Ezekiel 28 (BOKCV)
1 Neno la BWANA likanijia kusema: 2 “Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Kwa sababu moyo wako umejivunana umesema, “Mimi ni mungu;nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungukatika moyo wa bahari.”Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu,ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu. 3 Je, wewe una hekima kuliko Danieli?Je, hakuna siri iliyofichika kwako? 4 Kwa hekima yako na ufahamu wako,umejipatia utajiri,nawe umejikusanyia dhahabuna fedha katika hazina zako. 5 Kwa werevu wako mwingi katika biashara,umeongeza utajiri wakona kwa sababu ya utajiri wakomoyo wako umekuwa na kiburi. 6 “ ‘Kwa hiyo, hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Kwa sababu unafikiri una hekima,mwenye hekima kama mungu, 7 mimi nitawaleta wageni dhidi yako,taifa katili kuliko yote;watafuta panga zao dhidi ya uzuri wa hekima yako,na kuchafua fahari yako inayongʼaa. 8 Watakushusha chini shimoni,nawe utakufa kifo cha kikatilikatika moyo wa bahari. 9 Je, wakati huo utasema, “Mimi ni mungu,”mbele ya wale wanaokuua?Utakuwa mwanadamu tu, wala si mungu,mikononi mwa hao wanaokuua. 10 Utakufa kifo cha wasiotahiriwakwa mkono wa wageni.Kwa kuwa mimi nimenena, asema BWANA Mwenyezi.’ ” 11 Neno la BWANA likanijia kusema: 12 “Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu,ukiwa umejaa hekimana mkamilifu katika uzuri. 13 Ulikuwa ndani ya Edeni,bustani ya Mungu;kila kito cha thamani kilikupamba:akiki nyekundu, yakuti manjano na zumaridi,krisolitho, shohamu na yaspi,yakuti samawi, almasi na zabarajadi.Kuwekwa kwa hayo mapambo na kushikizwa kwakekulifanywa kwa dhahabu;siku ile ulipoumbwa yaliandaliwa tayari. 14 Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi,kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu.Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu;ulitembea katikati ya vito vya moto. 15 Ulikuwa mnyofu katika njia zakotangu siku ile ya kuumbwa kwako,hadi uovu ulipoonekana ndani yako. 16 Kutokana na biashara yako iliyoenea,ulijazwa na dhuluma,nawe ukatenda dhambi.Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu,nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi,kutoka katikati ya vito vya moto. 17 Moyo wako ukawa na kiburikwa ajili ya uzuri wako,nawe ukaiharibu hekima yakokwa sababu ya fahari yako.Kwa hiyo nikakutupa chini;nimekufanya kioja mbele ya wafalme. 18 Kwa dhambi zako nyingi na biashara yako ya dhuluma,umenajisi mahali pako patakatifu.Kwa hiyo nilifanya moto utoke ndani yako,nao ukakuteketeza,nami nikakufanya majivu juu ya nchi,machoni pa wote waliokuwa wakitazama. 19 Mataifa yote yaliyokujuayanakustajabia;umefikia mwisho wa kutishana hutakuwepo tena milele.’ ” 20 Neno la BWANA likanijia kusema: 21 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake, 22 nawe useme: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni,nami nitapata utukufu ndani yako.Nao watajua kwamba Mimi ndimi BWANA,nitakapotekeleza hukumu zanguna kuonyesha utakatifu wangu ndani yake. 23 Nitapeleka tauni ndani yakena kufanya damu itiririke katika barabara zake.Waliochinjwa wataanguka ndani yake,kwa upanga dhidi yake kila upande.Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi BWANA. 24 “ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi BWANA Mwenyezi. 25 “ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo. 26 Wataishi humo kwa salama na watajenga nyumba na kupanda mashamba ya mizabibu, wataishi kwa salama nitakapowaadhibu majirani zao wote ambao waliwafanyia uovu. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi BWANA, Mungu wao.’ ”
In Other Versions
Ezekiel 28 in the ANGEFD
Ezekiel 28 in the ANTPNG2D
Ezekiel 28 in the AS21
Ezekiel 28 in the BAGH
Ezekiel 28 in the BBPNG
