1 John 2 (BOKCV)

1 Watoto wangu wapendwa, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba: ndiye Yesu Kristo, Mwenye Haki. 2 Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. 3 Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake. 4 Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli. 5 Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake. 6 Yeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda. 7 Wapendwa, siwaandikii ninyi amri mpya bali ile ya zamani, ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilosikia. 8 Lakini nawaandikia amri mpya, yaani, lile neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli tayari inangʼaa. 9 Yeyote anayesema yumo nuruni lakini anamchukia ndugu yake bado yuko gizani. 10 Yeye ampendaye ndugu yake anakaa nuruni, wala hakuna kitu chochote ndani yake cha kumkwaza. 11 Lakini yeyote amchukiaye ndugu yake, yuko gizani na anaenenda gizani, wala hajui anakokwenda, kwa sababu giza limempofusha macho. 12 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo,kwa sababu dhambi zenuzimesamehewa kwa ajili ya Jina lake. 13 Nawaandikia ninyi, akina baba,kwa sababu mmemjuayeye aliye tangu mwanzo.Nawaandikia ninyi vijanakwa sababu mmemshinda yule mwovu.Nawaandikia ninyi watoto wadogo,kwa sababu mmemjua Baba. 14 Nawaandikia ninyi akina baba,kwa sababu mmemjuayeye aliye tangu mwanzo.Nawaandikia ninyi vijana,kwa sababu mna nguvu,na neno la Mungu linakaa ndani yenu,nanyi mmemshinda yule mwovu. 15 Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. 16 Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. 17 Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele. 18 Watoto wadogo, huu ni wakati wa mwisho! Kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo anakuja, hivyo basi wapinga Kristo wengi wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua kwamba huu ni wakati wa mwisho. 19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa maana kama wangelikuwa wa kwetu, wangelikaa pamoja nasi, lakini kutoka kwao kulionyesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kwetu. 20 Lakini ninyi mmetiwa mafuta na yeye Aliye Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli. 21 Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo utokao katika kweli. 22 Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana Baba na Mwana. 23 Hakuna yeyote amkanaye Mwana aliye na Baba. Yeyote anayemkubali Mwana anaye na Baba pia. 24 Hakikisheni kwamba lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu. Kama lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25 Hii ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele. 26 Nawaandikia mambo haya kuhusu wale watu ambao wanajaribu kuwapotosha. 27 Nanyi, upako mlioupata kutoka kwake unakaa ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu yeyote kuwafundisha. Lakini kama vile upako wake unavyowafundisha kuhusu mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama ulivyowafundisha kaeni ndani yake. 28 Sasa basi, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake wakati wa kuja kwake. 29 Kama mkijua kuwa yeye ni mwenye haki, mwajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa naye.

