1 Chronicles 22 (BOKCV)

1 Ndipo Daudi akasema, “Nyumba ya BWANA Mungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.” 2 Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu. 3 Daudi akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika. 4 Pia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi idadi kubwa ya mierezi. 5 Daudi akasema, “Mwanangu Solomoni bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili ya BWANA inatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake. 6 Kisha akamwita Solomoni mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili ya BWANA, Mungu wa Israeli. 7 Daudi akamwambia Solomoni: “Mwanangu, nilikuwa na jambo hili ndani ya moyo wangu kujenga nyumba kwa ajili ya Jina la BWANA Mungu wangu. 8 Lakini neno hili la BWANA likanijia, kusema: ‘Wewe umemwaga damu nyingi na kupigana vita vingi. Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu. 9 Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Solomoni, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake. 10 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu. Yeye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nami nitakifanya imara kiti chake cha enzi cha utawala wake katika Israeli milele.’ 11 “Sasa, mwanangu, BWANA awe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba ya BWANA Mungu wako, kama alivyosema utafanya. 12 BWANA na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya BWANA Mungu wako. 13 Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria BWANA alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa. 14 “Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la BWANA: talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. 15 Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi 16 wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye BWANA awe pamoja nawe.” 17 Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe. 18 Akawaambia, “Je, BWANA Mungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini ya BWANA na watu wake. 19 Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta BWANA Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya BWANA Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la BWANA na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la BWANA.”

