Jeremiah 22 (BOKCV)

1 Hili ndilo asemalo BWANA: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, utangaze ujumbe huu huko: 2 ‘Sikia neno la BWANA, ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi: wewe, maafisa wako na watu wako mnaopitia malango haya. 3 Hili ndilo BWANA asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa. 4 Kwa kuwa ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi, huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao. 5 Lakini kama hutayatii maagizo haya, asema BWANA, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ” 6 Kwa kuwa hili ndilo BWANA asemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda:“Ingawa uko kama Gileadi kwangu,kama kilele cha Lebanoni,hakika nitakufanya uwe kama jangwa,kama miji ambayo haijakaliwa na watu. 7 Nitawatuma waharabu dhidi yako,kila mtu akiwa na silaha zake,nao watazikata boriti zako nzuri za mierezina kuzitupa motoni. 8 “Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini BWANA amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’ 9 Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la BWANA, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ” 10 Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;badala yake, afadhali umlilie kwa uchunguyule aliyepelekwa uhamishoni,kwa sababu kamwe hatairudiawala kuiona tena nchi yake alikozaliwa. 11 Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Shalumu mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena. 12 Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.” 13 “Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma,vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,bila kuwalipa kwa utumishi wao. 14 Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme,na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,huweka kuta za mbao za mierezi,na kuipamba kwa rangi nyekundu. 15 “Je, inakufanya kuwa mfalmehuko kuongeza idadi ya mierezi?Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?Alifanya yaliyo sawa na haki,hivyo yeye akafanikiwa katika yote. 16 Aliwatetea maskini na wahitaji,hivyo yeye akafanikiwa katika yote.Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”asema BWANA. 17 “Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tukatika mapato ya udhalimu,kwa kumwaga damu isiyo na hatia,kwa uonevu na ukatili.” 18 Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:“Hawatamwombolezea wakisema:‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’Hawatamwombolezea wakisema:‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’ 19 Atazikwa maziko ya punda:ataburutwa na kutupwanje ya malango ya Yerusalemu.” 20 “Panda Lebanoni ukapige kelele,sauti yako na isikike huko Bashani,piga kelele toka Abarimu,kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa. 21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako;hujanitii mimi. 22 Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,na wale ulioungana nao wataenda uhamishoni.Kisha utaaibika na kufedhehekakwa sababu ya uovu wako wote. 23 Wewe uishiye Lebanoni,wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi,tazama jinsi utakavyoombolezamaumivu makali yatakapokupata,maumivu kama yale ya mwanamkemwenye utungu wa kuzaa! 24 “Hakika kama niishivyo,” asema BWANA, “hata kama wewe, Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo. 25 Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. 26 Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. 27 Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.” 28 Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa,chungu kilichovunjika,chombo kisichotakiwa na mtu yeyote?Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,na kutupwa kwenye nchi wasioijua? 29 Ee nchi, nchi, nchi,sikia neno la BWANA! 30 Hili ndilo BWANA asemalo:“Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto,mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote,kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa,wala kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudiwala kuendelea kutawala katika Yuda.”

In Other Versions

Jeremiah 22 in the ANGEFD

Jeremiah 22 in the ANTPNG2D

Jeremiah 22 in the AS21

Jeremiah 22 in the BAGH

Jeremiah 22 in the BBPNG

Jeremiah 22 in the BBT1E

Jeremiah 22 in the BDS

Jeremiah 22 in the BEV

Jeremiah 22 in the BHAD

Jeremiah 22 in the BIB

Jeremiah 22 in the BLPT

Jeremiah 22 in the BNT

Jeremiah 22 in the BNTABOOT

Jeremiah 22 in the BNTLV

Jeremiah 22 in the BOATCB

Jeremiah 22 in the BOATCB2

Jeremiah 22 in the BOBCV

Jeremiah 22 in the BOCNT

Jeremiah 22 in the BOECS

Jeremiah 22 in the BOGWICC

Jeremiah 22 in the BOHCB

Jeremiah 22 in the BOHCV

Jeremiah 22 in the BOHLNT

Jeremiah 22 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 22 in the BOICB

