Jeremiah 34 (BOKCV)
1 Wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli na jeshi lake lote, pamoja na falme zote na mataifa katika himaya aliyotawala walipokuwa wakipigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na miji yote inayoizunguka, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa BWANA: 2 “Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli, kusema: Nenda kwa Sedekia mfalme wa Yuda umwambie, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto. 3 Hutaweza kuepuka mkono wake, bali hakika utatekwa na kukabidhiwa kwake. Utamwona mfalme wa Babeli kwa macho yako mwenyewe, naye atazungumza nawe ana kwa ana. Nawe utakwenda Babeli. 4 “ ‘Lakini sikia ahadi ya BWANA, ee Sedekia mfalme wa Yuda. Hili ndilo asemalo BWANA kukuhusu: Hutakufa kwa upanga, 5 utakufa kwa amani. Kama vile watu walivyowasha moto wa maziko kwa heshima ya baba zako, wafalme waliokutangulia, ndivyo watu watakavyowasha moto kwa heshima yako na kuomboleza, wakisema: “Ole, Ee BWANA!” Mimi mwenyewe ninaweka ahadi hii, asema BWANA.’ ” 6 Ndipo nabii Yeremia akamwambia Sedekia mfalme wa Yuda mambo haya yote huko Yerusalemu, 7 wakati jeshi la mfalme wa Babeli lilipokuwa likipigana dhidi ya Yerusalemu na miji mingine ya Yuda ambayo bado ilikuwa imara, yaani Lakishi na Azeka. Hii ilikuwa miji pekee yenye ngome iliyobaki katika Yuda. 8 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa BWANA, baada ya Mfalme Sedekia kufanya agano na watu wote huko Yerusalemu ili kutangaza uhuru kwa watumwa. 9 Kila mmoja alipaswa kuwaacha huru watumwa wake wa Kiebrania, wanawake na wanaume. Hakuna yeyote aliyeruhusiwa kumshikilia Myahudi mwenzake kama mtumwa. 10 Kwa hiyo maafisa wote na watu walioingia katika agano hili wakakubali kwamba watawaacha huru watumwa wao wa kiume na wa kike, na hawatawashikilia tena kama watumwa. Wakakubali na wakawaacha huru. 11 Lakini baadaye wakabadili mawazo yao, na kuwarudisha wale watumwa waliokuwa wamewaacha huru, wakawafanya tena watumwa. 12 Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia kusema: 13 “Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: Nilifanya agano na baba zenu nilipowatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. Nilisema, 14 ‘Kila mwaka wa saba, kila mmoja wenu ni lazima amwache huru mtumwa ambaye ni Mwebrania mwenzenu aliyejiuza kwenu. Baada ya kukutumikia kwa miaka sita, ni lazima umwache huru aende zake.’ Hata hivyo baba zenu hawakunisikiliza wala kunijali. 15 Hivi karibuni tu mlitubu na kufanya yaliyo sawa machoni pangu: Kila mmoja wenu aliwatangazia uhuru Waebrania wake. Hata mlifanya agano mbele zangu ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu. 16 Lakini sasa mmegeuka na kulinajisi jina langu. Kila mmoja wenu amemrudisha mtumwa wa kiume na wa kike ambao mlikuwa mmewaacha huru waende zao walikotaka. Mmewalazimisha kuwa watumwa wenu tena. 17 “Kwa hiyo, hili ndilo asemalo BWANA: Hamkunitii mimi. Hamkutangaza uhuru kwa ndugu zenu. Hivyo sasa, ninawatangazia ninyi ‘uhuru,’ asema BWANA: ‘uhuru’ ili kuanguka kwa upanga, tauni na njaa. Nitawafanya mwe chukizo kwa falme zote za dunia. 18 Watu waliovunja agano langu, na ambao hawakutunza masharti ya agano walilofanya mbele zangu, nitawafanya kama ndama waliyemkata vipande viwili, kisha wakatembea kati ya vile vipande vya huyo ndama. 19 Viongozi wa Yuda na Yerusalemu, maafisa wa mahakama, makuhani na watu wote wa nchi waliopita kati ya vile vipande vya ndama, 20 nitawatia mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao. Maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi. 21 “Nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda na maafisa wake mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao, kwa jeshi la mfalme wa Babeli, lililokuwa limeondoka kwenu. 22 Nitatoa amri, asema BWANA, nami nitawarudisha tena katika mji huu. Watapigana dhidi yake, wautwae na kuuteketeza kwa moto. Nami nitaiangamiza miji ya Yuda hivyo pasiwe na yeyote atakayeweza kuishi humo.”
