Psalms 29 (BOKCV)
undefined Zaburi ya Daudi. 1 Mpeni BWANA, enyi mashujaa,mpeni BWANA utukufu na nguvu. 2 Mpeni BWANA utukufu unaostahili jina lake;mwabuduni BWANA katika uzuri wa utakatifu wake. 3 Sauti ya BWANA iko juu ya maji;Mungu wa utukufu hupiga radi, BWANA hupiga radi juu ya maji makuu. 4 Sauti ya BWANA ina nguvu;sauti ya BWANA ni tukufu. 5 Sauti ya BWANA huvunja mierezi; BWANA huvunja vipande vipandemierezi ya Lebanoni. 6 Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,Sirioni urukaruke kama mwana nyati. 7 Sauti ya BWANA hupiga kwa mialiya umeme wa radi. 8 Sauti ya BWANA hutikisa jangwa; BWANA hutikisa Jangwa la Kadeshi. 9 Sauti ya BWANA huzalisha ayala,na huuacha msitu wazi.Hekaluni mwake wote wasema,“Utukufu!” 10 BWANA huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; BWANA ametawazwa kuwa Mfalme milele. 11 BWANA huwapa watu wake nguvu; BWANA huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.