Genesis 50 (BOKCV)
1 Basi Yosefu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu. 2 Ndipo Yosefu akawaagiza matabibu waliokuwa wakimhudumia, wamtie baba yake Israeli dawa ili asioze. Hivyo matabibu wakamtia dawa asioze, 3 wakatumia siku arobaini, kwa maana ndio muda uliotakiwa wa kutia dawa ili asioze. Nao Wamisri wakamwombolezea Yakobo kwa siku sabini. 4 Siku za kumwombolezea zilipokwisha, Yosefu akawaambia washauri wa Farao, “Kama nimepata kibali machoni penu semeni na Farao kwa ajili yangu. Mwambieni, 5 ‘Baba yangu aliniapisha na kuniambia, “Mimi niko karibu kufa; unizike katika kaburi lile nililochimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani.” Sasa nakuomba uniruhusu niende kumzika baba yangu, nami nitarudi.’ ” 6 Farao akasema, “Panda, uende kumzika baba yako, kama alivyokuapiza kufanya.” 7 Hivyo Yosefu akapanda kwenda kumzika baba yake. Maafisa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, watu mashuhuri wa baraza lake na watu mashuhuri wote wa Misri. 8 Hawa ni mbali na watu wote wa nyumbani kwa Yosefu, na ndugu zake, na wale wote wa nyumbani mwa baba yake. Ni watoto wao, makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe tu waliobakia katika nchi ya Gosheni. 9 Magari makubwa na wapanda farasi pia walipanda pamoja naye. Likawa kundi kubwa sana. 10 Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu; Yosefu akapumzika huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake. 11 Wakanaani walioishi huko walipoona maombolezo yaliyofanyika katika sakafu ile ya kupuria ya Atadi, wakasema, “Wamisri wanafanya maombolezo makubwa.” Kwa hiyo mahali pale karibu na Yordani pakaitwa Abel-Mizraimu. 12 Hivyo wana wa Yakobo wakafanya kama baba yao alivyowaagiza: 13 Wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Abrahamu alilinunua kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia. 14 Baada ya Yosefu kumzika baba yake, akarudi Misri pamoja na ndugu zake na wale wote waliokuwa wamekwenda naye kumzika baba yake. 15 Ndugu zake Yosefu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje kama Yosefu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?” 16 Kwa hiyo wakampelekea Yosefu ujumbe, wakasema, “Kabla baba yako hajafa aliacha maagizo haya: 17 ‘Hili ndilo mtakalomwambia Yosefu: Ninakuomba uwasamehe ndugu zako dhambi na mabaya kwa vile walivyokutenda vibaya.’ Sasa tafadhali samehe dhambi za watumishi wa Mungu wa baba yako.” Ujumbe huu ulipomfikia, Yosefu akalia. 18 Ndipo ndugu zake wakaja na kujitupa chini mbele yake. Wakasema, “Sisi ni watumwa wako.” 19 Lakini Yosefu akawaambia, “Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? 20 Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. 21 Hivyo basi, msiogope. Mimi nitawatunza ninyi nyote pamoja na watoto wenu.” Akawahakikishia na kusema nao kwa wema. 22 Yosefu akakaa katika nchi ya Misri, yeye pamoja na jamaa yote ya baba yake. Akaishi miaka 110, 23 naye akaona kizazi cha tatu cha watoto wa Efraimu. Pia akaona watoto wa Makiri mwana wa Manase, wakawekwa magotini mwa Yosefu walipozaliwa. 24 Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Abrahamu, Isaki na Yakobo.” 25 Naye Yosefu akawaapisha wana wa Israeli na kuwaambia, “Hakika Mungu atawasaidia, nanyi ni lazima mhakikishe mmepandisha mifupa yangu kutoka mahali hapa.” 26 Kwa hiyo Yosefu akafa akiwa na umri wa miaka 110. Baada ya kumtia dawa ili asioze, akawekwa kwenye jeneza huko Misri.
