1 Corinthians 7 (BOKCV)

1 Basi kuhusu mambo yale mliyoyaandika: Ni vyema mwanaume asimguse mwanamke. 2 Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. 3 Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe. 4 Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe. 5 Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi. 6 Nasema haya kama ushauri na si amri. 7 Laiti watu wangekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa kipawa chake kutoka kwa Mungu, mmoja ana kipawa cha namna hii na mwingine ana cha namna ile. 8 Kwa wale wasiooa na kwa wajane, nasema hivi, ingekuwa vizuri wasioe. 9 Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa. 10 Kwa wale waliooana nawapa amri (si mimi ila ni Bwana): Mke asitengane na mumewe. 11 Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka. 12 Lakini kwa wengine nasema (si Bwana ila ni mimi): Kama ndugu ana mke asiyeamini, naye huyo mke anakubali kuishi pamoja naye, basi asimwache. 13 Naye mwanamke aaminiye kama ameolewa na mwanaume asiyeamini na huyo mume anakubali kuishi naye, basi huyo mwanamke asimwache. 14 Kwa maana huyo mume asiyeamini anatakaswa kupitia mkewe, naye mke asiyeamini anatakaswa kupitia mumewe anayeamini. Kama isingalikuwa hivyo watoto wenu wangalikuwa si safi, lakini ilivyo sasa wao ni watakatifu. 15 Lakini kama yule asiyeamini akijitenga, basi afanye hivyo. Katika hali kama hiyo mwanamke au mwanaume aaminiye hafungwi, kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani. 16 Wewe mke, unajuaje kama utamwokoa mumeo? Au wewe mume unajuaje kama utamwokoa mkeo? 17 Lakini kila mtu na aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, yale Mungu aliyomwitia. Hii ni sheria ninayoiweka kwa makanisa yote. 18 Je, mtu alikuwa tayari ametahiriwa alipoitwa? Asijifanye asiyetahiriwa. Je, mtu alikuwa hajatahiriwa alipoitwa? Asitahiriwe. 19 Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu. Lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu. 20 Basi kila mmoja wenu na abaki katika hali aliyoitwa nayo. 21 Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Ingawaje unaweza kupata uhuru, tumia nafasi uliyo nayo sasa kuliko wakati mwingine wowote. 22 Kwa maana yeyote aliyeitwa katika Bwana akiwa mtumwa yeye ni mtu huru kwa Bwana, kama vile yeyote aliyekuwa huru alipoitwa yeye ni mtumwa wa Kristo. 23 Mlinunuliwa kwa gharama; msiwe watumwa wa wanadamu. 24 Ndugu zangu, kama kila mtu alivyoitwa, akae katika wito wake alioitiwa na Mungu. 25 Basi, kuhusu wale walio bikira, mimi sina amri kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa shauri kama mtu ambaye ni mwaminifu kwa rehema za Bwana. 26 Kwa sababu ya shida iliyoko kwa sasa, naona ni vyema mkibaki kama mlivyo. 27 Je, umeolewa? Basi usitake talaka. Je, hujaoa? Usitafute mke. 28 Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa, hajatenda dhambi. Lakini wale wanaooa watakabiliana na matatizo mengi katika maisha haya, nami nataka kuwazuilia hayo. 29 Lakini ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa wale waliooa waishi kama wasio na wake; 30 nao wanaoomboleza, kama ambao hawaombolezi; wenye furaha kama wasiokuwa nayo; wale wanaonunua, kama vile vitu walivyonunua si mali yao; 31 nao wale wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama ambao hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inapita. 32 Ningetaka msiwe na masumbufu. Mwanaume ambaye hajaoa anajishughulisha na mambo ya Bwana, jinsi ya kumpendeza Bwana. 33 Lakini mwanaume aliyeoa anajishughulisha na mambo ya dunia, jinsi ya kumfurahisha mkewe, 34 na mawazo yake yamegawanyika. Mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana: lengo lake ni awe mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini yule aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyoweza kumfurahisha mumewe. 35 Ninasema haya kwa faida yenu wenyewe, sio ili kuwawekea vizuizi bali mpate kuishi kwa jinsi ilivyo vyema bila kuvutwa pengine katika kujitoa kwenu kwa Bwana. 36 Kama mtu yeyote anadhani kwamba hamtendei ilivyo sawa mwanamwali ambaye amemposa, naye akiwa umri wake unazidi kuendelea na mtu huyo anajisikia kwamba inampasa kuoa, afanye kama atakavyo. Yeye hatendi dhambi. Yawapasa waoane. 37 Lakini mwanaume ambaye ameamua moyoni mwake kutooa bila kulazimishwa na mtu yeyote, bali anaweza kuzitawala tamaa zake kutomwoa huyo mwanamwali, basi anafanya ipasavyo. 38 Hivyo basi, mwanaume amwoaye mwanamwali afanya vyema, lakini yeye asiyemwoa afanya vyema zaidi. 39 Mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria maadamu mumewe yu hai. Lakini mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, lakini lazima awe katika Bwana. 40 Lakini kwa maoni yangu, angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo. Nami nadhani pia nina Roho wa Mungu.

