Genesis 48 (BOKCV)
1 Baada ya muda Yosefu akaambiwa kwamba, “Baba yako ni mgonjwa.” Kwa hiyo akawachukua wanawe wawili Manase na Efraimu, pamoja naye. 2 Yakobo alipoambiwa, “Mwanao Yosefu amekujia kukuona,” Israeli akakusanya nguvu zake, akaketi kitandani. 3 Yakobo akamwambia Yosefu, “Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani, huko akanibariki, 4 naye akaniambia, ‘Nitakufanya ustawi na kuongezeka hesabu yako, nitakufanya kuwa jamii ya mataifa, nami nitakupa nchi hii uimiliki milele wewe na wazao wako baada yako.’ 5 “Sasa basi, wanao wawili waliozaliwa kwako huku Misri kabla sijaja hapa kwako watahesabiwa kuwa ni wangu; Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama vile Reubeni na Simeoni walivyo wangu. 6 Lakini watoto utakaowazaa baada yao watakuwa wako. Katika nchi watakayoirithi, watatambuliwa kwa jina la ndugu zao. 7 Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani, katika huzuni yangu Raheli alifariki katika nchi ya Kanaani tulipokuwa tungali tukisafiri, tukiwa karibu kufika Efrathi. Kwa hiyo nilimzika huko, kando ya njia iendayo Efrathi” (yaani Bethlehemu). 8 Wakati Israeli alipowaona wana wa Yosefu, akauliza, “Hawa ni nani?” 9 Yosefu akamjibu baba yake, “Hawa ni wana ambao Mungu amenipa nikiwa huku.”Ndipo Israeli akasema, “Walete kwangu ili niwabariki.” 10 Basi macho ya Israeli yalikuwa hayaoni vizuri kwa sababu ya uzee, naye aliona kwa shida. Kwa hiyo Yosefu akawaleta wanawe karibu na baba yake, Israeli akawabusu na akawakumbatia. 11 Israeli akamwambia Yosefu, “Kamwe sikutazamia kuuona uso wako tena, lakini sasa Mungu ameniruhusu kuwaona watoto wako pia.” 12 Ndipo Yosefu akawaondoa wanawe magotini mwa Israeli naye akasujudu hadi nchi. 13 Yosefu akachukua wale wana wawili, Efraimu kwenye mkono wake wa kuume akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kushoto akimwelekeza kwenye mkono wa kuume wa Israeli, akawaleta karibu na babu yao. 14 Lakini Israeli akaupeleka mkono wake wa kuume, akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, ingawa alikuwa ndiye mdogo, na mkono wake wa kushoto akaukatisha, akauweka juu ya kichwa cha Manase, ingawa Manase alikuwa ndiye mzaliwa wa kwanza. 15 Ndipo akambariki Yosefu akisema,“Mungu ambaye baba zanguAbrahamu na Isaki walimtii,Mungu ambaye amekuwa mchungajiwa maisha yangu yote mpaka leo hii, 16 Malaika ambaye aliniokoa kutoka madhara yote,yeye na awabariki vijana hawa.Na waitwe kwa jina languna kwa majina ya baba zangu Abrahamu na Isaki,wao na waongezeke kwa wingikatika dunia.” 17 Yosefu alipoona baba yake akiweka mkono wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, hakupendezwa, kwa hiyo akauchukua mkono wa baba yake kutoka kichwa cha Efraimu na kuuweka juu ya kichwa cha Manase. 18 Yosefu akamwambia, “Hapana, baba yangu, huyu ndiye mzaliwa wa kwanza; uweke mkono wako wa kuume juu ya kichwa chake.” 19 Lakini baba yake akakataa, akasema, “Ninajua, mwanangu, ninajua. Yeye pia atakuwa taifa, naye pia atakuwa mkuu. Hata hivyo, ndugu yake mdogo atakuwa mkuu kuliko yeye, nao wazao wake watakuwa kundi la mataifa.” 20 Akawabarikia siku ile na kusema,“Kwa jina lenu Israeli watatamka baraka hii:‘Mungu na awafanye kama Efraimu na Manase.’ ”Kwa hiyo akamtanguliza Efraimu mbele ya Manase. 21 Ndipo Israeli akamwambia Yosefu, “Mimi ninakaribia kufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, na atawarudisha katika nchi ya baba zenu. 22 Kwako wewe, kama aliye juu ya ndugu zako, ninakupa sehemu moja zaidi ya ndugu zako, lile eneo nililoteka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu.”
