Psalms 70 (BOKCV)
undefined Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi. 1 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;Ee BWANA, njoo hima unisaidie. 2 Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,waaibishwe na kufadhaishwa;wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,warudishwe nyuma kwa aibu. 3 Wale waniambiao, “Aha! Aha!”warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao. 4 Lakini wote wakutafutaowashangilie na kukufurahia,wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,“Mungu na atukuzwe!” 5 Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;Ee Mungu, unijie haraka.Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;Ee BWANA, usikawie.