Zechariah 1 (BOKCV)
1 Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema: 2 “BWANA aliwakasirikia sana baba zako wa zamani. 3 Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 4 Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema BWANA. 5 Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele? 6 Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu?”“Kisha walitubu na kusema, ‘BWANA Mwenye Nguvu Zote ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’ ” 7 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido. 8 Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe. 9 Nikauliza, “Hivi ni vitu gani bwana wangu?”Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, “Nitakuonyesha kuwa ni nini.” 10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambao BWANA amewatuma waende duniani kote.” 11 Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa BWANA, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, “Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.” 12 Kisha malaika wa BWANA akasema, “BWANA Mwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?” 13 Kwa hiyo BWANA akazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami. 14 Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, “Tangaza neno hili: Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni, 15 lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.’ 16 “Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo BWANA: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. 17 “Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote: ‘Miji yangu itafurika tena ustawi na BWANA atamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ ” 18 Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! 19 Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?”Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.” 20 Kisha BWANA akanionyesha mafundi wanne. 21 Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?”Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.”
In Other Versions
Zechariah 1 in the ANGEFD
Zechariah 1 in the ANTPNG2D
Zechariah 1 in the AS21
Zechariah 1 in the BAGH
Zechariah 1 in the BBPNG
Zechariah 1 in the BBT1E
Zechariah 1 in the BDS
Zechariah 1 in the BEV
Zechariah 1 in the BHAD
Zechariah 1 in the BIB
Zechariah 1 in the BLPT
Zechariah 1 in the BNT
Zechariah 1 in the BNTABOOT
Zechariah 1 in the BNTLV
Zechariah 1 in the BOATCB
Zechariah 1 in the BOATCB2
Zechariah 1 in the BOBCV
Zechariah 1 in the BOCNT
Zechariah 1 in the BOECS
Zechariah 1 in the BOGWICC
Zechariah 1 in the BOHCB
Zechariah 1 in the BOHCV
Zechariah 1 in the BOHLNT
Zechariah 1 in the BOHNTLTAL
Zechariah 1 in the BOICB
Zechariah 1 in the BOILNTAP
Zechariah 1 in the BOITCV
Zechariah 1 in the BOKCV2
Zechariah 1 in the BOKHWOG
Zechariah 1 in the BOKSSV
Zechariah 1 in the BOLCB
Zechariah 1 in the BOLCB2
Zechariah 1 in the BOMCV
Zechariah 1 in the BONAV
Zechariah 1 in the BONCB
Zechariah 1 in the BONLT
Zechariah 1 in the BONUT2
Zechariah 1 in the BOPLNT
Zechariah 1 in the BOSCB
Zechariah 1 in the BOSNC
Zechariah 1 in the BOTLNT
Zechariah 1 in the BOVCB
Zechariah 1 in the BOYCB
Zechariah 1 in the BPBB
Zechariah 1 in the BPH
Zechariah 1 in the BSB
Zechariah 1 in the CCB
Zechariah 1 in the CUV
Zechariah 1 in the CUVS
Zechariah 1 in the DBT
Zechariah 1 in the DGDNT
Zechariah 1 in the DHNT
Zechariah 1 in the DNT
Zechariah 1 in the ELBE
Zechariah 1 in the EMTV
Zechariah 1 in the ESV
Zechariah 1 in the FBV
Zechariah 1 in the FEB
Zechariah 1 in the GGMNT
Zechariah 1 in the GNT
Zechariah 1 in the HARY
Zechariah 1 in the HNT
Zechariah 1 in the IRVA
Zechariah 1 in the IRVB
Zechariah 1 in the IRVG
Zechariah 1 in the IRVH
Zechariah 1 in the IRVK
Zechariah 1 in the IRVM
Zechariah 1 in the IRVM2
Zechariah 1 in the IRVO
Zechariah 1 in the IRVP
Zechariah 1 in the IRVT
Zechariah 1 in the IRVT2
Zechariah 1 in the IRVU
Zechariah 1 in the ISVN
Zechariah 1 in the JSNT
Zechariah 1 in the KAPI
Zechariah 1 in the KBT1ETNIK
Zechariah 1 in the KBV
Zechariah 1 in the KJV
Zechariah 1 in the KNFD
Zechariah 1 in the LBA
Zechariah 1 in the LBLA
Zechariah 1 in the LNT
Zechariah 1 in the LSV
Zechariah 1 in the MAAL
Zechariah 1 in the MBV
Zechariah 1 in the MBV2
Zechariah 1 in the MHNT
Zechariah 1 in the MKNFD
Zechariah 1 in the MNG
Zechariah 1 in the MNT
Zechariah 1 in the MNT2
Zechariah 1 in the MRS1T
Zechariah 1 in the NAA
Zechariah 1 in the NASB
Zechariah 1 in the NBLA
Zechariah 1 in the NBS
Zechariah 1 in the NBVTP
Zechariah 1 in the NET2
Zechariah 1 in the NIV11
Zechariah 1 in the NNT
Zechariah 1 in the NNT2
Zechariah 1 in the NNT3
Zechariah 1 in the PDDPT
Zechariah 1 in the PFNT
Zechariah 1 in the RMNT
Zechariah 1 in the SBIAS
Zechariah 1 in the SBIBS
Zechariah 1 in the SBIBS2
Zechariah 1 in the SBICS
Zechariah 1 in the SBIDS
Zechariah 1 in the SBIGS
Zechariah 1 in the SBIHS
Zechariah 1 in the SBIIS
Zechariah 1 in the SBIIS2
Zechariah 1 in the SBIIS3
Zechariah 1 in the SBIKS
Zechariah 1 in the SBIKS2
Zechariah 1 in the SBIMS
Zechariah 1 in the SBIOS
Zechariah 1 in the SBIPS
Zechariah 1 in the SBISS
Zechariah 1 in the SBITS
Zechariah 1 in the SBITS2
Zechariah 1 in the SBITS3
Zechariah 1 in the SBITS4
Zechariah 1 in the SBIUS
Zechariah 1 in the SBIVS
Zechariah 1 in the SBT
Zechariah 1 in the SBT1E
Zechariah 1 in the SCHL
Zechariah 1 in the SNT
Zechariah 1 in the SUSU
Zechariah 1 in the SUSU2
Zechariah 1 in the SYNO
Zechariah 1 in the TBIAOTANT
Zechariah 1 in the TBT1E
Zechariah 1 in the TBT1E2
Zechariah 1 in the TFTIP
Zechariah 1 in the TFTU
Zechariah 1 in the TGNTATF3T
Zechariah 1 in the THAI
Zechariah 1 in the TNFD
Zechariah 1 in the TNT
Zechariah 1 in the TNTIK
Zechariah 1 in the TNTIL
Zechariah 1 in the TNTIN
Zechariah 1 in the TNTIP
Zechariah 1 in the TNTIZ
Zechariah 1 in the TOMA
Zechariah 1 in the TTENT
Zechariah 1 in the UBG
Zechariah 1 in the UGV
Zechariah 1 in the UGV2
Zechariah 1 in the UGV3
Zechariah 1 in the VBL
Zechariah 1 in the VDCC
Zechariah 1 in the YALU
Zechariah 1 in the YAPE
Zechariah 1 in the YBVTP
Zechariah 1 in the ZBP