Judges 7 (BOKCV)

1 Ndipo Yerub-Baali (yaani Gideoni) na lile jeshi lililokuwa pamoja naye, wakaondoka asubuhi na mapema na kupiga kambi kando ya chemchemi ya Harodi. Kambi ya Wamidiani ilikuwa kaskazini yao katika bonde karibu na kilima cha More. 2 BWANA akamwambia Gideoni, “Jeshi lililo pamoja nawe ni kubwa sana kwa mimi kuwatia Wamidiani mikononi mwao. Ili kwamba Israeli asije akajisifu juu yangu akisema, ‘Mkono wangu ndio ulioniokoa, 3 kwa hiyo sasa tangaza jeshi lote likiwa linasikia, kwamba: Yeyote anayeogopa na kutetemeka, yeye na arudi nyumbani, aondoke katika Mlima Gileadi.’ ” Hivyo watu 22,000 walirudi, wakabaki 10,000. 4 Lakini BWANA akamwambia Gideoni, “Idadi ya jeshi bado ni kubwa. Wapeleke chini katika maji nami nitawajaribu huko kwa ajili yako. Kama nikikuambia, ‘Huyu atakwenda pamoja nawe,’ yeye atakwenda; lakini kama nikisema, ‘Huyu hatakwenda pamoja nawe,’ yeye hatakwenda.” 5 Hivyo Gideoni akalileta lile jeshi chini kwenye maji naye BWANA akamwambia Gideoni, “Watenge upande mmoja wale wote wanywao maji kwa ulimi, kama vile mbwa anywavyo, wale wote wapigao magoti ili kunywa wakipeleka mikono yao vinywani mwao, waweke upande mwingine.” 6 Idadi ya wale waliokunywa kwa kuramba ramba walikuwa 300, lakini wengine wote katika jeshi walipiga magoti ili kunywa. 7 BWANA akamwambia Gideoni, “Kwa hao watu 300 walioramba maji nitawaokoa ninyi, nami nitawatia Wamidiani mkononi mwako. Waache hao watu wengine wote warudi kila mmoja nyumbani mwake.” 8 Hivyo Gideoni akawaacha wale Waisraeli wengine kila mmoja aende kwenye hema yake. Akabakia na wale 300, ambao walichukua vyakula na tarumbeta za wale wenzao.Basi kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake bondeni. 9 Usiku ule ule BWANA akamwambia Gideoni, “Ondoka, ushuke kambini, kwa kuwa nimeitia mkononi mwako. 10 Lakini kama unaogopa kushambulia, shuka kambini pamoja na mtumishi wako Pura, 11 nawe sikiliza wanayosema. Hatimaye, utatiwa moyo kushambulia kambi.” Basi yeye na Pura mtumishi wake wakashuka na kufikia walinzi wa mbele wenye silaha waliokuwa mle kambini. 12 Wamidiani, Waamaleki na mataifa mengine yote ya mashariki walikaa bondeni, nao walikuwa mfano wa nzige kwa wingi wao. Ngamia zao hazikuhesabika, wingi wao ulikuwa kama mchanga wa ufuoni mwa bahari. 