Leviticus 26 (BOKCV)

1 “ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, au mnara, wala jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu. 2 “ ‘Zishikeni Sabato zangu na kuheshimu mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi BWANA. 3 “ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu, 4 nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 5 Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu. Pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu. 6 “ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na yeyote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu. 7 Mtawafukuza adui zenu, nanyi mtawaua kwa upanga mbele yenu. 8 Watu wenu watano watafukuza adui mia, watu wenu mia watafukuza adui elfu kumi, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu. 9 “ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika Agano langu na ninyi. 10 Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya. 11 Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia. 12 Nitatembea katikati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu. 13 Mimi ndimi BWANA Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja kongwa lenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu. 14 “ ‘Lakini kama hamtanisikiliza na kutimiza maagizo haya yote, 15 nanyi kama mtazikataa amri zangu na kuzichukia sheria zangu, tena mkishindwa kutimiza amri zangu na hivyo mkavunja agano langu, 16 ndipo nitakapowafanyia hili: Nitawaletea juu yenu hofu ya ghafula, magonjwa ya kufisha, na homa itakayopofusha macho yenu na kuwaondolea uhai wenu. Mtapanda mbegu bila mafanikio, kwa sababu adui zenu wataila. 17 Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza. 18 “ ‘Kama baada ya haya yote hamtanisikiliza, nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu. 19 Nitakivunja kiburi chenu cha ukaidi na kuifanya anga iliyo juu yenu iwe kama chuma, na ardhi yenu kama shaba. 20 Nguvu zenu zitatumika bila ya mafanikio, kwa sababu ardhi yenu haitawazalia mazao yake, wala miti ya nchi yenu haitazaa matunda yake. 21 “ ‘Kama mtaendelea kuwa na uadui nami, na kukataa kunisikiliza, nitawazidishia mateso yenu mara saba zaidi, kama dhambi zenu zinavyostahili. 22 Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ngʼombe wenu, na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo, hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu. 23 “ ‘Ikiwa pamoja na mambo haya hamtakubali maonyo yangu lakini mkaendelea kuweka uadui nami, 24 mimi mwenyewe nitaweka uadui nanyi, na kuwatesa kwa ajili ya dhambi zenu mara saba zaidi. 25 Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja Agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni katikati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu. 26 Nitakapowaondolea upatikanaji wa mkate wenu, wanawake kumi wataoka mkate wenu katika tanuru moja, nao wataugawa mkate kidogo kwa kupima. Mtakula, lakini hamtashiba. 27 “ ‘Kama hata baada ya haya bado hamtanisikiliza lakini mkaendelea kuweka uadui nami, 28 ndipo katika hasira yangu nitaweka uadui nanyi, nami mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 29 Mtakula nyama ya wana wenu na nyama ya binti zenu. 30 Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nibomoe madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana. 31 Nitaifanya miji yenu kuwa magofu, na kuharibu mahali patakatifu penu pa kuabudia, nami sitapendezwa na harufu nzuri ya sadaka zenu. 32 Nitaiharibu nchi, ili adui zenu watakaokuja kuishi humo washangae. 33 Nitawatawanya ninyi miongoni mwa mataifa, na kuufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itaharibiwa, nayo miji yenu itakuwa magofu. 34 Ndipo nchi itafurahia Sabato zake muda wote ule itakapokuwa ukiwa, nanyi mkiwa katika nchi ya adui zenu. Ndipo nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake. 35 Wakati wote nchi itakapobaki ukiwa, itapumzika na kufurahia Sabato zake ambazo haikuzipata mlipokuwa mnaishi humo. 36 “ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza. 37 Watajikwaa mmoja juu ya mwingine kama wakimbiao upanga, hata ingawa hakuna anayewafuatia. Hivyo hamtaweza kusimama mbele ya adui zenu. 38 Mtaangamia katikati ya mataifa; nchi ya adui zenu itawala. 39 Wale wenu watakaobaki wataangamia katika nchi za adui zao kwa sababu ya dhambi zao; pia kwa sababu ya dhambi za baba zao wataangamia. 40 “ ‘Lakini kama watatubu dhambi zao na dhambi za baba zao, udanganyifu wao dhidi yangu na uadui wao kwangu, 41 ambao ulinifanya niwe na uadui nao hata nikawapeleka katika nchi ya adui zao, wakati mioyo yao isiyotahiriwa itanyenyekea na kutubu dhambi yao, 42 nami nitakumbuka agano langu na Yakobo, na agano langu na Isaki, na agano langu na Abrahamu, nami nitaikumbuka nchi. 43 Kwa kuwa wataiacha nchi ukiwa, nayo itafurahia Sabato zake wakati itakuwa ukiwa bila wao. Wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu walizikataa sheria zangu na kuzichukia amri zangu. 44 Lakini pamoja na hili, wakati watakuwa katika nchi ya adui zao, sitawakataa wala kuwachukia kiasi cha kuwaharibu kabisa na kuvunja agano langu nao. Mimi ndimi BWANA Mungu wao. 45 Lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano langu na baba zao, ambao niliwatoa Misri mbele ya mataifa ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi BWANA.’ ” 46 Hizi ndizo amri, sheria na pia masharti ambazo BWANA alifanya kati yake mwenyewe na Waisraeli katika Mlima Sinai kupitia kwa Mose.

