Job 42 (BOKCV)

1 Ndipo Ayubu akamjibu BWANA: 2 “Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika. 3 Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi,mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua. 4 “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena;nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’ 5 Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,lakini sasa macho yangu yamekuona. 6 Kwa hiyo najidharau mwenyewe,na kutubu katika mavumbi na majivu.” 7 Baada ya BWANA kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu. 8 Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.” 9 Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi wakafanya kama BWANA alivyowaambia; naye BWANA akayakubali maombi ya Ayubu. 10 Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, BWANA akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni. 11 Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote BWANA aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu. 12 BWANA akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja. 13 Tena alikuwa na wana saba na binti watatu. 14 Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki. 15 Hapakuwepo mahali popote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao. 16 Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne. 17 Hivyo Ayubu akafa, akiwa mzee aliyekuwa ameshiba siku.

In Other Versions

Job 42 in the ANGEFD

Job 42 in the ANTPNG2D

Job 42 in the AS21

Job 42 in the BAGH

Job 42 in the BBPNG

Job 42 in the BBT1E

Job 42 in the BDS

Job 42 in the BEV

Job 42 in the BHAD

Job 42 in the BIB

Job 42 in the BLPT

Job 42 in the BNT

Job 42 in the BNTABOOT

Job 42 in the BNTLV

Job 42 in the BOATCB

Job 42 in the BOATCB2

Job 42 in the BOBCV

Job 42 in the BOCNT

Job 42 in the BOECS

Job 42 in the BOGWICC

Job 42 in the BOHCB

Job 42 in the BOHCV

Job 42 in the BOHLNT

Job 42 in the BOHNTLTAL

Job 42 in the BOICB

Job 42 in the BOILNTAP

Job 42 in the BOITCV

Job 42 in the BOKCV2

Job 42 in the BOKHWOG

Job 42 in the BOKSSV

Job 42 in the BOLCB

Job 42 in the BOLCB2

Job 42 in the BOMCV

Job 42 in the BONAV

Job 42 in the BONCB

Job 42 in the BONLT

Job 42 in the BONUT2

Job 42 in the BOPLNT

Job 42 in the BOSCB

Job 42 in the BOSNC

Job 42 in the BOTLNT

Job 42 in the BOVCB

Job 42 in the BOYCB

Job 42 in the BPBB

Job 42 in the BPH

Job 42 in the BSB

Job 42 in the CCB

Job 42 in the CUV

Job 42 in the CUVS

Job 42 in the DBT

Job 42 in the DGDNT

Job 42 in the DHNT

Job 42 in the DNT

Job 42 in the ELBE

Job 42 in the EMTV

Job 42 in the ESV

Job 42 in the FBV

Job 42 in the FEB

Job 42 in the GGMNT

Job 42 in the GNT

Job 42 in the HARY

Job 42 in the HNT

Job 42 in the IRVA

Job 42 in the IRVB

Job 42 in the IRVG

Job 42 in the IRVH

Job 42 in the IRVK

Job 42 in the IRVM

Job 42 in the IRVM2

Job 42 in the IRVO

Job 42 in the IRVP

Job 42 in the IRVT

Job 42 in the IRVT2

Job 42 in the IRVU

Job 42 in the ISVN

Job 42 in the JSNT

Job 42 in the KAPI

Job 42 in the KBT1ETNIK

Job 42 in the KBV

Job 42 in the KJV

Job 42 in the KNFD

Job 42 in the LBA

Job 42 in the LBLA

Job 42 in the LNT

Job 42 in the LSV

Job 42 in the MAAL

Job 42 in the MBV

Job 42 in the MBV2

Job 42 in the MHNT

Job 42 in the MKNFD

Job 42 in the MNG

Job 42 in the MNT

Job 42 in the MNT2

Job 42 in the MRS1T

Job 42 in the NAA

Job 42 in the NASB

Job 42 in the NBLA

Job 42 in the NBS

Job 42 in the NBVTP

Job 42 in the NET2

Job 42 in the NIV11

Job 42 in the NNT

Job 42 in the NNT2

Job 42 in the NNT3

Job 42 in the PDDPT

Job 42 in the PFNT

Job 42 in the RMNT

Job 42 in the SBIAS

Job 42 in the SBIBS

Job 42 in the SBIBS2

Job 42 in the SBICS

Job 42 in the SBIDS

Job 42 in the SBIGS

Job 42 in the SBIHS

Job 42 in the SBIIS

Job 42 in the SBIIS2

Job 42 in the SBIIS3

Job 42 in the SBIKS

Job 42 in the SBIKS2

Job 42 in the SBIMS

Job 42 in the SBIOS

Job 42 in the SBIPS

Job 42 in the SBISS

Job 42 in the SBITS

Job 42 in the SBITS2

Job 42 in the SBITS3

Job 42 in the SBITS4

Job 42 in the SBIUS

Job 42 in the SBIVS

Job 42 in the SBT

Job 42 in the SBT1E

Job 42 in the SCHL

Job 42 in the SNT

Job 42 in the SUSU

Job 42 in the SUSU2

Job 42 in the SYNO

Job 42 in the TBIAOTANT

Job 42 in the TBT1E

Job 42 in the TBT1E2

Job 42 in the TFTIP

Job 42 in the TFTU

Job 42 in the TGNTATF3T

Job 42 in the THAI

Job 42 in the TNFD

Job 42 in the TNT

Job 42 in the TNTIK

Job 42 in the TNTIL

Job 42 in the TNTIN

Job 42 in the TNTIP

Job 42 in the TNTIZ

Job 42 in the TOMA

Job 42 in the TTENT

Job 42 in the UBG

Job 42 in the UGV

Job 42 in the UGV2

Job 42 in the UGV3

Job 42 in the VBL

Job 42 in the VDCC

Job 42 in the YALU

Job 42 in the YAPE

Job 42 in the YBVTP

Job 42 in the ZBP