In Other Versions
Jeremiah 34 in the ANGEFD
Jeremiah 34 in the ANTPNG2D
Jeremiah 34 in the AS21
Jeremiah 34 in the BAGH
Jeremiah 34 in the BBPNG
Jeremiah 34 in the BBT1E
Jeremiah 34 in the BDS
Jeremiah 34 in the BEV
Jeremiah 34 in the BHAD
Jeremiah 34 in the BIB
Jeremiah 34 in the BLPT
Jeremiah 34 in the BNT
Jeremiah 34 in the BNTABOOT
Jeremiah 34 in the BNTLV
Jeremiah 34 in the BOATCB
Jeremiah 34 in the BOATCB2
Jeremiah 34 in the BOBCV
Jeremiah 34 in the BOCNT
Jeremiah 34 in the BOECS
Jeremiah 34 in the BOGWICC
Jeremiah 34 in the BOHCB
Jeremiah 34 in the BOHCV
Jeremiah 34 in the BOHLNT
Jeremiah 34 in the BOHNTLTAL
Jeremiah 34 in the BOICB
Jeremiah 34 in the BOILNTAP
Jeremiah 34 in the BOITCV
Jeremiah 34 in the BOKCV2
Jeremiah 34 in the BOKHWOG
Jeremiah 34 in the BOKSSV
Jeremiah 34 in the BOLCB
Jeremiah 34 in the BOLCB2
Jeremiah 34 in the BOMCV
Jeremiah 34 in the BONAV
Jeremiah 34 in the BONCB
Jeremiah 34 in the BONLT
Jeremiah 34 in the BONUT2
Jeremiah 34 in the BOPLNT
Jeremiah 34 in the BOSCB
Jeremiah 34 in the BOSNC
Jeremiah 34 in the BOTLNT
Jeremiah 34 in the BOVCB
Jeremiah 34 in the BOYCB
Jeremiah 34 in the BPBB
Jeremiah 34 in the BPH
Jeremiah 34 in the BSB
Jeremiah 34 in the CCB
Jeremiah 34 in the CUV
Jeremiah 34 in the CUVS
Jeremiah 34 in the DBT
Jeremiah 34 in the DGDNT
Jeremiah 34 in the DHNT
Jeremiah 34 in the DNT
Jeremiah 34 in the ELBE
Jeremiah 34 in the EMTV
Jeremiah 34 in the ESV
Jeremiah 34 in the FBV
Jeremiah 34 in the FEB
Jeremiah 34 in the GGMNT
Jeremiah 34 in the GNT
Jeremiah 34 in the HARY
Jeremiah 34 in the HNT
Jeremiah 34 in the IRVA
Jeremiah 34 in the IRVB
Jeremiah 34 in the IRVG
Jeremiah 34 in the IRVH
Jeremiah 34 in the IRVK
Jeremiah 34 in the IRVM
Jeremiah 34 in the IRVM2
Jeremiah 34 in the IRVO
Jeremiah 34 in the IRVP
Jeremiah 34 in the IRVT
Jeremiah 34 in the IRVT2
Jeremiah 34 in the IRVU
Jeremiah 34 in the ISVN
Jeremiah 34 in the JSNT
Jeremiah 34 in the KAPI
Jeremiah 34 in the KBT1ETNIK
Jeremiah 34 in the KBV
Jeremiah 34 in the KJV
Jeremiah 34 in the KNFD
Jeremiah 34 in the LBA
Jeremiah 34 in the LBLA
Jeremiah 34 in the LNT
Jeremiah 34 in the LSV
Jeremiah 34 in the MAAL
Jeremiah 34 in the MBV
Jeremiah 34 in the MBV2
Jeremiah 34 in the MHNT
Jeremiah 34 in the MKNFD
Jeremiah 34 in the MNG
Jeremiah 34 in the MNT
Jeremiah 34 in the MNT2
Jeremiah 34 in the MRS1T
Jeremiah 34 in the NAA
Jeremiah 34 in the NASB
Jeremiah 34 in the NBLA
Jeremiah 34 in the NBS
Jeremiah 34 in the NBVTP
Jeremiah 34 in the NET2
Jeremiah 34 in the NIV11
Jeremiah 34 in the NNT
Jeremiah 34 in the NNT2
Jeremiah 34 in the NNT3
Jeremiah 34 in the PDDPT
Jeremiah 34 in the PFNT
Jeremiah 34 in the RMNT
Jeremiah 34 in the SBIAS
Jeremiah 34 in the SBIBS
Jeremiah 34 in the SBIBS2
Jeremiah 34 in the SBICS
Jeremiah 34 in the SBIDS
Jeremiah 34 in the SBIGS
Jeremiah 34 in the SBIHS
Jeremiah 34 in the SBIIS
Jeremiah 34 in the SBIIS2
Jeremiah 34 in the SBIIS3
Jeremiah 34 in the SBIKS
Jeremiah 34 in the SBIKS2
Jeremiah 34 in the SBIMS
Jeremiah 34 in the SBIOS
Jeremiah 34 in the SBIPS
Jeremiah 34 in the SBISS
Jeremiah 34 in the SBITS
Jeremiah 34 in the SBITS2
Jeremiah 34 in the SBITS3
Jeremiah 34 in the SBITS4
Jeremiah 34 in the SBIUS
Jeremiah 34 in the SBIVS
Jeremiah 34 in the SBT
Jeremiah 34 in the SBT1E
Jeremiah 34 in the SCHL
Jeremiah 34 in the SNT
Jeremiah 34 in the SUSU
Jeremiah 34 in the SUSU2
Jeremiah 34 in the SYNO
Jeremiah 34 in the TBIAOTANT
Jeremiah 34 in the TBT1E
Jeremiah 34 in the TBT1E2
Jeremiah 34 in the TFTIP
Jeremiah 34 in the TFTU
Jeremiah 34 in the TGNTATF3T
Jeremiah 34 in the THAI
Jeremiah 34 in the TNFD
Jeremiah 34 in the TNT
Jeremiah 34 in the TNTIK
Jeremiah 34 in the TNTIL
Jeremiah 34 in the TNTIN
Jeremiah 34 in the TNTIP
Jeremiah 34 in the TNTIZ
Jeremiah 34 in the TOMA
Jeremiah 34 in the TTENT
Jeremiah 34 in the UBG
Jeremiah 34 in the UGV
Jeremiah 34 in the UGV2
Jeremiah 34 in the UGV3
Jeremiah 34 in the VBL
Jeremiah 34 in the VDCC
Jeremiah 34 in the YALU
Jeremiah 34 in the YAPE
Jeremiah 34 in the YBVTP
Jeremiah 34 in the ZBP