Deuteronomy 5 (BOKCV)
1 Mose akawaita Israeli wote, akawaambia:Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata. 2 BWANA Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu. 3 Si kwamba BWANA alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo. 4 BWANA alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima. 5 (Wakati huo nilisimama kati ya BWANA na ninyi kuwatangazia neno la BWANA, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema: 6 “Mimi ndimi BWANA Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. 7 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 8 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji. 9 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 10 lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu. 11 Usilitaje bure jina la BWANA Mungu wako, kwa kuwa BWANA hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. 12 Adhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kama BWANA Mungu wako alivyokuagiza. 13 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote. 14 Lakini siku ya Saba ni Sabato kwa BWANA, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ngʼombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe. 15 Kumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, na BWANA Mungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo BWANA Mungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato. 16 Waheshimu baba yako na mama yako, kama BWANA Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi BWANA Mungu wako anayokupa. 17 Usiue. 18 Usizini. 19 Usiibe. 20 Usimshuhudie jirani yako uongo. 21 Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.” 22 Hizi ndizo amri alizozitangaza BWANA kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi. 23 Mliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi. 24 Nanyi mkasema, “BWANA Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. 25 Lakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya BWANA Mungu wetu zaidi. 26 Ni mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi? 27 Sogea karibu usikie yale yote asemayo BWANA Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho BWANA Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.” 28 BWANA aliwasikia wakati mlipozungumza nami, na BWANA akaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri. 29 Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele! 30 “Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao. 31 Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.” 32 Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale BWANA Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto. 33 Fuateni yale yote ambayo BWANA Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.
In Other Versions
Deuteronomy 5 in the ANGEFD
Deuteronomy 5 in the ANTPNG2D
Deuteronomy 5 in the AS21
Deuteronomy 5 in the BAGH
Deuteronomy 5 in the BBPNG
Deuteronomy 5 in the BBT1E
Deuteronomy 5 in the BDS
Deuteronomy 5 in the BEV
Deuteronomy 5 in the BHAD
Deuteronomy 5 in the BIB
Deuteronomy 5 in the BLPT
Deuteronomy 5 in the BNT
Deuteronomy 5 in the BNTABOOT
Deuteronomy 5 in the BNTLV
Deuteronomy 5 in the BOATCB
Deuteronomy 5 in the BOATCB2
Deuteronomy 5 in the BOBCV
Deuteronomy 5 in the BOCNT
Deuteronomy 5 in the BOECS
Deuteronomy 5 in the BOGWICC
Deuteronomy 5 in the BOHCB
Deuteronomy 5 in the BOHCV
Deuteronomy 5 in the BOHLNT
Deuteronomy 5 in the BOHNTLTAL
Deuteronomy 5 in the BOICB
Deuteronomy 5 in the BOILNTAP
Deuteronomy 5 in the BOITCV
Deuteronomy 5 in the BOKCV2
Deuteronomy 5 in the BOKHWOG
