1 Timothy 1 (BOKCV)

1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Kristo Yesu tumaini letu. 2 Kwa Timotheo, mwanangu halisi katika imani:Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. 3 Kama nilivyokusihi wakati nilipokwenda Makedonia, endelea kubaki Efeso, ili kwamba upate kuwaagiza watu wasiendelee kufundisha mafundisho ya uongo 4 wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani. 5 Kusudi la maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli. 6 Watu wengine wamepotoka kutoka haya na kugeukia majadiliano yasiyo na maana kwa kuwa, 7 wanataka kuwa walimu wa sheria, lakini hawajui mambo yale wanayosema wala hayo wanayoyatumainia kwa uthabiti. 8 Tunajua kwamba sheria ni njema ikiwa inatumika kwa halali kama ilivyokusudiwa. 9 Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru; kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji, 10 kwa wazinzi na wahanithi, kwa wale wauzao watu, na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa chochote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli, 11 ambayo yanakubaliana na Injili ya utukufu wa Mungu anayehimidiwa, ambayo mimi nimewekewa amana. 12 Namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona mwaminifu, akaniteua kwa kazi yake. 13 Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri, lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutojua na kutoamini kwangu. 14 Neema ya Bwana wetu ilimiminwa juu yangu kwa wingi, ikiambatana na imani na upendo ulio katika Kristo Yesu. 15 Msemo huu ni wa kweli na unaostahili kukubalika, usemao kwamba: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi, ambao mimi ndiye niliye mbaya kuliko wote. 16 Lakini kwa sababu hiyo nilipata rehema, ili katika mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo Yesu apate kuonyesha uvumilivu wake usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini na wapate uzima wa milele. 17 Basi Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen. 18 Mwanangu Timotheo, ninakupa agizo hili, kwa kadiri ya maneno ya unabii yaliyosemwa kukuhusu, ili kwa kuyafuata upate kupigana vita vizuri, 19 ukiishikilia imani na dhamiri njema, ambazo wengine wamevikataa, na hivyo wakaangamia kwa habari ya imani yao. 20 Miongoni mwao wako Himenayo na Aleksanda, ambao nimemkabidhi Shetani ili wafundishwe wasije wakakufuru.

