Psalms 122 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 1 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,“Twende nyumbani ya BWANA.” 2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimamamalangoni mwako. 3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mjiambao umeshikamanishwa pamoja. 4 Huko ndiko makabila hukwea,makabila ya BWANA,kulisifu jina la BWANA kulingana na maagizowaliopewa Israeli. 5 Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa,viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. 6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:“Wote wakupendao na wawe salama. 7 Amani na iwepo ndani ya kuta zakona usalama ndani ya ngome zako.” 8 Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki,nitasema, “Amani iwe ndani yako.” 9 Kwa ajili ya nyumba ya BWANA Mungu wetu,nitatafuta mafanikio yako.