2 Chronicles 33 (BOKCV)

1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na mitano. 2 Akafanya maovu machoni pa Bwana, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo Bwana aliyafukuza mbele ya Waisraeli. 3 Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa, pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akalisujudia jeshi lote la angani na kuliabudu. 4 Akajenga madhabahu katika Hekalu la BWANA ambamo BWANA alikuwa amesema, “Jina langu litadumu Yerusalemu milele.” 5 Katika nyua zote mbili za Hekalu la BWANA akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la angani. 6 Akawatoa wanawe kuwa kafara kwa kuwapitisha katika moto katika Bonde la Ben-Hinomu, akafanya ulozi, uaguzi na uchawi, akataka ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa BWANA, akaichochea hasira yake. 7 Akachukua ile sanamu aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu la Mungu ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Solomoni, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu niliouchagua kutoka kabila zote za Israeli, nitaliweka Jina langu milele. 8 Sitaifanya tena miguu ya Waisraeli iondoke tena katika nchi niliyowapa baba zenu, ikiwa watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru kuhusu sheria zote, maagizo na amri zilizotolewa kwa mkono wa Mose.” 9 Lakini Manase akawaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu katika upotovu, kiasi kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo BWANA aliwaangamiza mbele ya Waisraeli. 10 BWANA akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali. 11 Hivyo BWANA akaleta juu yao majemadari wa jeshi la mfalme wa Ashuru, ambao walimchukua Manase kwenda kifungoni, wakaweka ndoana katika pua yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli. 12 Katika dhiki yake akamsihi BWANA Mungu wake na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. 13 Naye alipomwomba, BWANA akaguswa na kule kusihi kwake na akasikiliza kilio chake, kwa hiyo akamrudisha Yerusalemu na kwenye ufalme wake. Ndipo Manase akatambua kwamba BWANA ndiye Mungu. 14 Baadaye akajenga ukuta wa nje wa Mji wa Daudi, magharibi mwa chemchemi ya Gihoni katika bonde, hadi kufikia ingilio la Lango la Samaki na akakizunguka kilima cha Ofeli, pia akaufanya kuwa mrefu zaidi. Akawaweka majemadari katika miji yote ya Yuda iliyokuwa imejengewa ngome. 15 Akaondolea mbali miungu ya kigeni na kuondoa sanamu kutoka Hekalu la BWANA pamoja na madhabahu zote alizozijenga katika kile kilima kilichojengwa Hekalu na katika Yerusalemu, akazitupa nje ya mji. 16 Kisha akarudisha madhabahu ya BWANA na kutolea juu yake dhabihu za sadaka za amani pamoja na sadaka za shukrani, naye akawaamuru Yuda wamtumikie BWANA, Mungu wa Israeli. 17 Lakini hata hivyo watu wakaendelea kutoa dhabihu mahali pa juu pa kuabudia miungu, lakini wakimtolea BWANA Mungu wao peke yake. 18 Matukio mengine ya utawala wa Manase, maombi yake kwa Mungu wake na maneno aliyoambiwa na waonaji walionena naye kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. 19 Maombi yake, pamoja na jinsi Mungu alivyoguswa na kusihi kwake, pia dhambi zake zote na kukosa kwake uaminifu pamoja na sehemu alizojenga mahali pa juu pa kuabudia miungu, kule kusimamisha nguzo za Ashera na sanamu kabla ya kujinyenyekeza kwake, yote yameandikwa katika kumbukumbu za waonaji. 20 Manase akalala pamoja na baba zake akazikwa katika jumba lake la kifalme. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake. 21 Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili, alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. 22 Akatenda maovu machoni mwa Bwana, kama baba yake Manase alivyofanya. Amoni akaabudu na kutoa dhabihu kwa sanamu zote alizokuwa ametengeneza Manase. 23 Lakini tofauti na Manase baba yake, hakujinyenyekeza mbele za BWANA, badala yake Amoni aliongeza hatia zaidi na zaidi. 24 Watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, nao wakamuulia kwake nyumbani. 25 Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamefanya hila dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.

