Jeremiah 37 (BOKCV)

1 Sedekia mwana wa Yosia akafanywa kuwa mfalme wa Yuda na Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye akatawala mahali pa Yehoyakini mwana wa Yehoyakimu. 2 Lakini sio Sedekia, wala watumishi wake, wala watu wa nchi walisikiliza maneno ya BWANA aliyonena kupitia kwa nabii Yeremia. 3 Hata hivyo, Mfalme Sedekia akamtuma Yehukali mwana wa Shelemia, pamoja na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwa nabii Yeremia na ujumbe huu: “Tafadhali utuombee kwa BWANA, Mungu wetu.” 4 Wakati huu Yeremia alikuwa huru kuingia na kutoka katikati ya watu, kwa sababu alikuwa bado hajatiwa gerezani. 5 Jeshi la Farao lilikuwa limetoka Misri, nao Wakaldayo waliokuwa wameuzunguka Yerusalemu kwa majeshi waliposikia taarifa kuhusu jeshi hilo walijiondoa Yerusalemu. 6 Ndipo neno la BWANA likamjia nabii Yeremia kusema: 7 “Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: Mwambie mfalme wa Yuda aliyekutuma uniulize mimi, ‘Jeshi la Farao lililotoka kuja kukusaidia litarudi katika nchi yake yenyewe, yaani Misri. 8 Kisha Wakaldayo watarudi na kushambulia mji huu, watauteka na kuuchoma moto.’ 9 “Hili ndilo BWANA asemalo: Msijidanganye wenyewe mkifikiri, ‘Hakika Wakaldayo watatuacha na kwenda zao.’ Hakika hawatawaacha! 10 Hata kama mngelishinda jeshi lote la Wakaldayo linalowashambulia ninyi, na wakawa ni watu waliojeruhiwa tu waliobaki kwenye mahema yao, wangetoka na kuuchoma mji huu moto.” 11 Baada ya jeshi la Wakaldayo kujiondoa kutoka Yerusalemu kwa sababu ya jeshi la Farao, 12 Yeremia akaanza kuondoka mjini ili kwenda nchi ya Benyamini ili akapate sehemu yake ya milki miongoni mwa watu huko. 13 Lakini alipofika kwenye Lango la Benyamini, mkuu wa walinzi, ambaye jina lake lilikuwa Iriya mwana wa Shelemia mwana wa Hanania, akamkamata Yeremia na kusema, “Wewe unakwenda kujiunga na Wakaldayo!” 14 Yeremia akasema, “Hiyo si kweli, mimi sijiungi na Wakaldayo.” Lakini Iriya hakumsikiliza; badala yake, akamkamata Yeremia na kumpeleka kwa maafisa. 15 Wakamkasirikia Yeremia, wakaamuru apigwe, na akafungwa katika nyumba ya Yonathani mwandishi waliyokuwa wameifanya gereza. 16 Yeremia akawekwa kwenye chumba kilichofukuliwa chini, kilichojengwa kwa zege ndani ya gereza chini ya ngome, akakaa huko kwa muda mrefu. 17 Kisha Mfalme Sedekia akatumana aletwe katika jumba la kifalme, mahali alipomuuliza kwa siri, “Je, kuna neno lolote kutoka kwa BWANA?”Yeremia akajibu, “Ndiyo, utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli.” 18 Kisha Yeremia akamwambia Mfalme Sedekia, “Nimefanya kosa gani dhidi yako na maafisa wako au watu hawa, hata ukanitia gerezani? 19 Wako wapi manabii wako waliokutabiria wakisema, ‘Mfalme wa Babeli hatakushambulia wewe wala nchi hii?’ 20 Lakini sasa, bwana wangu mfalme, tafadhali sikiliza. Niruhusu nilete maombi yangu mbele yako, usinirudishe kwenye nyumba ya Yonathani mwandishi, nisije nikafia humo.” 21 Ndipo Mfalme Sedekia akatoa maagizo Yeremia awekwe katika ua wa walinzi, na apewe mkate kutoka mitaa ya waokaji kila siku mpaka mikate yote katika mji itakapokwisha. Kwa hiyo Yeremia akabaki katika ua wa walinzi.

In Other Versions

Jeremiah 37 in the ANGEFD

Jeremiah 37 in the ANTPNG2D

Jeremiah 37 in the AS21

Jeremiah 37 in the BAGH

Jeremiah 37 in the BBPNG

Jeremiah 37 in the BBT1E

Jeremiah 37 in the BDS

Jeremiah 37 in the BEV

Jeremiah 37 in the BHAD

Jeremiah 37 in the BIB

Jeremiah 37 in the BLPT

Jeremiah 37 in the BNT

Jeremiah 37 in the BNTABOOT

Jeremiah 37 in the BNTLV

Jeremiah 37 in the BOATCB

Jeremiah 37 in the BOATCB2

Jeremiah 37 in the BOBCV

Jeremiah 37 in the BOCNT

Jeremiah 37 in the BOECS

Jeremiah 37 in the BOGWICC

Jeremiah 37 in the BOHCB

Jeremiah 37 in the BOHCV

Jeremiah 37 in the BOHLNT

Jeremiah 37 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 37 in the BOICB

