Psalms 61 (BOKCV)
undefined Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi. 1 Ee Mungu, sikia kilio changu,usikilize maombi yangu. 2 Kutoka miisho ya dunia ninakuita,ninaita huku moyo wangu unadhoofika;uniongoze kwenye mwambaule ulio juu kuliko mimi. 3 Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu,ngome imara dhidi ya adui. 4 Natamani kukaa hemani mwako milele,na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako. 5 Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu,umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako. 6 Mwongezee mfalme siku za maisha yake,miaka yake kwa vizazi vingi. 7 Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele;amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde. 8 Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lakona kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.