Jeremiah 22 in the BOILNTAP

Jeremiah 22 in the BOITCV

Jeremiah 22 in the BOKCV2

Jeremiah 22 in the BOKHWOG

Jeremiah 22 in the BOKSSV

Jeremiah 22 in the BOLCB

Jeremiah 22 in the BOLCB2

Jeremiah 22 in the BOMCV

Jeremiah 22 in the BONAV

Jeremiah 22 in the BONCB

Jeremiah 22 in the BONLT

Jeremiah 22 in the BONUT2

Jeremiah 22 in the BOPLNT

Jeremiah 22 in the BOSCB

Jeremiah 22 in the BOSNC

Jeremiah 22 in the BOTLNT

Jeremiah 22 in the BOVCB

Jeremiah 22 in the BOYCB

Jeremiah 22 in the BPBB

Jeremiah 22 in the BPH

Jeremiah 22 in the BSB

Jeremiah 22 in the CCB

Jeremiah 22 in the CUV

Jeremiah 22 in the CUVS

Jeremiah 22 in the DBT

Jeremiah 22 in the DGDNT

Jeremiah 22 in the DHNT

Jeremiah 22 in the DNT

Jeremiah 22 in the ELBE

Jeremiah 22 in the EMTV

Jeremiah 22 in the ESV

Jeremiah 22 in the FBV

Jeremiah 22 in the FEB

Jeremiah 22 in the GGMNT

Jeremiah 22 in the GNT

Jeremiah 22 in the HARY

Jeremiah 22 in the HNT

Jeremiah 22 in the IRVA

Jeremiah 22 in the IRVB

Jeremiah 22 in the IRVG

Jeremiah 22 in the IRVH

Jeremiah 22 in the IRVK

Jeremiah 22 in the IRVM

Jeremiah 22 in the IRVM2

Jeremiah 22 in the IRVO

Jeremiah 22 in the IRVP

Jeremiah 22 in the IRVT

Jeremiah 22 in the IRVT2

Jeremiah 22 in the IRVU

Jeremiah 22 in the ISVN

Jeremiah 22 in the JSNT

Jeremiah 22 in the KAPI

Jeremiah 22 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 22 in the KBV

Jeremiah 22 in the KJV

Jeremiah 22 in the KNFD

Jeremiah 22 in the LBA

Jeremiah 22 in the LBLA

Jeremiah 22 in the LNT

Jeremiah 22 in the LSV

Jeremiah 22 in the MAAL

Jeremiah 22 in the MBV

Jeremiah 22 in the MBV2

Jeremiah 22 in the MHNT

Jeremiah 22 in the MKNFD

Jeremiah 22 in the MNG

Jeremiah 22 in the MNT

Jeremiah 22 in the MNT2

Jeremiah 22 in the MRS1T

Jeremiah 22 in the NAA

Jeremiah 22 in the NASB

Jeremiah 22 in the NBLA

Jeremiah 22 in the NBS

Jeremiah 22 in the NBVTP

Jeremiah 22 in the NET2

Jeremiah 22 in the NIV11

Jeremiah 22 in the NNT

Jeremiah 22 in the NNT2

Jeremiah 22 in the NNT3

Jeremiah 22 in the PDDPT

Jeremiah 22 in the PFNT

Jeremiah 22 in the RMNT

Jeremiah 22 in the SBIAS

Jeremiah 22 in the SBIBS

Jeremiah 22 in the SBIBS2

Jeremiah 22 in the SBICS

Jeremiah 22 in the SBIDS

Jeremiah 22 in the SBIGS

Jeremiah 22 in the SBIHS

Jeremiah 22 in the SBIIS

Jeremiah 22 in the SBIIS2

Jeremiah 22 in the SBIIS3

Jeremiah 22 in the SBIKS

Jeremiah 22 in the SBIKS2

Jeremiah 22 in the SBIMS

Jeremiah 22 in the SBIOS

Jeremiah 22 in the SBIPS

Jeremiah 22 in the SBISS

Jeremiah 22 in the SBITS

Jeremiah 22 in the SBITS2

Jeremiah 22 in the SBITS3

Jeremiah 22 in the SBITS4

Jeremiah 22 in the SBIUS

Jeremiah 22 in the SBIVS

Jeremiah 22 in the SBT

Jeremiah 22 in the SBT1E

Jeremiah 22 in the SCHL

Jeremiah 22 in the SNT

Jeremiah 22 in the SUSU

Jeremiah 22 in the SUSU2

Jeremiah 22 in the SYNO

Jeremiah 22 in the TBIAOTANT

Jeremiah 22 in the TBT1E

Jeremiah 22 in the TBT1E2

Jeremiah 22 in the TFTIP

Jeremiah 22 in the TFTU

Jeremiah 22 in the TGNTATF3T

Jeremiah 22 in the THAI

Jeremiah 22 in the TNFD

Jeremiah 22 in the TNT

Jeremiah 22 in the TNTIK

Jeremiah 22 in the TNTIL

Jeremiah 22 in the TNTIN

Jeremiah 22 in the TNTIP

Jeremiah 22 in the TNTIZ

Jeremiah 22 in the TOMA

Jeremiah 22 in the TTENT

Jeremiah 22 in the UBG

Jeremiah 22 in the UGV

Jeremiah 22 in the UGV2

Jeremiah 22 in the UGV3

Jeremiah 22 in the VBL

Jeremiah 22 in the VDCC

Jeremiah 22 in the YALU

Jeremiah 22 in the YAPE

Jeremiah 22 in the YBVTP

Jeremiah 22 in the ZBP