13 Gideoni alifika wakati huo huo kukiwa na mtu mmoja aliyekuwa anamweleza mwenzake ndoto yake, akisema, “Niliota ndoto: Tazama mkate wa shayiri ulioviringana ulianguka katika kambi moja ya Wamidiani, ukaipiga na ikaanguka nao ukaipindua juu chini na hema ikaporomoka chini.” 14 Rafiki yake akamjibu, “Habari hii si kitu kingine zaidi ya upanga wa Gideoni mwana wa Yoashi, Mwisraeli. Mungu amewatia Wamidiani na jeshi lote mkononi mwake.” 15 Gideoni alipoisikia hiyo ndoto na tafsiri yake, akamwabudu Mungu. Akarudi kwenye kambi ya Israeli na kusema, “Inukeni! BWANA amelitia jeshi la Wamidiani mikononi mwenu.” 16 Akawagawa wale watu 300 katika makundi matatu, akawakabidhi tarumbeta mikononi mwao wote na mitungi isiyokuwa na maji yenye mienge ndani yake. 17 Akawaambia, “Nitazameni, fanyeni kama nitakavyofanya, nitakapofika mwisho wa kambi mfanye kama nitakavyofanya. 18 Wakati mimi na wale walio pamoja nami wote, tutakapopiga tarumbeta zetu, ninyi nanyi pigeni tarumbeta pande zote za kambi na mpige kelele, mseme, ‘Upanga wa BWANA na wa Gideoni.’ ” 19 Gideoni na wale watu 100 waliokuwa pamoja naye wakafika mwisho wa kambi usiku mwanzoni mwa zamu ya kati, mara tu walipokuwa wamebadili zamu. Wakapiga zile tarumbeta zao na kuvunja ile mitungi iliyokuwa mikononi mwao. 20 Yale makundi matatu yakapiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Wakashika mienge kwa mikono yao ya kushoto na katika mikono yao ya kuume tarumbeta ili kuzipiga, wakapaza sauti zao, “Upanga wa BWANA na wa Gideoni!” 21 Wakasimama kila mtu mahali pake kuizunguka kambi pande zote, Wamidiani wote wakakimbia, huku wakipiga kelele. 22 Walipozipiga zile tarumbeta 300, BWANA akafanya watu katika kambi yote kugeuziana upanga kila mmoja na mwenziwe. Jeshi likakimbia mpaka Beth-Shita kuelekea Serera hadi mpakani mwa Abel-Mehola karibu na Tabathi. 23 Watu wa Israeli wakaitwa kutoka Naftali, Asheri na Manase, wakawafuatia Wamidiani. 24 Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima vya Efraimu akisema, “Teremkeni dhidi ya Wamidiani na mkazuie vivuko vya maji mbele yao hadi Beth-Bara na pia Yordani.”Hivyo watu wote wa Efraimu wakakutanika pamoja na kuzingira mto wa Yordani hadi Beth-Bara. 25 Wakawakamata wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu. Wakamuulia Orebu pale penye mwamba wa Orebu, na Zeebu wakamuulia penye shinikizo la kukamulia divai la Zeebu. Wakawafuatia Wamidiani na kuleta vichwa vya Orebu na Zeebu kwa Gideoni, huko ngʼambo ya Yordani.

