1 Kings 17 (BOKCV)

1 Basi Eliya, Mtishbi kutoka Tishbi katika Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninamtumikia, hapatakuwa na umande wala mvua katika miaka hii, isipokuwa kwa neno langu.” 2 Kisha neno la BWANA likamjia Eliya, kusema, 3 “Ondoka hapa, elekea upande wa mashariki ukajifiche katika Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani. 4 Utakunywa maji kutoka kile kijito, nami nimeagiza kunguru wakulishe huko.” 5 Hivyo akafanya kile alichoambiwa na BWANA. Akaenda katika Kijito cha Kerithi, mashariki ya Yordani na akakaa huko. 6 Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji kutoka kile kijito. 7 Baada ya muda, kile kijito kikakauka kwa sababu mvua haikuwa imenyesha katika nchi. 8 Kisha neno la BWANA likamjia, kusema, 9 “Ondoka, uende Sarepta ya Sidoni na ukae huko. Nimemwagiza mjane katika sehemu ile akupatie chakula.” 10 Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, mjane alikuwa huko akiokota kuni. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.” 11 Alipokuwa anakwenda kumletea, akamwita akasema, “Tafadhali niletee pia kipande cha mkate.” 12 Akamjibu, “Hakika kama BWANA Mungu wako aishivyo, sina mkate wowote, isipokuwa konzi ya unga kwenye gudulia na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili kwamba tule, kiishe, tukafe.” 13 Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda nyumbani ukafanye kama ulivyosema. Lakini kwanza unitengenezee mimi mkate mdogo kutoka vile ulivyo navyo kisha uniletee na ndipo utayarishe chochote kwa ajili yako na mwanao. 14 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Lile gudulia la unga halitakwisha wala ile chupa ya mafuta haitakauka hadi siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi.’ ” 15 Akaondoka na kufanya kama Eliya alivyomwambia. Kwa hiyo kukawa na chakula kila siku kwa ajili ya Eliya, yule mwanamke na jamaa yake. 16 Kwa kuwa lile gudulia la unga halikwisha na ile chupa ya mafuta haikukauka, sawasawa na lile neno la BWANA alilosema Eliya. 17 Baada ya muda, mwana wa yule mwanamke mwenye nyumba akaugua. Hali yake ikaendelea kuwa mbaya sana, na hatimaye akaacha kupumua. 18 Akamwambia Eliya, “Una nini dhidi yangu, ewe mtu wa Mungu? Umekuja ili kukumbushia dhambi yangu na kusababisha kifo cha mwanangu?” 19 Eliya akamjibu, “Nipe mwanao.” Eliya akampokea kutoka kifuani mwake, akambeba mpaka chumba cha juu alipokuwa anaishi, akamlaza kitandani mwake. 20 Kisha akamlilia BWANA, akasema “Ee BWANA Mungu wangu, je, pia umeleta msiba juu ya mjane huyu ninayeishi pamoja naye, kwa kusababisha mwanawe kufa?” 21 Kisha akajinyoosha juu ya kijana mara tatu na kumlilia BWANA, akisema, “Ee BWANA Mungu wangu, nakuomba roho ya huyu kijana imrudie!” 22 BWANA akasikia kilio cha Eliya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka. 23 Eliya akamtwaa kijana na kumbeba kutoka chumbani mwake akamshusha kumpeleka kwenye nyumba. Akampa mama yake na kusema, “Tazama, mwanao yu hai!” 24 Ndipo yule mwanamke akamwambia Eliya, “Sasa ninajua kwamba wewe ni mtu wa Mungu, na kwamba neno la BWANA kutoka kinywani mwako ni kweli.”