Jeremiah 37 in the BOILNTAP

Jeremiah 37 in the BOITCV

Jeremiah 37 in the BOKCV2

Jeremiah 37 in the BOKHWOG

Jeremiah 37 in the BOKSSV

Jeremiah 37 in the BOLCB

Jeremiah 37 in the BOLCB2

Jeremiah 37 in the BOMCV

Jeremiah 37 in the BONAV

Jeremiah 37 in the BONCB

Jeremiah 37 in the BONLT

Jeremiah 37 in the BONUT2

Jeremiah 37 in the BOPLNT

Jeremiah 37 in the BOSCB

Jeremiah 37 in the BOSNC

Jeremiah 37 in the BOTLNT

Jeremiah 37 in the BOVCB

Jeremiah 37 in the BOYCB

Jeremiah 37 in the BPBB

Jeremiah 37 in the BPH

Jeremiah 37 in the BSB

Jeremiah 37 in the CCB

Jeremiah 37 in the CUV

Jeremiah 37 in the CUVS

Jeremiah 37 in the DBT

Jeremiah 37 in the DGDNT

Jeremiah 37 in the DHNT

Jeremiah 37 in the DNT

Jeremiah 37 in the ELBE

Jeremiah 37 in the EMTV

Jeremiah 37 in the ESV

Jeremiah 37 in the FBV

Jeremiah 37 in the FEB

Jeremiah 37 in the GGMNT

Jeremiah 37 in the GNT

Jeremiah 37 in the HARY

Jeremiah 37 in the HNT

Jeremiah 37 in the IRVA

Jeremiah 37 in the IRVB

Jeremiah 37 in the IRVG

Jeremiah 37 in the IRVH

Jeremiah 37 in the IRVK

Jeremiah 37 in the IRVM

Jeremiah 37 in the IRVM2

Jeremiah 37 in the IRVO

Jeremiah 37 in the IRVP

Jeremiah 37 in the IRVT

Jeremiah 37 in the IRVT2

Jeremiah 37 in the IRVU

Jeremiah 37 in the ISVN

Jeremiah 37 in the JSNT

Jeremiah 37 in the KAPI

Jeremiah 37 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 37 in the KBV

Jeremiah 37 in the KJV

Jeremiah 37 in the KNFD

Jeremiah 37 in the LBA

Jeremiah 37 in the LBLA

Jeremiah 37 in the LNT

Jeremiah 37 in the LSV

Jeremiah 37 in the MAAL

Jeremiah 37 in the MBV

Jeremiah 37 in the MBV2

Jeremiah 37 in the MHNT

Jeremiah 37 in the MKNFD

Jeremiah 37 in the MNG

Jeremiah 37 in the MNT

Jeremiah 37 in the MNT2

Jeremiah 37 in the MRS1T

Jeremiah 37 in the NAA

Jeremiah 37 in the NASB

Jeremiah 37 in the NBLA

Jeremiah 37 in the NBS

Jeremiah 37 in the NBVTP

Jeremiah 37 in the NET2

Jeremiah 37 in the NIV11

Jeremiah 37 in the NNT

Jeremiah 37 in the NNT2

Jeremiah 37 in the NNT3

Jeremiah 37 in the PDDPT

Jeremiah 37 in the PFNT

Jeremiah 37 in the RMNT

Jeremiah 37 in the SBIAS

Jeremiah 37 in the SBIBS

Jeremiah 37 in the SBIBS2

Jeremiah 37 in the SBICS

Jeremiah 37 in the SBIDS

Jeremiah 37 in the SBIGS

Jeremiah 37 in the SBIHS

Jeremiah 37 in the SBIIS

Jeremiah 37 in the SBIIS2

Jeremiah 37 in the SBIIS3

Jeremiah 37 in the SBIKS

Jeremiah 37 in the SBIKS2

Jeremiah 37 in the SBIMS

Jeremiah 37 in the SBIOS

Jeremiah 37 in the SBIPS

Jeremiah 37 in the SBISS

Jeremiah 37 in the SBITS

Jeremiah 37 in the SBITS2

Jeremiah 37 in the SBITS3

Jeremiah 37 in the SBITS4

Jeremiah 37 in the SBIUS

Jeremiah 37 in the SBIVS

Jeremiah 37 in the SBT

Jeremiah 37 in the SBT1E

Jeremiah 37 in the SCHL

Jeremiah 37 in the SNT

Jeremiah 37 in the SUSU

Jeremiah 37 in the SUSU2

Jeremiah 37 in the SYNO

Jeremiah 37 in the TBIAOTANT

Jeremiah 37 in the TBT1E

Jeremiah 37 in the TBT1E2

Jeremiah 37 in the TFTIP

Jeremiah 37 in the TFTU

Jeremiah 37 in the TGNTATF3T

Jeremiah 37 in the THAI

Jeremiah 37 in the TNFD

Jeremiah 37 in the TNT

Jeremiah 37 in the TNTIK

Jeremiah 37 in the TNTIL

Jeremiah 37 in the TNTIN

Jeremiah 37 in the TNTIP

Jeremiah 37 in the TNTIZ

Jeremiah 37 in the TOMA

Jeremiah 37 in the TTENT

Jeremiah 37 in the UBG

Jeremiah 37 in the UGV

Jeremiah 37 in the UGV2

Jeremiah 37 in the UGV3

Jeremiah 37 in the VBL

Jeremiah 37 in the VDCC

Jeremiah 37 in the YALU

Jeremiah 37 in the YAPE

Jeremiah 37 in the YBVTP

Jeremiah 37 in the ZBP