Genesis 20 (BOKCV)
1 Basi Abrahamu akaendelea mbele kutoka huko hadi nchi ya Negebu na akaishi kati ya Kadeshi na Shuri. Kwa muda mfupi alikaa Gerari kama mgeni, 2 huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua. 3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto wakati wa usiku na kumwambia, “Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu.” 4 Wakati huo Abimeleki alikuwa bado hajamsogelea, kwa hiyo akasema, “Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia? 5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi.” 6 Kisha Mungu akamwambia katika ndoto, “Ndiyo, najua ya kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse. 7 Sasa umrudishe huyo mke wa mtu, kwa maana ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini kama hutamrudisha, ujue kwa hakika kuwa wewe na watu wako wote mtakufa.” 8 Kesho yake asubuhi na mapema Abimeleki akawaita maafisa wake wote, na baada ya kuwaambia yote yaliyotokea, waliogopa sana. 9 Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu na kumwambia, “Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii juu yangu na ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika.” 10 Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?” 11 Abrahamu akajibu, “Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. 13 Wakati BWANA aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, “Huyu ni kaka yangu.” ’ ” 14 Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ngʼombe, na watumwa wa kiume na wa kike akampa Abrahamu, akamrudisha Sara kwa mumewe. 15 Abimeleki akasema, “Nchi yangu iko mbele yako, ishi popote unapotaka.” 16 Akamwambia Sara, “Ninampa kaka yako shekeli elfu moja za fedha. Hii ni kufidia kosa lililofanyika dhidi yako mbele ya wote walio pamoja nawe; haki yako imethibitishwa kabisa.” 17 Kisha Abrahamu akamwomba Mungu, naye Mungu akamponya Abimeleki, mke wake, na watumwa wake wa kike kwamba waweze kupata watoto tena, 18 kwa kuwa BWANA alikuwa ameyafunga matumbo ya wote katika nyumba ya Abimeleki kwa sababu ya Sara, mke wa Abrahamu.
In Other Versions
Genesis 20 in the ANGEFD
Genesis 20 in the ANTPNG2D
Genesis 20 in the AS21
Genesis 20 in the BAGH
Genesis 20 in the BBPNG
Genesis 20 in the BBT1E
Genesis 20 in the BDS
Genesis 20 in the BEV
Genesis 20 in the BHAD
Genesis 20 in the BIB
Genesis 20 in the BLPT
Genesis 20 in the BNT
Genesis 20 in the BNTABOOT
Genesis 20 in the BNTLV
Genesis 20 in the BOATCB
Genesis 20 in the BOATCB2
Genesis 20 in the BOBCV
Genesis 20 in the BOCNT
Genesis 20 in the BOECS
Genesis 20 in the BOGWICC
Genesis 20 in the BOHCB
Genesis 20 in the BOHCV
Genesis 20 in the BOHLNT
Genesis 20 in the BOHNTLTAL
Genesis 20 in the BOICB
Genesis 20 in the BOILNTAP
Genesis 20 in the BOITCV
Genesis 20 in the BOKCV2
Genesis 20 in the BOKHWOG
Genesis 20 in the BOKSSV
Genesis 20 in the BOLCB
Genesis 20 in the BOLCB2
Genesis 20 in the BOMCV
Genesis 20 in the BONAV
Genesis 20 in the BONCB
Genesis 20 in the BONLT
