Daniel 7 (BOKCV)

1 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, nayo maono yakapita mawazoni yake alipokuwa amelala kitandani mwake. Akayaandika mambo aliyoyaona katika ndoto yake. 2 Danieli akasema: “Katika maono yangu usiku nilitazama, na hapo mbele yangu kulikuwepo na upepo kutoka pande nne za mbingu, ukivuruga bahari kuu. 3 Wanyama wanne wakubwa, kila mmoja tofauti na mwenzake, wakajitokeza kutoka bahari. 4 “Mnyama wa kwanza alifanana na simba, naye alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikatazama mpaka mabawa yake yalipongʼolewa, naye akainuliwa katika nchi, akasimama kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa binadamu. 5 “Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, ambaye alionekana kama dubu. Upande wake mmoja ulikuwa umeinuka, na alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama mpaka ushibe!’ 6 “Baada ya huyo, nilitazama, na mbele yangu kulikuwa na mnyama mwingine, aliyefanana na chui. Juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege. Mnyama huyu alikuwa na vichwa vinne, naye akapewa mamlaka ya kutawala. 7 “Baada ya huyo, katika maono yangu usiku nilitazama, na mbele yangu kulikuwa na mnyama wa nne, mwenye kutisha na kuogofya, tena mwenye nguvu nyingi. Alikuwa na meno makubwa ya chuma; akapondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chini ya nyayo zake chochote kilichosalia. Alikuwa tofauti na wanyama wote waliotangulia, naye alikuwa na pembe kumi. 8 “Wakati nilipokuwa ninafikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ambayo ni ndogo, iliyojitokeza miongoni mwa zile kumi; pembe tatu za mwanzoni zilingʼolewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu, na mdomo ulionena kwa majivuno. 9 “Nilipoendelea kutazama,“viti vya enzi vikawekwa,naye Mzee wa Siku akaketi.Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji;nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu.Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto,nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto. 10 Mto wa moto ulikuwa unatiririka,ukipita mbele yake.Maelfu elfu wakamhudumia;kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake.Mahakama ikakaa kuhukumu,na vitabu vikafunguliwa. 11 “Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia mpaka yule mnyama alipouawa, na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto uliowaka. 12 (Wanyama wengine walikuwa wamevuliwa mamlaka yao, lakini waliruhusiwa kuishi kwa muda fulani.) 13 “Katika maono yangu ya usiku nilitazama, na mbele yangu nikamwona anayefanana na mwanadamu, akija pamoja na mawingu ya mbinguni. Akamkaribia huyo Mzee wa Siku, na akaongozwa mbele zake. 14 Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu; nao watu wa kabila zote, mataifa, na watu wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa. 15 “Mimi, Danieli, nilipata mahangaiko rohoni, nayo maono yale yaliyopita ndani ya mawazo yangu yalinisumbua. 16 Nikamkaribia mmoja wa wale waliosimama pale na kumuuliza maana halisi ya haya yote.“Basi akaniambia na kunipa tafsiri ya vitu hivi: 17 ‘Hao wanyama wanne wakubwa ni falme nne zitakazoinuka duniani. 18 Lakini watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana watapokea ufalme na kuumiliki milele: naam, milele na milele.’ 19 “Kisha nilitaka kufahamu maana ya kweli ya mnyama yule wa nne, ambaye alikuwa tofauti na wale wengine wote, tena wa kutisha sana, na meno yake ya chuma na makucha ya shaba: mnyama ambaye alipondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chochote kilichosalia. 20 Pia mimi nilitaka kujua kuhusu zile pembe kumi juu ya kichwa chake, na pia kuhusu ile pembe nyingine iliyojitokeza, ambayo mbele yake zile tatu za mwanzoni zilianguka, ile pembe ambayo ilionekana kuvutia macho zaidi kuliko zile nyingine, na ambayo ilikuwa na macho na kinywa kilichonena kwa majivuno. 21 Nilipoendelea kutazama, pembe hii ilikuwa inapigana vita dhidi ya watakatifu na kuwashinda, 22 mpaka huyo Mzee wa Siku alipokuja na kutamka hukumu kwa kuwapa ushindi watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana, na wakati ukawadia walipoumiliki ufalme. 23 “Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote, nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda. 24 Zile pembe kumi ni wafalme kumi watakaotokana na ufalme huu. Baada yao mfalme mwingine atainuka, ambaye atakuwa tofauti na wale waliotangulia, naye atawaangusha wafalme watatu. 25 Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwaonea watakatifu wake, huku akijaribu kubadili majira na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati. 26 “ ‘Lakini mahakama itakaa kuhukumu, nayo mamlaka yake yataondolewa na kuangamizwa kabisa milele. 27 Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote utakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’ 28 “Huu ndio mwisho wa jambo lile. Mimi Danieli nilitaabika sana katika mawazo yangu, nao uso wangu ukabadilika, lakini nililiweka jambo hilo moyoni mwangu.”

