Genesis 42 (BOKCV)

1 Wakati Yakobo alipofahamu kuwa kuna nafaka huko Misri, akawaambia wanawe, “Mbona mnakaa tu hapa mnatazamana?” 2 Akaendelea kuwaambia, “Nimesikia kuwa huko Misri kuna nafaka. Telemkeni huko mkanunue chakula kwa ajili yetu, ili tuweze kuishi wala tusife.” 3 Ndipo wale ndugu kumi wa Yosefu, wakateremka huko Misri kununua nafaka. 4 Lakini Yakobo hakumtuma Benyamini, ndugu yake Yosefu, pamoja na wengine, kwa sababu aliogopa asije akapatwa na madhara. 5 Hivyo wana wa Israeli walikuwa miongoni mwa wale waliokwenda Misri kununua nafaka, kwani njaa ilikuwa katika nchi ya Kanaani pia. 6 Wakati huo Yosefu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, naye alikuwa ndiye aliwauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yosefu walipofika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi. 7 Mara Yosefu alipowaona ndugu zake, akawatambua, lakini akajifanya mgeni na kuzungumza nao kwa ukali, akiwauliza, “Ninyi mnatoka wapi?”Wakamjibu, “Tumetoka katika nchi ya Kanaani kuja kununua chakula.” 8 Ingawa Yosefu aliwatambua ndugu zake, wao hawakumtambua. 9 Ndipo Yosefu alipokumbuka ndoto zake kuwahusu wao, akawaambia, “Ninyi ni wapelelezi! Mmekuja kuangalia mahali ambapo nchi yetu haina ulinzi.” 10 Wakamjibu, “Sivyo bwana wangu. Watumishi wako wamekuja kununua chakula. 11 Sisi sote ni wana wa baba mmoja. Watumishi wako ni watu waaminifu, wala sio wapelelezi.” 12 Akawaambia, “La hasha! Mmekuja kuangalia mahali ambapo nchi yetu haina ulinzi.” 13 Lakini wakamjibu, “Watumishi wako walikuwa kumi na wawili, wana wa mtu mmoja ambaye anaishi katika nchi ya Kanaani. Sasa mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu na mwingine alikufa.” 14 Yosefu akawaambia, “Ni sawa kabisa kama nilivyowaambia: Ninyi ni wapelelezi! 15 Na hivi ndivyo mtakavyojaribiwa: Hakika kama Farao aishivyo, hamtaondoka mahali hapa mpaka ndugu yenu mdogo aje hapa. 16 Tumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu, wengine mtawekwa gerezani, ili maneno yenu yajaribiwe kuona kama mnasema kweli. La sivyo, hakika kama Farao aishivyo ninyi ni wapelelezi!” 17 Akawaweka wote chini ya ulinzi kwa siku tatu. 18 Siku ya tatu Yosefu akawaambia, “Fanyeni hili nanyi mtaishi, kwa maana namwogopa Mungu: 19 Ikiwa ninyi ni watu waaminifu, mmoja wa ndugu zenu na abaki kifungoni, nanyi wengine pelekeni nafaka kwa jamaa yenu wanaoteseka kwa njaa. 20 Lakini ni lazima mniletee ndugu yenu mdogo hapa, ili maneno yenu yathibitike na kwamba msife.” Wakakubali kufanya hivyo. 21 Wakaambiana wao kwa wao, “Hakika tunaadhibiwa kwa sababu ya ndugu yetu. Tuliona jinsi alivyohuzunika alipokuwa anatusihi kuponya maisha yake, lakini hatukumsikiliza, hiyo ndiyo sababu dhiki hii imetupata.” 