1 Chronicles 26 (BOKCV)

1 Hii ndiyo migawanyo ya mabawabu: Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa: Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu. 2 Meshelemia alikuwa na wana wafuatao:Zekaria mzaliwa wa kwanza,Yediaeli wa pili,Zebadia wa tatu,Yathnieli wa nne, 3 Elamu wa tanoYehohanani wa sitana Eliehoenai wa saba. 4 Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao:Shemaya mzaliwa wa kwanza,Yehozabadi wa pili,Yoa wa tatu,Sakari wa nne,Nethaneli wa tano, 5 Amieli wa sita,Isakari wa saba,na Peulethai wa nane.(Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.) 6 Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. 7 Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo. 8 Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili. 9 Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane. 10 Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza), 11 Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu. 12 Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa BWANA kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 13 Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo. 14 Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 15 Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 16 Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: 17 Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. 18 Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe. 19 Hii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari. 20 Katika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu. 21 Wazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli, 22 wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu la BWANA. 23 Kutoka kwa wana wa Amramu, wana wa Ishari, wana wa Hebroni na wana wa Uzieli: 24 Shebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Mose, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina. 25 Jamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi. 26 Shelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi. 27 Baadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la BWANA. 28 Kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake. 29 Kutoka kwa wana wa Ishari: Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli. 30 Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za BWANA na utumishi wa mfalme. 31 Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi. 32 Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.

