Numbers 19 (BOKCV)
1 BWANA akamwambia Mose na Aroni: 2 “Hivi ndivyo sheria ambayo BWANA ameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa, na ambaye hajapata kufungwa nira. 3 Mpeni kuhani Eleazari huyo mtamba; naye atatolewa nje ya kambi na kuchinjwa mbele yake huyo kuhani. 4 Kisha kuhani Eleazari atachukua baadhi ya damu yake kwenye kidole chake na kuinyunyiza mara saba kuelekea upande wa mbele ya Hema la Kukutania. 5 Wakati angali akitazama, mtamba huyo atateketezwa: ngozi yake, nyama yake, damu na sehemu zake za ndani. 6 Kuhani atachukua kuni za mti wa mwerezi, hisopo na sufu nyekundu, na kuvitupa kwenye huyo mtamba anayeungua. 7 Baada ya hayo, kuhani lazima afue nguo zake, na aoge mwili wake kwa maji. Kisha anaweza kurudi kambini, lakini atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni. 8 Mtu amchomaye huyo mtamba lazima naye pia afue nguo zake na kuoga kwa maji, naye pia atakuwa najisi mpaka jioni. 9 “Mtu ambaye ni safi atakusanya majivu ya mtamba huyo na kuyaweka mahali ambapo ni safi nje ya kambi kwa taratibu za kiibada. Yatahifadhiwa na jumuiya ya Kiisraeli kwa matumizi katika maji ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa kutoka dhambini. 10 Mtu akusanyaye majivu ya huyo mtamba ni lazima pia afue nguo zake, kadhalika naye pia atakuwa najisi hadi jioni. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa Waisraeli na kwa wageni wanaoishi miongoni mwao. 11 “Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote atakuwa najisi kwa siku saba. 12 Ni lazima ajitakase mwenyewe kwa maji katika siku ya tatu na siku ya saba, ndipo atakuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu na ya saba, hatakuwa safi. 13 Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani ya BWANA. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake. 14 “Hii ndiyo sheria itumikayo wakati mtu amekufa ndani ya hema: Yeyote aingiaye ndani ya hema hilo na yeyote aliye ndani yake watakuwa najisi kwa muda wa siku saba, 15 nacho kila chombo kisicho na kifuniko juu yake kitakuwa najisi. 16 “Mtu yeyote aliyeko nje mahali pa wazi agusaye mtu aliyeuawa kwa upanga au mtu aliyekufa kwa kifo cha kawaida, au mtu yeyote agusaye mfupa wa mtu aliyekufa au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba. 17 “Kwa mtu aliye najisi, weka majivu ya sadaka ya utakaso wa dhambi ndani ya chombo, umimine maji safi juu yao. 18 Kisha mtu aliye safi kwa kawaida za kiibada atachukua hisopo, achovye ndani ya maji, na kunyunyizia hema na vifaa vyote pamoja na watu ambao walikuwamo. Pia ni lazima amnyunyizie mtu yeyote ambaye amegusa mfupa wa mtu aliyekufa, au kaburi, au mtu ambaye ameuawa, au mtu ambaye amekufa kifo cha kawaida. 19 Mtu ambaye ni safi ndiye atakayemnyunyizia yeyote ambaye ni najisi siku ya tatu na siku ya saba, na katika siku ya saba atamtakasa mtu huyo. Mtu ambaye ametakaswa lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji, na jioni ile atakuwa safi. 20 Lakini ikiwa mtu ambaye ni najisi hakujitakasa mwenyewe, ni lazima akatiliwe mbali na jumuiya, kwa sababu ameinajisi Maskani ya BWANA. Maji ya utakaso hayajanyunyizwa juu yake, naye ni najisi. 21 Hii ni sheria ya kudumu kwao.“Mtu yeyote ambaye ananyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na yeyote ambaye hugusa maji ya utakaso atakuwa najisi mpaka jioni. 22 Kitu chochote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na yeyote akigusaye huwa najisi mpaka jioni.”
