2 Chronicles 15 (BOKCV)

1 Roho wa BWANA akamjia Azaria mwana wa Odedi. 2 Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. BWANA yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi. 3 Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria. 4 Lakini katika taabu yao walimrudia BWANA, Mungu wa Israeli na kumtafuta, naye akaonekana kwao. 5 Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa yeyote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa. 6 Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina. 7 Lakini kwa habari yenu ninyi, kuweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu.” 8 Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya BWANA iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la BWANA. 9 Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba BWANA Mungu wake alikuwa pamoja naye. 10 Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. 11 Wakati huo wakamtolea BWANA dhabihu za ngʼombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka zile nyara walizoteka. 12 Wakafanya agano kumtafuta BWANA, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote. 13 Wale wote ambao hawangemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke. 14 Wakamwapia BWANA kwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu. 15 Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo BWANA akawastarehesha pande zote. 16 Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. 17 Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika Israeli, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote. 18 Akaleta ndani ya Hekalu la Mungu fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu. 19 Hapakuwepo vita tena mpaka mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.

In Other Versions

2 Chronicles 15 in the ANGEFD

2 Chronicles 15 in the ANTPNG2D

2 Chronicles 15 in the AS21

2 Chronicles 15 in the BAGH

2 Chronicles 15 in the BBPNG

2 Chronicles 15 in the BBT1E

2 Chronicles 15 in the BDS

2 Chronicles 15 in the BEV

2 Chronicles 15 in the BHAD

2 Chronicles 15 in the BIB

2 Chronicles 15 in the BLPT

2 Chronicles 15 in the BNT

2 Chronicles 15 in the BNTABOOT

2 Chronicles 15 in the BNTLV

2 Chronicles 15 in the BOATCB

2 Chronicles 15 in the BOATCB2

2 Chronicles 15 in the BOBCV

2 Chronicles 15 in the BOCNT

2 Chronicles 15 in the BOECS

2 Chronicles 15 in the BOGWICC

2 Chronicles 15 in the BOHCB

2 Chronicles 15 in the BOHCV

2 Chronicles 15 in the BOHLNT

2 Chronicles 15 in the BOHNTLTAL

2 Chronicles 15 in the BOICB

2 Chronicles 15 in the BOILNTAP

2 Chronicles 15 in the BOITCV

2 Chronicles 15 in the BOKCV2

2 Chronicles 15 in the BOKHWOG

2 Chronicles 15 in the BOKSSV

2 Chronicles 15 in the BOLCB

2 Chronicles 15 in the BOLCB2

2 Chronicles 15 in the BOMCV

2 Chronicles 15 in the BONAV

2 Chronicles 15 in the BONCB

2 Chronicles 15 in the BONLT

2 Chronicles 15 in the BONUT2

2 Chronicles 15 in the BOPLNT

2 Chronicles 15 in the BOSCB

2 Chronicles 15 in the BOSNC

2 Chronicles 15 in the BOTLNT

2 Chronicles 15 in the BOVCB

2 Chronicles 15 in the BOYCB

2 Chronicles 15 in the BPBB

2 Chronicles 15 in the BPH

2 Chronicles 15 in the BSB

2 Chronicles 15 in the CCB

2 Chronicles 15 in the CUV

2 Chronicles 15 in the CUVS

2 Chronicles 15 in the DBT