Deuteronomy 5 in the BOKSSV
Deuteronomy 5 in the BOLCB
Deuteronomy 5 in the BOLCB2
Deuteronomy 5 in the BOMCV
Deuteronomy 5 in the BONAV
Deuteronomy 5 in the BONCB
Deuteronomy 5 in the BONLT
Deuteronomy 5 in the BONUT2
Deuteronomy 5 in the BOPLNT
Deuteronomy 5 in the BOSCB
Deuteronomy 5 in the BOSNC
Deuteronomy 5 in the BOTLNT
Deuteronomy 5 in the BOVCB
Deuteronomy 5 in the BOYCB
Deuteronomy 5 in the BPBB
Deuteronomy 5 in the BPH
Deuteronomy 5 in the BSB
Deuteronomy 5 in the CCB
Deuteronomy 5 in the CUV
Deuteronomy 5 in the CUVS
Deuteronomy 5 in the DBT
Deuteronomy 5 in the DGDNT
Deuteronomy 5 in the DHNT
Deuteronomy 5 in the DNT
Deuteronomy 5 in the ELBE
Deuteronomy 5 in the EMTV
Deuteronomy 5 in the ESV
Deuteronomy 5 in the FBV
Deuteronomy 5 in the FEB
Deuteronomy 5 in the GGMNT
Deuteronomy 5 in the GNT
Deuteronomy 5 in the HARY
Deuteronomy 5 in the HNT
Deuteronomy 5 in the IRVA
Deuteronomy 5 in the IRVB
Deuteronomy 5 in the IRVG
Deuteronomy 5 in the IRVH
Deuteronomy 5 in the IRVK
Deuteronomy 5 in the IRVM
Deuteronomy 5 in the IRVM2
Deuteronomy 5 in the IRVO
Deuteronomy 5 in the IRVP
Deuteronomy 5 in the IRVT
Deuteronomy 5 in the IRVT2
Deuteronomy 5 in the IRVU
Deuteronomy 5 in the ISVN
Deuteronomy 5 in the JSNT
Deuteronomy 5 in the KAPI
Deuteronomy 5 in the KBT1ETNIK
Deuteronomy 5 in the KBV
Deuteronomy 5 in the KJV
Deuteronomy 5 in the KNFD
Deuteronomy 5 in the LBA
Deuteronomy 5 in the LBLA
Deuteronomy 5 in the LNT
Deuteronomy 5 in the LSV
Deuteronomy 5 in the MAAL
Deuteronomy 5 in the MBV
Deuteronomy 5 in the MBV2
Deuteronomy 5 in the MHNT
Deuteronomy 5 in the MKNFD
Deuteronomy 5 in the MNG
Deuteronomy 5 in the MNT
Deuteronomy 5 in the MNT2
Deuteronomy 5 in the MRS1T
Deuteronomy 5 in the NAA
Deuteronomy 5 in the NASB
Deuteronomy 5 in the NBLA
Deuteronomy 5 in the NBS
Deuteronomy 5 in the NBVTP
Deuteronomy 5 in the NET2
Deuteronomy 5 in the NIV11
Deuteronomy 5 in the NNT
Deuteronomy 5 in the NNT2
Deuteronomy 5 in the NNT3
Deuteronomy 5 in the PDDPT
Deuteronomy 5 in the PFNT
Deuteronomy 5 in the RMNT
Deuteronomy 5 in the SBIAS
Deuteronomy 5 in the SBIBS
Deuteronomy 5 in the SBIBS2
Deuteronomy 5 in the SBICS
Deuteronomy 5 in the SBIDS
Deuteronomy 5 in the SBIGS
Deuteronomy 5 in the SBIHS
Deuteronomy 5 in the SBIIS
Deuteronomy 5 in the SBIIS2
Deuteronomy 5 in the SBIIS3
Deuteronomy 5 in the SBIKS
Deuteronomy 5 in the SBIKS2
Deuteronomy 5 in the SBIMS
Deuteronomy 5 in the SBIOS
Deuteronomy 5 in the SBIPS
Deuteronomy 5 in the SBISS
Deuteronomy 5 in the SBITS
Deuteronomy 5 in the SBITS2
Deuteronomy 5 in the SBITS3
Deuteronomy 5 in the SBITS4
Deuteronomy 5 in the SBIUS
Deuteronomy 5 in the SBIVS
Deuteronomy 5 in the SBT
Deuteronomy 5 in the SBT1E
Deuteronomy 5 in the SCHL
Deuteronomy 5 in the SNT
Deuteronomy 5 in the SUSU
Deuteronomy 5 in the SUSU2
Deuteronomy 5 in the SYNO
Deuteronomy 5 in the TBIAOTANT
Deuteronomy 5 in the TBT1E
Deuteronomy 5 in the TBT1E2
Deuteronomy 5 in the TFTIP
Deuteronomy 5 in the TFTU
Deuteronomy 5 in the TGNTATF3T
Deuteronomy 5 in the THAI
Deuteronomy 5 in the TNFD
Deuteronomy 5 in the TNT
Deuteronomy 5 in the TNTIK
Deuteronomy 5 in the TNTIL
Deuteronomy 5 in the TNTIN
Deuteronomy 5 in the TNTIP
Deuteronomy 5 in the TNTIZ
Deuteronomy 5 in the TOMA
Deuteronomy 5 in the TTENT
Deuteronomy 5 in the UBG
Deuteronomy 5 in the UGV
Deuteronomy 5 in the UGV2
Deuteronomy 5 in the UGV3
Deuteronomy 5 in the VBL
Deuteronomy 5 in the VDCC
Deuteronomy 5 in the YALU
Deuteronomy 5 in the YAPE
Deuteronomy 5 in the YBVTP
Deuteronomy 5 in the ZBP