In Other Versions

Leviticus 26 in the ANGEFD

Leviticus 26 in the ANTPNG2D

Leviticus 26 in the AS21

Leviticus 26 in the BAGH

Leviticus 26 in the BBPNG

Leviticus 26 in the BBT1E

Leviticus 26 in the BDS

Leviticus 26 in the BEV

Leviticus 26 in the BHAD

Leviticus 26 in the BIB

Leviticus 26 in the BLPT

Leviticus 26 in the BNT

Leviticus 26 in the BNTABOOT

Leviticus 26 in the BNTLV

Leviticus 26 in the BOATCB

Leviticus 26 in the BOATCB2

Leviticus 26 in the BOBCV

Leviticus 26 in the BOCNT

Leviticus 26 in the BOECS

Leviticus 26 in the BOGWICC

Leviticus 26 in the BOHCB

Leviticus 26 in the BOHCV

Leviticus 26 in the BOHLNT

Leviticus 26 in the BOHNTLTAL

Leviticus 26 in the BOICB

Leviticus 26 in the BOILNTAP

Leviticus 26 in the BOITCV

Leviticus 26 in the BOKCV2

Leviticus 26 in the BOKHWOG

Leviticus 26 in the BOKSSV

Leviticus 26 in the BOLCB

Leviticus 26 in the BOLCB2

Leviticus 26 in the BOMCV

Leviticus 26 in the BONAV

Leviticus 26 in the BONCB

Leviticus 26 in the BONLT

Leviticus 26 in the BONUT2

Leviticus 26 in the BOPLNT

Leviticus 26 in the BOSCB

Leviticus 26 in the BOSNC

Leviticus 26 in the BOTLNT

Leviticus 26 in the BOVCB

Leviticus 26 in the BOYCB

Leviticus 26 in the BPBB

Leviticus 26 in the BPH

Leviticus 26 in the BSB

Leviticus 26 in the CCB

Leviticus 26 in the CUV

Leviticus 26 in the CUVS

Leviticus 26 in the DBT

Leviticus 26 in the DGDNT

Leviticus 26 in the DHNT

Leviticus 26 in the DNT

Leviticus 26 in the ELBE

Leviticus 26 in the EMTV

Leviticus 26 in the ESV

Leviticus 26 in the FBV

Leviticus 26 in the FEB

Leviticus 26 in the GGMNT

Leviticus 26 in the GNT

Leviticus 26 in the HARY

Leviticus 26 in the HNT

Leviticus 26 in the IRVA

Leviticus 26 in the IRVB

Leviticus 26 in the IRVG

Leviticus 26 in the IRVH

Leviticus 26 in the IRVK

Leviticus 26 in the IRVM

Leviticus 26 in the IRVM2

Leviticus 26 in the IRVO

Leviticus 26 in the IRVP

Leviticus 26 in the IRVT

Leviticus 26 in the IRVT2

Leviticus 26 in the IRVU

Leviticus 26 in the ISVN

Leviticus 26 in the JSNT

Leviticus 26 in the KAPI

Leviticus 26 in the KBT1ETNIK

Leviticus 26 in the KBV

Leviticus 26 in the KJV