Genesis 20 in the BONUT2
Genesis 20 in the BOPLNT
Genesis 20 in the BOSCB
Genesis 20 in the BOSNC
Genesis 20 in the BOTLNT
Genesis 20 in the BOVCB
Genesis 20 in the BOYCB
Genesis 20 in the BPBB
Genesis 20 in the BPH
Genesis 20 in the BSB
Genesis 20 in the CCB
Genesis 20 in the CUV
Genesis 20 in the CUVS
Genesis 20 in the DBT
Genesis 20 in the DGDNT
Genesis 20 in the DHNT
Genesis 20 in the DNT
Genesis 20 in the ELBE
Genesis 20 in the EMTV
Genesis 20 in the ESV
Genesis 20 in the FBV
Genesis 20 in the FEB
Genesis 20 in the GGMNT
Genesis 20 in the GNT
Genesis 20 in the HARY
Genesis 20 in the HNT
Genesis 20 in the IRVA
Genesis 20 in the IRVB
Genesis 20 in the IRVG
Genesis 20 in the IRVH
Genesis 20 in the IRVK
Genesis 20 in the IRVM
Genesis 20 in the IRVM2
Genesis 20 in the IRVO
Genesis 20 in the IRVP
Genesis 20 in the IRVT
Genesis 20 in the IRVT2
Genesis 20 in the IRVU
Genesis 20 in the ISVN
Genesis 20 in the JSNT
Genesis 20 in the KAPI
Genesis 20 in the KBT1ETNIK
Genesis 20 in the KBV
Genesis 20 in the KJV
Genesis 20 in the KNFD
Genesis 20 in the LBA
Genesis 20 in the LBLA
Genesis 20 in the LNT
Genesis 20 in the LSV
Genesis 20 in the MAAL
Genesis 20 in the MBV
Genesis 20 in the MBV2
Genesis 20 in the MHNT
Genesis 20 in the MKNFD
Genesis 20 in the MNG
Genesis 20 in the MNT
Genesis 20 in the MNT2
Genesis 20 in the MRS1T
Genesis 20 in the NAA
Genesis 20 in the NASB
Genesis 20 in the NBLA
Genesis 20 in the NBS
Genesis 20 in the NBVTP
Genesis 20 in the NET2
Genesis 20 in the NIV11
Genesis 20 in the NNT
Genesis 20 in the NNT2
Genesis 20 in the NNT3
Genesis 20 in the PDDPT
Genesis 20 in the PFNT
Genesis 20 in the RMNT
Genesis 20 in the SBIAS
Genesis 20 in the SBIBS
Genesis 20 in the SBIBS2
Genesis 20 in the SBICS
Genesis 20 in the SBIDS
Genesis 20 in the SBIGS
Genesis 20 in the SBIHS
Genesis 20 in the SBIIS
Genesis 20 in the SBIIS2
Genesis 20 in the SBIIS3
Genesis 20 in the SBIKS
Genesis 20 in the SBIKS2
Genesis 20 in the SBIMS
Genesis 20 in the SBIOS
Genesis 20 in the SBIPS
Genesis 20 in the SBISS
Genesis 20 in the SBITS
Genesis 20 in the SBITS2
Genesis 20 in the SBITS3
Genesis 20 in the SBITS4
Genesis 20 in the SBIUS
Genesis 20 in the SBIVS
Genesis 20 in the SBT
Genesis 20 in the SBT1E
Genesis 20 in the SCHL
Genesis 20 in the SNT
Genesis 20 in the SUSU
Genesis 20 in the SUSU2
Genesis 20 in the SYNO
Genesis 20 in the TBIAOTANT
Genesis 20 in the TBT1E
Genesis 20 in the TBT1E2
Genesis 20 in the TFTIP
Genesis 20 in the TFTU
Genesis 20 in the TGNTATF3T
Genesis 20 in the THAI
Genesis 20 in the TNFD
Genesis 20 in the TNT
Genesis 20 in the TNTIK
Genesis 20 in the TNTIL
Genesis 20 in the TNTIN
Genesis 20 in the TNTIP
Genesis 20 in the TNTIZ
Genesis 20 in the TOMA
Genesis 20 in the TTENT
Genesis 20 in the UBG
Genesis 20 in the UGV
Genesis 20 in the UGV2
Genesis 20 in the UGV3
Genesis 20 in the VBL
Genesis 20 in the VDCC
Genesis 20 in the YALU
Genesis 20 in the YAPE
Genesis 20 in the YBVTP
Genesis 20 in the ZBP