1 Samuel 16 (BOKCV)

1 BWANA akamwambia Samweli, “Utamlilia Sauli mpaka lini, maadamu nimemkataa asiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli? Jaza pembe yako mafuta, ushike njia uende; ninakutuma kwa Yese huko Bethlehemu. Nimemchagua mmoja wa wanawe kuwa mfalme.” 2 Lakini Samweli akasema, “Nitakwendaje? Sauli atasikia juu ya jambo hili na ataniua.” BWANA akamwambia, “Chukua mtamba wa ngʼombe na useme, ‘Nimekuja kumtolea BWANA dhabihu.’ 3 Mwalike Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakalofanya. Utamtia mafuta kwa ajili yangu yule nitakayekuonyesha.” 4 Samweli akafanya kile BWANA alichosema. Alipofika Bethlehemu, wazee wa mji wakatetemeka walipomlaki. Wakauliza, “Je, umekuja kwa amani?” 5 Samweli akajibu, “Ndiyo, kwa amani; nimekuja kumtolea BWANA dhabihu. Jiwekeni wakfu na mje kwenye dhabihu pamoja nami.” Ndipo akamweka Yese wakfu pamoja na wanawe na kuwaalika kwenye dhabihu. 6 Walipofika, Samweli akamwona Eliabu, naye akafikiri, “Hakika mpakwa mafuta wa BWANA anasimama hapa mbele za BWANA.” 7 Lakini BWANA akamwambia Samweli, “Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. BWANA hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini BWANA hutazama moyoni.” 8 Kisha Yese akamwita Abinadabu na kumpitisha mbele ya Samweli. Lakini Samweli akasema, “Hata huyu BWANA hakumchagua.” 9 Kisha Yese akampitisha Shama, lakini Samweli akasema, “Wala huyu BWANA hakumchagua.” 10 Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “BWANA hajawachagua hawa.” 11 Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?”Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.”Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.” 12 Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.Ndipo BWANA akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.” 13 Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa BWANA akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama. 14 Basi Roho wa BWANA alikuwa ameondoka kwa Sauli, nayo roho mbaya ikaachiwa nafasi na BWANA ili imtese. 15 Watumishi wa Sauli wakamwambia, “Angalia, roho mbaya imeachiwa nafasi na BWANA nayo inakutesa. 16 Basi bwana wetu na aamuru watumishi wake walioko hapa kutafuta mtu ambaye anaweza kupiga kinubi. Atakipiga kinubi wakati roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikujiapo, nawe utajisikia vizuri.” 17 Basi Sauli akawaambia watumishi wake, “Mtafuteni mtu apigaye kinubi vizuri mkamlete kwangu.” 18 Mmoja wa watumishi wake akajibu, “Nimemwona mwana wa Yese Mbethlehemu ambaye anajua kupiga kinubi. Yeye ni mtu hodari na shujaa wa vita. Ni mwenye busara katika kunena, mtu mzuri wa umbo. BWANA yu pamoja naye.” 19 Ndipo Sauli akatuma wajumbe kwa Yese na kumwambia, “Nitumie mwanao Daudi, ambaye anachunga kondoo.” 20 Kwa hiyo Yese akamchukua punda aliyepakizwa mikate, kiriba cha divai na mwana-mbuzi, na kuvipeleka vitu hivyo kwa Sauli pamoja na Daudi mwanawe. 21 Daudi akafika kwa Sauli na kuingia kwenye kazi yake. Sauli akampenda sana, naye Daudi akawa mmoja wa wabeba silaha wake. 22 Basi Sauli akatuma ujumbe kwa Yese, akisema, “Mruhusu Daudi abaki katika utumishi wangu, kwa kuwa ninapendezwa naye.” 23 Kila mara roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ilipomjia Sauli, Daudi alichukua kinubi chake na kupiga. Ndipo Sauli angetulizwa na kujisikia vizuri, nayo ile roho mbaya ingemwacha.