In Other Versions

Daniel 7 in the ANGEFD

Daniel 7 in the ANTPNG2D

Daniel 7 in the AS21

Daniel 7 in the BAGH

Daniel 7 in the BBPNG

Daniel 7 in the BBT1E

Daniel 7 in the BDS

Daniel 7 in the BEV

Daniel 7 in the BHAD

Daniel 7 in the BIB

Daniel 7 in the BLPT

Daniel 7 in the BNT

Daniel 7 in the BNTABOOT

Daniel 7 in the BNTLV

Daniel 7 in the BOATCB

Daniel 7 in the BOATCB2

Daniel 7 in the BOBCV

Daniel 7 in the BOCNT

Daniel 7 in the BOECS

Daniel 7 in the BOGWICC

Daniel 7 in the BOHCB

Daniel 7 in the BOHCV

Daniel 7 in the BOHLNT

Daniel 7 in the BOHNTLTAL

Daniel 7 in the BOICB

Daniel 7 in the BOILNTAP

Daniel 7 in the BOITCV

Daniel 7 in the BOKCV2

Daniel 7 in the BOKHWOG

Daniel 7 in the BOKSSV

Daniel 7 in the BOLCB

Daniel 7 in the BOLCB2

Daniel 7 in the BOMCV

Daniel 7 in the BONAV

Daniel 7 in the BONCB

Daniel 7 in the BONLT

Daniel 7 in the BONUT2

Daniel 7 in the BOPLNT

Daniel 7 in the BOSCB

Daniel 7 in the BOSNC

Daniel 7 in the BOTLNT

Daniel 7 in the BOVCB

Daniel 7 in the BOYCB

Daniel 7 in the BPBB

Daniel 7 in the BPH

Daniel 7 in the BSB

Daniel 7 in the CCB

Daniel 7 in the CUV

Daniel 7 in the CUVS

Daniel 7 in the DBT

Daniel 7 in the DGDNT

Daniel 7 in the DHNT

Daniel 7 in the DNT

Daniel 7 in the ELBE

Daniel 7 in the EMTV

Daniel 7 in the ESV

Daniel 7 in the FBV

Daniel 7 in the FEB

Daniel 7 in the GGMNT

Daniel 7 in the GNT

Daniel 7 in the HARY

Daniel 7 in the HNT

Daniel 7 in the IRVA

Daniel 7 in the IRVB

Daniel 7 in the IRVG

Daniel 7 in the IRVH

Daniel 7 in the IRVK

Daniel 7 in the IRVM

Daniel 7 in the IRVM2

Daniel 7 in the IRVO

Daniel 7 in the IRVP

Daniel 7 in the IRVT

Daniel 7 in the IRVT2

Daniel 7 in the IRVU

Daniel 7 in the ISVN

Daniel 7 in the JSNT

Daniel 7 in the KAPI

Daniel 7 in the KBT1ETNIK

Daniel 7 in the KBV

Daniel 7 in the KJV

Daniel 7 in the KNFD

Daniel 7 in the LBA

Daniel 7 in the LBLA

Daniel 7 in the LNT

Daniel 7 in the LSV

Daniel 7 in the MAAL

Daniel 7 in the MBV

Daniel 7 in the MBV2

Daniel 7 in the MHNT

Daniel 7 in the MKNFD

Daniel 7 in the MNG

Daniel 7 in the MNT

Daniel 7 in the MNT2

Daniel 7 in the MRS1T

Daniel 7 in the NAA

Daniel 7 in the NASB

Daniel 7 in the NBLA

Daniel 7 in the NBS

Daniel 7 in the NBVTP

Daniel 7 in the NET2

Daniel 7 in the NIV11

Daniel 7 in the NNT

Daniel 7 in the NNT2

Daniel 7 in the NNT3

Daniel 7 in the PDDPT

Daniel 7 in the PFNT

Daniel 7 in the RMNT

Daniel 7 in the SBIAS

Daniel 7 in the SBIBS

Daniel 7 in the SBIBS2

Daniel 7 in the SBICS

Daniel 7 in the SBIDS

Daniel 7 in the SBIGS

Daniel 7 in the SBIHS

Daniel 7 in the SBIIS

Daniel 7 in the SBIIS2

Daniel 7 in the SBIIS3

Daniel 7 in the SBIKS

Daniel 7 in the SBIKS2

Daniel 7 in the SBIMS

Daniel 7 in the SBIOS

Daniel 7 in the SBIPS

Daniel 7 in the SBISS

Daniel 7 in the SBITS

Daniel 7 in the SBITS2

Daniel 7 in the SBITS3

Daniel 7 in the SBITS4

Daniel 7 in the SBIUS

Daniel 7 in the SBIVS

Daniel 7 in the SBT

Daniel 7 in the SBT1E

Daniel 7 in the SCHL

Daniel 7 in the SNT

Daniel 7 in the SUSU

Daniel 7 in the SUSU2

Daniel 7 in the SYNO

Daniel 7 in the TBIAOTANT

Daniel 7 in the TBT1E

Daniel 7 in the TBT1E2

Daniel 7 in the TFTIP

Daniel 7 in the TFTU

Daniel 7 in the TGNTATF3T

Daniel 7 in the THAI

Daniel 7 in the TNFD

Daniel 7 in the TNT

Daniel 7 in the TNTIK

Daniel 7 in the TNTIL

Daniel 7 in the TNTIN

Daniel 7 in the TNTIP

Daniel 7 in the TNTIZ

Daniel 7 in the TOMA

Daniel 7 in the TTENT

Daniel 7 in the UBG

Daniel 7 in the UGV

Daniel 7 in the UGV2

Daniel 7 in the UGV3

Daniel 7 in the VBL

Daniel 7 in the VDCC

Daniel 7 in the YALU

Daniel 7 in the YAPE

Daniel 7 in the YBVTP

Daniel 7 in the ZBP