22 Reubeni akawajibu, “Sikuwaambieni msitende dhambi dhidi ya kijana? Lakini hamkunisikiliza! Sasa ni lazima tuadhibiwe kwa ajili ya damu yake.” 23 Hawakujua kuwa Yosefu angewaelewa, kwa sababu alitumia mkalimani. 24 Yosefu akajitenga nao akaanza kulia, kisha akawarudia na kuzungumza nao tena. Akataka Simeoni akamatwe na kufungwa mbele yao. 25 Yosefu akatoa amri ya kujaza magunia yao nafaka na kuweka fedha ya kila mmoja ndani ya gunia lake, kisha wapewe mahitaji ya njiani. Baada ya kufanyiwa hayo yote, 26 wakapakiza nafaka juu ya punda zao, wakaondoka. 27 Walipofika mahali pa kulala huko njiani mmoja wao akafungua gunia lake ili amlishe punda wake, akakuta fedha yake kwenye mdomo wa gunia lake. 28 Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Iko ndani ya gunia langu.”Mioyo yao ikazimia, na kila mmoja akamgeukia mwenzake wakitetemeka, wakaulizana, “Ni nini hiki Mungu alichotufanyia?” 29 Walipofika kwa Yakobo baba yao katika nchi ya Kanaani, wakamweleza mambo yote yaliyowapata. Wakasema, 30 “Huyo mtu ambaye ndiye bwana katika nchi hiyo alisema nasi kwa ukali, akatutendea kana kwamba sisi tulikuwa tunaipeleleza nchi. 31 Lakini tulimwambia, ‘Sisi ni watu waaminifu, sio wapelelezi. 32 Tulizaliwa ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja. Mmoja alikufa, na mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu huko Kanaani.’ 33 “Ndipo huyo mtu aliye bwana katika nchi hiyo alipotuambia, ‘Hivi ndivyo nitafahamu kuwa ninyi ni watu waaminifu: Mwacheni mmoja wa ndugu zenu pamoja nami hapa, kisha nendeni mpeleke chakula kwa ajili ya jamaa yenu inayoteseka kwa njaa. 34 Lakini mleteni huyo ndugu yenu mdogo kwangu, ndipo nitajua kuwa ninyi sio wapelelezi, ila ni watu waaminifu. Kisha nitamrudisha ndugu yenu, nanyi mtaweza kufanya biashara katika nchi hii.’ ” 35 Walipokuwa wanamimina nafaka kutoka kwenye magunia yao, ndani ya gunia la kila mtu kulikuwa na mfuko wa fedha! Wakati wao na baba yao walipoona mifuko ya fedha, wakaogopa. 36 Yakobo baba yao akawaambia, “Ninyi mmenipokonya watoto wangu. Yosefu hayupo na Simeoni hayupo tena na sasa mnataka kumchukua Benyamini. Kila kitu ni kinyume nami!” 37 Ndipo Reubeni akamwambia baba yake, “Waweza kuwaua wanangu wote wawili, ikiwa sitamrudisha Benyamini kwako. Mkabidhi Benyamini katika uangalizi wangu, nami nitamrudisha.” 38 Lakini Yakobo akasema, “Mwanangu hatashuka huko pamoja nanyi; ndugu yake amekufa naye ndiye peke yake aliyebaki. Ikiwa atapatwa na madhara katika safari mnayoiendea, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini kwa masikitiko.”

