Exodus 27 (BOKCV)
1 “Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu; itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano. 2 Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba. 3 Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto. 4 Kisha tengenezea hayo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila moja ya hizo pembe nne za huo wavu. 5 Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. 6 Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, na uifunike kwa shaba. 7 Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe pande mbili za madhabahu inapobebwa. 8 Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani. 9 “Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, 10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11 Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 12 “Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini, nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi. 13 Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 15 Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16 “Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne. 17 Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba. 18 Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba. 19 Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba. 20 “Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake mfululizo. 21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Aroni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za BWANA. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo.
In Other Versions
Exodus 27 in the ANGEFD
Exodus 27 in the ANTPNG2D
Exodus 27 in the AS21
Exodus 27 in the BAGH
Exodus 27 in the BBPNG
Exodus 27 in the BBT1E
Exodus 27 in the BDS
Exodus 27 in the BEV
Exodus 27 in the BHAD
Exodus 27 in the BIB
Exodus 27 in the BLPT
Exodus 27 in the BNT
Exodus 27 in the BNTABOOT
Exodus 27 in the BNTLV
Exodus 27 in the BOATCB
Exodus 27 in the BOATCB2
Exodus 27 in the BOBCV
Exodus 27 in the BOCNT
Exodus 27 in the BOECS
Exodus 27 in the BOGWICC
Exodus 27 in the BOHCB
Exodus 27 in the BOHCV
Exodus 27 in the BOHLNT
Exodus 27 in the BOHNTLTAL
Exodus 27 in the BOICB
Exodus 27 in the BOILNTAP
Exodus 27 in the BOITCV
Exodus 27 in the BOKCV2
Exodus 27 in the BOKHWOG
Exodus 27 in the BOKSSV
Exodus 27 in the BOLCB
Exodus 27 in the BOLCB2
Exodus 27 in the BOMCV
Exodus 27 in the BONAV
Exodus 27 in the BONCB
Exodus 27 in the BONLT
Exodus 27 in the BONUT2
Exodus 27 in the BOPLNT
Exodus 27 in the BOSCB
Exodus 27 in the BOSNC
Exodus 27 in the BOTLNT
Exodus 27 in the BOVCB
Exodus 27 in the BOYCB
Exodus 27 in the BPBB
Exodus 27 in the BPH
Exodus 27 in the BSB
Exodus 27 in the CCB
Exodus 27 in the CUV
Exodus 27 in the CUVS
Exodus 27 in the DBT
Exodus 27 in the DGDNT
Exodus 27 in the DHNT
Exodus 27 in the DNT
Exodus 27 in the ELBE
Exodus 27 in the EMTV
Exodus 27 in the ESV
Exodus 27 in the FBV
Exodus 27 in the FEB
Exodus 27 in the GGMNT
Exodus 27 in the GNT
Exodus 27 in the HARY
Exodus 27 in the HNT
Exodus 27 in the IRVA
Exodus 27 in the IRVB
Exodus 27 in the IRVG
Exodus 27 in the IRVH
Exodus 27 in the IRVK
Exodus 27 in the IRVM
Exodus 27 in the IRVM2
Exodus 27 in the IRVO
Exodus 27 in the IRVP
Exodus 27 in the IRVT
Exodus 27 in the IRVT2
Exodus 27 in the IRVU
Exodus 27 in the ISVN
Exodus 27 in the JSNT
Exodus 27 in the KAPI
Exodus 27 in the KBT1ETNIK
Exodus 27 in the KBV
Exodus 27 in the KJV
Exodus 27 in the KNFD
Exodus 27 in the LBA
Exodus 27 in the LBLA
Exodus 27 in the LNT
Exodus 27 in the LSV
Exodus 27 in the MAAL
Exodus 27 in the MBV
Exodus 27 in the MBV2
Exodus 27 in the MHNT
Exodus 27 in the MKNFD
Exodus 27 in the MNG
Exodus 27 in the MNT
Exodus 27 in the MNT2
Exodus 27 in the MRS1T
Exodus 27 in the NAA
Exodus 27 in the NASB
Exodus 27 in the NBLA
Exodus 27 in the NBS
Exodus 27 in the NBVTP
Exodus 27 in the NET2
Exodus 27 in the NIV11
Exodus 27 in the NNT
Exodus 27 in the NNT2
Exodus 27 in the NNT3
Exodus 27 in the PDDPT
Exodus 27 in the PFNT
Exodus 27 in the RMNT
Exodus 27 in the SBIAS
Exodus 27 in the SBIBS
Exodus 27 in the SBIBS2
Exodus 27 in the SBICS
Exodus 27 in the SBIDS
Exodus 27 in the SBIGS
Exodus 27 in the SBIHS
Exodus 27 in the SBIIS
Exodus 27 in the SBIIS2
Exodus 27 in the SBIIS3
Exodus 27 in the SBIKS
Exodus 27 in the SBIKS2
Exodus 27 in the SBIMS
Exodus 27 in the SBIOS
Exodus 27 in the SBIPS
Exodus 27 in the SBISS
Exodus 27 in the SBITS
Exodus 27 in the SBITS2
Exodus 27 in the SBITS3
Exodus 27 in the SBITS4
Exodus 27 in the SBIUS
Exodus 27 in the SBIVS
Exodus 27 in the SBT
Exodus 27 in the SBT1E
Exodus 27 in the SCHL
Exodus 27 in the SNT
Exodus 27 in the SUSU
Exodus 27 in the SUSU2
Exodus 27 in the SYNO
Exodus 27 in the TBIAOTANT
Exodus 27 in the TBT1E
Exodus 27 in the TBT1E2
Exodus 27 in the TFTIP
Exodus 27 in the TFTU
Exodus 27 in the TGNTATF3T
Exodus 27 in the THAI
Exodus 27 in the TNFD
Exodus 27 in the TNT
Exodus 27 in the TNTIK
Exodus 27 in the TNTIL
Exodus 27 in the TNTIN
Exodus 27 in the TNTIP
Exodus 27 in the TNTIZ
Exodus 27 in the TOMA
Exodus 27 in the TTENT
Exodus 27 in the UBG
Exodus 27 in the UGV
Exodus 27 in the UGV2
Exodus 27 in the UGV3
Exodus 27 in the VBL
Exodus 27 in the VDCC
Exodus 27 in the YALU
Exodus 27 in the YAPE
Exodus 27 in the YBVTP
Exodus 27 in the ZBP