In Other Versions

1 Corinthians 7 in the ANGEFD

1 Corinthians 7 in the ANTPNG2D

1 Corinthians 7 in the AS21

1 Corinthians 7 in the BAGH

1 Corinthians 7 in the BBPNG

1 Corinthians 7 in the BBT1E

1 Corinthians 7 in the BDS

1 Corinthians 7 in the BEV

1 Corinthians 7 in the BHAD

1 Corinthians 7 in the BIB

1 Corinthians 7 in the BLPT

1 Corinthians 7 in the BNT

1 Corinthians 7 in the BNTABOOT

1 Corinthians 7 in the BNTLV

1 Corinthians 7 in the BOATCB

1 Corinthians 7 in the BOATCB2

1 Corinthians 7 in the BOBCV

1 Corinthians 7 in the BOCNT

1 Corinthians 7 in the BOECS

1 Corinthians 7 in the BOGWICC

1 Corinthians 7 in the BOHCB

1 Corinthians 7 in the BOHCV

1 Corinthians 7 in the BOHLNT

1 Corinthians 7 in the BOHNTLTAL

1 Corinthians 7 in the BOICB

1 Corinthians 7 in the BOILNTAP

1 Corinthians 7 in the BOITCV

1 Corinthians 7 in the BOKCV2

1 Corinthians 7 in the BOKHWOG

1 Corinthians 7 in the BOKSSV

1 Corinthians 7 in the BOLCB

1 Corinthians 7 in the BOLCB2

1 Corinthians 7 in the BOMCV

1 Corinthians 7 in the BONAV

1 Corinthians 7 in the BONCB

1 Corinthians 7 in the BONLT

1 Corinthians 7 in the BONUT2

1 Corinthians 7 in the BOPLNT

1 Corinthians 7 in the BOSCB

1 Corinthians 7 in the BOSNC

1 Corinthians 7 in the BOTLNT

1 Corinthians 7 in the BOVCB

1 Corinthians 7 in the BOYCB

1 Corinthians 7 in the BPBB

1 Corinthians 7 in the BPH

1 Corinthians 7 in the BSB

1 Corinthians 7 in the CCB

1 Corinthians 7 in the CUV

1 Corinthians 7 in the CUVS

1 Corinthians 7 in the DBT

1 Corinthians 7 in the DGDNT

1 Corinthians 7 in the DHNT

1 Corinthians 7 in the DNT

1 Corinthians 7 in the ELBE

1 Corinthians 7 in the EMTV

1 Corinthians 7 in the ESV

1 Corinthians 7 in the FBV

1 Corinthians 7 in the FEB

1 Corinthians 7 in the GGMNT

1 Corinthians 7 in the GNT

1 Corinthians 7 in the HARY

1 Corinthians 7 in the HNT

1 Corinthians 7 in the IRVA

1 Corinthians 7 in the IRVB

1 Corinthians 7 in the IRVG

1 Corinthians 7 in the IRVH

1 Corinthians 7 in the IRVK

1 Corinthians 7 in the IRVM

1 Corinthians 7 in the IRVM2

1 Corinthians 7 in the IRVO

1 Corinthians 7 in the IRVP

1 Corinthians 7 in the IRVT

1 Corinthians 7 in the IRVT2

1 Corinthians 7 in the IRVU

1 Corinthians 7 in the ISVN

1 Corinthians 7 in the JSNT

1 Corinthians 7 in the KAPI

1 Corinthians 7 in the KBT1ETNIK

1 Corinthians 7 in the KBV

1 Corinthians 7 in the KJV

