Jeremiah 11 (BOKCV)
1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa BWANA: 2 “Sikia maneno ya agano hili, nawe uwaambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu. 3 Waambie kwamba hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Amelaaniwa mtu ambaye hatayatii maneno ya agano hili, 4 maneno niliyowaamuru baba zenu nilipowatoa katika nchi ya Misri, kutoka tanuru la kuyeyushia vyuma.’ Nilisema, ‘Nitiini mimi na mfanye kila kitu ninachowaamuru, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. 5 Kisha nitatimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi itiririkayo maziwa na asali,’ nchi ambayo mnaimiliki leo.”Nikajibu, “Amen, BWANA.” 6 BWANA akaniambia, “Tangaza maneno haya yote katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu: ‘Sikilizeni maneno ya agano hili na kuyafuata. 7 Tangu wakati ule niliwapandisha baba zenu kutoka Misri mpaka leo, niliwaonya tena na tena, nikisema “Nitiini mimi.” 8 Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Hivyo nikaleta juu yao laana zote za agano nililokuwa nimewaamuru wao kulifuata, lakini wao hawakulishika.’ ” 9 Kisha BWANA akaniambia, “Kuna shauri baya linaloendelea miongoni mwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu. 10 Wamerudia dhambi za baba zao, waliokataa kusikiliza maneno yangu. Wameifuata miungu mingine kuitumikia. Nyumba zote mbili za Israeli na Yuda zimelivunja agano nililofanya na baba zao. 11 Kwa hivyo, hili ndilo asemalo BWANA: ‘Nitaleta juu yao maafa ambayo hawawezi kuyakimbia. Hata kama wakinililia, sitawasikiliza. 12 Miji ya Yuda na watu wa Yerusalemu watakwenda kuililia miungu ambayo wameifukizia uvumba, lakini haitawasaidia kamwe wakati maafa yatakapowapiga. 13 Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kufukizia uvumba huyo mungu wa aibu Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’ 14 “Wewe usiwaombee watu hawa wala kufanya maombezi yoyote au kunisihi kwa ajili yao, kwa sababu sitawasikiliza watakaponiita wakati wa taabu yao. 15 “Mpenzi wangu anafanya nini hekaluni mwangu,anapofanya mashauri yake maovu na wengi?Je, nyama iliyowekwa wakfu yawezakuondolea mbali adhabu yako?Unapojiingiza katika ubaya wako,ndipo unashangilia.” 16 BWANA alikuita mti wa mzeituni uliostawiulio na matunda mazuri kwa sura.Lakini kwa ngurumo ya mawimbi makuuatautia moto,nayo matawi yake yatavunjika. 17 BWANA Mwenye Nguvu Zote, aliyekupanda, ametamka maafa kwa ajili yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba. 18 Kwa sababu BWANA alinifunulia hila zao mbaya, nilizifahamu, kwa kuwa wakati ule alinionyesha yale waliyokuwa wanayafanya. 19 Nilikuwa kama mwana-kondoo mpole aliyeongozwa machinjoni; mimi sikutambua kwamba walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yangu, wakisema,“Sisi na tuuangamize mti na matunda yake;nasi tumkatilie mbali kutoka nchi ya walio hai,ili jina lake lisikumbukwe tena.” 20 Lakini, Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, wewe uhukumuye kwa haki,nawe uchunguzaye moyo na akili,wacha nione ukiwalipiza wao kisasi,kwa maana kwako nimeweka shauri langu. 21 “Kwa hiyo hili ndilo BWANA asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la BWANA, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’: 22 kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu. Vijana wao waume watakufa kwa upanga, wana wao na binti zao kwa njaa. 23 Hawatasaziwa hata mabaki kwao, kwa sababu nitaleta maafa kwa watu wa Anathothi katika mwaka wa adhabu yao.’ ”
In Other Versions
Jeremiah 11 in the ANGEFD
Jeremiah 11 in the ANTPNG2D
Jeremiah 11 in the AS21
Jeremiah 11 in the BAGH
Jeremiah 11 in the BBPNG
Jeremiah 11 in the BBT1E
Jeremiah 11 in the BDS
Jeremiah 11 in the BEV
Jeremiah 11 in the BHAD
Jeremiah 11 in the BIB
Jeremiah 11 in the BLPT
