Deuteronomy 7 (BOKCV)
1 BWANA Mungu wako akuletapo katika nchi unayoingia kuimiliki, na awafukuzapo mbele yako mataifa mengi, yaani Wahiti, Wagirgashi, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, mataifa saba makubwa tena yenye nguvu kuliko wewe, 2 pia BWANA Mungu wako atakapowatia mkononi mwako na ukawashinda, basi ni lazima uwaangamize wote kabisa. Usifanye agano nao, wala usiwahurumie. 3 Usioane nao. Usimtoe binti yako kuolewa na mwanawe, au kumchukua binti yake aolewe na mwanao. 4 Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira ya BWANA itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula. 5 Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia, katakata nguzo zao za Ashera na kuchoma sanamu zao kwa moto. 6 Kwa kuwa wewe ni taifa takatifu kwa BWANA Mungu wako. BWANA Mungu wako amekuchagua wewe kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia kuwa watu wake, hazina yake ya thamani. 7 BWANA hakuweka upendo wake juu yenu na kuwachagua kwa sababu mlikuwa wengi mno kuliko watu wengine, kwa maana ninyi ndio mliokuwa wachache sana kuliko mataifa yote. 8 Lakini ni kwa sababu BWANA aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri. 9 Basi ujue kwamba BWANA Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake. 10 Lakinikwa wale wanaomchukiaatawalipiza kwenye nyuso zaokwa maangamizi;hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zaowale wamchukiao. 11 Kwa hiyo, kuweni waangalifu kufuata maagizo, amri na sheria ninazowapa leo. 12 Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi BWANA Mungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu. 13 Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama za ngʼombe wa makundi yenu, na kondoo za makundi yenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu. 14 Mtabarikiwa kuliko mataifa mengine yote, hakuna wanaume wala wanawake kwenu watakaokosa watoto, wala mifugo yenu haitakuwa tasa. 15 BWANA atawakinga na kila ugonjwa. Mungu hatatia juu yenu ugonjwa wowote mbaya mlioufahamu huko Misri, lakini atatia ugonjwa juu ya wale wote wanaokuchukia. 16 Ni lazima mwangamize watu wote ambao BWANA Mungu wenu atawatia mikononi mwenu. Msiwatazame kwa kuwahurumia na msiitumikie miungu yao, kwa kuwa itakuwa mtego kwenu. 17 Mnaweza kujiuliza wenyewe “Mataifa haya ni yenye nguvu kuliko sisi. Tutawezaje kuwafukuza?” 18 Lakini msiwaogope. Kumbukeni vyema jinsi BWANA Mungu wenu alivyofanya kwa Farao na kwa wote huko Misri. 19 Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huo BWANA Mungu wenu aliwatoa mtoke Misri. BWANA Mungu wenu atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa. 20 Zaidi ya hayo, BWANA Mungu wenu atatuma manyigu miongoni mwao hadi yale mabaki watakaojificha waangamie. 21 Msiingiwe na hofu kwa sababu yao, kwa kuwa BWANA Mungu wenu, ambaye yupo miongoni mwenu ni mkuu naye ni Mungu wa kutisha. 22 BWANA Mungu wenu atawafukuza mataifa hayo mbele yenu kidogo kidogo. Hamtaruhusiwa kuwaondoa wote kwa mara moja, la sivyo wanyama mwitu wataongezeka na kuwa karibu nanyi. 23 Lakini BWANA Mungu wenu atawatia watu hao mikononi mwenu, akiwatia katika kuchanganyikiwa kukubwa mpaka wawe wameangamizwa. 24 Atawatia wafalme wao mikononi mwenu, nanyi mtayafuta majina yao chini ya mbingu. Hakuna hata mmoja atakayeweza kusimama dhidi yenu bali mtawaangamiza. 25 Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwa BWANA Mungu wenu. 26 Msilete vitu vya machukizo katika nyumba zenu kwani ninyi, mtatengwa kama vitu hivyo kwa maangamizo. Ukichukie kabisa kitu hicho kwa kuwa kimetengwa kwa maangamizo.
