1 Chronicles 27 (BOKCV)

1 Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000. 2 Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake. 3 Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza. 4 Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 5 Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000. 6 Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye alikuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake. 7 Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 8 Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 9 Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 10 Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 11 Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 12 Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 13 Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 14 Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 15 Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. 16 Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa: Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri;kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka; 17 kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli;kwa Aroni: Sadoki; 18 kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi;kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli; 19 kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia;kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli; 20 kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia;kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya; 21 kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri; 22 kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli. 23 Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu BWANA alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. 24 Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi. 25 Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme.Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia. 26 Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba. 27 Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu.Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa. 28 Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi.Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni. 29 Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa makundi ya ngʼombe waliojilisha huko Sharoni.Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ngʼombe yaliyokuwa makondeni. 30 Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia.Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda. 31 Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi. 32 Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme. 33 Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme. 34 Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari.Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.

In Other Versions

1 Chronicles 27 in the ANGEFD

1 Chronicles 27 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 27 in the AS21

1 Chronicles 27 in the BAGH

1 Chronicles 27 in the BBPNG

1 Chronicles 27 in the BBT1E

1 Chronicles 27 in the BDS

1 Chronicles 27 in the BEV

1 Chronicles 27 in the BHAD

1 Chronicles 27 in the BIB

1 Chronicles 27 in the BLPT

1 Chronicles 27 in the BNT

1 Chronicles 27 in the BNTABOOT

1 Chronicles 27 in the BNTLV

1 Chronicles 27 in the BOATCB

1 Chronicles 27 in the BOATCB2

1 Chronicles 27 in the BOBCV

1 Chronicles 27 in the BOCNT

1 Chronicles 27 in the BOECS

1 Chronicles 27 in the BOGWICC

1 Chronicles 27 in the BOHCB

1 Chronicles 27 in the BOHCV

1 Chronicles 27 in the BOHLNT

1 Chronicles 27 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 27 in the BOICB

1 Chronicles 27 in the BOILNTAP

1 Chronicles 27 in the BOITCV

1 Chronicles 27 in the BOKCV2

1 Chronicles 27 in the BOKHWOG

1 Chronicles 27 in the BOKSSV

1 Chronicles 27 in the BOLCB

1 Chronicles 27 in the BOLCB2