In Other Versions
Numbers 19 in the ANGEFD
Numbers 19 in the ANTPNG2D
Numbers 19 in the AS21
Numbers 19 in the BAGH
Numbers 19 in the BBPNG
Numbers 19 in the BBT1E
Numbers 19 in the BDS
Numbers 19 in the BEV
Numbers 19 in the BHAD
Numbers 19 in the BIB
Numbers 19 in the BLPT
Numbers 19 in the BNT
Numbers 19 in the BNTABOOT
Numbers 19 in the BNTLV
Numbers 19 in the BOATCB
Numbers 19 in the BOATCB2
Numbers 19 in the BOBCV
Numbers 19 in the BOCNT
Numbers 19 in the BOECS
Numbers 19 in the BOGWICC
Numbers 19 in the BOHCB
Numbers 19 in the BOHCV
Numbers 19 in the BOHLNT
Numbers 19 in the BOHNTLTAL
Numbers 19 in the BOICB
Numbers 19 in the BOILNTAP
Numbers 19 in the BOITCV
Numbers 19 in the BOKCV2
Numbers 19 in the BOKHWOG
Numbers 19 in the BOKSSV
Numbers 19 in the BOLCB
Numbers 19 in the BOLCB2
Numbers 19 in the BOMCV
Numbers 19 in the BONAV
Numbers 19 in the BONCB
Numbers 19 in the BONLT
Numbers 19 in the BONUT2
Numbers 19 in the BOPLNT
Numbers 19 in the BOSCB
Numbers 19 in the BOSNC
Numbers 19 in the BOTLNT
Numbers 19 in the BOVCB
Numbers 19 in the BOYCB
Numbers 19 in the BPBB
Numbers 19 in the BPH
Numbers 19 in the BSB
Numbers 19 in the CCB
Numbers 19 in the CUV
Numbers 19 in the CUVS
Numbers 19 in the DBT
Numbers 19 in the DGDNT
Numbers 19 in the DHNT
Numbers 19 in the DNT
Numbers 19 in the ELBE
Numbers 19 in the EMTV
Numbers 19 in the ESV
Numbers 19 in the FBV
Numbers 19 in the FEB
Numbers 19 in the GGMNT
Numbers 19 in the GNT
Numbers 19 in the HARY
Numbers 19 in the HNT
Numbers 19 in the IRVA
Numbers 19 in the IRVB
Numbers 19 in the IRVG
Numbers 19 in the IRVH
Numbers 19 in the IRVK
Numbers 19 in the IRVM
Numbers 19 in the IRVM2
Numbers 19 in the IRVO
Numbers 19 in the IRVP
Numbers 19 in the IRVT
Numbers 19 in the IRVT2
Numbers 19 in the IRVU
Numbers 19 in the ISVN
Numbers 19 in the JSNT
Numbers 19 in the KAPI
Numbers 19 in the KBT1ETNIK
Numbers 19 in the KBV
Numbers 19 in the KJV
Numbers 19 in the KNFD
Numbers 19 in the LBA
Numbers 19 in the LBLA
Numbers 19 in the LNT
Numbers 19 in the LSV
Numbers 19 in the MAAL
Numbers 19 in the MBV
Numbers 19 in the MBV2
Numbers 19 in the MHNT
Numbers 19 in the MKNFD
Numbers 19 in the MNG
Numbers 19 in the MNT
Numbers 19 in the MNT2
Numbers 19 in the MRS1T
Numbers 19 in the NAA
Numbers 19 in the NASB
Numbers 19 in the NBLA
Numbers 19 in the NBS
Numbers 19 in the NBVTP
Numbers 19 in the NET2
Numbers 19 in the NIV11
Numbers 19 in the NNT
Numbers 19 in the NNT2
Numbers 19 in the NNT3
Numbers 19 in the PDDPT
Numbers 19 in the PFNT
Numbers 19 in the RMNT
Numbers 19 in the SBIAS
Numbers 19 in the SBIBS
Numbers 19 in the SBIBS2
Numbers 19 in the SBICS
Numbers 19 in the SBIDS
Numbers 19 in the SBIGS
Numbers 19 in the SBIHS
Numbers 19 in the SBIIS
Numbers 19 in the SBIIS2
Numbers 19 in the SBIIS3
Numbers 19 in the SBIKS
Numbers 19 in the SBIKS2
Numbers 19 in the SBIMS
Numbers 19 in the SBIOS
Numbers 19 in the SBIPS
Numbers 19 in the SBISS
Numbers 19 in the SBITS
Numbers 19 in the SBITS2
Numbers 19 in the SBITS3
Numbers 19 in the SBITS4
Numbers 19 in the SBIUS
Numbers 19 in the SBIVS
Numbers 19 in the SBT
Numbers 19 in the SBT1E
Numbers 19 in the SCHL
Numbers 19 in the SNT
Numbers 19 in the SUSU
Numbers 19 in the SUSU2
Numbers 19 in the SYNO
Numbers 19 in the TBIAOTANT
Numbers 19 in the TBT1E
Numbers 19 in the TBT1E2
Numbers 19 in the TFTIP
Numbers 19 in the TFTU
Numbers 19 in the TGNTATF3T
Numbers 19 in the THAI
Numbers 19 in the TNFD
Numbers 19 in the TNT
Numbers 19 in the TNTIK
Numbers 19 in the TNTIL
Numbers 19 in the TNTIN
Numbers 19 in the TNTIP
Numbers 19 in the TNTIZ
Numbers 19 in the TOMA
Numbers 19 in the TTENT
Numbers 19 in the UBG
Numbers 19 in the UGV
Numbers 19 in the UGV2
Numbers 19 in the UGV3
Numbers 19 in the VBL
Numbers 19 in the VDCC
Numbers 19 in the YALU
Numbers 19 in the YAPE
Numbers 19 in the YBVTP
Numbers 19 in the ZBP