Psalms 134 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. 1 Msifuni BWANA, ninyi nyote watumishi wa BWANA,ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya BWANA. 2 Inueni mikono yenu katika pale patakatifuna kumsifu BWANA. 3 Naye BWANA, Muumba wa mbingu na dunia,awabariki kutoka Sayuni.