1 Chronicles 27 in the BOMCV

1 Chronicles 27 in the BONAV

1 Chronicles 27 in the BONCB

1 Chronicles 27 in the BONLT

1 Chronicles 27 in the BONUT2

1 Chronicles 27 in the BOPLNT

1 Chronicles 27 in the BOSCB

1 Chronicles 27 in the BOSNC

1 Chronicles 27 in the BOTLNT

1 Chronicles 27 in the BOVCB

1 Chronicles 27 in the BOYCB

1 Chronicles 27 in the BPBB

1 Chronicles 27 in the BPH

1 Chronicles 27 in the BSB

1 Chronicles 27 in the CCB

1 Chronicles 27 in the CUV

1 Chronicles 27 in the CUVS

1 Chronicles 27 in the DBT

1 Chronicles 27 in the DGDNT

1 Chronicles 27 in the DHNT

1 Chronicles 27 in the DNT

1 Chronicles 27 in the ELBE

1 Chronicles 27 in the EMTV

1 Chronicles 27 in the ESV

1 Chronicles 27 in the FBV

1 Chronicles 27 in the FEB

1 Chronicles 27 in the GGMNT

1 Chronicles 27 in the GNT

1 Chronicles 27 in the HARY

1 Chronicles 27 in the HNT

1 Chronicles 27 in the IRVA

1 Chronicles 27 in the IRVB

1 Chronicles 27 in the IRVG

1 Chronicles 27 in the IRVH

1 Chronicles 27 in the IRVK

1 Chronicles 27 in the IRVM

1 Chronicles 27 in the IRVM2

1 Chronicles 27 in the IRVO

1 Chronicles 27 in the IRVP

1 Chronicles 27 in the IRVT

1 Chronicles 27 in the IRVT2

1 Chronicles 27 in the IRVU

1 Chronicles 27 in the ISVN

1 Chronicles 27 in the JSNT

1 Chronicles 27 in the KAPI

1 Chronicles 27 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 27 in the KBV

1 Chronicles 27 in the KJV

1 Chronicles 27 in the KNFD

1 Chronicles 27 in the LBA

1 Chronicles 27 in the LBLA

1 Chronicles 27 in the LNT

1 Chronicles 27 in the LSV

1 Chronicles 27 in the MAAL

1 Chronicles 27 in the MBV

1 Chronicles 27 in the MBV2

1 Chronicles 27 in the MHNT

1 Chronicles 27 in the MKNFD

1 Chronicles 27 in the MNG

1 Chronicles 27 in the MNT

1 Chronicles 27 in the MNT2

1 Chronicles 27 in the MRS1T

1 Chronicles 27 in the NAA

1 Chronicles 27 in the NASB

1 Chronicles 27 in the NBLA

1 Chronicles 27 in the NBS

1 Chronicles 27 in the NBVTP

1 Chronicles 27 in the NET2

1 Chronicles 27 in the NIV11

1 Chronicles 27 in the NNT

1 Chronicles 27 in the NNT2

1 Chronicles 27 in the NNT3

1 Chronicles 27 in the PDDPT

1 Chronicles 27 in the PFNT

1 Chronicles 27 in the RMNT

1 Chronicles 27 in the SBIAS

1 Chronicles 27 in the SBIBS

1 Chronicles 27 in the SBIBS2

1 Chronicles 27 in the SBICS

1 Chronicles 27 in the SBIDS

1 Chronicles 27 in the SBIGS

1 Chronicles 27 in the SBIHS

1 Chronicles 27 in the SBIIS

1 Chronicles 27 in the SBIIS2

1 Chronicles 27 in the SBIIS3

1 Chronicles 27 in the SBIKS

1 Chronicles 27 in the SBIKS2

1 Chronicles 27 in the SBIMS

1 Chronicles 27 in the SBIOS

1 Chronicles 27 in the SBIPS

1 Chronicles 27 in the SBISS

1 Chronicles 27 in the SBITS

1 Chronicles 27 in the SBITS2

1 Chronicles 27 in the SBITS3

1 Chronicles 27 in the SBITS4

1 Chronicles 27 in the SBIUS

1 Chronicles 27 in the SBIVS

1 Chronicles 27 in the SBT

1 Chronicles 27 in the SBT1E

1 Chronicles 27 in the SCHL

1 Chronicles 27 in the SNT

1 Chronicles 27 in the SUSU

1 Chronicles 27 in the SUSU2

1 Chronicles 27 in the SYNO

1 Chronicles 27 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 27 in the TBT1E

1 Chronicles 27 in the TBT1E2

1 Chronicles 27 in the TFTIP

1 Chronicles 27 in the TFTU

1 Chronicles 27 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 27 in the THAI

1 Chronicles 27 in the TNFD

1 Chronicles 27 in the TNT

1 Chronicles 27 in the TNTIK

1 Chronicles 27 in the TNTIL

1 Chronicles 27 in the TNTIN

1 Chronicles 27 in the TNTIP

1 Chronicles 27 in the TNTIZ

1 Chronicles 27 in the TOMA

1 Chronicles 27 in the TTENT

1 Chronicles 27 in the UBG

1 Chronicles 27 in the UGV

1 Chronicles 27 in the UGV2

1 Chronicles 27 in the UGV3

1 Chronicles 27 in the VBL

1 Chronicles 27 in the VDCC

1 Chronicles 27 in the YALU

1 Chronicles 27 in the YAPE

1 Chronicles 27 in the YBVTP

1 Chronicles 27 in the ZBP