2 Chronicles 15 in the DGDNT

2 Chronicles 15 in the DHNT

2 Chronicles 15 in the DNT

2 Chronicles 15 in the ELBE

2 Chronicles 15 in the EMTV

2 Chronicles 15 in the ESV

2 Chronicles 15 in the FBV

2 Chronicles 15 in the FEB

2 Chronicles 15 in the GGMNT

2 Chronicles 15 in the GNT

2 Chronicles 15 in the HARY

2 Chronicles 15 in the HNT

2 Chronicles 15 in the IRVA

2 Chronicles 15 in the IRVB

2 Chronicles 15 in the IRVG

2 Chronicles 15 in the IRVH

2 Chronicles 15 in the IRVK

2 Chronicles 15 in the IRVM

2 Chronicles 15 in the IRVM2

2 Chronicles 15 in the IRVO

2 Chronicles 15 in the IRVP

2 Chronicles 15 in the IRVT

2 Chronicles 15 in the IRVT2

2 Chronicles 15 in the IRVU

2 Chronicles 15 in the ISVN

2 Chronicles 15 in the JSNT

2 Chronicles 15 in the KAPI

2 Chronicles 15 in the KBT1ETNIK

2 Chronicles 15 in the KBV

2 Chronicles 15 in the KJV

2 Chronicles 15 in the KNFD

2 Chronicles 15 in the LBA

2 Chronicles 15 in the LBLA

2 Chronicles 15 in the LNT

2 Chronicles 15 in the LSV

2 Chronicles 15 in the MAAL

2 Chronicles 15 in the MBV

2 Chronicles 15 in the MBV2

2 Chronicles 15 in the MHNT

2 Chronicles 15 in the MKNFD

2 Chronicles 15 in the MNG

2 Chronicles 15 in the MNT

2 Chronicles 15 in the MNT2

2 Chronicles 15 in the MRS1T

2 Chronicles 15 in the NAA

2 Chronicles 15 in the NASB

2 Chronicles 15 in the NBLA

2 Chronicles 15 in the NBS

2 Chronicles 15 in the NBVTP

2 Chronicles 15 in the NET2

2 Chronicles 15 in the NIV11

2 Chronicles 15 in the NNT

2 Chronicles 15 in the NNT2

2 Chronicles 15 in the NNT3

2 Chronicles 15 in the PDDPT

2 Chronicles 15 in the PFNT

2 Chronicles 15 in the RMNT

2 Chronicles 15 in the SBIAS

2 Chronicles 15 in the SBIBS

2 Chronicles 15 in the SBIBS2

2 Chronicles 15 in the SBICS

2 Chronicles 15 in the SBIDS

2 Chronicles 15 in the SBIGS

2 Chronicles 15 in the SBIHS

2 Chronicles 15 in the SBIIS

2 Chronicles 15 in the SBIIS2

2 Chronicles 15 in the SBIIS3

2 Chronicles 15 in the SBIKS

2 Chronicles 15 in the SBIKS2

2 Chronicles 15 in the SBIMS

2 Chronicles 15 in the SBIOS

2 Chronicles 15 in the SBIPS

2 Chronicles 15 in the SBISS

2 Chronicles 15 in the SBITS

2 Chronicles 15 in the SBITS2

2 Chronicles 15 in the SBITS3

2 Chronicles 15 in the SBITS4

2 Chronicles 15 in the SBIUS

2 Chronicles 15 in the SBIVS

2 Chronicles 15 in the SBT

2 Chronicles 15 in the SBT1E

2 Chronicles 15 in the SCHL

2 Chronicles 15 in the SNT

2 Chronicles 15 in the SUSU

2 Chronicles 15 in the SUSU2

2 Chronicles 15 in the SYNO

2 Chronicles 15 in the TBIAOTANT

2 Chronicles 15 in the TBT1E

2 Chronicles 15 in the TBT1E2

2 Chronicles 15 in the TFTIP

2 Chronicles 15 in the TFTU

2 Chronicles 15 in the TGNTATF3T

2 Chronicles 15 in the THAI

2 Chronicles 15 in the TNFD

2 Chronicles 15 in the TNT

2 Chronicles 15 in the TNTIK

2 Chronicles 15 in the TNTIL

2 Chronicles 15 in the TNTIN

2 Chronicles 15 in the TNTIP

2 Chronicles 15 in the TNTIZ

2 Chronicles 15 in the TOMA

2 Chronicles 15 in the TTENT

2 Chronicles 15 in the UBG

2 Chronicles 15 in the UGV

2 Chronicles 15 in the UGV2

2 Chronicles 15 in the UGV3

2 Chronicles 15 in the VBL

2 Chronicles 15 in the VDCC

2 Chronicles 15 in the YALU

2 Chronicles 15 in the YAPE

2 Chronicles 15 in the YBVTP

2 Chronicles 15 in the ZBP