Leviticus 26 in the KNFD

Leviticus 26 in the LBA

Leviticus 26 in the LBLA

Leviticus 26 in the LNT

Leviticus 26 in the LSV

Leviticus 26 in the MAAL

Leviticus 26 in the MBV

Leviticus 26 in the MBV2

Leviticus 26 in the MHNT

Leviticus 26 in the MKNFD

Leviticus 26 in the MNG

Leviticus 26 in the MNT

Leviticus 26 in the MNT2

Leviticus 26 in the MRS1T

Leviticus 26 in the NAA

Leviticus 26 in the NASB

Leviticus 26 in the NBLA

Leviticus 26 in the NBS

Leviticus 26 in the NBVTP

Leviticus 26 in the NET2

Leviticus 26 in the NIV11

Leviticus 26 in the NNT

Leviticus 26 in the NNT2

Leviticus 26 in the NNT3

Leviticus 26 in the PDDPT

Leviticus 26 in the PFNT

Leviticus 26 in the RMNT

Leviticus 26 in the SBIAS

Leviticus 26 in the SBIBS

Leviticus 26 in the SBIBS2

Leviticus 26 in the SBICS

Leviticus 26 in the SBIDS

Leviticus 26 in the SBIGS

Leviticus 26 in the SBIHS

Leviticus 26 in the SBIIS

Leviticus 26 in the SBIIS2

Leviticus 26 in the SBIIS3

Leviticus 26 in the SBIKS

Leviticus 26 in the SBIKS2

Leviticus 26 in the SBIMS

Leviticus 26 in the SBIOS

Leviticus 26 in the SBIPS

Leviticus 26 in the SBISS

Leviticus 26 in the SBITS

Leviticus 26 in the SBITS2

Leviticus 26 in the SBITS3

Leviticus 26 in the SBITS4

Leviticus 26 in the SBIUS

Leviticus 26 in the SBIVS

Leviticus 26 in the SBT

Leviticus 26 in the SBT1E

Leviticus 26 in the SCHL

Leviticus 26 in the SNT

Leviticus 26 in the SUSU

Leviticus 26 in the SUSU2

Leviticus 26 in the SYNO

Leviticus 26 in the TBIAOTANT

Leviticus 26 in the TBT1E

Leviticus 26 in the TBT1E2

Leviticus 26 in the TFTIP

Leviticus 26 in the TFTU

Leviticus 26 in the TGNTATF3T

Leviticus 26 in the THAI

Leviticus 26 in the TNFD

Leviticus 26 in the TNT

Leviticus 26 in the TNTIK

Leviticus 26 in the TNTIL

Leviticus 26 in the TNTIN

Leviticus 26 in the TNTIP

Leviticus 26 in the TNTIZ

Leviticus 26 in the TOMA

Leviticus 26 in the TTENT

Leviticus 26 in the UBG

Leviticus 26 in the UGV

Leviticus 26 in the UGV2

Leviticus 26 in the UGV3

Leviticus 26 in the VBL

Leviticus 26 in the VDCC

Leviticus 26 in the YALU

Leviticus 26 in the YAPE

Leviticus 26 in the YBVTP

Leviticus 26 in the ZBP