In Other Versions
Genesis 48 in the ANGEFD
Genesis 48 in the ANTPNG2D
Genesis 48 in the AS21
Genesis 48 in the BAGH
Genesis 48 in the BBPNG
Genesis 48 in the BBT1E
Genesis 48 in the BDS
Genesis 48 in the BEV
Genesis 48 in the BHAD
Genesis 48 in the BIB
Genesis 48 in the BLPT
Genesis 48 in the BNT
Genesis 48 in the BNTABOOT
Genesis 48 in the BNTLV
Genesis 48 in the BOATCB
Genesis 48 in the BOATCB2
Genesis 48 in the BOBCV
Genesis 48 in the BOCNT
Genesis 48 in the BOECS
Genesis 48 in the BOGWICC
Genesis 48 in the BOHCB
Genesis 48 in the BOHCV
Genesis 48 in the BOHLNT
Genesis 48 in the BOHNTLTAL
Genesis 48 in the BOICB
Genesis 48 in the BOILNTAP
Genesis 48 in the BOITCV
Genesis 48 in the BOKCV2
Genesis 48 in the BOKHWOG
Genesis 48 in the BOKSSV
Genesis 48 in the BOLCB
Genesis 48 in the BOLCB2
Genesis 48 in the BOMCV
Genesis 48 in the BONAV
Genesis 48 in the BONCB
Genesis 48 in the BONLT
Genesis 48 in the BONUT2
Genesis 48 in the BOPLNT
Genesis 48 in the BOSCB
Genesis 48 in the BOSNC
Genesis 48 in the BOTLNT
Genesis 48 in the BOVCB
Genesis 48 in the BOYCB
Genesis 48 in the BPBB
Genesis 48 in the BPH
Genesis 48 in the BSB
Genesis 48 in the CCB
Genesis 48 in the CUV
Genesis 48 in the CUVS
Genesis 48 in the DBT
Genesis 48 in the DGDNT
Genesis 48 in the DHNT
Genesis 48 in the DNT
Genesis 48 in the ELBE
Genesis 48 in the EMTV
Genesis 48 in the ESV
Genesis 48 in the FBV
Genesis 48 in the FEB
Genesis 48 in the GGMNT
Genesis 48 in the GNT
Genesis 48 in the HARY
Genesis 48 in the HNT
Genesis 48 in the IRVA
Genesis 48 in the IRVB
Genesis 48 in the IRVG
Genesis 48 in the IRVH
Genesis 48 in the IRVK
Genesis 48 in the IRVM
Genesis 48 in the IRVM2
Genesis 48 in the IRVO
Genesis 48 in the IRVP
Genesis 48 in the IRVT
Genesis 48 in the IRVT2
Genesis 48 in the IRVU
Genesis 48 in the ISVN
Genesis 48 in the JSNT
Genesis 48 in the KAPI
Genesis 48 in the KBT1ETNIK
Genesis 48 in the KBV
Genesis 48 in the KJV
Genesis 48 in the KNFD
Genesis 48 in the LBA
Genesis 48 in the LBLA
Genesis 48 in the LNT
Genesis 48 in the LSV
Genesis 48 in the MAAL
Genesis 48 in the MBV
Genesis 48 in the MBV2
Genesis 48 in the MHNT
Genesis 48 in the MKNFD
Genesis 48 in the MNG
Genesis 48 in the MNT
Genesis 48 in the MNT2
Genesis 48 in the MRS1T
Genesis 48 in the NAA
Genesis 48 in the NASB
Genesis 48 in the NBLA
Genesis 48 in the NBS
Genesis 48 in the NBVTP
Genesis 48 in the NET2
Genesis 48 in the NIV11
Genesis 48 in the NNT
Genesis 48 in the NNT2
Genesis 48 in the NNT3
Genesis 48 in the PDDPT
Genesis 48 in the PFNT
Genesis 48 in the RMNT
Genesis 48 in the SBIAS
Genesis 48 in the SBIBS
Genesis 48 in the SBIBS2
Genesis 48 in the SBICS
Genesis 48 in the SBIDS
Genesis 48 in the SBIGS
Genesis 48 in the SBIHS
Genesis 48 in the SBIIS
Genesis 48 in the SBIIS2
Genesis 48 in the SBIIS3
Genesis 48 in the SBIKS
Genesis 48 in the SBIKS2
Genesis 48 in the SBIMS
Genesis 48 in the SBIOS
Genesis 48 in the SBIPS
Genesis 48 in the SBISS
Genesis 48 in the SBITS
Genesis 48 in the SBITS2
Genesis 48 in the SBITS3
Genesis 48 in the SBITS4
Genesis 48 in the SBIUS
Genesis 48 in the SBIVS
Genesis 48 in the SBT
Genesis 48 in the SBT1E
Genesis 48 in the SCHL
Genesis 48 in the SNT
Genesis 48 in the SUSU
Genesis 48 in the SUSU2
Genesis 48 in the SYNO
Genesis 48 in the TBIAOTANT
Genesis 48 in the TBT1E
Genesis 48 in the TBT1E2
Genesis 48 in the TFTIP
Genesis 48 in the TFTU
Genesis 48 in the TGNTATF3T
Genesis 48 in the THAI
Genesis 48 in the TNFD
Genesis 48 in the TNT
Genesis 48 in the TNTIK
Genesis 48 in the TNTIL
Genesis 48 in the TNTIN
Genesis 48 in the TNTIP
Genesis 48 in the TNTIZ
Genesis 48 in the TOMA
Genesis 48 in the TTENT
Genesis 48 in the UBG
Genesis 48 in the UGV
Genesis 48 in the UGV2
Genesis 48 in the UGV3
Genesis 48 in the VBL
Genesis 48 in the VDCC
Genesis 48 in the YALU
Genesis 48 in the YAPE
Genesis 48 in the YBVTP
Genesis 48 in the ZBP