In Other Versions

1 Chronicles 26 in the ANGEFD

1 Chronicles 26 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 26 in the AS21

1 Chronicles 26 in the BAGH

1 Chronicles 26 in the BBPNG

1 Chronicles 26 in the BBT1E

1 Chronicles 26 in the BDS

1 Chronicles 26 in the BEV

1 Chronicles 26 in the BHAD

1 Chronicles 26 in the BIB

1 Chronicles 26 in the BLPT

1 Chronicles 26 in the BNT

1 Chronicles 26 in the BNTABOOT

1 Chronicles 26 in the BNTLV

1 Chronicles 26 in the BOATCB

1 Chronicles 26 in the BOATCB2

1 Chronicles 26 in the BOBCV

1 Chronicles 26 in the BOCNT

1 Chronicles 26 in the BOECS

1 Chronicles 26 in the BOGWICC

1 Chronicles 26 in the BOHCB

1 Chronicles 26 in the BOHCV

1 Chronicles 26 in the BOHLNT

1 Chronicles 26 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 26 in the BOICB

1 Chronicles 26 in the BOILNTAP

1 Chronicles 26 in the BOITCV

1 Chronicles 26 in the BOKCV2

1 Chronicles 26 in the BOKHWOG

1 Chronicles 26 in the BOKSSV

1 Chronicles 26 in the BOLCB

1 Chronicles 26 in the BOLCB2

1 Chronicles 26 in the BOMCV

1 Chronicles 26 in the BONAV

1 Chronicles 26 in the BONCB

1 Chronicles 26 in the BONLT

1 Chronicles 26 in the BONUT2

1 Chronicles 26 in the BOPLNT

1 Chronicles 26 in the BOSCB

1 Chronicles 26 in the BOSNC

1 Chronicles 26 in the BOTLNT

1 Chronicles 26 in the BOVCB

1 Chronicles 26 in the BOYCB

1 Chronicles 26 in the BPBB

1 Chronicles 26 in the BPH

1 Chronicles 26 in the BSB

1 Chronicles 26 in the CCB

1 Chronicles 26 in the CUV

1 Chronicles 26 in the CUVS

1 Chronicles 26 in the DBT

1 Chronicles 26 in the DGDNT

1 Chronicles 26 in the DHNT

1 Chronicles 26 in the DNT

1 Chronicles 26 in the ELBE

1 Chronicles 26 in the EMTV

1 Chronicles 26 in the ESV

1 Chronicles 26 in the FBV

1 Chronicles 26 in the FEB

1 Chronicles 26 in the GGMNT

1 Chronicles 26 in the GNT

1 Chronicles 26 in the HARY

1 Chronicles 26 in the HNT

1 Chronicles 26 in the IRVA

1 Chronicles 26 in the IRVB

1 Chronicles 26 in the IRVG

1 Chronicles 26 in the IRVH

1 Chronicles 26 in the IRVK

1 Chronicles 26 in the IRVM

1 Chronicles 26 in the IRVM2

1 Chronicles 26 in the IRVO

1 Chronicles 26 in the IRVP

1 Chronicles 26 in the IRVT

1 Chronicles 26 in the IRVT2

1 Chronicles 26 in the IRVU

1 Chronicles 26 in the ISVN

1 Chronicles 26 in the JSNT

1 Chronicles 26 in the KAPI

1 Chronicles 26 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 26 in the KBV

1 Chronicles 26 in the KJV

1 Chronicles 26 in the KNFD

1 Chronicles 26 in the LBA

1 Chronicles 26 in the LBLA

1 Chronicles 26 in the LNT

1 Chronicles 26 in the LSV

1 Chronicles 26 in the MAAL

1 Chronicles 26 in the MBV

1 Chronicles 26 in the MBV2

1 Chronicles 26 in the MHNT

1 Chronicles 26 in the MKNFD

1 Chronicles 26 in the MNG

1 Chronicles 26 in the MNT

1 Chronicles 26 in the MNT2

1 Chronicles 26 in the MRS1T

1 Chronicles 26 in the NAA

1 Chronicles 26 in the NASB

1 Chronicles 26 in the NBLA

1 Chronicles 26 in the NBS

1 Chronicles 26 in the NBVTP

1 Chronicles 26 in the NET2

1 Chronicles 26 in the NIV11

1 Chronicles 26 in the NNT

1 Chronicles 26 in the NNT2

1 Chronicles 26 in the NNT3

1 Chronicles 26 in the PDDPT

1 Chronicles 26 in the PFNT

1 Chronicles 26 in the RMNT

1 Chronicles 26 in the SBIAS

1 Chronicles 26 in the SBIBS

1 Chronicles 26 in the SBIBS2

1 Chronicles 26 in the SBICS

1 Chronicles 26 in the SBIDS

1 Chronicles 26 in the SBIGS

1 Chronicles 26 in the SBIHS

1 Chronicles 26 in the SBIIS

1 Chronicles 26 in the SBIIS2

1 Chronicles 26 in the SBIIS3

1 Chronicles 26 in the SBIKS

1 Chronicles 26 in the SBIKS2

1 Chronicles 26 in the SBIMS

1 Chronicles 26 in the SBIOS

1 Chronicles 26 in the SBIPS

1 Chronicles 26 in the SBISS

1 Chronicles 26 in the SBITS

1 Chronicles 26 in the SBITS2

1 Chronicles 26 in the SBITS3

1 Chronicles 26 in the SBITS4

1 Chronicles 26 in the SBIUS

1 Chronicles 26 in the SBIVS

1 Chronicles 26 in the SBT

1 Chronicles 26 in the SBT1E

1 Chronicles 26 in the SCHL

1 Chronicles 26 in the SNT

1 Chronicles 26 in the SUSU

1 Chronicles 26 in the SUSU2

1 Chronicles 26 in the SYNO

1 Chronicles 26 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 26 in the TBT1E

1 Chronicles 26 in the TBT1E2

1 Chronicles 26 in the TFTIP

1 Chronicles 26 in the TFTU

1 Chronicles 26 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 26 in the THAI

1 Chronicles 26 in the TNFD

1 Chronicles 26 in the TNT

1 Chronicles 26 in the TNTIK

1 Chronicles 26 in the TNTIL

1 Chronicles 26 in the TNTIN

1 Chronicles 26 in the TNTIP

1 Chronicles 26 in the TNTIZ

1 Chronicles 26 in the TOMA

1 Chronicles 26 in the TTENT

1 Chronicles 26 in the UBG

1 Chronicles 26 in the UGV

1 Chronicles 26 in the UGV2

1 Chronicles 26 in the UGV3

1 Chronicles 26 in the VBL

1 Chronicles 26 in the VDCC

1 Chronicles 26 in the YALU

1 Chronicles 26 in the YAPE

1 Chronicles 26 in the YBVTP

1 Chronicles 26 in the ZBP