Genesis 7 (BOKCV)

1 Ndipo BWANA akamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki. 2 Uchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike. 3 Pia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote. 4 Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.” 5 Noa akafanya yote kama BWANA alivyomwamuru. 6 Noa alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia. 7 Noa na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika. 8 Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vitambaavyo, 9 wa kiume na wa kike, walikuja kwa Noa wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Noa. 10 Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia. 11 Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Noa, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa. 12 Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini usiku na mchana. 13 Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina. 14 Nao walikuwa pamoja na kila mnyama wa mwituni kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake, na kila ndege kufuatana na aina yake, naam kila kiumbe chenye mabawa. 15 Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Noa viwili viwili, vikaingia katika safina. 16 Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Noa, ndipo BWANA akamfungia ndani. 17 Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi. 18 Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji. 19 Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. 20 Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano. 21 Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote. 22 Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa. 23 Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. 24 Maji yakaifunika dunia kwa siku 150.

In Other Versions

Genesis 7 in the ANGEFD

Genesis 7 in the ANTPNG2D

Genesis 7 in the AS21

Genesis 7 in the BAGH

Genesis 7 in the BBPNG

Genesis 7 in the BBT1E

Genesis 7 in the BDS

Genesis 7 in the BEV

Genesis 7 in the BHAD

Genesis 7 in the BIB

Genesis 7 in the BLPT

Genesis 7 in the BNT

Genesis 7 in the BNTABOOT

Genesis 7 in the BNTLV

Genesis 7 in the BOATCB

Genesis 7 in the BOATCB2

Genesis 7 in the BOBCV

Genesis 7 in the BOCNT

Genesis 7 in the BOECS

Genesis 7 in the BOGWICC

Genesis 7 in the BOHCB

Genesis 7 in the BOHCV

Genesis 7 in the BOHLNT

Genesis 7 in the BOHNTLTAL

Genesis 7 in the BOICB

Genesis 7 in the BOILNTAP

Genesis 7 in the BOITCV

Genesis 7 in the BOKCV2

Genesis 7 in the BOKHWOG

Genesis 7 in the BOKSSV

Genesis 7 in the BOLCB

Genesis 7 in the BOLCB2

Genesis 7 in the BOMCV

Genesis 7 in the BONAV

Genesis 7 in the BONCB

Genesis 7 in the BONLT

Genesis 7 in the BONUT2

Genesis 7 in the BOPLNT

Genesis 7 in the BOSCB

Genesis 7 in the BOSNC

Genesis 7 in the BOTLNT

Genesis 7 in the BOVCB

Genesis 7 in the BOYCB

Genesis 7 in the BPBB

Genesis 7 in the BPH

Genesis 7 in the BSB

Genesis 7 in the CCB

Genesis 7 in the CUV

Genesis 7 in the CUVS

Genesis 7 in the DBT

Genesis 7 in the DGDNT

Genesis 7 in the DHNT

Genesis 7 in the DNT

Genesis 7 in the ELBE

Genesis 7 in the EMTV

Genesis 7 in the ESV

Genesis 7 in the FBV

Genesis 7 in the FEB

Genesis 7 in the GGMNT

Genesis 7 in the GNT

Genesis 7 in the HARY

Genesis 7 in the HNT

Genesis 7 in the IRVA

Genesis 7 in the IRVB

Genesis 7 in the IRVG

Genesis 7 in the IRVH

Genesis 7 in the IRVK

Genesis 7 in the IRVM

Genesis 7 in the IRVM2

Genesis 7 in the IRVO

Genesis 7 in the IRVP

Genesis 7 in the IRVT

Genesis 7 in the IRVT2

Genesis 7 in the IRVU

Genesis 7 in the ISVN

Genesis 7 in the JSNT

Genesis 7 in the KAPI

Genesis 7 in the KBT1ETNIK

Genesis 7 in the KBV

Genesis 7 in the KJV

Genesis 7 in the KNFD

Genesis 7 in the LBA

Genesis 7 in the LBLA

Genesis 7 in the LNT

Genesis 7 in the LSV

Genesis 7 in the MAAL

Genesis 7 in the MBV

Genesis 7 in the MBV2

Genesis 7 in the MHNT

Genesis 7 in the MKNFD

Genesis 7 in the MNG

Genesis 7 in the MNT

Genesis 7 in the MNT2

Genesis 7 in the MRS1T

Genesis 7 in the NAA

Genesis 7 in the NASB

Genesis 7 in the NBLA

Genesis 7 in the NBS

Genesis 7 in the NBVTP

Genesis 7 in the NET2

Genesis 7 in the NIV11

Genesis 7 in the NNT

Genesis 7 in the NNT2

Genesis 7 in the NNT3

Genesis 7 in the PDDPT

Genesis 7 in the PFNT

Genesis 7 in the RMNT

Genesis 7 in the SBIAS

Genesis 7 in the SBIBS

Genesis 7 in the SBIBS2

Genesis 7 in the SBICS

Genesis 7 in the SBIDS

Genesis 7 in the SBIGS

Genesis 7 in the SBIHS

Genesis 7 in the SBIIS

Genesis 7 in the SBIIS2

Genesis 7 in the SBIIS3

Genesis 7 in the SBIKS

Genesis 7 in the SBIKS2

Genesis 7 in the SBIMS

Genesis 7 in the SBIOS

Genesis 7 in the SBIPS

Genesis 7 in the SBISS

Genesis 7 in the SBITS

Genesis 7 in the SBITS2

Genesis 7 in the SBITS3

Genesis 7 in the SBITS4

Genesis 7 in the SBIUS

Genesis 7 in the SBIVS

Genesis 7 in the SBT

Genesis 7 in the SBT1E

Genesis 7 in the SCHL

Genesis 7 in the SNT

Genesis 7 in the SUSU

Genesis 7 in the SUSU2

Genesis 7 in the SYNO

Genesis 7 in the TBIAOTANT

Genesis 7 in the TBT1E

Genesis 7 in the TBT1E2

Genesis 7 in the TFTIP

Genesis 7 in the TFTU

Genesis 7 in the TGNTATF3T

Genesis 7 in the THAI

Genesis 7 in the TNFD

Genesis 7 in the TNT

Genesis 7 in the TNTIK

Genesis 7 in the TNTIL

Genesis 7 in the TNTIN

Genesis 7 in the TNTIP

Genesis 7 in the TNTIZ

Genesis 7 in the TOMA

Genesis 7 in the TTENT

Genesis 7 in the UBG

Genesis 7 in the UGV

Genesis 7 in the UGV2

Genesis 7 in the UGV3

Genesis 7 in the VBL

Genesis 7 in the VDCC

Genesis 7 in the YALU

Genesis 7 in the YAPE

Genesis 7 in the YBVTP

Genesis 7 in the ZBP