In Other Versions

1 Kings 17 in the ANGEFD

1 Kings 17 in the ANTPNG2D

1 Kings 17 in the AS21

1 Kings 17 in the BAGH

1 Kings 17 in the BBPNG

1 Kings 17 in the BBT1E

1 Kings 17 in the BDS

1 Kings 17 in the BEV

1 Kings 17 in the BHAD

1 Kings 17 in the BIB

1 Kings 17 in the BLPT

1 Kings 17 in the BNT

1 Kings 17 in the BNTABOOT

1 Kings 17 in the BNTLV

1 Kings 17 in the BOATCB

1 Kings 17 in the BOATCB2

1 Kings 17 in the BOBCV

1 Kings 17 in the BOCNT

1 Kings 17 in the BOECS

1 Kings 17 in the BOGWICC

1 Kings 17 in the BOHCB

1 Kings 17 in the BOHCV

1 Kings 17 in the BOHLNT

1 Kings 17 in the BOHNTLTAL

1 Kings 17 in the BOICB

1 Kings 17 in the BOILNTAP

1 Kings 17 in the BOITCV

1 Kings 17 in the BOKCV2

1 Kings 17 in the BOKHWOG

1 Kings 17 in the BOKSSV

1 Kings 17 in the BOLCB

1 Kings 17 in the BOLCB2

1 Kings 17 in the BOMCV

1 Kings 17 in the BONAV

1 Kings 17 in the BONCB

1 Kings 17 in the BONLT

1 Kings 17 in the BONUT2

1 Kings 17 in the BOPLNT

1 Kings 17 in the BOSCB

1 Kings 17 in the BOSNC

1 Kings 17 in the BOTLNT

1 Kings 17 in the BOVCB

1 Kings 17 in the BOYCB

1 Kings 17 in the BPBB

1 Kings 17 in the BPH

1 Kings 17 in the BSB

1 Kings 17 in the CCB

1 Kings 17 in the CUV

1 Kings 17 in the CUVS

1 Kings 17 in the DBT

1 Kings 17 in the DGDNT

1 Kings 17 in the DHNT

1 Kings 17 in the DNT

1 Kings 17 in the ELBE

1 Kings 17 in the EMTV

1 Kings 17 in the ESV

1 Kings 17 in the FBV

1 Kings 17 in the FEB

1 Kings 17 in the GGMNT

1 Kings 17 in the GNT

1 Kings 17 in the HARY

1 Kings 17 in the HNT

1 Kings 17 in the IRVA

1 Kings 17 in the IRVB

1 Kings 17 in the IRVG

1 Kings 17 in the IRVH

1 Kings 17 in the IRVK

1 Kings 17 in the IRVM

1 Kings 17 in the IRVM2

1 Kings 17 in the IRVO

1 Kings 17 in the IRVP

1 Kings 17 in the IRVT

1 Kings 17 in the IRVT2

1 Kings 17 in the IRVU

1 Kings 17 in the ISVN

1 Kings 17 in the JSNT

1 Kings 17 in the KAPI

1 Kings 17 in the KBT1ETNIK

1 Kings 17 in the KBV

1 Kings 17 in the KJV

1 Kings 17 in the KNFD

1 Kings 17 in the LBA

1 Kings 17 in the LBLA

1 Kings 17 in the LNT

1 Kings 17 in the LSV

1 Kings 17 in the MAAL

1 Kings 17 in the MBV

1 Kings 17 in the MBV2

1 Kings 17 in the MHNT

1 Kings 17 in the MKNFD

1 Kings 17 in the MNG

1 Kings 17 in the MNT

1 Kings 17 in the MNT2

1 Kings 17 in the MRS1T

1 Kings 17 in the NAA

1 Kings 17 in the NASB

1 Kings 17 in the NBLA

1 Kings 17 in the NBS

1 Kings 17 in the NBVTP

1 Kings 17 in the NET2

1 Kings 17 in the NIV11

1 Kings 17 in the NNT

1 Kings 17 in the NNT2

1 Kings 17 in the NNT3

1 Kings 17 in the PDDPT

1 Kings 17 in the PFNT

1 Kings 17 in the RMNT

1 Kings 17 in the SBIAS

1 Kings 17 in the SBIBS

1 Kings 17 in the SBIBS2

1 Kings 17 in the SBICS

1 Kings 17 in the SBIDS

1 Kings 17 in the SBIGS

1 Kings 17 in the SBIHS

1 Kings 17 in the SBIIS

1 Kings 17 in the SBIIS2

1 Kings 17 in the SBIIS3

1 Kings 17 in the SBIKS

1 Kings 17 in the SBIKS2

1 Kings 17 in the SBIMS

1 Kings 17 in the SBIOS

1 Kings 17 in the SBIPS

1 Kings 17 in the SBISS

1 Kings 17 in the SBITS

1 Kings 17 in the SBITS2

1 Kings 17 in the SBITS3

1 Kings 17 in the SBITS4

1 Kings 17 in the SBIUS

1 Kings 17 in the SBIVS

1 Kings 17 in the SBT

1 Kings 17 in the SBT1E

1 Kings 17 in the SCHL

1 Kings 17 in the SNT

1 Kings 17 in the SUSU

1 Kings 17 in the SUSU2

1 Kings 17 in the SYNO

1 Kings 17 in the TBIAOTANT

1 Kings 17 in the TBT1E

1 Kings 17 in the TBT1E2

1 Kings 17 in the TFTIP

1 Kings 17 in the TFTU

1 Kings 17 in the TGNTATF3T

1 Kings 17 in the THAI

1 Kings 17 in the TNFD

1 Kings 17 in the TNT

1 Kings 17 in the TNTIK

1 Kings 17 in the TNTIL

1 Kings 17 in the TNTIN

1 Kings 17 in the TNTIP

1 Kings 17 in the TNTIZ

1 Kings 17 in the TOMA

1 Kings 17 in the TTENT

1 Kings 17 in the UBG

1 Kings 17 in the UGV

1 Kings 17 in the UGV2

1 Kings 17 in the UGV3

1 Kings 17 in the VBL

1 Kings 17 in the VDCC

1 Kings 17 in the YALU

1 Kings 17 in the YAPE

1 Kings 17 in the YBVTP

1 Kings 17 in the ZBP