Joshua 22 (BOKCV)

1 Ndipo Yoshua akawaita Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, 2 naye akawaambia, “Mmeshafanya yale yote Mose mtumishi wa BWANA aliyowaamuru, nanyi mmenitii kwa kila jambo nililowaamuru. 3 Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kazi BWANA Mungu wenu aliyowapa. 4 Sasa kwa kuwa BWANA Mungu wenu amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ile ambayo Mose mtumishi wa BWANA aliwapa ngʼambo ya Yordani. 5 Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria zile Mose mtumishi wa BWANA alizowapa: yaani kumpenda BWANA Mungu wenu na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.” 6 Ndipo Yoshua akawabariki na kuwaaga waende zao, nao wakaenda nyumbani mwao. 7 (Kwa nusu ya kabila la Manase Mose alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine ya hilo kabila Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi ya Yordani pamoja na ndugu zao). Yoshua alipowaaga waende zao nyumbani, aliwabariki, 8 akisema, “Rudini nyumbani mwenu na utajiri wenu mwingi, yaani makundi makubwa ya mifugo, mkiwa na fedha, dhahabu, shaba na chuma, pia wingi wa nguo, nanyi mkagawane na ndugu zenu hizo nyara zilizotoka kwa adui zenu.” 9 Kwa hiyo Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase wakawaacha Waisraeli huko Shilo katika nchi ya Kanaani ili kurudi Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoipata sawasawa na agizo la BWANA kupitia Mose. 10 Walipofika Gelilothi karibu na Yordani, katika nchi ya Kanaani, Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakajenga madhabahu ya fahari kubwa huko kando ya Yordani. 11 Waisraeli wengine waliposikia kwamba Wareubeni, Wagadi na ile nusu ya kabila la Manase walikuwa wamejenga madhabahu kwenye mpaka wa Kanaani huko Gelilothi karibu na Yordani kwenye upande wa Israeli, 12 kusanyiko lote la Israeli wakakusanyika huko Shilo ili wakapigane vita dhidi yao. 13 Kwa hiyo Waisraeli wengine wakamtuma Finehasi mwana wa kuhani Eleazari katika nchi ya Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase. 14 Wakatuma pamoja naye watu kumi ambao ni viongozi, mmoja kwa kila kabila la Israeli, kila mmoja aliyekuwa kiongozi katika mgawanyiko wa jamaa miongoni mwa koo za Israeli. 15 Walipofika Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, wakawaambia: 16 “Kusanyiko lote la BWANA lasema: ‘Je, mmewezaje kuacha kumwamini Mungu wa Israeli jinsi hii? Mmewezaje kumwacha BWANA na kujijengea madhabahu dhidi yake na kumwasi? 17 Je, dhambi ya Peori haikutosha? Hata ingawa kulikuja tauni juu ya kusanyiko la BWANA, mpaka leo hii hatujatakasika kutokana na dhambi hiyo! 18 Je, sasa ndiyo mnamwacha BWANA?“ ‘Kama mkimwasi BWANA leo, kesho atalikasirikia kusanyiko lote la Israeli. 