Jeremiah 11 in the BNT
Jeremiah 11 in the BNTABOOT
Jeremiah 11 in the BNTLV
Jeremiah 11 in the BOATCB
Jeremiah 11 in the BOATCB2
Jeremiah 11 in the BOBCV
Jeremiah 11 in the BOCNT
Jeremiah 11 in the BOECS
Jeremiah 11 in the BOGWICC
Jeremiah 11 in the BOHCB
Jeremiah 11 in the BOHCV
Jeremiah 11 in the BOHLNT
Jeremiah 11 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 11 in the BOICB
Jeremiah 11 in the BOILNTAP
Jeremiah 11 in the BOITCV
Jeremiah 11 in the BOKCV2
Jeremiah 11 in the BOKHWOG
Jeremiah 11 in the BOKSSV
Jeremiah 11 in the BOLCB
Jeremiah 11 in the BOLCB2
Jeremiah 11 in the BOMCV
Jeremiah 11 in the BONAV
Jeremiah 11 in the BONCB
Jeremiah 11 in the BONLT
Jeremiah 11 in the BONUT2
Jeremiah 11 in the BOPLNT
Jeremiah 11 in the BOSCB
Jeremiah 11 in the BOSNC
Jeremiah 11 in the BOTLNT
Jeremiah 11 in the BOVCB
Jeremiah 11 in the BOYCB
Jeremiah 11 in the BPBB
Jeremiah 11 in the BPH
Jeremiah 11 in the BSB
Jeremiah 11 in the CCB
Jeremiah 11 in the CUV
Jeremiah 11 in the CUVS
Jeremiah 11 in the DBT
Jeremiah 11 in the DGDNT
Jeremiah 11 in the DHNT
Jeremiah 11 in the DNT
Jeremiah 11 in the ELBE
Jeremiah 11 in the EMTV
Jeremiah 11 in the ESV
Jeremiah 11 in the FBV
Jeremiah 11 in the FEB
Jeremiah 11 in the GGMNT
Jeremiah 11 in the GNT
Jeremiah 11 in the HARY
Jeremiah 11 in the HNT
Jeremiah 11 in the IRVA
Jeremiah 11 in the IRVB
Jeremiah 11 in the IRVG
Jeremiah 11 in the IRVH
Jeremiah 11 in the IRVK
Jeremiah 11 in the IRVM
Jeremiah 11 in the IRVM2
Jeremiah 11 in the IRVO
Jeremiah 11 in the IRVP
Jeremiah 11 in the IRVT
Jeremiah 11 in the IRVT2
Jeremiah 11 in the IRVU
Jeremiah 11 in the ISVN
Jeremiah 11 in the JSNT
Jeremiah 11 in the KAPI
Jeremiah 11 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 11 in the KBV
Jeremiah 11 in the KJV
Jeremiah 11 in the KNFD
Jeremiah 11 in the LBA
Jeremiah 11 in the LBLA
Jeremiah 11 in the LNT
Jeremiah 11 in the LSV
Jeremiah 11 in the MAAL
Jeremiah 11 in the MBV
Jeremiah 11 in the MBV2
Jeremiah 11 in the MHNT
Jeremiah 11 in the MKNFD
Jeremiah 11 in the MNG
Jeremiah 11 in the MNT
Jeremiah 11 in the MNT2
Jeremiah 11 in the MRS1T
Jeremiah 11 in the NAA
Jeremiah 11 in the NASB
Jeremiah 11 in the NBLA
Jeremiah 11 in the NBS
Jeremiah 11 in the NBVTP
Jeremiah 11 in the NET2
Jeremiah 11 in the NIV11
Jeremiah 11 in the NNT
Jeremiah 11 in the NNT2
Jeremiah 11 in the NNT3
Jeremiah 11 in the PDDPT
Jeremiah 11 in the PFNT
Jeremiah 11 in the RMNT
Jeremiah 11 in the SBIAS
Jeremiah 11 in the SBIBS
Jeremiah 11 in the SBIBS2
Jeremiah 11 in the SBICS
Jeremiah 11 in the SBIDS
Jeremiah 11 in the SBIGS
Jeremiah 11 in the SBIHS
Jeremiah 11 in the SBIIS
Jeremiah 11 in the SBIIS2
Jeremiah 11 in the SBIIS3
Jeremiah 11 in the SBIKS
Jeremiah 11 in the SBIKS2
Jeremiah 11 in the SBIMS
Jeremiah 11 in the SBIOS
Jeremiah 11 in the SBIPS
Jeremiah 11 in the SBISS
Jeremiah 11 in the SBITS
Jeremiah 11 in the SBITS2
Jeremiah 11 in the SBITS3
Jeremiah 11 in the SBITS4
Jeremiah 11 in the SBIUS
Jeremiah 11 in the SBIVS
Jeremiah 11 in the SBT
Jeremiah 11 in the SBT1E
Jeremiah 11 in the SCHL
Jeremiah 11 in the SNT
Jeremiah 11 in the SUSU
Jeremiah 11 in the SUSU2
Jeremiah 11 in the SYNO
Jeremiah 11 in the TBIAOTANT
Jeremiah 11 in the TBT1E
Jeremiah 11 in the TBT1E2
Jeremiah 11 in the TFTIP
Jeremiah 11 in the TFTU
Jeremiah 11 in the TGNTATF3T
Jeremiah 11 in the THAI
Jeremiah 11 in the TNFD
Jeremiah 11 in the TNT
Jeremiah 11 in the TNTIK
Jeremiah 11 in the TNTIL
Jeremiah 11 in the TNTIN
Jeremiah 11 in the TNTIP
Jeremiah 11 in the TNTIZ
Jeremiah 11 in the TOMA
Jeremiah 11 in the TTENT
Jeremiah 11 in the UBG
Jeremiah 11 in the UGV
Jeremiah 11 in the UGV2
Jeremiah 11 in the UGV3
Jeremiah 11 in the VBL
Jeremiah 11 in the VDCC
Jeremiah 11 in the YALU
Jeremiah 11 in the YAPE
Jeremiah 11 in the YBVTP
Jeremiah 11 in the ZBP