In Other Versions

1 Samuel 16 in the ANGEFD

1 Samuel 16 in the ANTPNG2D

1 Samuel 16 in the AS21

1 Samuel 16 in the BAGH

1 Samuel 16 in the BBPNG

1 Samuel 16 in the BBT1E

1 Samuel 16 in the BDS

1 Samuel 16 in the BEV

1 Samuel 16 in the BHAD

1 Samuel 16 in the BIB

1 Samuel 16 in the BLPT

1 Samuel 16 in the BNT

1 Samuel 16 in the BNTABOOT

1 Samuel 16 in the BNTLV

1 Samuel 16 in the BOATCB

1 Samuel 16 in the BOATCB2

1 Samuel 16 in the BOBCV

1 Samuel 16 in the BOCNT

1 Samuel 16 in the BOECS

1 Samuel 16 in the BOGWICC

1 Samuel 16 in the BOHCB

1 Samuel 16 in the BOHCV

1 Samuel 16 in the BOHLNT

1 Samuel 16 in the BOHNTLTAL

1 Samuel 16 in the BOICB

1 Samuel 16 in the BOILNTAP

1 Samuel 16 in the BOITCV

1 Samuel 16 in the BOKCV2

1 Samuel 16 in the BOKHWOG

1 Samuel 16 in the BOKSSV

1 Samuel 16 in the BOLCB

1 Samuel 16 in the BOLCB2

1 Samuel 16 in the BOMCV

1 Samuel 16 in the BONAV

1 Samuel 16 in the BONCB

1 Samuel 16 in the BONLT

1 Samuel 16 in the BONUT2

1 Samuel 16 in the BOPLNT

1 Samuel 16 in the BOSCB

1 Samuel 16 in the BOSNC

1 Samuel 16 in the BOTLNT

1 Samuel 16 in the BOVCB

1 Samuel 16 in the BOYCB

1 Samuel 16 in the BPBB

1 Samuel 16 in the BPH

1 Samuel 16 in the BSB

1 Samuel 16 in the CCB

1 Samuel 16 in the CUV

1 Samuel 16 in the CUVS

1 Samuel 16 in the DBT

1 Samuel 16 in the DGDNT

1 Samuel 16 in the DHNT

1 Samuel 16 in the DNT

1 Samuel 16 in the ELBE

1 Samuel 16 in the EMTV

1 Samuel 16 in the ESV

1 Samuel 16 in the FBV

1 Samuel 16 in the FEB

1 Samuel 16 in the GGMNT

1 Samuel 16 in the GNT

1 Samuel 16 in the HARY

1 Samuel 16 in the HNT

1 Samuel 16 in the IRVA

1 Samuel 16 in the IRVB

1 Samuel 16 in the IRVG

1 Samuel 16 in the IRVH

1 Samuel 16 in the IRVK

1 Samuel 16 in the IRVM

1 Samuel 16 in the IRVM2

1 Samuel 16 in the IRVO

1 Samuel 16 in the IRVP

1 Samuel 16 in the IRVT

1 Samuel 16 in the IRVT2

1 Samuel 16 in the IRVU

1 Samuel 16 in the ISVN

1 Samuel 16 in the JSNT

1 Samuel 16 in the KAPI

1 Samuel 16 in the KBT1ETNIK

1 Samuel 16 in the KBV

1 Samuel 16 in the KJV

1 Samuel 16 in the KNFD

1 Samuel 16 in the LBA

1 Samuel 16 in the LBLA

1 Samuel 16 in the LNT

1 Samuel 16 in the LSV

1 Samuel 16 in the MAAL

1 Samuel 16 in the MBV

1 Samuel 16 in the MBV2

1 Samuel 16 in the MHNT

1 Samuel 16 in the MKNFD

1 Samuel 16 in the MNG

1 Samuel 16 in the MNT

1 Samuel 16 in the MNT2

1 Samuel 16 in the MRS1T

1 Samuel 16 in the NAA

1 Samuel 16 in the NASB

1 Samuel 16 in the NBLA

1 Samuel 16 in the NBS

1 Samuel 16 in the NBVTP

1 Samuel 16 in the NET2

1 Samuel 16 in the NIV11

1 Samuel 16 in the NNT

1 Samuel 16 in the NNT2

1 Samuel 16 in the NNT3

1 Samuel 16 in the PDDPT

1 Samuel 16 in the PFNT

1 Samuel 16 in the RMNT

1 Samuel 16 in the SBIAS

1 Samuel 16 in the SBIBS

1 Samuel 16 in the SBIBS2

1 Samuel 16 in the SBICS

1 Samuel 16 in the SBIDS

1 Samuel 16 in the SBIGS

1 Samuel 16 in the SBIHS

1 Samuel 16 in the SBIIS

1 Samuel 16 in the SBIIS2

1 Samuel 16 in the SBIIS3

1 Samuel 16 in the SBIKS

1 Samuel 16 in the SBIKS2

1 Samuel 16 in the SBIMS

1 Samuel 16 in the SBIOS

1 Samuel 16 in the SBIPS

1 Samuel 16 in the SBISS

1 Samuel 16 in the SBITS

1 Samuel 16 in the SBITS2

1 Samuel 16 in the SBITS3

1 Samuel 16 in the SBITS4

1 Samuel 16 in the SBIUS

1 Samuel 16 in the SBIVS

1 Samuel 16 in the SBT

1 Samuel 16 in the SBT1E

1 Samuel 16 in the SCHL

1 Samuel 16 in the SNT

1 Samuel 16 in the SUSU

1 Samuel 16 in the SUSU2

1 Samuel 16 in the SYNO

1 Samuel 16 in the TBIAOTANT

1 Samuel 16 in the TBT1E

1 Samuel 16 in the TBT1E2

1 Samuel 16 in the TFTIP

1 Samuel 16 in the TFTU

1 Samuel 16 in the TGNTATF3T

1 Samuel 16 in the THAI

1 Samuel 16 in the TNFD

1 Samuel 16 in the TNT

1 Samuel 16 in the TNTIK

1 Samuel 16 in the TNTIL

1 Samuel 16 in the TNTIN

1 Samuel 16 in the TNTIP

1 Samuel 16 in the TNTIZ

1 Samuel 16 in the TOMA

1 Samuel 16 in the TTENT

1 Samuel 16 in the UBG

1 Samuel 16 in the UGV

1 Samuel 16 in the UGV2

1 Samuel 16 in the UGV3

1 Samuel 16 in the VBL

1 Samuel 16 in the VDCC

1 Samuel 16 in the YALU

1 Samuel 16 in the YAPE

1 Samuel 16 in the YBVTP

1 Samuel 16 in the ZBP