19 Kama nchi mnayomiliki imenajisika, vukeni mje katika nchi ya BWANA, mahali Maskani ya BWANA ilipo, nanyi mkajitwalie sehemu miongoni mwetu, lakini msije mkaasi dhidi ya BWANA wala dhidi yetu sisi kwa kujijengea madhabahu, zaidi ya madhabahu ya BWANA Mungu wetu. 20 Wakati Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu kwa vitu vilivyowekwa wakfu, je, ghadhabu haikulipata kusanyiko lote la Israeli? Hakuwa yeye peke yake aliyekufa kwa ajili ya dhambi yake.’ ” 21 Ndipo Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walipowajibu viongozi wa koo za Israeli, wakisema: 22 “Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, BWANA! Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, BWANA! Yeye anajua! Israeli na wajue! Kama huu umekuwa ni uasi au kukosa utii kwa BWANA, msituache hai siku hii ya leo. 23 Kama tumejijengea madhabahu yetu wenyewe ili kumwacha BWANA na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, au kutoa sadaka za amani juu yake, BWANA mwenyewe na atupatilize leo. 24 “Sivyo! Tulifanya hivyo kwa hofu kwamba siku zijazo wazao wenu wanaweza wakawaambia wazao wetu, ‘Mna uhusiano gani na BWANA, Mungu wa Israeli? 25 BWANA ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa BWANA.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha BWANA. 26 “Hii ndiyo sababu tulisema, ‘Tujiweke tayari na tujenge madhabahu, lakini si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa au dhabihu.’ 27 Badala yake, itakuwa ni ushahidi kati yetu na ninyi na vizazi vijavyo, kwamba tutamwabudu BWANA katika mahali patakatifu pake pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa, dhabihu na sadaka za amani. Ndipo katika siku zijazo, wazao wenu hawataweza kuwaambia wazao wetu, ‘Ninyi hamna fungu katika BWANA.’ 28 “Nasi tulisema, ‘Ikiwa wakati wowote watatuambia hilo, au kuwaambia uzao wetu, tutawajibu hivi: Angalieni nakala hii ya madhabahu ya BWANA, ambayo baba zetu waliijenga, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu, bali kama ushahidi kati yetu na ninyi.’ 29 “Hili jambo la kumwasi BWANA na kumwacha siku hii ya leo kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na dhabihu, zaidi ya madhabahu ya BWANA Mungu wetu iliyo mbele ya maskani yake na liwe mbali nasi.” 30 Wakati kuhani Finehasi na viongozi wa kusanyiko na wakuu wa koo za Israeli, waliposikia hayo waliyosema Wareubeni, Wagadi na Manase, wakaridhika. 31 Naye Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, akawaambia Wareubeni, Wagadi na Manase, “Leo tunajua kwamba BWANA yuko pamoja nasi, kwa sababu hamkukosa uaminifu kwa BWANA katika jambo hili. Sasa mmewaokoa Waisraeli na mkono wa BWANA.” 32 Ndipo Finehasi, mwana wa kuhani Eleazari na viongozi wakarudi Kanaani kutoka kwenye kukutana kwao na Wareubeni na Wagadi huko Gileadi nao wakatoa taarifa kwa Waisraeli. 33 Walifurahi kusikia taarifa hiyo, na wakamhimidi Mungu. Wala hawakuzungumza tena habari za kupigana vita dhidi yao ili kuharibu nchi ambayo Wareubeni na Wagadi waliishi. 34 Nao Wareubeni na Wagadi wakayaita yale madhabahu Edi, yaani Shahidi: kwa kuwa itakuwa shahidi kati yetu na ninyi kwamba BWANA ndiye Mungu.