In Other Versions

1 Timothy 1 in the ANGEFD

1 Timothy 1 in the ANTPNG2D

1 Timothy 1 in the AS21

1 Timothy 1 in the BAGH

1 Timothy 1 in the BBPNG

1 Timothy 1 in the BBT1E

1 Timothy 1 in the BDS

1 Timothy 1 in the BEV

1 Timothy 1 in the BHAD

1 Timothy 1 in the BIB

1 Timothy 1 in the BLPT

1 Timothy 1 in the BNT

1 Timothy 1 in the BNTABOOT

1 Timothy 1 in the BNTLV

1 Timothy 1 in the BOATCB

1 Timothy 1 in the BOATCB2

1 Timothy 1 in the BOBCV

1 Timothy 1 in the BOCNT

1 Timothy 1 in the BOECS

1 Timothy 1 in the BOGWICC

1 Timothy 1 in the BOHCB

1 Timothy 1 in the BOHCV

1 Timothy 1 in the BOHLNT

1 Timothy 1 in the BOHNTLTAL

1 Timothy 1 in the BOICB

1 Timothy 1 in the BOILNTAP

1 Timothy 1 in the BOITCV

1 Timothy 1 in the BOKCV2

1 Timothy 1 in the BOKHWOG

1 Timothy 1 in the BOKSSV

1 Timothy 1 in the BOLCB

1 Timothy 1 in the BOLCB2

1 Timothy 1 in the BOMCV

1 Timothy 1 in the BONAV

1 Timothy 1 in the BONCB

1 Timothy 1 in the BONLT

1 Timothy 1 in the BONUT2

1 Timothy 1 in the BOPLNT

1 Timothy 1 in the BOSCB

1 Timothy 1 in the BOSNC

1 Timothy 1 in the BOTLNT

1 Timothy 1 in the BOVCB

1 Timothy 1 in the BOYCB

1 Timothy 1 in the BPBB

1 Timothy 1 in the BPH

1 Timothy 1 in the BSB

1 Timothy 1 in the CCB

1 Timothy 1 in the CUV

1 Timothy 1 in the CUVS

1 Timothy 1 in the DBT

1 Timothy 1 in the DGDNT

1 Timothy 1 in the DHNT

1 Timothy 1 in the DNT

1 Timothy 1 in the ELBE

1 Timothy 1 in the EMTV

1 Timothy 1 in the ESV

1 Timothy 1 in the FBV

1 Timothy 1 in the FEB

1 Timothy 1 in the GGMNT

1 Timothy 1 in the GNT

1 Timothy 1 in the HARY

1 Timothy 1 in the HNT

1 Timothy 1 in the IRVA

1 Timothy 1 in the IRVB

1 Timothy 1 in the IRVG

1 Timothy 1 in the IRVH

1 Timothy 1 in the IRVK

1 Timothy 1 in the IRVM

1 Timothy 1 in the IRVM2

1 Timothy 1 in the IRVO

1 Timothy 1 in the IRVP

1 Timothy 1 in the IRVT

1 Timothy 1 in the IRVT2

1 Timothy 1 in the IRVU

1 Timothy 1 in the ISVN

1 Timothy 1 in the JSNT

1 Timothy 1 in the KAPI

1 Timothy 1 in the KBT1ETNIK

1 Timothy 1 in the KBV

1 Timothy 1 in the KJV

1 Timothy 1 in the KNFD

1 Timothy 1 in the LBA

1 Timothy 1 in the LBLA

1 Timothy 1 in the LNT

1 Timothy 1 in the LSV

1 Timothy 1 in the MAAL

1 Timothy 1 in the MBV

1 Timothy 1 in the MBV2

1 Timothy 1 in the MHNT

1 Timothy 1 in the MKNFD

1 Timothy 1 in the MNG

1 Timothy 1 in the MNT

1 Timothy 1 in the MNT2

1 Timothy 1 in the MRS1T

1 Timothy 1 in the NAA

1 Timothy 1 in the NASB

1 Timothy 1 in the NBLA

1 Timothy 1 in the NBS

1 Timothy 1 in the NBVTP

1 Timothy 1 in the NET2

1 Timothy 1 in the NIV11

1 Timothy 1 in the NNT

1 Timothy 1 in the NNT2

1 Timothy 1 in the NNT3

1 Timothy 1 in the PDDPT

1 Timothy 1 in the PFNT

1 Timothy 1 in the RMNT

1 Timothy 1 in the SBIAS

1 Timothy 1 in the SBIBS

1 Timothy 1 in the SBIBS2

1 Timothy 1 in the SBICS

1 Timothy 1 in the SBIDS

1 Timothy 1 in the SBIGS

1 Timothy 1 in the SBIHS

1 Timothy 1 in the SBIIS

1 Timothy 1 in the SBIIS2

1 Timothy 1 in the SBIIS3

1 Timothy 1 in the SBIKS

1 Timothy 1 in the SBIKS2

1 Timothy 1 in the SBIMS

1 Timothy 1 in the SBIOS

1 Timothy 1 in the SBIPS

1 Timothy 1 in the SBISS

1 Timothy 1 in the SBITS

1 Timothy 1 in the SBITS2

1 Timothy 1 in the SBITS3

1 Timothy 1 in the SBITS4

1 Timothy 1 in the SBIUS

1 Timothy 1 in the SBIVS

1 Timothy 1 in the SBT

1 Timothy 1 in the SBT1E

1 Timothy 1 in the SCHL

1 Timothy 1 in the SNT

1 Timothy 1 in the SUSU

1 Timothy 1 in the SUSU2

1 Timothy 1 in the SYNO

1 Timothy 1 in the TBIAOTANT

1 Timothy 1 in the TBT1E

1 Timothy 1 in the TBT1E2

1 Timothy 1 in the TFTIP

1 Timothy 1 in the TFTU

1 Timothy 1 in the TGNTATF3T

1 Timothy 1 in the THAI

1 Timothy 1 in the TNFD

1 Timothy 1 in the TNT

1 Timothy 1 in the TNTIK

1 Timothy 1 in the TNTIL

1 Timothy 1 in the TNTIN

1 Timothy 1 in the TNTIP

1 Timothy 1 in the TNTIZ

1 Timothy 1 in the TOMA

1 Timothy 1 in the TTENT

1 Timothy 1 in the UBG

1 Timothy 1 in the UGV

1 Timothy 1 in the UGV2

1 Timothy 1 in the UGV3

1 Timothy 1 in the VBL

1 Timothy 1 in the VDCC

1 Timothy 1 in the YALU

1 Timothy 1 in the YAPE

1 Timothy 1 in the YBVTP

1 Timothy 1 in the ZBP