In Other Versions
Deuteronomy 7 in the ANGEFD
Deuteronomy 7 in the ANTPNG2D
Deuteronomy 7 in the AS21
Deuteronomy 7 in the BAGH
Deuteronomy 7 in the BBPNG
Deuteronomy 7 in the BBT1E
Deuteronomy 7 in the BDS
Deuteronomy 7 in the BEV
Deuteronomy 7 in the BHAD
Deuteronomy 7 in the BIB
Deuteronomy 7 in the BLPT
Deuteronomy 7 in the BNT
Deuteronomy 7 in the BNTABOOT
Deuteronomy 7 in the BNTLV
Deuteronomy 7 in the BOATCB
Deuteronomy 7 in the BOATCB2
Deuteronomy 7 in the BOBCV
Deuteronomy 7 in the BOCNT
Deuteronomy 7 in the BOECS
Deuteronomy 7 in the BOGWICC
Deuteronomy 7 in the BOHCB
Deuteronomy 7 in the BOHCV
Deuteronomy 7 in the BOHLNT
Deuteronomy 7 in the BOHNTLTAL
Deuteronomy 7 in the BOICB
Deuteronomy 7 in the BOILNTAP
Deuteronomy 7 in the BOITCV
Deuteronomy 7 in the BOKCV2
Deuteronomy 7 in the BOKHWOG
Deuteronomy 7 in the BOKSSV
Deuteronomy 7 in the BOLCB
Deuteronomy 7 in the BOLCB2
Deuteronomy 7 in the BOMCV
Deuteronomy 7 in the BONAV
Deuteronomy 7 in the BONCB
Deuteronomy 7 in the BONLT
Deuteronomy 7 in the BONUT2
Deuteronomy 7 in the BOPLNT
Deuteronomy 7 in the BOSCB
Deuteronomy 7 in the BOSNC
Deuteronomy 7 in the BOTLNT
Deuteronomy 7 in the BOVCB
Deuteronomy 7 in the BOYCB
Deuteronomy 7 in the BPBB
Deuteronomy 7 in the BPH
Deuteronomy 7 in the BSB
Deuteronomy 7 in the CCB
Deuteronomy 7 in the CUV
Deuteronomy 7 in the CUVS
Deuteronomy 7 in the DBT
Deuteronomy 7 in the DGDNT
Deuteronomy 7 in the DHNT
Deuteronomy 7 in the DNT
Deuteronomy 7 in the ELBE
Deuteronomy 7 in the EMTV
Deuteronomy 7 in the ESV
Deuteronomy 7 in the FBV
Deuteronomy 7 in the FEB
Deuteronomy 7 in the GGMNT
Deuteronomy 7 in the GNT
Deuteronomy 7 in the HARY
Deuteronomy 7 in the HNT
Deuteronomy 7 in the IRVA
Deuteronomy 7 in the IRVB
Deuteronomy 7 in the IRVG
Deuteronomy 7 in the IRVH
Deuteronomy 7 in the IRVK
Deuteronomy 7 in the IRVM
Deuteronomy 7 in the IRVM2
Deuteronomy 7 in the IRVO
Deuteronomy 7 in the IRVP
Deuteronomy 7 in the IRVT
Deuteronomy 7 in the IRVT2
Deuteronomy 7 in the IRVU
Deuteronomy 7 in the ISVN
Deuteronomy 7 in the JSNT
Deuteronomy 7 in the KAPI
Deuteronomy 7 in the KBT1ETNIK
Deuteronomy 7 in the KBV
Deuteronomy 7 in the KJV
Deuteronomy 7 in the KNFD
Deuteronomy 7 in the LBA
Deuteronomy 7 in the LBLA
Deuteronomy 7 in the LNT
Deuteronomy 7 in the LSV
Deuteronomy 7 in the MAAL
Deuteronomy 7 in the MBV
Deuteronomy 7 in the MBV2
Deuteronomy 7 in the MHNT
Deuteronomy 7 in the MKNFD
Deuteronomy 7 in the MNG
Deuteronomy 7 in the MNT
Deuteronomy 7 in the MNT2
Deuteronomy 7 in the MRS1T
Deuteronomy 7 in the NAA
Deuteronomy 7 in the NASB
Deuteronomy 7 in the NBLA
Deuteronomy 7 in the NBS
Deuteronomy 7 in the NBVTP
Deuteronomy 7 in the NET2
Deuteronomy 7 in the NIV11
Deuteronomy 7 in the NNT
Deuteronomy 7 in the NNT2
Deuteronomy 7 in the NNT3
Deuteronomy 7 in the PDDPT
Deuteronomy 7 in the PFNT
Deuteronomy 7 in the RMNT
Deuteronomy 7 in the SBIAS
Deuteronomy 7 in the SBIBS
Deuteronomy 7 in the SBIBS2
Deuteronomy 7 in the SBICS
Deuteronomy 7 in the SBIDS
Deuteronomy 7 in the SBIGS
Deuteronomy 7 in the SBIHS
Deuteronomy 7 in the SBIIS
Deuteronomy 7 in the SBIIS2
Deuteronomy 7 in the SBIIS3
Deuteronomy 7 in the SBIKS
Deuteronomy 7 in the SBIKS2
Deuteronomy 7 in the SBIMS
Deuteronomy 7 in the SBIOS
Deuteronomy 7 in the SBIPS
Deuteronomy 7 in the SBISS
Deuteronomy 7 in the SBITS
Deuteronomy 7 in the SBITS2
Deuteronomy 7 in the SBITS3
Deuteronomy 7 in the SBITS4
Deuteronomy 7 in the SBIUS
Deuteronomy 7 in the SBIVS
Deuteronomy 7 in the SBT
Deuteronomy 7 in the SBT1E
Deuteronomy 7 in the SCHL
Deuteronomy 7 in the SNT
Deuteronomy 7 in the SUSU
Deuteronomy 7 in the SUSU2
Deuteronomy 7 in the SYNO
Deuteronomy 7 in the TBIAOTANT
Deuteronomy 7 in the TBT1E
Deuteronomy 7 in the TBT1E2
Deuteronomy 7 in the TFTIP
Deuteronomy 7 in the TFTU
Deuteronomy 7 in the TGNTATF3T
Deuteronomy 7 in the THAI
Deuteronomy 7 in the TNFD
Deuteronomy 7 in the TNT
Deuteronomy 7 in the TNTIK
Deuteronomy 7 in the TNTIL
Deuteronomy 7 in the TNTIN
Deuteronomy 7 in the TNTIP
Deuteronomy 7 in the TNTIZ
Deuteronomy 7 in the TOMA
Deuteronomy 7 in the TTENT
Deuteronomy 7 in the UBG
Deuteronomy 7 in the UGV
Deuteronomy 7 in the UGV2
Deuteronomy 7 in the UGV3
Deuteronomy 7 in the VBL
Deuteronomy 7 in the VDCC
Deuteronomy 7 in the YALU
Deuteronomy 7 in the YAPE
Deuteronomy 7 in the YBVTP
Deuteronomy 7 in the ZBP