In Other Versions

Joshua 22 in the ANGEFD

Joshua 22 in the ANTPNG2D

Joshua 22 in the AS21

Joshua 22 in the BAGH

Joshua 22 in the BBPNG

Joshua 22 in the BBT1E

Joshua 22 in the BDS

Joshua 22 in the BEV

Joshua 22 in the BHAD

Joshua 22 in the BIB

Joshua 22 in the BLPT

Joshua 22 in the BNT

Joshua 22 in the BNTABOOT

Joshua 22 in the BNTLV

Joshua 22 in the BOATCB

Joshua 22 in the BOATCB2

Joshua 22 in the BOBCV

Joshua 22 in the BOCNT

Joshua 22 in the BOECS

Joshua 22 in the BOGWICC

Joshua 22 in the BOHCB

Joshua 22 in the BOHCV

Joshua 22 in the BOHLNT

Joshua 22 in the BOHNTLTAL

Joshua 22 in the BOICB

Joshua 22 in the BOILNTAP

Joshua 22 in the BOITCV

Joshua 22 in the BOKCV2

Joshua 22 in the BOKHWOG

Joshua 22 in the BOKSSV

Joshua 22 in the BOLCB

Joshua 22 in the BOLCB2

Joshua 22 in the BOMCV

Joshua 22 in the BONAV

Joshua 22 in the BONCB

Joshua 22 in the BONLT

Joshua 22 in the BONUT2

Joshua 22 in the BOPLNT

Joshua 22 in the BOSCB

Joshua 22 in the BOSNC

Joshua 22 in the BOTLNT

Joshua 22 in the BOVCB

Joshua 22 in the BOYCB

Joshua 22 in the BPBB

Joshua 22 in the BPH

Joshua 22 in the BSB

Joshua 22 in the CCB

Joshua 22 in the CUV

Joshua 22 in the CUVS

Joshua 22 in the DBT

Joshua 22 in the DGDNT

Joshua 22 in the DHNT

Joshua 22 in the DNT

Joshua 22 in the ELBE

Joshua 22 in the EMTV

Joshua 22 in the ESV

Joshua 22 in the FBV

Joshua 22 in the FEB

Joshua 22 in the GGMNT

Joshua 22 in the GNT

Joshua 22 in the HARY

Joshua 22 in the HNT

Joshua 22 in the IRVA

Joshua 22 in the IRVB

Joshua 22 in the IRVG

Joshua 22 in the IRVH

Joshua 22 in the IRVK

Joshua 22 in the IRVM

Joshua 22 in the IRVM2

Joshua 22 in the IRVO

Joshua 22 in the IRVP

Joshua 22 in the IRVT

Joshua 22 in the IRVT2

Joshua 22 in the IRVU

Joshua 22 in the ISVN

Joshua 22 in the JSNT

Joshua 22 in the KAPI

Joshua 22 in the KBT1ETNIK

Joshua 22 in the KBV

Joshua 22 in the KJV

Joshua 22 in the KNFD

Joshua 22 in the LBA

Joshua 22 in the LBLA

Joshua 22 in the LNT

Joshua 22 in the LSV

Joshua 22 in the MAAL

Joshua 22 in the MBV

Joshua 22 in the MBV2

Joshua 22 in the MHNT

Joshua 22 in the MKNFD

Joshua 22 in the MNG

Joshua 22 in the MNT

Joshua 22 in the MNT2

Joshua 22 in the MRS1T

Joshua 22 in the NAA

Joshua 22 in the NASB

Joshua 22 in the NBLA

Joshua 22 in the NBS

Joshua 22 in the NBVTP

Joshua 22 in the NET2

Joshua 22 in the NIV11

Joshua 22 in the NNT

Joshua 22 in the NNT2

Joshua 22 in the NNT3

Joshua 22 in the PDDPT

Joshua 22 in the PFNT

Joshua 22 in the RMNT

Joshua 22 in the SBIAS

Joshua 22 in the SBIBS

Joshua 22 in the SBIBS2

Joshua 22 in the SBICS

Joshua 22 in the SBIDS

Joshua 22 in the SBIGS

Joshua 22 in the SBIHS

Joshua 22 in the SBIIS

Joshua 22 in the SBIIS2

Joshua 22 in the SBIIS3

Joshua 22 in the SBIKS

Joshua 22 in the SBIKS2

Joshua 22 in the SBIMS

Joshua 22 in the SBIOS

Joshua 22 in the SBIPS

Joshua 22 in the SBISS

Joshua 22 in the SBITS

Joshua 22 in the SBITS2

Joshua 22 in the SBITS3

Joshua 22 in the SBITS4

Joshua 22 in the SBIUS

Joshua 22 in the SBIVS

Joshua 22 in the SBT

Joshua 22 in the SBT1E

Joshua 22 in the SCHL

Joshua 22 in the SNT

Joshua 22 in the SUSU

Joshua 22 in the SUSU2

Joshua 22 in the SYNO

Joshua 22 in the TBIAOTANT

Joshua 22 in the TBT1E

Joshua 22 in the TBT1E2

Joshua 22 in the TFTIP

Joshua 22 in the TFTU

Joshua 22 in the TGNTATF3T

Joshua 22 in the THAI

Joshua 22 in the TNFD

Joshua 22 in the TNT

Joshua 22 in the TNTIK

Joshua 22 in the TNTIL

Joshua 22 in the TNTIN

Joshua 22 in the TNTIP

Joshua 22 in the TNTIZ

Joshua 22 in the TOMA

Joshua 22 in the TTENT

Joshua 22 in the UBG

Joshua 22 in the UGV

Joshua 22 in the UGV2

Joshua 22 in the UGV3

Joshua 22 in the VBL

Joshua 22 in the VDCC

Joshua 22 in the YALU

Joshua 22 in the YAPE

Joshua 22 in the YBVTP

Joshua 22 in the ZBP