In Other Versions
Genesis 50 in the ANGEFD
Genesis 50 in the ANTPNG2D
Genesis 50 in the AS21
Genesis 50 in the BAGH
Genesis 50 in the BBPNG
Genesis 50 in the BBT1E
Genesis 50 in the BDS
Genesis 50 in the BEV
Genesis 50 in the BHAD
Genesis 50 in the BIB
Genesis 50 in the BLPT
Genesis 50 in the BNT
Genesis 50 in the BNTABOOT
Genesis 50 in the BNTLV
Genesis 50 in the BOATCB
Genesis 50 in the BOATCB2
Genesis 50 in the BOBCV
Genesis 50 in the BOCNT
Genesis 50 in the BOECS
Genesis 50 in the BOGWICC
Genesis 50 in the BOHCB
Genesis 50 in the BOHCV
Genesis 50 in the BOHLNT
Genesis 50 in the BOHNTLTAL
Genesis 50 in the BOICB
Genesis 50 in the BOILNTAP
Genesis 50 in the BOITCV
Genesis 50 in the BOKCV2
Genesis 50 in the BOKHWOG
Genesis 50 in the BOKSSV
Genesis 50 in the BOLCB
Genesis 50 in the BOLCB2
Genesis 50 in the BOMCV
Genesis 50 in the BONAV
Genesis 50 in the BONCB
Genesis 50 in the BONLT
Genesis 50 in the BONUT2
Genesis 50 in the BOPLNT
Genesis 50 in the BOSCB
Genesis 50 in the BOSNC
Genesis 50 in the BOTLNT
Genesis 50 in the BOVCB
Genesis 50 in the BOYCB
Genesis 50 in the BPBB
Genesis 50 in the BPH
Genesis 50 in the BSB
Genesis 50 in the CCB
Genesis 50 in the CUV
Genesis 50 in the CUVS
Genesis 50 in the DBT
Genesis 50 in the DGDNT
Genesis 50 in the DHNT
Genesis 50 in the DNT
Genesis 50 in the ELBE
Genesis 50 in the EMTV
Genesis 50 in the ESV
Genesis 50 in the FBV
Genesis 50 in the FEB
Genesis 50 in the GGMNT
Genesis 50 in the GNT
Genesis 50 in the HARY
Genesis 50 in the HNT
Genesis 50 in the IRVA
Genesis 50 in the IRVB
Genesis 50 in the IRVG
Genesis 50 in the IRVH
Genesis 50 in the IRVK
Genesis 50 in the IRVM
Genesis 50 in the IRVM2
Genesis 50 in the IRVO
Genesis 50 in the IRVP
Genesis 50 in the IRVT
Genesis 50 in the IRVT2
Genesis 50 in the IRVU
Genesis 50 in the ISVN
Genesis 50 in the JSNT
Genesis 50 in the KAPI
Genesis 50 in the KBT1ETNIK
Genesis 50 in the KBV
Genesis 50 in the KJV
Genesis 50 in the KNFD
Genesis 50 in the LBA
Genesis 50 in the LBLA
Genesis 50 in the LNT
Genesis 50 in the LSV
Genesis 50 in the MAAL
Genesis 50 in the MBV
Genesis 50 in the MBV2
Genesis 50 in the MHNT
Genesis 50 in the MKNFD
Genesis 50 in the MNG
Genesis 50 in the MNT
Genesis 50 in the MNT2
Genesis 50 in the MRS1T
Genesis 50 in the NAA
Genesis 50 in the NASB
Genesis 50 in the NBLA
Genesis 50 in the NBS
Genesis 50 in the NBVTP
Genesis 50 in the NET2
Genesis 50 in the NIV11
Genesis 50 in the NNT
Genesis 50 in the NNT2
Genesis 50 in the NNT3
Genesis 50 in the PDDPT
Genesis 50 in the PFNT
Genesis 50 in the RMNT
Genesis 50 in the SBIAS
Genesis 50 in the SBIBS
Genesis 50 in the SBIBS2
Genesis 50 in the SBICS
Genesis 50 in the SBIDS
Genesis 50 in the SBIGS
Genesis 50 in the SBIHS
Genesis 50 in the SBIIS
Genesis 50 in the SBIIS2
Genesis 50 in the SBIIS3
Genesis 50 in the SBIKS
Genesis 50 in the SBIKS2
Genesis 50 in the SBIMS
Genesis 50 in the SBIOS
Genesis 50 in the SBIPS
Genesis 50 in the SBISS
Genesis 50 in the SBITS
Genesis 50 in the SBITS2
Genesis 50 in the SBITS3
Genesis 50 in the SBITS4
Genesis 50 in the SBIUS
Genesis 50 in the SBIVS
Genesis 50 in the SBT
Genesis 50 in the SBT1E
Genesis 50 in the SCHL
Genesis 50 in the SNT
Genesis 50 in the SUSU
Genesis 50 in the SUSU2
Genesis 50 in the SYNO
Genesis 50 in the TBIAOTANT
Genesis 50 in the TBT1E
Genesis 50 in the TBT1E2
Genesis 50 in the TFTIP
Genesis 50 in the TFTU
Genesis 50 in the TGNTATF3T
Genesis 50 in the THAI
Genesis 50 in the TNFD
Genesis 50 in the TNT
Genesis 50 in the TNTIK
Genesis 50 in the TNTIL
Genesis 50 in the TNTIN
Genesis 50 in the TNTIP
Genesis 50 in the TNTIZ
Genesis 50 in the TOMA
Genesis 50 in the TTENT
Genesis 50 in the UBG
Genesis 50 in the UGV
Genesis 50 in the UGV2
Genesis 50 in the UGV3
Genesis 50 in the VBL
Genesis 50 in the VDCC
Genesis 50 in the YALU
Genesis 50 in the YAPE
Genesis 50 in the YBVTP
Genesis 50 in the ZBP