In Other Versions

Genesis 42 in the ANGEFD

Genesis 42 in the ANTPNG2D

Genesis 42 in the AS21

Genesis 42 in the BAGH

Genesis 42 in the BBPNG

Genesis 42 in the BBT1E

Genesis 42 in the BDS

Genesis 42 in the BEV

Genesis 42 in the BHAD

Genesis 42 in the BIB

Genesis 42 in the BLPT

Genesis 42 in the BNT

Genesis 42 in the BNTABOOT

Genesis 42 in the BNTLV

Genesis 42 in the BOATCB

Genesis 42 in the BOATCB2

Genesis 42 in the BOBCV

Genesis 42 in the BOCNT

Genesis 42 in the BOECS

Genesis 42 in the BOGWICC

Genesis 42 in the BOHCB

Genesis 42 in the BOHCV

Genesis 42 in the BOHLNT

Genesis 42 in the BOHNTLTAL

Genesis 42 in the BOICB

Genesis 42 in the BOILNTAP

Genesis 42 in the BOITCV

Genesis 42 in the BOKCV2

Genesis 42 in the BOKHWOG

Genesis 42 in the BOKSSV

Genesis 42 in the BOLCB

Genesis 42 in the BOLCB2

Genesis 42 in the BOMCV

Genesis 42 in the BONAV

Genesis 42 in the BONCB

Genesis 42 in the BONLT

Genesis 42 in the BONUT2

Genesis 42 in the BOPLNT

Genesis 42 in the BOSCB

Genesis 42 in the BOSNC

Genesis 42 in the BOTLNT

Genesis 42 in the BOVCB

Genesis 42 in the BOYCB

Genesis 42 in the BPBB

Genesis 42 in the BPH

Genesis 42 in the BSB

Genesis 42 in the CCB

Genesis 42 in the CUV

Genesis 42 in the CUVS

Genesis 42 in the DBT

Genesis 42 in the DGDNT

Genesis 42 in the DHNT

Genesis 42 in the DNT

Genesis 42 in the ELBE

Genesis 42 in the EMTV

Genesis 42 in the ESV

Genesis 42 in the FBV

Genesis 42 in the FEB

Genesis 42 in the GGMNT

Genesis 42 in the GNT

Genesis 42 in the HARY

Genesis 42 in the HNT

Genesis 42 in the IRVA

Genesis 42 in the IRVB

Genesis 42 in the IRVG

Genesis 42 in the IRVH

Genesis 42 in the IRVK

Genesis 42 in the IRVM

Genesis 42 in the IRVM2

Genesis 42 in the IRVO

Genesis 42 in the IRVP

Genesis 42 in the IRVT

Genesis 42 in the IRVT2

Genesis 42 in the IRVU

Genesis 42 in the ISVN

Genesis 42 in the JSNT

Genesis 42 in the KAPI

Genesis 42 in the KBT1ETNIK

Genesis 42 in the KBV

Genesis 42 in the KJV

Genesis 42 in the KNFD

Genesis 42 in the LBA

Genesis 42 in the LBLA

Genesis 42 in the LNT

Genesis 42 in the LSV

Genesis 42 in the MAAL

Genesis 42 in the MBV

Genesis 42 in the MBV2

Genesis 42 in the MHNT

Genesis 42 in the MKNFD

Genesis 42 in the MNG

Genesis 42 in the MNT

Genesis 42 in the MNT2

Genesis 42 in the MRS1T

Genesis 42 in the NAA

Genesis 42 in the NASB

Genesis 42 in the NBLA

Genesis 42 in the NBS

Genesis 42 in the NBVTP

Genesis 42 in the NET2

Genesis 42 in the NIV11

Genesis 42 in the NNT

Genesis 42 in the NNT2

Genesis 42 in the NNT3

Genesis 42 in the PDDPT

Genesis 42 in the PFNT

Genesis 42 in the RMNT

Genesis 42 in the SBIAS

Genesis 42 in the SBIBS

Genesis 42 in the SBIBS2

Genesis 42 in the SBICS

Genesis 42 in the SBIDS

Genesis 42 in the SBIGS

Genesis 42 in the SBIHS

Genesis 42 in the SBIIS

Genesis 42 in the SBIIS2

Genesis 42 in the SBIIS3

Genesis 42 in the SBIKS

Genesis 42 in the SBIKS2

Genesis 42 in the SBIMS

Genesis 42 in the SBIOS

Genesis 42 in the SBIPS

Genesis 42 in the SBISS

Genesis 42 in the SBITS

Genesis 42 in the SBITS2

Genesis 42 in the SBITS3

Genesis 42 in the SBITS4

Genesis 42 in the SBIUS

Genesis 42 in the SBIVS

Genesis 42 in the SBT

Genesis 42 in the SBT1E

Genesis 42 in the SCHL

Genesis 42 in the SNT

Genesis 42 in the SUSU

Genesis 42 in the SUSU2

Genesis 42 in the SYNO

Genesis 42 in the TBIAOTANT

Genesis 42 in the TBT1E

Genesis 42 in the TBT1E2

Genesis 42 in the TFTIP

Genesis 42 in the TFTU

Genesis 42 in the TGNTATF3T

Genesis 42 in the THAI

Genesis 42 in the TNFD

Genesis 42 in the TNT

Genesis 42 in the TNTIK

Genesis 42 in the TNTIL

Genesis 42 in the TNTIN

Genesis 42 in the TNTIP

Genesis 42 in the TNTIZ

Genesis 42 in the TOMA

Genesis 42 in the TTENT

Genesis 42 in the UBG

Genesis 42 in the UGV

Genesis 42 in the UGV2

Genesis 42 in the UGV3

Genesis 42 in the VBL

Genesis 42 in the VDCC

Genesis 42 in the YALU

Genesis 42 in the YAPE

Genesis 42 in the YBVTP

Genesis 42 in the ZBP