1 Samuel 24 (BOKCV)
1 Baada ya Sauli kurudi kuwafuatia Wafilisti, akaambiwa kwamba, “Daudi yuko katika Jangwa la En-Gedi.” 2 Basi Sauli akachukua watu hodari 3,000 kutoka Israeli yote kwenda kumsaka Daudi na watu wake karibu na Majabali ya Mbuzi-Mwitu. 3 Akaja mpaka kwenye mazizi ya kondoo kando ya njia, hapo palikuwa na pango, na Sauli akaingia ndani kujipumzisha. Daudi na watu wake walikuwa wamo mle pangoni kwa ndani zaidi. 4 Watu wa Daudi wakasema, “Hii ndiyo siku aliyonena BWANA akikuambia, ‘Nitamtia adui yako mikononi mwako ili wewe umtendee utakavyo.’ ” Basi Daudi akanyemelea bila kuonekana na kukata upindo wa joho la Sauli. 5 Baada ya hilo, dhamiri ya Daudi ikataabika kwa kukata upindo wa joho la Sauli. 6 Akawaambia watu wake, “BWANA na apishie mbali nisije nikafanya jambo kama hilo kwa bwana wangu, yeye ambaye ni mpakwa mafuta wa BWANA, au kuinua mkono wangu dhidi yake; kwani yeye ni mpakwa mafuta wa BWANA.” 7 Kwa maneno haya Daudi akawaonya watu wake na hakuwaruhusu wamshambulie Sauli. Naye Sauli akaondoka pangoni na kwenda zake. 8 Ndipo Daudi naye akatoka pangoni na kumwita Sauli akisema, “Mfalme, bwana wangu!” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama na kusujudu uso wake mpaka nchi. 9 Akamwambia Sauli, “Kwa nini unasikiliza wakati watu wanapokuambia, ‘Daudi amenuia kukudhuru’? 10 Leo umeona kwa macho yako mwenyewe jinsi BWANA alivyokutia mikononi mwangu huko pangoni. Watu wengine walisisitiza nikuue, lakini nilikuacha, nikisema, ‘Sitainua mkono wangu dhidi ya bwana wangu, kwa sababu yeye ni mpakwa mafuta wa BWANA.’ 11 Tazama, baba yangu, ona kipande hiki cha joho lako mkononi mwangu! Nilikata upindo wa joho lako lakini sikukuua. Basi ujue na kutambua kuwa sina hatia ya kutenda mabaya wala ya kuasi. Wewe sijakukosea, lakini wewe unaniwinda mimi ili kuuondoa uhai wangu. 12 BWANA na ahukumu kati yangu na wewe. Naye BWANA alipize mabaya unayonitendea, lakini mkono wangu hautakugusa. 13 Kama msemo wa kale usemavyo, ‘Kutoka kwa watenda maovu hutoka matendo maovu,’ kwa hiyo mkono wangu hautakugusa wewe. 14 “Je, mfalme wa Israeli ametoka dhidi ya nani? Ni nani unayemfuatia? Je, ni mbwa mfu? Ni kiroboto? 15 BWANA na awe mwamuzi wetu, yeye na aamue kati yetu. Yeye na anitetee shauri langu; anihesabie haki kwa kuniokoa mkononi mwako.” 16 Daudi alipomaliza kusema haya, Sauli akamuuliza, “Je, hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?” Ndipo Sauli akalia kwa sauti kuu, akisema, 17 “Wewe ni mwenye haki kuliko mimi; umenitendea mema, lakini mimi nimekutendea mabaya. 18 Sasa umeniambia juu ya mema uliyonitendea. BWANA alinitia mikononi mwako, lakini wewe hukuniua. 19 Je, mtu ampatapo adui yake, humwacha aende zake bila kumdhuru? BWANA na akulipe mema kwa jinsi ulivyonitenda leo. 20 Ninajua kwamba hakika utakuwa mfalme na ya kwamba ufalme wa Israeli utakuwa imara mikononi mwako. 21 Sasa niapie kwa BWANA kwamba hutakatilia mbali uzao wangu wala kulifuta jina langu kutoka jamaa ya baba yangu.” 22 Basi Daudi akamwapia Sauli. Kisha Sauli akarudi zake nyumbani, lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.