In Other Versions

1 John 2 in the ANGEFD

1 John 2 in the ANTPNG2D

1 John 2 in the AS21

1 John 2 in the BAGH

1 John 2 in the BBPNG

1 John 2 in the BBT1E

1 John 2 in the BDS

1 John 2 in the BEV

1 John 2 in the BHAD

1 John 2 in the BIB

1 John 2 in the BLPT

1 John 2 in the BNT

1 John 2 in the BNTABOOT

1 John 2 in the BNTLV

1 John 2 in the BOATCB

1 John 2 in the BOATCB2

1 John 2 in the BOBCV

1 John 2 in the BOCNT

1 John 2 in the BOECS

1 John 2 in the BOGWICC

1 John 2 in the BOHCB

1 John 2 in the BOHCV

1 John 2 in the BOHLNT

1 John 2 in the BOHNTLTAL

1 John 2 in the BOICB

1 John 2 in the BOILNTAP

1 John 2 in the BOITCV

1 John 2 in the BOKCV2

1 John 2 in the BOKHWOG

1 John 2 in the BOKSSV

1 John 2 in the BOLCB

1 John 2 in the BOLCB2

1 John 2 in the BOMCV

1 John 2 in the BONAV

1 John 2 in the BONCB

1 John 2 in the BONLT

1 John 2 in the BONUT2

1 John 2 in the BOPLNT

1 John 2 in the BOSCB

1 John 2 in the BOSNC

1 John 2 in the BOTLNT

1 John 2 in the BOVCB

1 John 2 in the BOYCB

1 John 2 in the BPBB

1 John 2 in the BPH

1 John 2 in the BSB

1 John 2 in the CCB

1 John 2 in the CUV

1 John 2 in the CUVS

1 John 2 in the DBT

1 John 2 in the DGDNT

1 John 2 in the DHNT

1 John 2 in the DNT

1 John 2 in the ELBE

1 John 2 in the EMTV

1 John 2 in the ESV

1 John 2 in the FBV

1 John 2 in the FEB

1 John 2 in the GGMNT

1 John 2 in the GNT

1 John 2 in the HARY

1 John 2 in the HNT

1 John 2 in the IRVA

1 John 2 in the IRVB

1 John 2 in the IRVG

1 John 2 in the IRVH

1 John 2 in the IRVK

1 John 2 in the IRVM

1 John 2 in the IRVM2

1 John 2 in the IRVO

1 John 2 in the IRVP

1 John 2 in the IRVT

1 John 2 in the IRVT2

1 John 2 in the IRVU

1 John 2 in the ISVN

1 John 2 in the JSNT

1 John 2 in the KAPI

1 John 2 in the KBT1ETNIK

1 John 2 in the KBV

1 John 2 in the KJV

1 John 2 in the KNFD

1 John 2 in the LBA

1 John 2 in the LBLA

1 John 2 in the LNT

1 John 2 in the LSV

1 John 2 in the MAAL

1 John 2 in the MBV

1 John 2 in the MBV2

1 John 2 in the MHNT

1 John 2 in the MKNFD

1 John 2 in the MNG

1 John 2 in the MNT

1 John 2 in the MNT2

1 John 2 in the MRS1T

1 John 2 in the NAA

1 John 2 in the NASB

1 John 2 in the NBLA

1 John 2 in the NBS

1 John 2 in the NBVTP

1 John 2 in the NET2

1 John 2 in the NIV11

1 John 2 in the NNT

1 John 2 in the NNT2

1 John 2 in the NNT3

1 John 2 in the PDDPT

1 John 2 in the PFNT

1 John 2 in the RMNT

1 John 2 in the SBIAS

1 John 2 in the SBIBS

1 John 2 in the SBIBS2

1 John 2 in the SBICS

1 John 2 in the SBIDS

1 John 2 in the SBIGS

1 John 2 in the SBIHS

1 John 2 in the SBIIS

1 John 2 in the SBIIS2

1 John 2 in the SBIIS3

1 John 2 in the SBIKS

1 John 2 in the SBIKS2

1 John 2 in the SBIMS

1 John 2 in the SBIOS

1 John 2 in the SBIPS

1 John 2 in the SBISS

1 John 2 in the SBITS

1 John 2 in the SBITS2

1 John 2 in the SBITS3

1 John 2 in the SBITS4

1 John 2 in the SBIUS

1 John 2 in the SBIVS

1 John 2 in the SBT

1 John 2 in the SBT1E

1 John 2 in the SCHL

1 John 2 in the SNT

1 John 2 in the SUSU

1 John 2 in the SUSU2

1 John 2 in the SYNO

1 John 2 in the TBIAOTANT

1 John 2 in the TBT1E

1 John 2 in the TBT1E2

1 John 2 in the TFTIP

1 John 2 in the TFTU

1 John 2 in the TGNTATF3T

1 John 2 in the THAI

1 John 2 in the TNFD

1 John 2 in the TNT

1 John 2 in the TNTIK

1 John 2 in the TNTIL

1 John 2 in the TNTIN

1 John 2 in the TNTIP

1 John 2 in the TNTIZ

1 John 2 in the TOMA

1 John 2 in the TTENT

1 John 2 in the UBG

1 John 2 in the UGV

1 John 2 in the UGV2

1 John 2 in the UGV3

1 John 2 in the VBL

1 John 2 in the VDCC

1 John 2 in the YALU

1 John 2 in the YAPE

1 John 2 in the YBVTP

1 John 2 in the ZBP