In Other Versions

2 Chronicles 33 in the ANGEFD

2 Chronicles 33 in the ANTPNG2D

2 Chronicles 33 in the AS21

2 Chronicles 33 in the BAGH

2 Chronicles 33 in the BBPNG

2 Chronicles 33 in the BBT1E

2 Chronicles 33 in the BDS

2 Chronicles 33 in the BEV

2 Chronicles 33 in the BHAD

2 Chronicles 33 in the BIB

2 Chronicles 33 in the BLPT

2 Chronicles 33 in the BNT

2 Chronicles 33 in the BNTABOOT

2 Chronicles 33 in the BNTLV

2 Chronicles 33 in the BOATCB

2 Chronicles 33 in the BOATCB2

2 Chronicles 33 in the BOBCV

2 Chronicles 33 in the BOCNT

2 Chronicles 33 in the BOECS

2 Chronicles 33 in the BOGWICC

2 Chronicles 33 in the BOHCB

2 Chronicles 33 in the BOHCV

2 Chronicles 33 in the BOHLNT

2 Chronicles 33 in the BOHNTLTAL

2 Chronicles 33 in the BOICB

2 Chronicles 33 in the BOILNTAP

2 Chronicles 33 in the BOITCV

2 Chronicles 33 in the BOKCV2

2 Chronicles 33 in the BOKHWOG

2 Chronicles 33 in the BOKSSV

2 Chronicles 33 in the BOLCB

2 Chronicles 33 in the BOLCB2

2 Chronicles 33 in the BOMCV

2 Chronicles 33 in the BONAV

2 Chronicles 33 in the BONCB

2 Chronicles 33 in the BONLT

2 Chronicles 33 in the BONUT2

2 Chronicles 33 in the BOPLNT

2 Chronicles 33 in the BOSCB

2 Chronicles 33 in the BOSNC

2 Chronicles 33 in the BOTLNT

2 Chronicles 33 in the BOVCB

2 Chronicles 33 in the BOYCB

2 Chronicles 33 in the BPBB

2 Chronicles 33 in the BPH

2 Chronicles 33 in the BSB

2 Chronicles 33 in the CCB

2 Chronicles 33 in the CUV

2 Chronicles 33 in the CUVS

2 Chronicles 33 in the DBT

2 Chronicles 33 in the DGDNT

2 Chronicles 33 in the DHNT

2 Chronicles 33 in the DNT

2 Chronicles 33 in the ELBE

2 Chronicles 33 in the EMTV

2 Chronicles 33 in the ESV

2 Chronicles 33 in the FBV

2 Chronicles 33 in the FEB

2 Chronicles 33 in the GGMNT

2 Chronicles 33 in the GNT

2 Chronicles 33 in the HARY

2 Chronicles 33 in the HNT

2 Chronicles 33 in the IRVA

2 Chronicles 33 in the IRVB

2 Chronicles 33 in the IRVG

2 Chronicles 33 in the IRVH

2 Chronicles 33 in the IRVK

2 Chronicles 33 in the IRVM

2 Chronicles 33 in the IRVM2

2 Chronicles 33 in the IRVO

2 Chronicles 33 in the IRVP

2 Chronicles 33 in the IRVT

2 Chronicles 33 in the IRVT2

2 Chronicles 33 in the IRVU

2 Chronicles 33 in the ISVN

2 Chronicles 33 in the JSNT

2 Chronicles 33 in the KAPI

2 Chronicles 33 in the KBT1ETNIK

2 Chronicles 33 in the KBV

2 Chronicles 33 in the KJV

2 Chronicles 33 in the KNFD

2 Chronicles 33 in the LBA

2 Chronicles 33 in the LBLA

2 Chronicles 33 in the LNT

2 Chronicles 33 in the LSV

2 Chronicles 33 in the MAAL

2 Chronicles 33 in the MBV

2 Chronicles 33 in the MBV2

2 Chronicles 33 in the MHNT

2 Chronicles 33 in the MKNFD

2 Chronicles 33 in the MNG

2 Chronicles 33 in the MNT

2 Chronicles 33 in the MNT2

2 Chronicles 33 in the MRS1T

2 Chronicles 33 in the NAA

2 Chronicles 33 in the NASB

2 Chronicles 33 in the NBLA

2 Chronicles 33 in the NBS

2 Chronicles 33 in the NBVTP

2 Chronicles 33 in the NET2

2 Chronicles 33 in the NIV11

2 Chronicles 33 in the NNT

2 Chronicles 33 in the NNT2

2 Chronicles 33 in the NNT3

2 Chronicles 33 in the PDDPT

2 Chronicles 33 in the PFNT

2 Chronicles 33 in the RMNT

2 Chronicles 33 in the SBIAS

2 Chronicles 33 in the SBIBS

2 Chronicles 33 in the SBIBS2

2 Chronicles 33 in the SBICS

2 Chronicles 33 in the SBIDS

2 Chronicles 33 in the SBIGS

2 Chronicles 33 in the SBIHS

2 Chronicles 33 in the SBIIS

2 Chronicles 33 in the SBIIS2

2 Chronicles 33 in the SBIIS3

2 Chronicles 33 in the SBIKS

2 Chronicles 33 in the SBIKS2

2 Chronicles 33 in the SBIMS

2 Chronicles 33 in the SBIOS

2 Chronicles 33 in the SBIPS

2 Chronicles 33 in the SBISS

2 Chronicles 33 in the SBITS

2 Chronicles 33 in the SBITS2

2 Chronicles 33 in the SBITS3

2 Chronicles 33 in the SBITS4

2 Chronicles 33 in the SBIUS

2 Chronicles 33 in the SBIVS

2 Chronicles 33 in the SBT

2 Chronicles 33 in the SBT1E

2 Chronicles 33 in the SCHL

2 Chronicles 33 in the SNT

2 Chronicles 33 in the SUSU

2 Chronicles 33 in the SUSU2

2 Chronicles 33 in the SYNO

2 Chronicles 33 in the TBIAOTANT

2 Chronicles 33 in the TBT1E

2 Chronicles 33 in the TBT1E2

2 Chronicles 33 in the TFTIP

2 Chronicles 33 in the TFTU

2 Chronicles 33 in the TGNTATF3T

2 Chronicles 33 in the THAI

2 Chronicles 33 in the TNFD

2 Chronicles 33 in the TNT

2 Chronicles 33 in the TNTIK

2 Chronicles 33 in the TNTIL

2 Chronicles 33 in the TNTIN

2 Chronicles 33 in the TNTIP

2 Chronicles 33 in the TNTIZ

2 Chronicles 33 in the TOMA

2 Chronicles 33 in the TTENT

2 Chronicles 33 in the UBG

2 Chronicles 33 in the UGV

2 Chronicles 33 in the UGV2

2 Chronicles 33 in the UGV3

2 Chronicles 33 in the VBL

2 Chronicles 33 in the VDCC

2 Chronicles 33 in the YALU

2 Chronicles 33 in the YAPE

2 Chronicles 33 in the YBVTP

2 Chronicles 33 in the ZBP