1 Corinthians 7 in the KNFD

1 Corinthians 7 in the LBA

1 Corinthians 7 in the LBLA

1 Corinthians 7 in the LNT

1 Corinthians 7 in the LSV

1 Corinthians 7 in the MAAL

1 Corinthians 7 in the MBV

1 Corinthians 7 in the MBV2

1 Corinthians 7 in the MHNT

1 Corinthians 7 in the MKNFD

1 Corinthians 7 in the MNG

1 Corinthians 7 in the MNT

1 Corinthians 7 in the MNT2

1 Corinthians 7 in the MRS1T

1 Corinthians 7 in the NAA

1 Corinthians 7 in the NASB

1 Corinthians 7 in the NBLA

1 Corinthians 7 in the NBS

1 Corinthians 7 in the NBVTP

1 Corinthians 7 in the NET2

1 Corinthians 7 in the NIV11

1 Corinthians 7 in the NNT

1 Corinthians 7 in the NNT2

1 Corinthians 7 in the NNT3

1 Corinthians 7 in the PDDPT

1 Corinthians 7 in the PFNT

1 Corinthians 7 in the RMNT

1 Corinthians 7 in the SBIAS

1 Corinthians 7 in the SBIBS

1 Corinthians 7 in the SBIBS2

1 Corinthians 7 in the SBICS

1 Corinthians 7 in the SBIDS

1 Corinthians 7 in the SBIGS

1 Corinthians 7 in the SBIHS

1 Corinthians 7 in the SBIIS

1 Corinthians 7 in the SBIIS2

1 Corinthians 7 in the SBIIS3

1 Corinthians 7 in the SBIKS

1 Corinthians 7 in the SBIKS2

1 Corinthians 7 in the SBIMS

1 Corinthians 7 in the SBIOS

1 Corinthians 7 in the SBIPS

1 Corinthians 7 in the SBISS

1 Corinthians 7 in the SBITS

1 Corinthians 7 in the SBITS2

1 Corinthians 7 in the SBITS3

1 Corinthians 7 in the SBITS4

1 Corinthians 7 in the SBIUS

1 Corinthians 7 in the SBIVS

1 Corinthians 7 in the SBT

1 Corinthians 7 in the SBT1E

1 Corinthians 7 in the SCHL

1 Corinthians 7 in the SNT

1 Corinthians 7 in the SUSU

1 Corinthians 7 in the SUSU2

1 Corinthians 7 in the SYNO

1 Corinthians 7 in the TBIAOTANT

1 Corinthians 7 in the TBT1E

1 Corinthians 7 in the TBT1E2

1 Corinthians 7 in the TFTIP

1 Corinthians 7 in the TFTU

1 Corinthians 7 in the TGNTATF3T

1 Corinthians 7 in the THAI

1 Corinthians 7 in the TNFD

1 Corinthians 7 in the TNT

1 Corinthians 7 in the TNTIK

1 Corinthians 7 in the TNTIL

1 Corinthians 7 in the TNTIN

1 Corinthians 7 in the TNTIP

1 Corinthians 7 in the TNTIZ

1 Corinthians 7 in the TOMA

1 Corinthians 7 in the TTENT

1 Corinthians 7 in the UBG

1 Corinthians 7 in the UGV

1 Corinthians 7 in the UGV2

1 Corinthians 7 in the UGV3

1 Corinthians 7 in the VBL

1 Corinthians 7 in the VDCC

1 Corinthians 7 in the YALU

1 Corinthians 7 in the YAPE

1 Corinthians 7 in the YBVTP

1 Corinthians 7 in the ZBP