Ezekiel 28 in the BBT1E
Ezekiel 28 in the BDS
Ezekiel 28 in the BEV
Ezekiel 28 in the BHAD
Ezekiel 28 in the BIB
Ezekiel 28 in the BLPT
Ezekiel 28 in the BNT
Ezekiel 28 in the BNTABOOT
Ezekiel 28 in the BNTLV
Ezekiel 28 in the BOATCB
Ezekiel 28 in the BOATCB2
Ezekiel 28 in the BOBCV
Ezekiel 28 in the BOCNT
Ezekiel 28 in the BOECS
Ezekiel 28 in the BOGWICC
Ezekiel 28 in the BOHCB
Ezekiel 28 in the BOHCV
Ezekiel 28 in the BOHLNT
Ezekiel 28 in the BOHNTLTAL
Ezekiel 28 in the BOICB
Ezekiel 28 in the BOILNTAP
Ezekiel 28 in the BOITCV
Ezekiel 28 in the BOKCV2
Ezekiel 28 in the BOKHWOG
Ezekiel 28 in the BOKSSV
Ezekiel 28 in the BOLCB
Ezekiel 28 in the BOLCB2
Ezekiel 28 in the BOMCV
Ezekiel 28 in the BONAV
Ezekiel 28 in the BONCB
Ezekiel 28 in the BONLT
Ezekiel 28 in the BONUT2
Ezekiel 28 in the BOPLNT
Ezekiel 28 in the BOSCB
Ezekiel 28 in the BOSNC
Ezekiel 28 in the BOTLNT
Ezekiel 28 in the BOVCB
Ezekiel 28 in the BOYCB
Ezekiel 28 in the BPBB
Ezekiel 28 in the BPH
Ezekiel 28 in the BSB
Ezekiel 28 in the CCB
Ezekiel 28 in the CUV
Ezekiel 28 in the CUVS
Ezekiel 28 in the DBT
Ezekiel 28 in the DGDNT
Ezekiel 28 in the DHNT
Ezekiel 28 in the DNT
Ezekiel 28 in the ELBE
Ezekiel 28 in the EMTV
Ezekiel 28 in the ESV
Ezekiel 28 in the FBV
Ezekiel 28 in the FEB
Ezekiel 28 in the GGMNT
Ezekiel 28 in the GNT
Ezekiel 28 in the HARY
Ezekiel 28 in the HNT
Ezekiel 28 in the IRVA
Ezekiel 28 in the IRVB
Ezekiel 28 in the IRVG
Ezekiel 28 in the IRVH
Ezekiel 28 in the IRVK
Ezekiel 28 in the IRVM
Ezekiel 28 in the IRVM2
Ezekiel 28 in the IRVO
Ezekiel 28 in the IRVP
Ezekiel 28 in the IRVT
Ezekiel 28 in the IRVT2
Ezekiel 28 in the IRVU
Ezekiel 28 in the ISVN
Ezekiel 28 in the JSNT
Ezekiel 28 in the KAPI
Ezekiel 28 in the KBT1ETNIK
Ezekiel 28 in the KBV
Ezekiel 28 in the KJV
Ezekiel 28 in the KNFD
Ezekiel 28 in the LBA
Ezekiel 28 in the LBLA
Ezekiel 28 in the LNT
Ezekiel 28 in the LSV
Ezekiel 28 in the MAAL
Ezekiel 28 in the MBV
Ezekiel 28 in the MBV2
Ezekiel 28 in the MHNT
Ezekiel 28 in the MKNFD
Ezekiel 28 in the MNG
Ezekiel 28 in the MNT
Ezekiel 28 in the MNT2
Ezekiel 28 in the MRS1T
Ezekiel 28 in the NAA
Ezekiel 28 in the NASB
Ezekiel 28 in the NBLA
Ezekiel 28 in the NBS
Ezekiel 28 in the NBVTP
Ezekiel 28 in the NET2
Ezekiel 28 in the NIV11
Ezekiel 28 in the NNT
Ezekiel 28 in the NNT2
Ezekiel 28 in the NNT3
Ezekiel 28 in the PDDPT
Ezekiel 28 in the PFNT
Ezekiel 28 in the RMNT
Ezekiel 28 in the SBIAS
Ezekiel 28 in the SBIBS
Ezekiel 28 in the SBIBS2
Ezekiel 28 in the SBICS
Ezekiel 28 in the SBIDS
Ezekiel 28 in the SBIGS
Ezekiel 28 in the SBIHS
Ezekiel 28 in the SBIIS
Ezekiel 28 in the SBIIS2
Ezekiel 28 in the SBIIS3
Ezekiel 28 in the SBIKS
Ezekiel 28 in the SBIKS2
Ezekiel 28 in the SBIMS
Ezekiel 28 in the SBIOS
Ezekiel 28 in the SBIPS
Ezekiel 28 in the SBISS
Ezekiel 28 in the SBITS
Ezekiel 28 in the SBITS2
Ezekiel 28 in the SBITS3
Ezekiel 28 in the SBITS4
Ezekiel 28 in the SBIUS
Ezekiel 28 in the SBIVS
Ezekiel 28 in the SBT
Ezekiel 28 in the SBT1E
Ezekiel 28 in the SCHL
Ezekiel 28 in the SNT
Ezekiel 28 in the SUSU
Ezekiel 28 in the SUSU2
Ezekiel 28 in the SYNO
Ezekiel 28 in the TBIAOTANT
Ezekiel 28 in the TBT1E
Ezekiel 28 in the TBT1E2
Ezekiel 28 in the TFTIP
Ezekiel 28 in the TFTU
Ezekiel 28 in the TGNTATF3T
Ezekiel 28 in the THAI
Ezekiel 28 in the TNFD
Ezekiel 28 in the TNT
Ezekiel 28 in the TNTIK
Ezekiel 28 in the TNTIL
Ezekiel 28 in the TNTIN
Ezekiel 28 in the TNTIP
Ezekiel 28 in the TNTIZ
Ezekiel 28 in the TOMA
Ezekiel 28 in the TTENT
Ezekiel 28 in the UBG
Ezekiel 28 in the UGV
Ezekiel 28 in the UGV2
Ezekiel 28 in the UGV3
Ezekiel 28 in the VBL
Ezekiel 28 in the VDCC
Ezekiel 28 in the YALU
Ezekiel 28 in the YAPE
Ezekiel 28 in the YBVTP
Ezekiel 28 in the ZBP