In Other Versions
1 Samuel 24 in the ANGEFD
1 Samuel 24 in the ANTPNG2D
1 Samuel 24 in the AS21
1 Samuel 24 in the BAGH
1 Samuel 24 in the BBPNG
1 Samuel 24 in the BBT1E
1 Samuel 24 in the BDS
1 Samuel 24 in the BEV
1 Samuel 24 in the BHAD
1 Samuel 24 in the BIB
1 Samuel 24 in the BLPT
1 Samuel 24 in the BNT
1 Samuel 24 in the BNTABOOT
1 Samuel 24 in the BNTLV
1 Samuel 24 in the BOATCB
1 Samuel 24 in the BOATCB2
1 Samuel 24 in the BOBCV
1 Samuel 24 in the BOCNT
1 Samuel 24 in the BOECS
1 Samuel 24 in the BOGWICC
1 Samuel 24 in the BOHCB
1 Samuel 24 in the BOHCV
1 Samuel 24 in the BOHLNT
1 Samuel 24 in the BOHNTLTAL
1 Samuel 24 in the BOICB
1 Samuel 24 in the BOILNTAP
1 Samuel 24 in the BOITCV
1 Samuel 24 in the BOKCV2
1 Samuel 24 in the BOKHWOG
1 Samuel 24 in the BOKSSV
1 Samuel 24 in the BOLCB
1 Samuel 24 in the BOLCB2
1 Samuel 24 in the BOMCV
1 Samuel 24 in the BONAV
1 Samuel 24 in the BONCB
1 Samuel 24 in the BONLT
1 Samuel 24 in the BONUT2
1 Samuel 24 in the BOPLNT
1 Samuel 24 in the BOSCB
1 Samuel 24 in the BOSNC
1 Samuel 24 in the BOTLNT
1 Samuel 24 in the BOVCB
1 Samuel 24 in the BOYCB
1 Samuel 24 in the BPBB
1 Samuel 24 in the BPH
1 Samuel 24 in the BSB
1 Samuel 24 in the CCB
1 Samuel 24 in the CUV
1 Samuel 24 in the CUVS
1 Samuel 24 in the DBT
1 Samuel 24 in the DGDNT
1 Samuel 24 in the DHNT
1 Samuel 24 in the DNT
1 Samuel 24 in the ELBE
1 Samuel 24 in the EMTV
1 Samuel 24 in the ESV
1 Samuel 24 in the FBV
1 Samuel 24 in the FEB
1 Samuel 24 in the GGMNT
1 Samuel 24 in the GNT
1 Samuel 24 in the HARY
1 Samuel 24 in the HNT
1 Samuel 24 in the IRVA
1 Samuel 24 in the IRVB
1 Samuel 24 in the IRVG
1 Samuel 24 in the IRVH
1 Samuel 24 in the IRVK
1 Samuel 24 in the IRVM
1 Samuel 24 in the IRVM2
1 Samuel 24 in the IRVO
1 Samuel 24 in the IRVP
1 Samuel 24 in the IRVT
1 Samuel 24 in the IRVT2
1 Samuel 24 in the IRVU
1 Samuel 24 in the ISVN
1 Samuel 24 in the JSNT
1 Samuel 24 in the KAPI
1 Samuel 24 in the KBT1ETNIK
1 Samuel 24 in the KBV
1 Samuel 24 in the KJV
1 Samuel 24 in the KNFD
1 Samuel 24 in the LBA
1 Samuel 24 in the LBLA
1 Samuel 24 in the LNT
1 Samuel 24 in the LSV
1 Samuel 24 in the MAAL
1 Samuel 24 in the MBV
1 Samuel 24 in the MBV2
1 Samuel 24 in the MHNT
1 Samuel 24 in the MKNFD
1 Samuel 24 in the MNG
1 Samuel 24 in the MNT
1 Samuel 24 in the MNT2
1 Samuel 24 in the MRS1T
1 Samuel 24 in the NAA
1 Samuel 24 in the NASB
1 Samuel 24 in the NBLA
1 Samuel 24 in the NBS
1 Samuel 24 in the NBVTP
1 Samuel 24 in the NET2
1 Samuel 24 in the NIV11
1 Samuel 24 in the NNT
1 Samuel 24 in the NNT2
1 Samuel 24 in the NNT3
1 Samuel 24 in the PDDPT
1 Samuel 24 in the PFNT
1 Samuel 24 in the RMNT
1 Samuel 24 in the SBIAS
1 Samuel 24 in the SBIBS
1 Samuel 24 in the SBIBS2
1 Samuel 24 in the SBICS
1 Samuel 24 in the SBIDS
1 Samuel 24 in the SBIGS
1 Samuel 24 in the SBIHS
1 Samuel 24 in the SBIIS
1 Samuel 24 in the SBIIS2
1 Samuel 24 in the SBIIS3
1 Samuel 24 in the SBIKS
1 Samuel 24 in the SBIKS2
1 Samuel 24 in the SBIMS
1 Samuel 24 in the SBIOS
1 Samuel 24 in the SBIPS
1 Samuel 24 in the SBISS
1 Samuel 24 in the SBITS
1 Samuel 24 in the SBITS2
1 Samuel 24 in the SBITS3
1 Samuel 24 in the SBITS4
1 Samuel 24 in the SBIUS
1 Samuel 24 in the SBIVS
1 Samuel 24 in the SBT
1 Samuel 24 in the SBT1E
1 Samuel 24 in the SCHL
1 Samuel 24 in the SNT
1 Samuel 24 in the SUSU
1 Samuel 24 in the SUSU2
1 Samuel 24 in the SYNO
1 Samuel 24 in the TBIAOTANT
1 Samuel 24 in the TBT1E
1 Samuel 24 in the TBT1E2
1 Samuel 24 in the TFTIP
1 Samuel 24 in the TFTU
1 Samuel 24 in the TGNTATF3T
1 Samuel 24 in the THAI
1 Samuel 24 in the TNFD
1 Samuel 24 in the TNT
1 Samuel 24 in the TNTIK
1 Samuel 24 in the TNTIL
1 Samuel 24 in the TNTIN
1 Samuel 24 in the TNTIP
1 Samuel 24 in the TNTIZ
1 Samuel 24 in the TOMA
1 Samuel 24 in the TTENT
1 Samuel 24 in the UBG
1 Samuel 24 in the UGV
1 Samuel 24 in the UGV2
1 Samuel 24 in the UGV3
1 Samuel 24 in the VBL
1 Samuel 24 in the VDCC
1 Samuel 24 in the YALU
1 Samuel 24 in the YAPE
1 Samuel 24 in the YBVTP
1 Samuel 24 in the ZBP