Genesis 5 (BOKCV)
1 Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. 2 Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.” 3 Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi. 4 Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 5 Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa. 6 Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi. 7 Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 8 Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa. 9 Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. 10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 11 Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa. 12 Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 14 Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa. 15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. 16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 17 Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa. 18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki. 19 Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 20 Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa. 21 Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 22 Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 23 Enoki aliishi jumla ya miaka 365. 24 Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua. 25 Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki. 26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 27 Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa. 28 Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana. 29 Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na BWANA.” 30 Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 31 Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa. 32 Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.
In Other Versions
Genesis 5 in the ANGEFD
Genesis 5 in the ANTPNG2D
Genesis 5 in the AS21
Genesis 5 in the BAGH
Genesis 5 in the BBPNG
Genesis 5 in the BBT1E
Genesis 5 in the BDS
Genesis 5 in the BEV
Genesis 5 in the BHAD
Genesis 5 in the BIB
Genesis 5 in the BLPT
Genesis 5 in the BNT
Genesis 5 in the BNTABOOT
Genesis 5 in the BNTLV
Genesis 5 in the BOATCB
Genesis 5 in the BOATCB2
Genesis 5 in the BOBCV
Genesis 5 in the BOCNT
Genesis 5 in the BOECS
Genesis 5 in the BOGWICC
Genesis 5 in the BOHCB
Genesis 5 in the BOHCV
Genesis 5 in the BOHLNT
Genesis 5 in the BOHNTLTAL
Genesis 5 in the BOICB
Genesis 5 in the BOILNTAP
Genesis 5 in the BOITCV
Genesis 5 in the BOKCV2
Genesis 5 in the BOKHWOG
Genesis 5 in the BOKSSV
Genesis 5 in the BOLCB
Genesis 5 in the BOLCB2
Genesis 5 in the BOMCV
Genesis 5 in the BONAV
Genesis 5 in the BONCB
Genesis 5 in the BONLT
Genesis 5 in the BONUT2
Genesis 5 in the BOPLNT
Genesis 5 in the BOSCB
Genesis 5 in the BOSNC
Genesis 5 in the BOTLNT
Genesis 5 in the BOVCB
Genesis 5 in the BOYCB
Genesis 5 in the BPBB
Genesis 5 in the BPH
Genesis 5 in the BSB
Genesis 5 in the CCB
Genesis 5 in the CUV
Genesis 5 in the CUVS
Genesis 5 in the DBT
Genesis 5 in the DGDNT
Genesis 5 in the DHNT
Genesis 5 in the DNT
Genesis 5 in the ELBE
Genesis 5 in the EMTV
Genesis 5 in the ESV
Genesis 5 in the FBV
Genesis 5 in the FEB
Genesis 5 in the GGMNT
Genesis 5 in the GNT
Genesis 5 in the HARY
Genesis 5 in the HNT
Genesis 5 in the IRVA
Genesis 5 in the IRVB
Genesis 5 in the IRVG
Genesis 5 in the IRVH
Genesis 5 in the IRVK
Genesis 5 in the IRVM
Genesis 5 in the IRVM2
Genesis 5 in the IRVO
Genesis 5 in the IRVP
Genesis 5 in the IRVT
Genesis 5 in the IRVT2
Genesis 5 in the IRVU
Genesis 5 in the ISVN
Genesis 5 in the JSNT
Genesis 5 in the KAPI
Genesis 5 in the KBT1ETNIK
Genesis 5 in the KBV
Genesis 5 in the KJV
Genesis 5 in the KNFD
Genesis 5 in the LBA
Genesis 5 in the LBLA
Genesis 5 in the LNT
Genesis 5 in the LSV
Genesis 5 in the MAAL
Genesis 5 in the MBV
Genesis 5 in the MBV2
Genesis 5 in the MHNT
Genesis 5 in the MKNFD
Genesis 5 in the MNG
Genesis 5 in the MNT
Genesis 5 in the MNT2
Genesis 5 in the MRS1T
Genesis 5 in the NAA
Genesis 5 in the NASB
Genesis 5 in the NBLA
Genesis 5 in the NBS
Genesis 5 in the NBVTP
Genesis 5 in the NET2
Genesis 5 in the NIV11
Genesis 5 in the NNT
Genesis 5 in the NNT2
Genesis 5 in the NNT3
Genesis 5 in the PDDPT
Genesis 5 in the PFNT
Genesis 5 in the RMNT
Genesis 5 in the SBIAS
Genesis 5 in the SBIBS
Genesis 5 in the SBIBS2
Genesis 5 in the SBICS
Genesis 5 in the SBIDS
Genesis 5 in the SBIGS
Genesis 5 in the SBIHS
Genesis 5 in the SBIIS
Genesis 5 in the SBIIS2
Genesis 5 in the SBIIS3
Genesis 5 in the SBIKS
Genesis 5 in the SBIKS2
Genesis 5 in the SBIMS
Genesis 5 in the SBIOS
Genesis 5 in the SBIPS
Genesis 5 in the SBISS
Genesis 5 in the SBITS
Genesis 5 in the SBITS2
Genesis 5 in the SBITS3
Genesis 5 in the SBITS4
Genesis 5 in the SBIUS
Genesis 5 in the SBIVS
Genesis 5 in the SBT
Genesis 5 in the SBT1E
Genesis 5 in the SCHL
Genesis 5 in the SNT
Genesis 5 in the SUSU
Genesis 5 in the SUSU2
Genesis 5 in the SYNO
Genesis 5 in the TBIAOTANT
Genesis 5 in the TBT1E
Genesis 5 in the TBT1E2
Genesis 5 in the TFTIP
Genesis 5 in the TFTU
Genesis 5 in the TGNTATF3T
Genesis 5 in the THAI
Genesis 5 in the TNFD
Genesis 5 in the TNT
Genesis 5 in the TNTIK
Genesis 5 in the TNTIL
Genesis 5 in the TNTIN
Genesis 5 in the TNTIP
Genesis 5 in the TNTIZ
Genesis 5 in the TOMA
Genesis 5 in the TTENT
Genesis 5 in the UBG
Genesis 5 in the UGV
Genesis 5 in the UGV2
Genesis 5 in the UGV3
Genesis 5 in the VBL
Genesis 5 in the VDCC
Genesis 5 in the YALU
Genesis 5 in the YAPE
Genesis 5 in the YBVTP
Genesis 5 in the ZBP