SBIIS2

Exodus 10 in the SBIIS3

Exodus 10 in the SBIKS

Exodus 10 in the SBIKS2

Exodus 10 in the SBIMS

Exodus 10 in the SBIOS

Exodus 10 in the SBIPS

Exodus 10 in the SBISS

Exodus 10 in the SBITS

Exodus 10 in the SBITS2

Exodus 10 in the SBITS3

Exodus 10 in the SBITS4

Exodus 10 in the SBIUS

Exodus 10 in the SBIVS

Exodus 10 in the SBT

Exodus 10 in the SBT1E

Exodus 10 in the SCHL

Exodus 10 in the SNT

Exodus 10 in the SUSU

Exodus 10 in the SUSU2

Exodus 10 in the SYNO

Exodus 10 in the TBIAOTANT

Exodus 10 in the TBT1E

Exodus 10 in the TBT1E2

Exodus 10 in the TFTIP

Exodus 10 in the TFTU

Exodus 10 in the TGNTATF3T

Exodus 10 in the THAI

Exodus 10 in the TNFD

Exodus 10 in the TNT

Exodus 10 in the TNTIK

Exodus 10 in the TNTIL

Exodus 10 in the TNTIN

Exodus 10 in the TNTIP

Exodus 10 in the TNTIZ

Exodus 10 in the TOMA

Exodus 10 in the TTENT

Exodus 10 in the UBG

Exodus 10 in the UGV

Exodus 10 in the UGV2

Exodus 10 in the UGV3

Exodus 10 in the VBL

Exodus 10 in the VDCC

Exodus 10 in the YALU

Exodus 10 in the YAPE

Exodus 10 in the YBVTP

Exodus 10 in the ZBP