In Other Versions

Judges 7 in the ANGEFD

Judges 7 in the ANTPNG2D

Judges 7 in the AS21

Judges 7 in the BAGH

Judges 7 in the BBPNG

Judges 7 in the BBT1E

Judges 7 in the BDS

Judges 7 in the BEV

Judges 7 in the BHAD

Judges 7 in the BIB

Judges 7 in the BLPT

Judges 7 in the BNT

Judges 7 in the BNTABOOT

Judges 7 in the BNTLV

Judges 7 in the BOATCB

Judges 7 in the BOATCB2

Judges 7 in the BOBCV

Judges 7 in the BOCNT

Judges 7 in the BOECS

Judges 7 in the BOGWICC

Judges 7 in the BOHCB

Judges 7 in the BOHCV

Judges 7 in the BOHLNT

Judges 7 in the BOHNTLTAL

Judges 7 in the BOICB

Judges 7 in the BOILNTAP

Judges 7 in the BOITCV

Judges 7 in the BOKCV2

Judges 7 in the BOKHWOG

Judges 7 in the BOKSSV

Judges 7 in the BOLCB

Judges 7 in the BOLCB2

Judges 7 in the BOMCV

Judges 7 in the BONAV

Judges 7 in the BONCB

Judges 7 in the BONLT

Judges 7 in the BONUT2

Judges 7 in the BOPLNT

Judges 7 in the BOSCB

Judges 7 in the BOSNC

Judges 7 in the BOTLNT

Judges 7 in the BOVCB

Judges 7 in the BOYCB

Judges 7 in the BPBB

Judges 7 in the BPH

Judges 7 in the BSB

Judges 7 in the CCB

Judges 7 in the CUV

Judges 7 in the CUVS

Judges 7 in the DBT

Judges 7 in the DGDNT

Judges 7 in the DHNT

Judges 7 in the DNT

Judges 7 in the ELBE

Judges 7 in the EMTV

Judges 7 in the ESV

Judges 7 in the FBV

Judges 7 in the FEB

Judges 7 in the GGMNT

Judges 7 in the GNT

Judges 7 in the HARY

Judges 7 in the HNT

Judges 7 in the IRVA

Judges 7 in the IRVB

Judges 7 in the IRVG

Judges 7 in the IRVH

Judges 7 in the IRVK

Judges 7 in the IRVM

Judges 7 in the IRVM2

Judges 7 in the IRVO

Judges 7 in the IRVP

Judges 7 in the IRVT

Judges 7 in the IRVT2

Judges 7 in the IRVU

Judges 7 in the ISVN

Judges 7 in the JSNT

Judges 7 in the KAPI

Judges 7 in the KBT1ETNIK

Judges 7 in the KBV

Judges 7 in the KJV

Judges 7 in the KNFD

Judges 7 in the LBA

Judges 7 in the LBLA

Judges 7 in the LNT

Judges 7 in the LSV

Judges 7 in the MAAL

Judges 7 in the MBV

Judges 7 in the MBV2

Judges 7 in the MHNT

Judges 7 in the MKNFD

Judges 7 in the MNG

Judges 7 in the MNT

Judges 7 in the MNT2

Judges 7 in the MRS1T

Judges 7 in the NAA

Judges 7 in the NASB

Judges 7 in the NBLA

Judges 7 in the NBS

Judges 7 in the NBVTP

Judges 7 in the NET2

Judges 7 in the NIV11

Judges 7 in the NNT

Judges 7 in the NNT2

Judges 7 in the NNT3

Judges 7 in the PDDPT

Judges 7 in the PFNT

Judges 7 in the RMNT

Judges 7 in the SBIAS

Judges 7 in the SBIBS

Judges 7 in the SBIBS2

Judges 7 in the SBICS

Judges 7 in the SBIDS

Judges 7 in the SBIGS

Judges 7 in the SBIHS

Judges 7 in the SBIIS

Judges 7 in the SBIIS2

Judges 7 in the SBIIS3

Judges 7 in the SBIKS

Judges 7 in the SBIKS2

Judges 7 in the SBIMS

Judges 7 in the SBIOS

Judges 7 in the SBIPS

Judges 7 in the SBISS

Judges 7 in the SBITS

Judges 7 in the SBITS2

Judges 7 in the SBITS3

Judges 7 in the SBITS4

Judges 7 in the SBIUS

Judges 7 in the SBIVS

Judges 7 in the SBT

Judges 7 in the SBT1E

Judges 7 in the SCHL

Judges 7 in the SNT

Judges 7 in the SUSU

Judges 7 in the SUSU2

Judges 7 in the SYNO

Judges 7 in the TBIAOTANT

Judges 7 in the TBT1E

Judges 7 in the TBT1E2

Judges 7 in the TFTIP

Judges 7 in the TFTU

Judges 7 in the TGNTATF3T

Judges 7 in the THAI

Judges 7 in the TNFD

Judges 7 in the TNT

Judges 7 in the TNTIK

Judges 7 in the TNTIL

Judges 7 in the TNTIN

Judges 7 in the TNTIP

Judges 7 in the TNTIZ

Judges 7 in the TOMA

Judges 7 in the TTENT

Judges 7 in the UBG

Judges 7 in the UGV

Judges 7 in the UGV2

Judges 7 in the UGV3

Judges 7 in the VBL

Judges 7 in the VDCC

Judges 7 in the YALU

Judges 7 in the YAPE

Judges 7 in the YBVTP

Judges 7 in the ZBP