In Other Versions

1 Chronicles 22 in the ANGEFD

1 Chronicles 22 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 22 in the AS21

1 Chronicles 22 in the BAGH

1 Chronicles 22 in the BBPNG

1 Chronicles 22 in the BBT1E

1 Chronicles 22 in the BDS

1 Chronicles 22 in the BEV

1 Chronicles 22 in the BHAD

1 Chronicles 22 in the BIB

1 Chronicles 22 in the BLPT

1 Chronicles 22 in the BNT

1 Chronicles 22 in the BNTABOOT

1 Chronicles 22 in the BNTLV

1 Chronicles 22 in the BOATCB

1 Chronicles 22 in the BOATCB2

1 Chronicles 22 in the BOBCV

1 Chronicles 22 in the BOCNT

1 Chronicles 22 in the BOECS

1 Chronicles 22 in the BOGWICC

1 Chronicles 22 in the BOHCB

1 Chronicles 22 in the BOHCV

1 Chronicles 22 in the BOHLNT

1 Chronicles 22 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 22 in the BOICB

1 Chronicles 22 in the BOILNTAP

1 Chronicles 22 in the BOITCV

1 Chronicles 22 in the BOKCV2

1 Chronicles 22 in the BOKHWOG

1 Chronicles 22 in the BOKSSV

1 Chronicles 22 in the BOLCB

1 Chronicles 22 in the BOLCB2

1 Chronicles 22 in the BOMCV

1 Chronicles 22 in the BONAV

1 Chronicles 22 in the BONCB

1 Chronicles 22 in the BONLT

1 Chronicles 22 in the BONUT2

1 Chronicles 22 in the BOPLNT

1 Chronicles 22 in the BOSCB

1 Chronicles 22 in the BOSNC

1 Chronicles 22 in the BOTLNT

1 Chronicles 22 in the BOVCB

1 Chronicles 22 in the BOYCB

1 Chronicles 22 in the BPBB

1 Chronicles 22 in the BPH

1 Chronicles 22 in the BSB

1 Chronicles 22 in the CCB

1 Chronicles 22 in the CUV

1 Chronicles 22 in the CUVS

1 Chronicles 22 in the DBT

1 Chronicles 22 in the DGDNT

1 Chronicles 22 in the DHNT

1 Chronicles 22 in the DNT

1 Chronicles 22 in the ELBE

1 Chronicles 22 in the EMTV

1 Chronicles 22 in the ESV

1 Chronicles 22 in the FBV

1 Chronicles 22 in the FEB

1 Chronicles 22 in the GGMNT

1 Chronicles 22 in the GNT

1 Chronicles 22 in the HARY

1 Chronicles 22 in the HNT

1 Chronicles 22 in the IRVA

1 Chronicles 22 in the IRVB

1 Chronicles 22 in the IRVG

1 Chronicles 22 in the IRVH

1 Chronicles 22 in the IRVK

1 Chronicles 22 in the IRVM

1 Chronicles 22 in the IRVM2

1 Chronicles 22 in the IRVO

1 Chronicles 22 in the IRVP

1 Chronicles 22 in the IRVT

1 Chronicles 22 in the IRVT2

1 Chronicles 22 in the IRVU

1 Chronicles 22 in the ISVN

1 Chronicles 22 in the JSNT

1 Chronicles 22 in the KAPI

1 Chronicles 22 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 22 in the KBV

1 Chronicles 22 in the KJV

1 Chronicles 22 in the KNFD

1 Chronicles 22 in the LBA

1 Chronicles 22 in the LBLA

1 Chronicles 22 in the LNT

1 Chronicles 22 in the LSV

1 Chronicles 22 in the MAAL

1 Chronicles 22 in the MBV

1 Chronicles 22 in the MBV2

1 Chronicles 22 in the MHNT

1 Chronicles 22 in the MKNFD

1 Chronicles 22 in the MNG

1 Chronicles 22 in the MNT

1 Chronicles 22 in the MNT2

1 Chronicles 22 in the MRS1T

1 Chronicles 22 in the NAA

1 Chronicles 22 in the NASB

1 Chronicles 22 in the NBLA

1 Chronicles 22 in the NBS

1 Chronicles 22 in the NBVTP

1 Chronicles 22 in the NET2

1 Chronicles 22 in the NIV11

1 Chronicles 22 in the NNT

1 Chronicles 22 in the NNT2

1 Chronicles 22 in the NNT3

1 Chronicles 22 in the PDDPT

1 Chronicles 22 in the PFNT

1 Chronicles 22 in the RMNT

1 Chronicles 22 in the SBIAS

1 Chronicles 22 in the SBIBS

1 Chronicles 22 in the SBIBS2

1 Chronicles 22 in the SBICS

1 Chronicles 22 in the SBIDS

1 Chronicles 22 in the SBIGS

1 Chronicles 22 in the SBIHS

1 Chronicles 22 in the SBIIS

1 Chronicles 22 in the SBIIS2

1 Chronicles 22 in the SBIIS3

1 Chronicles 22 in the SBIKS

1 Chronicles 22 in the SBIKS2

1 Chronicles 22 in the SBIMS

1 Chronicles 22 in the SBIOS

1 Chronicles 22 in the SBIPS

1 Chronicles 22 in the SBISS

1 Chronicles 22 in the SBITS

1 Chronicles 22 in the SBITS2

1 Chronicles 22 in the SBITS3

1 Chronicles 22 in the SBITS4

1 Chronicles 22 in the SBIUS

1 Chronicles 22 in the SBIVS

1 Chronicles 22 in the SBT

1 Chronicles 22 in the SBT1E

1 Chronicles 22 in the SCHL

1 Chronicles 22 in the SNT

1 Chronicles 22 in the SUSU

1 Chronicles 22 in the SUSU2

1 Chronicles 22 in the SYNO

1 Chronicles 22 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 22 in the TBT1E

1 Chronicles 22 in the TBT1E2

1 Chronicles 22 in the TFTIP

1 Chronicles 22 in the TFTU

1 Chronicles 22 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 22 in the THAI

1 Chronicles 22 in the TNFD

1 Chronicles 22 in the TNT

1 Chronicles 22 in the TNTIK

1 Chronicles 22 in the TNTIL

1 Chronicles 22 in the TNTIN

1 Chronicles 22 in the TNTIP

1 Chronicles 22 in the TNTIZ

1 Chronicles 22 in the TOMA

1 Chronicles 22 in the TTENT

1 Chronicles 22 in the UBG

1 Chronicles 22 in the UGV

1 Chronicles 22 in the UGV2

1 Chronicles 22 in the UGV3

1 Chronicles 22 in the VBL

1 Chronicles 22 in the VDCC

1 Chronicles 22 in the YALU

1 Chronicles 22 in the YAPE

1 Chronicles 22 in the YBVTP

1 Chronicles 22 in the ZBP