Genesis 15 (BOKCV)
1 Baada ya jambo hili, neno la BWANA likamjia Abramu katika maono:“Usiogope, Abramu.Mimi ni ngao yako,na thawabu yako kubwa sana.” 2 Lakini Abramu akasema, “Ee BWANA Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” 3 Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.” 4 Ndipo neno la BWANA lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.” 5 Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.” 6 Abramu akamwamini BWANA, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki. 7 Pia akamwambia, “Mimi ndimi BWANA, niliyekutoa toka Uru ya Wakaldayo nikupe nchi hii uimiliki.” 8 Lakini Abramu akasema, “Ee BWANA Mwenyezi, nitawezaje kujua kwamba nitapata kuimiliki?” 9 Ndipo BWANA akamwambia, “Niletee mtamba wa ngʼombe, mbuzi na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa.” 10 Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege, hakuwapasua vipande viwili. 11 Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza. 12 Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake. 13 Kisha BWANA akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne. 14 Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi. 15 Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee mwema. 16 Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.” 17 Wakati jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama. 18 Siku hiyo BWANA akafanya Agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri hadi mto ule mkubwa, Frati, 19 yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, 20 Wahiti, Waperizi, Warefai, 21 Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”
In Other Versions
Genesis 15 in the ANGEFD
Genesis 15 in the ANTPNG2D
Genesis 15 in the AS21
Genesis 15 in the BAGH
Genesis 15 in the BBPNG
Genesis 15 in the BBT1E
Genesis 15 in the BDS
Genesis 15 in the BEV
Genesis 15 in the BHAD
Genesis 15 in the BIB
Genesis 15 in the BLPT
Genesis 15 in the BNT
Genesis 15 in the BNTABOOT
Genesis 15 in the BNTLV
Genesis 15 in the BOATCB
Genesis 15 in the BOATCB2
Genesis 15 in the BOBCV
Genesis 15 in the BOCNT
Genesis 15 in the BOECS
Genesis 15 in the BOGWICC
Genesis 15 in the BOHCB
Genesis 15 in the BOHCV
Genesis 15 in the BOHLNT
Genesis 15 in the BOHNTLTAL
Genesis 15 in the BOICB
Genesis 15 in the BOILNTAP
Genesis 15 in the BOITCV
Genesis 15 in the BOKCV2
Genesis 15 in the BOKHWOG
Genesis 15 in the BOKSSV
Genesis 15 in the BOLCB
Genesis 15 in the BOLCB2
Genesis 15 in the BOMCV
Genesis 15 in the BONAV
Genesis 15 in the BONCB
Genesis 15 in the BONLT
Genesis 15 in the BONUT2
Genesis 15 in the BOPLNT
Genesis 15 in the BOSCB
Genesis 15 in the BOSNC
Genesis 15 in the BOTLNT
Genesis 15 in the BOVCB
Genesis 15 in the BOYCB
Genesis 15 in the BPBB
Genesis 15 in the BPH
Genesis 15 in the BSB
Genesis 15 in the CCB
Genesis 15 in the CUV
Genesis 15 in the CUVS
Genesis 15 in the DBT
Genesis 15 in the DGDNT
Genesis 15 in the DHNT
Genesis 15 in the DNT
Genesis 15 in the ELBE
Genesis 15 in the EMTV
Genesis 15 in the ESV
Genesis 15 in the FBV
Genesis 15 in the FEB
Genesis 15 in the GGMNT
Genesis 15 in the GNT
Genesis 15 in the HARY
Genesis 15 in the HNT
Genesis 15 in the IRVA
Genesis 15 in the IRVB
Genesis 15 in the IRVG
Genesis 15 in the IRVH
Genesis 15 in the IRVK
Genesis 15 in the IRVM
Genesis 15 in the IRVM2
Genesis 15 in the IRVO
Genesis 15 in the IRVP
Genesis 15 in the IRVT
Genesis 15 in the IRVT2
Genesis 15 in the IRVU
Genesis 15 in the ISVN
Genesis 15 in the JSNT
Genesis 15 in the KAPI
Genesis 15 in the KBT1ETNIK
Genesis 15 in the KBV
Genesis 15 in the KJV
Genesis 15 in the KNFD
Genesis 15 in the LBA
Genesis 15 in the LBLA
Genesis 15 in the LNT
Genesis 15 in the LSV
Genesis 15 in the MAAL
Genesis 15 in the MBV
Genesis 15 in the MBV2
Genesis 15 in the MHNT
Genesis 15 in the MKNFD
Genesis 15 in the MNG
Genesis 15 in the MNT
Genesis 15 in the MNT2
Genesis 15 in the MRS1T
Genesis 15 in the NAA
Genesis 15 in the NASB
Genesis 15 in the NBLA
Genesis 15 in the NBS
Genesis 15 in the NBVTP
Genesis 15 in the NET2
Genesis 15 in the NIV11
Genesis 15 in the NNT
Genesis 15 in the NNT2
Genesis 15 in the NNT3
Genesis 15 in the PDDPT
Genesis 15 in the PFNT
Genesis 15 in the RMNT
Genesis 15 in the SBIAS
Genesis 15 in the SBIBS
Genesis 15 in the SBIBS2
Genesis 15 in the SBICS
Genesis 15 in the SBIDS
Genesis 15 in the SBIGS
Genesis 15 in the SBIHS
Genesis 15 in the SBIIS
Genesis 15 in the SBIIS2
Genesis 15 in the SBIIS3
Genesis 15 in the SBIKS
Genesis 15 in the SBIKS2
Genesis 15 in the SBIMS
Genesis 15 in the SBIOS
Genesis 15 in the SBIPS
Genesis 15 in the SBISS
Genesis 15 in the SBITS
Genesis 15 in the SBITS2
Genesis 15 in the SBITS3
Genesis 15 in the SBITS4
Genesis 15 in the SBIUS
Genesis 15 in the SBIVS
Genesis 15 in the SBT
Genesis 15 in the SBT1E
Genesis 15 in the SCHL
Genesis 15 in the SNT
Genesis 15 in the SUSU
Genesis 15 in the SUSU2
Genesis 15 in the SYNO
Genesis 15 in the TBIAOTANT
Genesis 15 in the TBT1E
Genesis 15 in the TBT1E2
Genesis 15 in the TFTIP
Genesis 15 in the TFTU
Genesis 15 in the TGNTATF3T
Genesis 15 in the THAI
Genesis 15 in the TNFD
Genesis 15 in the TNT
Genesis 15 in the TNTIK
Genesis 15 in the TNTIL
Genesis 15 in the TNTIN
Genesis 15 in the TNTIP
Genesis 15 in the TNTIZ
Genesis 15 in the TOMA
Genesis 15 in the TTENT
Genesis 15 in the UBG
Genesis 15 in the UGV
Genesis 15 in the UGV2
Genesis 15 in the UGV3
Genesis 15 in the VBL
Genesis 15 in the VDCC
Genesis 15 in the YALU
Genesis 15 in the YAPE
Genesis 15 in the YBVTP
Genesis 15 in the ZBP